Hadithi: Madam President

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Mtunzi ni CK Allan
Madam President
Juni 1998
Ilikua jioni nzuri kabisa ambapo sehemu mbali mbali za jiji la Tanga Kuna Hali ya baridi na mvua nyepesi zilikua zimeanza, nikiwa na Rafiki yangu Jacob tulikua mwisho kabisa ya mstari kuingia kwenye Basi la shule tayari kwenda Tanga mjini ambapo kesho yake mashindano ya mkoa umiseta yalikua yanaanza,

Mimi na Jacob Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wengine tulikua na Furaha kabisa ya kutoka eneo la shule na kwenda kwenye mashindano hayo... Mimi nilikua nacheza mpira wa miguu na Jacob yeye alikua mchezaji mahiri wa mpira wa kikapu..

Tulipenda kumuita Joo tukikatisha jina la Jordan tukimfananisha na mchezaji mahiri Michael Jordan,

Hakika alifanya vizuri lakini pia umbo lake lilimbeba kwani alikua mrefu ...

Kwenye mpira wa miguu Mimi nilicheza Kama winga wa kulia namba 7, pamoja na Mambo mengine lakini nami nilipewa jina la Beckam kutokana na kuwa mahiri katika kucheza mipira iliyokufa,
Tulisogea kwenye basi huku tukishikilia mabegi yetu na Safari ikaanza ...


**************

Ni saa 3 tuliwasili Shule ya Tanga technical ambapo Kama ilivyo kawaida wanafunzi walipiga makelele na Furaha huku wakigombania kushuka,

Ilikua Ni Mara ya kwanza kufika eneo Hilo hivyo nilihakikisha kila kitu kimekaa vizuri kabisa Kisha nikashika begi langu na kusogea kuelekea kwenye mabweni ya wavulana ambayo tulikua tumeandaliwa...

"Dah mwanangu angalia watoto walivyo wazuri kweli hii ndio Tanga! Tutatoka kweli?"
Alisema Jacob akinisukuma bega kidogo,

"Hapana kaka Mimi siwezi kumsaliti Mary kabisa" nilisema huku nikionyesha dalili za kukasirika kidogo tulipanda ngazi na kuelekea vyumbani huku ratiba zingine zikifuata!

*************
Mechi ziliendelea huku Timu yetu ya wilaya ya Korogwe ikiwa kwenye nafasi ya pili baada ya Tanga jiji kwenye mpira wa miguu huku mpira wa kikapu tukiwa tunaongoza kwenye kundi letu,

Tanga jiji walikuwa mbele kwa points mbili dhidi yetu na mechi ya mwisho ndio ambayo ilikua na ushindani Kwani ndio ambayo ingetoa mshindi wa kundi, kwa kuzingatia Hilo mechi yetu ambayo tulicheza dhidi ya Muheza Mimi, Joackim , Abdi na Musa Mwalimu alitupumzisha ili tusipate majeraha kusudi tucheze mechi ya mwisho dhidi ya Tanga jiji,

Kutokana na presha na ushindani wa Timu zote mbili mechi ilibidi kuhamishiwa kwenye uwanja wa mkwakwani na mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa,

Ilikuwa Ni Mara yangu ya kwanza kucheza kwenye umati mkubwa namna Ile,

Mechi ilianza kwa utulivu na umakini mkubwa huku kila Timu ikiepuka kufanya makosa, hata hivyo kwenye dakika ya 34 hivi wenyeji tanga jiji walipata penati baada ya beki wetu Abdi kucheza rafu ..

Mchezaji wa tanga jiji alicheza penati kwa ufundi wa Hali ya juu na kupelekea Hadi mapumziko tukiwa nyuma kwa goli moja...

Wakati tukiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Mwalimu alituambia kuwa tuna nafasi kubwa ya kushinda mchezo hususani Kama tutatumia nafasi za pembeni nakumbuka kocha alinifokea Sana kwa kushindwa kuwasoma mabeki wa Timu pinzani kuwa walikuwa wazito kufanya maamuzi ..

" Allan tumia zile nafasi, wanapoanza kupasiana golini hebu kimbia kwa spidi wanyang'anye mpira usisubiri kuletewa..." Mwalimu James aliongea huku akinitolea macho yake makali...

Nilijikuta natamani turudi uwanjani sekunde Ile ile ..

Wakati tunarudi uwanjani Jacob alikuja pia akinitakia kila la kheri tukarudi uwanjani...

****************
Tulibaki tumetazamana na kuduwaa maana wakati tanga jiji wanaanza mpira moja kwa moja wakapiga mpira mrefu na winga wao wa pembeni akakimbia na kuachia krosi nzuri na wakati Abdi anataka kuokoa akajifunga!

Hakika nilijikuta nakaa chini, macho yangu yalishindwa kutazama jukwaani hata hivyo kapteni wetu Joackim alichukua mpira haraka na kuupeleka katikati Kisha akatupigia makofi ya kututia Moyo,

Hatimaye niliona kocha wetu Mr James nae akitabasamu! Kana kwamba hakuna kitu kilichotokea

Nakumbuka baada ya kuanza mpira Joackim alirudisha nyuma kwa Abdi Tena ambaye alituliza Kisha akapiga shuti kubwa kwenda langoni kwa Tanga jiji,

Wakati beki wa tanga jiji anatuliza mpira

Nilikumbuka maneno ya kocha na hivyo nikakimbia kwa spidi Kali na kumpoka ule mpira Yule beki....nilisikia uwanja mzima ukizizima wakati naelekea golini na kipa aliposogea nikaubetua na kutumbukiza wavuni!

Uwanja mzima ulizizima kwa furaha nilikimbilia mpira golini na kuuweka Kati Kati ya uwanja...

Nilimtazama kocha wangu ambaye alionyesha Hali ya kukasirika naam Mr James ama Mzee wa vise versa tulipenda kumuita alikuwa sio mtu wa kutabirika anaweza kukupongeza unapokosea na akakufokea unapofanya vizuri!

Hatimaye dakika ya 60 tukapata Kona upande wa kulia na nikaenda kuicheza wakati nasogea Abdi alinionyeshea mkono kuwa nimpelekee pale alipo,
Nami bila kusita nikapiga shuti Kali kuelekea langoni na Abdi akaruka kichwa Safi kabisa na kuweka mpira wavuni ..

Mbili mbili!! Tulikumbatiana na kushangilia kwa nguvu huko nje ilikua Ni makelele na polisi ikawalazimu kufanya kazi ya ziada kuweka Hali sawa...

Tuliendelea kushambuliana kwa zamu na wakati zimeongezwa dakika mbili kocha wetu alisema tupande wote kushambulia kwenye dakika ya mwisho kabisa nilipokea mpira nikiwa katikati ya uwanja nikatoa pasi kwa Joackim Kisha nikasogea Tena wakati napokea mpira nikachungulia golini na kumuona kipa wa Tanga jiji amesogea mbele bila kujiuliza maswali nilivuta pumzi ndefu Kisha nikajivuta na kuachia shuti Kali la juu ambalo lilimshinda goli kipa wa Tanga jiji na kutinga moja kwa moja wavuni!

Nilikimbilia nje kwa furaha na wenzangu wakanifuata huku Mwalimu wetu akishangilia kwa nguvu hakika ilikua Ni furaha kubwa Sana,

Hatimaye mechi ikamalizika na tukaibuka washindi kwa goli 3-2,

Bila hiyana nikachaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mechi ,
Wakati tunatoka upande wa getini Mkuu wa mkoa alikuja kutusalimia huku akinipongeza Binafsi kwa kunipa mkono

"Hongera Sana Allan"

Sauti nyingine ya kike ilisikika
"Ooh huyu Ni binti yangu Janet, amevutiwa Sana na uchezaji wako"

Alisema Mr Kibwana Mkuu wa mkoa..

"Asante dada Janet" nilisema huku nikimpa mkono
Hata hivyo nilishangaa anashikilia mkono wangu zaidi...

"Uko form ngap?" Aliniuliza
"Form 5" nilijibu
" Ah Mimi Niko form 6" alisema , nimependa unavyocheza unajituma Sana nitakuwa na zawadi yako kesho !

Alisema huku akiniachia mkono wangu,

Tuliondoka Hadi bwenini ambapo ilikua Ni furaha Sana kwetu...
**************

Kesho yake kwenye majira ya saa 4 asubuhi nilipata ujumbe kuwa Kuna mgeni alikuja Jacob..

"Kaka una bonge la zali yaani Yule demu kaja"

"Demu yupi?"
Nilisema

"Ah kaka Yule mtoto wa Mkuu wa mkoa"

Alisema Jacob

"Ah, anasemaje kwani?"
Nilisema nikivaa Kanda mbili zilizokuwepo pale ndani Kisha tukatoka na Jacob

Wakati tunakaribia Janeth alinikimbilia Kisha akanikumbatia
Nilipigwa na mshangao mno huku vijana wengine wakipiga kelele za shangwe pale...


Ni Kama Janet alistuka hivi kwa kuona aibu kidogo Kisha akasema twende nje tukaongee .

"Nimekuletea zawadi yako iko hapo nje" alisema akinivuta mkono Jacob alibaki kuduwaa Kama afuate ama abaki...

Tulitoka nje ya geti Kisha Janet akaenda kwenye Gari akatoka na mfuko mmoja wa Rambo hivi,

'Hii hapa zawadi yako Allan' alisema

"Asante Sana Janet"
Nilisema nikipokea mfuko huo

Tulisogea mpaka uwanjani ambapo wanafunzi wengine walikua wanaendelea na mazoezi mbali mbali Kisha tukakaa chini,

Nakumbuka Janet aliniambia wazi wazi kuwa ananipenda Sana na anatamani tuwe wapenzi...

Hata Hivyo kiuhalisia sikuwa na upendo wowote kwake nikilinganisha na jinsi nilivyokuwa nikimpenda Mary mpenzi wangu ambaye nae alikua kidato Cha 5 pale mombo sekondari nilimlinganisha na Janet nikaona Janet akiachwa mbali Sana, nilitamani kumueleza Janet kuwa hanivutii hata kidogo Ila nilijikuta nashindwa nikabaki kimya tu..

"Tafadhali niambie unanipenda Allan" Janet alinistua katika mawazo yangu hayo...

"Yaani Janet nashindwa niseme Nini ngoja kwanza nirudi bwenini" nilisema Kisha nikasimama Janet aliahidi kuja Tena kesho asubuhi,

Nilirudi ndani kwa unyonge na kukuta Jacob akiwa na wanafunzi wengine wakinisubiri
Wote waliponiona walinikimbilia na kuninyang'anya ule mfuko

"Dah mwanangu umepata bonge la zali, mtoto wa Mkuu wa mkoa kakuganda, dah bonge la zali" walisema huku wakifungua ule mfuko na kutoa track suit nzuri Sana

"Kwahyo mnasemaje Sasa kuhusu huyu demu?" Niliwauliza

"Ohoooo ushaanza Tena kuuliza ujinga, huyo unatakiwa umalize we vipi?" Jacob alidakia huku wenzake wakiongezea , Kama ujuavyo msomaji Basi akili za wanafunzi wa kiume nikajikuta nalewa ujinga wao hivyo siku iliyofuata nilimkubalia Janet huku moyoni nikiwa Sina hata chembe ya upendo kwake,


***********************

Tulirudi shuleni na Janet alizidi kuniandikia barua na yeye alimaliza kidato Cha sita na akajiunga na chuo kikuu Cha Dar es salaam akisomea Mambo ya utawala,


Mimi nilimaliza kidato Cha sita na kujiunga na chuo Cha ualimu Marangu ,nikisomea stashahada ya ualimu...

Niliendelea kuwasiliana na Mary ambaye yeye alikua amejiunga na Masomo ya udaktari katika chuo Cha kcmc Moshi hivyo Mara nyingine siku za weekend tuliwasiliana na wakati mwingine yeye angefika chuoni au Mimi ningekwenda hospitalini hakika tulipendana Sana na tulishaweka Mipango ya kuoana..


Ni muda mrefu ulipita bila kuwa na mawasiliano na Janet , Mara ya mwisho alinitumia barua nikiwa namalizia kidato Cha sita na kwa makusudi sikujibu Ile barua yake ili kupoteza mawasiliano kabisa, kwa ufupi tuseme nilisahau kila kitu kuhusu Janet,



*****************

Novemba 2004

"Walimu Kama nilivyosema atakuja hapa waziri wa elimu na jopo lake hivyo tuhakikishe Mambo yanakuwa vizuri kabisa"

Mkuu wa Shule yetu Bwana Alfred alikua anatoa taarifa fupi kuhusu ugeni ambao ungefika shuleni kwetu Segera sekondari,


Ndio waziri wa elimu alikua na ziara ya kikazi mkoani Tanga na katika sehemu ambazo angepitia ilikua Ni kwenye shule yetu kuja kuzindua Jengo la maabara,


Ni miaka miwili Sasa ilikuwa imepita Tangu niajiriwe Rasmi kuwa Mwalimu katika shule hii ya segera Mara baada ya kumaliza mafunzo yangu ya ualimu chuo Cha Marangu Moshi,

Mary alikua na miezi mitatu Sasa akiwa ameajiriwa hospital ya Magunga wilayani Korogwe, na pia huu ilikuwa Ni mwaka wetu mmoja tukiwa ndani ya ndoa,

Tayari tulikua na mtoto mdogo wa miezi miwili


Mary alikua na likizo yake ya uzazi.


Msafara wa magari ulikua unaingia Sasa shuleni kwetu Mimi niliendelea na kipindi darasani Hadi pale tulipoitwa kukusanyika,



Ni wakati naangaza macho huku na kule ndipo macho yangu yakamuona Janet!


Ndio Ni yeye akiwa ananong'onezana Jambo na waziri wa Elimu nilirudi nyuma na kujichanganya na walimu wenzangu ili kusudi nisionekane ..


Waziri alitoa hotuba yake Kisha akawatambulisha aliongozana nao

"Huyu Ni madam Janet yupo ofisi ya Raisi akishughulika na Mambo ya utawala Bora, nadhani mlisikia kuhusu uteuzi wake hivi karibuni, na Yule Ni Bwana Joeli Ni mhasibu wa wizara na....."
Masikio yangu yalishindwa kuamini yanachokisikia

Ni kweli nilisikia kuhusu uteuzi katika ofisi ya Raisi , lakini hata sikuweza kuhisi kama ndie Yule Janet ninayemfahamu

Waliongea mengi na ilipofika zamu ya Janet aliongea Mambo machache lakini alipongeza Sana walimu kwa kazi nzuri ya kufundisha na kuwaongoza wanafunzi....wakati anamaliza aliomba Tena kuongea kitu alichokuwa amesahau...



"Jamani ngoja nisisahau nimeona kitu Cha tofauti kwenye hii shule, wakati napitia mazingira nimeona Kuna ubao mmoja hivi pale Kuna gazeti la shule na wanafunzi wanaandika Hadithi, wanachora vikatuni na kuandika makala mbali mbali, Ni kitu ambacho hatujakiona kabisa kwenye shule Nyingine hivyo kipekee kabisa nataka nimpongeze huyo Mwalimu aliyesimamia Hilo gazeti ,Mkuu wa Shule tafadhali niitie huyo Mwalimu" Janet alisema huku akifungua pochi yake,



"Mwalimu Allan tafadhali huku mbele"

Mkuu wangu Bwana Alfred aliniita kwa Mara ya kwanza nilitamani litokeee shimo ghafla niingie..

Nilitamani kumwambia Mkuu asinitaje Ila kwa ujasiri wa ajabu nikajikuta nasogea mbele,

"Liwalo na liwe" nilijisemea nikisogea mbele
kupiga hatua moja zaidi mpaka sehemu Mkuu wa shule aliponionyesha kusimama wanafunzi walipiga makofi nilitulia tuli na macho yetu yakagongana Mimi na Janet,

Ni Kama alishikwa na mshangao na kigugumizi Cha ghafla hivi,


"You?" Alisema akinipa Mkono
"Yeah, it's me" nilisema ,

"Mwalimu unafanya kazi nzuri Sana na kwakweli pokea hii zawadi," alisema huku akitoa laki moja kwenye mkoba wake,

Niliipokea Kisha nikarudi zangu kwa wenzangu,

Mapigo ya moyo yalikua yankwenda Kasi sikutegemea kuonana na hiki kiumbe kabisa,


Nilikumbuka barua yake ya mwisho Janet alisema hawezi kuolewa na mtu mwingine zaidi yangu , na japokuwa eti nimekaa kimya lakini atanitafuta na ole wangu anikute na mwanamke mwingine!


Wakati macho yetu yanakutana hakika Ni Kama alikua anasema "kumbuka Ile barua yangu kenge wewe!"



Tulitoka pale asembly na kwenda maabara ambako waziri alifungua Lile Jengo Kisha akapata nafasi ya kuongea na wajumbe wa bodi na walimu,

Janet Mara kwa Mara alikua akinitupia jicho huku akiendelea kuandika Mambo kadhaa kwenye notebook yake,


Baada ya kumaliza shughuli waziri na jopo lake waliaga na kuondoka ,

*****************

Miezi mitatu baadae

Nikiwa nimetoka kwenye kipindi nilikua nanawa mikono ili niingie kwenye ofisi ya walimu kupata chai ndipo Mkuu aliniita


Hivyo badala ya kuingia ofisi ya walimu nikatoka na kuzunguuka nyuma ya Jengo ambapo ndipo ilipokuwa ofisi ya Mkuu wa Shule,



"Sijui niseme Nini, lakini maisha ndivyo yalivyo, Sina namna" alianza Mkuu wa shule kwa sauti ya huzuni

"Mkuu mbona sielewi" nilisema nikikaa vizuri kwenye Kochi


Mr Alfred hakuongea zaidi alifungua faili moja pale mezani Kisha akatoa barua moja na kunikabidhi

Nilipokea na kuifungua haraka
Niliangalia kichwa Cha barua haraka
Yah : kuteuliwa kuwa afisa michezo na utamaduni wilaya ya Pwani


Niliifunga haraka kisha nikamwangalia Mkuu wa Shule ambaye nae aliniangalia tu,

"Ndio hivyo hongera Sana" alisema huku akitabasamu...



"Duh" nilisema huku nikichukua Ile barua na kutoka nje nilifika ofisini nikanywa chai Kisha nikatoka nje kwenye kivuli nikaagiza kiti nikakaa,


Nilipitia Ile barua Tena na ilionyesha wazi imetoka utumishi na nilitakiwa kuripoti kituo changu ndani ya siku 14 zijazo na nitagharamiwa kila kitu niliwaza na kuwazua na mwishowe nilibaini Lazima Janet atakuwa na mkono wake katika Hili Jambo.



Baada ya wiki moja nilifika Pwani kuripoti na nikaonyeshwa ofisi yangu pamoja na muongozo wa majukumu na zaidi ya yote Bwana Luda afisa michezo aliyekuwa hapo alinipokea na kunielekeza Mambo muhimu kwa ufupi kwani alipaswa kuondoka kesho yake kwenda kigoma ambapo ndipo alipangwa kituo kipya baada ya aliyekuwepo huko kustaafu.



Kwa ufupi hakukuwa na majukumu mengi Kama kufundisha darasani ilikua Ni kufuatilia masuala ya michezo wilayani hususani kwenye shule.


Nilirudi kuhamisha familia yangu na kuaga ndugu na jamaa Kisha nikahamia Rasmi Pwani Kama afisa michezo na utamaduni wilaya.

Itaendelea huko kwenye comment
 
Madam president 2

Ni baada ya wiki mbili kupita siku hiyo nikiwa ofisini napanga vitu baadhi , nilipokea ujumbe kuwa nahitajika kwa mkurugenzi,


Basi nilirudishia mlango Kisha nikatoka kupanda ngazi, njiani nilipishana na jamaa ambaye sura yake haikuwa ngeni Sana hata Hivyo sikumjali Sana,


Ndipo nikafika kwa katibu muhtasi ambaye alitabasamu tu na kunielekeza nipite..


Nilifungua mlango Kisha nikaingia ndani na kupigwa na butwaa,

Mbele yangu Janet alikua amekaa na mkurugenzi wakiongea Mambo kadha wa kadha,


Basi niliwasalimia Kisha nikakaa kwenye kiti..

"Ndio Afisa huyu Ni madam Janet kutoka Ofisi ya Raisi,

Ni mgeni wako!" Aliongea huku akimtazama Janet,

"Hello Allan, nadhani Ni Mara ya pili kuonana hongera kwa uteuzi nadhani Mara ya mwisho tulionana kule Segera sekondari"

Alianza Janet huku dimpo zake zikionekana,


"Ah tunajua Hali ya mkoa wa Pwani wanafunzi hawana muamko Sana na elimu, kwahiyo Kama Ofisi tukaona tuje na program fulani hivi ambayo itasaidia watoto kupenda shule na ndipo Sasa tukaona kupitia maafisa michezo wa Wilaya mnaweza kuja na wazo zuri ambalo linaweza kuwa Chachu sambamba na Hilo ,kwa wiki moja hii tutambelea shule zote za sekondari katika Wilaya hii kuongea machache na walimu wa michezo kwahiyo sasa kajiandae tuanze safari,"

Alisema Janet Kama Mwalimu anayeongea na mwanafunzi wake,


"Afisa, kajiandae saa 6 kamili ziara itaanza wewe ndio mwenyeji, na pia Ni wakati wako kujua baadhi ya zile shule ambazo hamjafika, usijali ofisi italipa allowance zote kajiandae bhana"



Bwana shija ambaye tulipenda kumuita Broo aliongea Basi nilitoka nje na nikachukua boda boda Hadi kwangu,


Nilimwambia mke wangu Hali ilivyokua,


"Kwahiyo Kuna siku Nitakuwa narudi usiku Sana ama nisirudi kabisa, but Ni wiki moja tu d"

Nilisema baada ya kuchukua begi langu na nguo kadhaa,



Nilifika na kupanda kwenye Gari na Kama nilivyotabiri msafara haukuwa na watu wengi Sana,


"Nimekwisha"

Niliwaza Gari ikiondoka tulikaa na Janet Siti moja ya nyuma kabisa huku kila mmoja akiwa anasubiri mwenzake aanze kuongea...


"Hatimaye tumeonana Allan"

Alianza Janet akitabasamu,

"Yeah Asante Sana kwa kunipa Shavu aisee"

Nami nilisema,


"Shavu gani Tena" aliuliza Janet huku akishikilia vizuri mkono wake wakati landcruiser ikichanja mbuga,


"Ningezeeka kule kwenye chaki aisee"

Nilisema nikicheka,


"Hahaha umejuaje Kama Ni Mimi?"

Aliuliza

"Ah who else? Ni wewe tu bhana " nilisema,

"Hata hivyo kasome bado Kuna nafasi nyingi kwa ajili yako"

Alisema Janet

"Okay dereva Kuna iyo njia hapo pinda kulia tuingie hapo Kuna shule tunaweza kuanza nayo"


"Ah shule gani Tena hebu achana na izo mishe Mimi nimekuja kukutembelea mpenzi wangu tule Bata kwa wiki moja hii, huko tunaweza kutuma maafisa elimu kata" alisema Janet Sasa nilitamani kuruka dirishani,


Wakati mwingine nilitamani kucheka,.

"Whaaaat?"
Nilihamaki,

"Yes, baby,!, Kumbuka nilichokuambia nakupenda Allan kila siku nilijaribu kukutafuta kila sehemu mpaka pale nilipokukuta Segera , believe me nilitaka upate cheo kikubwa zaidi lakini bado Kuna vigezo haukutimiza"


Alisema Janet kauli ambayo ilitoka kabisa ndani ya moyo wake,


"Asante Janet kwa kunipenda lakini......"


alinikatisha.


"Usiseme kitu, usiseme chochote usiseme kitu naomba usiseme kitu "

Alisema Janet

"Eeh Mungu nisaidie dhidi ya hiki kiumbe, natokaje hapa"


"John twende pale new Ambassador hotel"


Aliongea Janet ,

Dereva alikata Kona na kuelekea kwenye hotel hiyo kubwa Sana ambayo ilikua Ni kituo Cha vigogo kwa mkoa mzima wa Pwani, kwa haraka wageni katika hii hotel walipata huduma zote ambazo wangepata katika hotel kubwa kubwa za kule Jijini Dar,

Kwa unyongea nilishuka na kuelekea hapo Hotelini Kama vile mbuzi anayekwenda machinjoni,

"Balaa gani Hili Tena"
Nilijisemea nikipiga hatua kumfuata Janet

"Karibu Sana Allan, wewe John unaweza kutafuta meza yako tuu"

Alisema Janet huku akinivutia kiti niweze kukaa,

Ilikua Kama saa 7 kasoro hivi Hivyo tuliagiza chakula na kuanza kula,


"Yaani Nina hamu na wewe balaa miaka yote hiyo nilikua nakuwaza wewe tu mpenzi niambie Sasa maisha yako yakoje"

Alianza Janet,


"Ah tunamshukuru Mungu Mambo yako vizuri kabisa things goes on"


Nilisema huku nikipiga msosi lakini mawazo yangu yalikua maili kadhaa huko,

Nilimuwaza mke wangu pamoja na mtoto wangu ambao maskini hawakujua kinachoendelea huku,

hauko sawa Allan, huonyeshi kufurahia , huonyeshi kujali yaani Ni Kama hauko hapa,..

Niambie kitu gani unacho wewe,"

Janet Sasa aliacha kula Kisha akanitazama,



Nilitamani kumwambia kuwa tayari nimeoa na nina mtoto ,

Ila sauti nyingine ikaniambia huo Ni uoga,.


"Acha ujinga Allan piga chombo hiyo"


Sauti nyingine bila shaka ilitoka kwa Shetani ilininong'oneza


"Hapana ujue wakati natoka sikufunga ofisi yaani hapa nawaza kweli aisee" nilisema huku nikiwa nakaa sawa...



"Ooh hivyo tu na kumbe nimesahau huna Simu Afisa, okay subir"

Alisema Kisha akatoa Simu yake ya mkononi Aina ya Motorola ya kufunua hivi akabonyeza bonyeza namba Kisha akaweka sikioni,


"Ndio mkurugenzi, Niko na Afisa Michezo hapa , tunaelekea huko vijijini na kutokana na mizunguuko ya wiki hii naomba mkaimishe mtu ofisi yake kwa muda"



Alisema Kisha akazima Simu yake hiyo kwa kuifunika,



"Haya kingine?, Hakuna, Basi Endelea kula" alisema Janet akiwa anatabasamu


"Naamini tuna mengi ya kuongea Allan, let's go"

Alisema Kisha akanyanyuka,


Aliongea na Dereva wake Kisha John akaniaga akasepa zake,


Tulipanda juu ghorofani ambapo kulikua na chumba kizuri sana chenye sebule kubwa,



Nilivua koti langu Kisha nikakaa sebuleni, wakati huo Janet alipitiliza bafuni kuoga Kisha akatoka akiwa amejifunga Taulo
"Vipi huogi?"


"Aah nakuja we oga kwanza bhana"

Nilisema huku nikimaliza kuomba Sala za mwisho...



"Potelea pote,"

Nilisema Kisha nikaenda bafuni kuoga.


****************

Siku tatu tulibaki pale Hotelini Ni Mara chache tu John alikuja kuleta taarifa mbali mbali tu Janet,



Mapenzi yalikolea kwani hatukuelewa Kama Ni mchana au usiku, ilikua Ni kulala na kulala na kufanya mapenzi tu, ..


😊😊
 
MADAM PRESIDENT 03

Wiki moja iliisha na tulipitia shule chache tu Kisha nikarudi ofisini kuendelea na kazi,

Nilijisikia vibaya moyoni kwa yote niliofanya na Janet lakini sikuwa na ujasiri wa kumueleza mke wangu chochote,

Janet aliendelea kunitumia pesa nyingi ambapo nilinunua eneo kibaha Kisha nikajenga nyumba kimya kimya bila kumwambia mke wangu,
Mke wangu nilimhamishia hospitali ya mlandizi ambako ilikua karibu na sehemu tuliyoishi,


********************

Mwaka 2010

Nilikua nimetoka kazini mapema ili kujiandaa kumpokea mdogo wake mke wangu ambaye alikua anakwenda chuo Cha uuguzi muhimbili,

Tuliona Ni Busara apitie kwetu walau tumuongezee mahitaji kidogo .
Ilikuwa Ni mwezi wa sita ambapo chama tawala Tanzania ilikua Ni siku yao ya kupitisha jina moja la mgombea uraisi kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,
Kwa miaka miwili mfulululizo hatukuwahi kuonana na Janet zaidi ya kuwasiliana tu kwenye simu na kwa njia ya mtandao,

Bila kuelewa chochote nilishindwa kumueleza Janet kuwa nimeoa

Nakumbuka nilimshirikisha rafiki yangu Jacob ambaye kwa kipindi hicho alikua katika chuo Cha jeshi Monduli katika maongezi yetu aliniambia

Nihakikishe nimeshajipanga vizuri kiuchumi ikiwemo kuwa na miradi ya Siri, Kisha nimwambie Janet wazi wazi kuwa nimeoa na Mambo mengine yatajitengeneza yenyewe.....

Kwa miaka miwili hii nilihakikisha najenga nyumba tatu ambazo zote nilipangisha ,

Kisha nikamfungulia mke wangu duka kubwa la dawa kibaha mjini, hakika maisha yalikwenda vizuri...
Sikuona umuhimu wa Janet Sasa katika maisha yangu Tena, hata wakati mwingine anapiga Simu Ningeweza kupokea kwa kujisikia ..

Niliyawaza hayo nikiwa sebuleni kwangu wakati nawasha tv yangu..

"Na chama Tawala Tanzania kimemteua Bi Janet Abraham Shayo kuwa mgombea uraisi mwaka huu 2010, ukumbukwe hii Ni nafasi kubwa kabisa ya kwanza kwa mwanamke kuwahi kushika tangu nchi hiyo kupata Uhuru,..."


Alikua mtangazi wa KTN akiongea katika taarifa hiyo fupi ...
"Ohooooooo"

Nilijisemea nikitetemeka
Janet alipitishwa kuwa mgombea Uraisi na hatimaye akapita kwa kura zaidi ya asilimia 70 na akatangazwa kuwa Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,


Binafsi nilifurahi kwakuwa nilijua Sasa mahusiano yetu yamefikia mwisho,


Wakati anaapishwa Janet alifika uwanjani akiwa na mwanaume ambaye alisadikika ndie mume wake pamoja na watoto wawili,

Kwa muda wote niliokaa na Janet sikuwahi kumuona akiwasiliana na mume wake huyo,

Hata hivyo nilifurahi tu kwakuwa Sasa ningeweza kuwa huru na maisha yangu,
Nilishazoea kazi yangu pale halmashauri na tayari nilishazoeana na marafiki pale ofisini...

Ilipita wiki moja ambapo siku hiyo nakumbuka ilikua ijumaa Jacob alinipigia Simu kuwa ameacha kazi jeshini!


Nilipigwa na butwaa Sana kwani Jacob ninayemjua alipenda kazi ya Jeshi kuliko hata kula, kila Mara alipotoka kwenye mpira wa kikapu aliwaza jeshi,
Eti leo hii anaacha kazi kwa hiari yake nilishangaa Sana,
Hata hivyo mwishoni mwa mazungumzo yake niligundua Kuna ujumbe alikua ananitumia nakumbuka tukiwa shule tulipenda kuongea kwa mafumbo hususani katika Mambo yaliyohusu wasichana,


"Ndio hivyo kaka, hata ukisoma mhubiri 3 kwenye Biblia utaona kila Jambo na wakati wake, naamini muda wangu Jeshini umeisha
Kumbuka Sana haya maneno"

Alimalizia Jacob

Niliwaza hayo maneno Kisha nikachukua Bibilia na kuangalia huo mstari ..

kila Jambo na wakati wake na kusudi lake chini ya mbingu

Nilijikuta natabasamu baada ya kuona Hilo neno chini ya mbingu..
Siku moja tukiwa tumekaa na Jacob aliniambia kuwa unapofanya kazi jeshini unafanya kazi chini ya mbingu,
Siku zote amri na mamlaka zote jeshini zinatoka juu kwenye mbingu kwahiyo kazi yao Ni kutii mbingu!


"Kaka tuko chini ya mbingu"


Hivyo bila shaka Jacob alikua haachi kazi Ila labda alikua anabadili kitengo,


Kama nilivyohisi Jacob aliniambia anasafiri nje ya nchi kwenda kutafuta maisha ughaibuni,


"Unajua kaka sisi ukishaacha kazi ukiendelea kubaki mtaani mtaa wa pili mtu akiiba kuku unaambiwa Ni wewe"

Jacob alikua anasema wakati tunapata chakula nyumbani kwangu baada ya yeye kuja kuniaga.

**********


Baada ya mwezi mmoja Sasa nilichokihofia kilianza kutokea,


Wakati natoka ofisini kwangu natembea kuelekea ilipo stendi ghafla alijitokeza mtu mmoja kana kwamba Alikua ananisubiri..



"Oya Broo subiri kidogo"

Alisema nikageuka bila kujali Sana akanitolea Simu yake kana kwamba Kuna kitu ananionyesha,


Nilipoichukua alinionyeshea ishara niweke sikioni,

"Ndio Allan mpenzi Mimi Janet , utapewa mzigo wako na hao vijana na maelezo mengine jumapili tuonane"

Simu ikakatika.

Nilibaki nimeduwaa Yule jamaa akanielekeza sehemu ya kupita ambapo tulifika na kutokea kwenye Gari lililokua na vioo vyeusi, akanitolea begi moja na bahasha ndogo ya kaki Kisha wakasepa zao...

Nilibaki na Lile begi na bahasha nikiwa nimeduwaa ...

Niliiweka Ile bahasha kwenye begi upande wa juu tu Kisha nikazunguuka kutokea stendi Kisha nikaenda upande wa kwenye vyoo vya wasafiri ,
Nililipa shilingi 100 Kisha nikaingia chooni,.

Nilifungua begi na kukuta suti mbili nzuri mmoja nyeusi na Nyingine rangi ya kijani,
Pamoja na saa ya mkononi na Simu moja Aina ya Sony Erikson nzuri Sana,
Nilitabasamu Kisha nikatoa Ile bahasha ambapo nilikuta Dola za kimarekani kadhaa, pamoja na ujumbe mfupi kwenye kikaratasi..
vaa upendeze dear
_Njoo jumatatu ikulu
Ukifika waonyeshe hiyo saa

Niliiweka kile kimeseji mfukoni Kisha nikaangalia Ile saa Tena,

"Ah watajua wenyewe!"

Nilijisemea nikitoka pale chooni,
Sikutaka kwenda na Ile mizigo nyumbani hivyo kwa dakika kadhaa nikawaza niupeleke wapi ule mzigo....


"Aaah Aida"

Niliwaza haraka kisha nikatoa Simu yangu...


"Ndio Shemeji yake"

Nilisema baada ya simu kupokelewa...

"Haya wewe mzungu leo kunipigia Simu mchana!"

Alisema huku akicheka...


"Ah nakuja aisee Nina hamu Sana na wali Nazi"

Nilisema huku nikimkonyeza boda boda mmoja..

"Hahaha karibu Sana Kama umeotea vile ndio napika hivyoo"
Nilikata Simu na kupanda piki piki kuelekea kwa Aida ilikua Ni Mwendo wa dakika tano tu ....
Aida nilifahamiana nae wakati natafuta kiwanja alikua Ana mgahawa wake mkubwa pale mjini kabla hajabomolewa kupisha barabara,
Wakati natafuta eneo la kujenga nilimtumia na hata nilipoanza ujenzi kimya kimya nilimuachia baadhi ya pesa kulipa mafundi....
Aida hakuwa na mume Ila alikua na watoto wawili, hakuna ajuae baba wa watoto wake isipokuwa Aida mwenyewe, wapo waliosema Raisi mstaafu , wengine walisema sijui jaji Mkuu, ili mradi wabongo tu hawakukosa la kusema,
Nilichompendea Aida ilikua Ni usiri wake,
Nilishafanya dili nyingi Sana na Aida,
Nilifika kwake na kumkuta kweli anakuna Nazi...
"Haha Shemeji yake kumbe kweli kitu Nazi kabisa!"

Nilisema nikiingia ndani,....

"Karibu bosi wangu hivi nimekuona najua leo lazima Nile kuku"

Alisema akinisimama,
"Sasa sikia, sikai ujue nimetoka job Sasa kuna huu mzigo nitaupitia jmos jioni au jumapili asubuhi Sana , naona Soo kwenda nao home si unajua Tena"
Sikia kula huyo huku bhana ngoja niwahi"
Nilisema nikitoa elfu 10 na kumpa Kisha nikarudi kwenye piki piki kurudi kwangu,
****************
Jumapili saa 5 asubuhi nilikua kwenye geti la kwanza ikulu,
Sikuwa na hofu yoyote nilishaingia mtegoni sikua na namna ya kujinasua....

Nilijitambulisha Kama mgeni wa madam,
Na kutokana na suti niliyovaa hata mke wangu angeweza kupishana na Mimi!
Kwa haraka ungeweza kudhani Ni muwekezaji hivi,

Nilipita geti la pili na la tatu hatimaye nikafika geti kuu ..kulikua na mlinzi mmoja tu...
Hakuongea zaidi ya kuninyooshea mkono Kama anayetaka kitu....
Haraka nilivua saa na kumkabidhi..
Aliichukua na kuichomeka mahali Kisha akanionyesha sehemu ya kusimama nikasimama akabonyeza bonyeza Tena kwenye computer yake Kisha akaniruhusu kupita.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom