CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,729
- 5,923
Karibuni Tena katika story hii
Kama kawaida ni mwanzo mpaka mwisho hakuna kuishia njiani
Kutoka "madam president" na ",kesi ya Mzee Mnyoka"
Ssa Leo tunaanza kisa kingine Cha Mpangaji
Mtunzi ni Mimi mwenyewe CK Allan
(0746 Mia mbili sitini na sita mia mbili sitini na Saba)
MPANGAJI 01
Hakuna mpangaji yoyote ambaye alikuwa anafahamu asili ya Yule mpangaji mwenzao, hata jina lake la ‘Sele’ wapo waliosema halikua jina lake halisi, lakini yote kwa yote Sele kama unavyoweza kusema alikua mpangaji wa kudumu wa mzee Mhina, miaka ilikatika na sio mzee Mhina wala wapangaji ama watoto wake walijua kazi halisi ya Sele.
Wapo waliosema sele alijihusisha na kazi ya kuzibua vyoo huko mjini mbali na hapo, wengine walisema sele Alikuwa mtu wa ‘kitengo” na kama ilivyo kawaida ya wabongo basi wengine walizua kuwa sele ni jahili mzoefu,
Kwanza Sele asingetoka nje ya chumba chake bila kuitwa, na kwakuwa chumba chake kilikua ni selfu basi huwezi kujua kama sele yupo ndani au ametoka.
Mama mwajuma hawezi kusahau yeye na wapangaji wenzake walivyoumbuka siku hiyo walitumia masaa zaidi ya mawili kumsengenya Sele kwa sauti ya juu kabisa.
“Tena nakuambia huyu Sele itakuwa anafuga majini, mwanaume gani huwezi kumkuta yuko nje na wenzake, nyumba haina redio wala tivii halo halooo!”.
“halafu hata siku moja sio mwanaume wala mwanamke aliwahi kuingia hicho chumba!”
“hakuna hata ndugu yake mmoja aliyewahi kuja hapa nakuambia mwaka wa sita huu mimi niko hapa!” wapangaji wenzake walikua wakiendelea kumzodoa sele,
Mama Mwajuma alikua amekazana kuongoza maongezi hayo bila kujua sele alikua ndani akiwasikiliza tu,
Ni mpaka pale waliongea hadi wakachoka ndipo Sele alitoka akiwa na mkoba wake.
Alimsalimia mama Mwajuma kwa heshima kama ilivyokuwa kawaida yake kisha akatoa elfu tano na kumpa mama Mwajuma ambaye alishikwa na kigugumizi.
“hii hela ya umeme utampa kaka Efraimu hapo tutaonana baadae” alisema Sele akitoka zake..
Huku nyuma wale wanawake waliangua kicheko
“tumeumbuka shoga, umbea huuu”
Alisema aisha akirudi ndani kwake..
****************************
Kama kawaida siku hiyo saa tatu usiku Sele alirejea zake nyumbani kwake aliwapita wanawake kadhaa waliokuwa bado hawajamaliza kupika vyakula vyao vya usiku, aliwasalimia kana kwamba hakuna chochote kilichotokea asubuhi ile kisha akafungua mlango na kujitosa ndani.
Huku nyuma vicheko vilisikika kama kawaida lakini aliwapotezea, hakuwa na muda wa kubishana nao kwanza ukimtoa Ephraim, wapangaji wengine walimkuta akiwa pale, kwanini ahangaike nao.
Usiku wa manane Sele alistushwa na kelele za wapangaji huko nje ya chumba chake alijaribu kutega sikio kusikiliza vizuri na kugundua ulikua ugomvi wa mke na mume tu, kama kawaida hakujishughulisha na ugomvi usiomhusu akavuta shuka lake na kulala.
Alfajiri alistuka mlango wake ukigongwa kwa nguvu na Ephraim , alimtambua sauti yake
“labda ni pesa ya umeme” aliwaza akitoka akivaa “malapa” yake na tisheti kisha akafungua mlango na kutoka
‘OI, broo’ alisema Sele
‘kuna kikao mshkaj njoo chap ‘ alisema Ephraim akirudi zake, kwa muda wote aliokaa pale hakuwahi kumuelewa Sele, kuna wakati alijaribu kumzoea lakini alijikuta akishindwa na hakuna hata siku moja alifanikiwa kukaa nae zaidi ya dakika tano.
Hata kwenye vikao vya usafi, umeme na maji, Sele hakuchangia chochote alisubiri makubaliano tu kisha alitoa pesa yoyote itakayokubaliwa.
Hata mzee Mhina alikua akimtolea mfano kuhusu ulipaji kodi, haijawahi kutokea Sele akapitisha mwezi bila kulipa kodi ya pango.
Tofauti na vikao vingine , siku hiyo mzee Mhina na balozi wa nyumba walikuwepo kwenye kikao cha siku hiyo kidogo sele alistuka lakini hakuonyesha mshangao wake wazi akasogea na kukaa kwenye mkeka kama wenzake.
“nadhani wotetupo sasa tuendelee ili wengine waende kutafuta riziki”
Alisema mzee Mhina. Wote waliitikia kisha Balozi akamkonyeza mzee Mhina kumuashiria atoe hoja kikao kianze
“ sasa ndugu zangu nimepata malalamiko kuhusu Bwana Sele hapa” alianza Mzee Mhina,
‘Jana usiku kulikua na ugomvi miongoni mwa wapangaji na walitoka na kupigana bado kidogo wauane, wapangaji wote walitoka kuamua na kusaidia lakini ndugu yetu Sele yeye wala hakujisumbua kutoka, sio jana tu lakini hata wakati ule chumba cha mama Isa kilipopata hitilafu Bwana Sele pia hakutoka kabisa.
Nakumbuka pia hata wakati wa sherehe ambayo niliandaa mimi mwenyewe wakati binti yangu Rehema akifunga ndoa Bwana Sele pia hakuhudhuria hivyo kwa mazingira haya naona kabisa kuna kitu huyu mwenzetu anacho anajaribu kutuficha nikaona balozi uje kidogo utusaidie,” alimaliza Mzee Mhina huku wapangaji wote wakipiga jicho kwa Sele.
‘ ooh Kijana wangu Sele, hebu niangalie, hivi kweli leo hii hata nikikuambia unitajie majina ya wapangaji wenzako utawajua kweli?’ aliuliza Balozi huku wapangaji wengine wakicheka.
“huyu anamjua Ephraim tu ndio mwenzake huyoo” alidakia mama Mwajuma.
‘ Hapana nawajua wote!” alidakia Sele kisha akaendelea.
‘wewe ni mzee Lota, una watoto wanne , watatu wa kike na mdogo wa mwisho wa kiume, Yule ni Aisha na mumewe Mkude, Yule ni mama Mama Mwajuma na mume wake Ngoda, pale ni Isa, kule ni John na hapa ni kaka Ephraim na mke wake mama Joan’ alimaliza Sele huku akiwaacha wapangaji wote mdomo wazi, hususani huyu mpangaji John ambaye alikua na siku ya pili tu!
“Wewe mwana wewe, umejuaje mpaka hawa wapangaji wapya? Umeona sasa Balozi tukisema sisi tunaishi na zimwi.. zimwi..” alidakia mama Mwajuma huku wapangaji wote wakiangua kicheko.
“ Mama Mwajuma, tumalize kikao ili usichelewe kumuandalia mgeni wako Ester anayekuja leo kutoka Lindi!” alisema Sele akitoka zake kurudi chumbani!
‘Bwana sele hatujamaliza lakini!” alisema Mzee Mhina lakini sele alirudi zake chumbani kumalizia usingizi wake,
“makubwa haya, makubwa haya sasa kuhusu Huyu Ester huyu Sele kajuaje jamani” alisema mama Mwajuma huku akiondoka.
Kikao kile kilivuruga kabisa mtazamo wao kuhusu Sele, wapangaji waligawanyika huku wengine wakitaka afukuzwe, na wengine wakisema hawajaona kosa
“sasa afukuzwe kwa kosa gani?
Bili zote analipa, usafi analipa, kodi ya watu analipa, hawajawahi kugombana na mtu kaka wa watu, muacheni bhana!”
Alisema Ngoda na kisha kikao kikaishia hapo
Inaendelea