Habibu Mchange aikacha ACT-wazalendo na kuachana na siasa

Kaenda kozi ya uchakachuaji kisha atajiunga na Lipumba kuwasaidia kudhoofisha upinzani.
 
Njaa ya sasa hv ni Kali sana bora ukalime matikiti kuliko kuishia kupayuka alafu unashuka jukwaani hauna haya hela ya kutuliza kiu.
 
Ni kazi sana jamani kujenga chama kipya. Natamani sana upinzani wangeungana wote na kuwa pamoja kuwa na nguvu ya pamoja.

Watu waweke unafiki pembeni, kubadili badili gia angani,, waache kununuliwa kirahisi na kusaliti chama, wakubali changamoto na mawazo mapya, na waache kungangania madaraka, mawazo mbadala yaongoze siasa za Tanzania zingeenda mbali,,

Lakini pia vyama vya siasa vijue kuwa wapinzani au chama Tawala siyo vita au maadaui, kwamba mwenzako akiwa chama tawala au mpnzani basi nyie ni maadui, sisi wote ni watanzania jamani kwa umoja wetu jamani, tupendane wote hata kama tunapishana katika hoja na mitazamo.

Changamoto ndo zinatujenga na kutupeleka mbele zaidi. Nchi haiwezi kwenda mbele kwa kukubaliana tu na kila kitu. Uwepo wa watu wanaopinga baadhi ya mambo ni kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika yale yanayofanyika, na siyo uhasama.

Tupendane, tuheshimiane ndugu zangu iwe mtu yupo ccm, chadema cuf, act,, etc..

Kwa pamoja Tanzania tutaijenga, kwa chuki Tanzania tutaibomoa.
 
Ni kazi sana jamani kujenga chama kipya. Natamani sana upinzani wangeungana wote na kuwa pamoja kuwa na nguvu ya pamoja.

Watu waweke unafiki pembeni, kubadili badili gia angani,, waache kununuliwa kirahisi na kusaliti chama, wakubali changamoto na mawazo mapya, na waache kungangania madaraka, mawazo mbadala yaongoze siasa za Tanzania zingeenda mbali,,

Lakini pia vyama vya siasa vijue kuwa wapinzani au chama Tawala siyo vita au maadaui, kwamba mwenzako akiwa chama tawala au mpnzani basi nyie ni maadui, sisi wote ni watanzania jamani kwa umoja wetu jamani, tupendane wote hata kama tunapishana katika hoja na mitazamo.

Changamoto ndo zinatujenga na kutupeleka mbele zaidi. Nchi haiwezi kwenda mbele kwa kukubaliana tu na kila kitu. Uwepo wa watu wanaopinga baadhi ya mambo ni kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika yale yanayofanyika, na siyo uhasama.

Tupendane, tuheshimiane ndugu zangu iwe mtu yupo ccm, chadema cuf, act,, etc..

Kwa pamoja Tanzania tutaijenga, kwa chuki Tanzania tutaibomoa.
Ushauri mzuri,ila uko mwishoni sio kwa sizonje huyu..!!
 
Mchange ana matatizo makubwa ya kifamilia kiasi kwamba wanamuona kituko yeye kuendelea na siasa.nayafahamu mengi yanayo muhusu ila kwa sasa ngoja niyaache kwanza.
Zitto kamtumia vya kutosha sana mchange,ilifikia mahali mchange akaamini kabisa kua bila zitto maisha hata yaweza.
 
Mchange ameandamwa na ufukara huku malengo yake yakienda hovyohovyo nilikuwa nakereka naye sana ila juzi nilipopata stori zake nikaishia kumuonea huruma! Nenda Mchange na kumbuka kuwa kuanza upya siyo ujinga. Jijenge kimaisha kwanza!!
 
Kutoka kwa HABIBU MCHANGE.

TAARIFA KWA UMMA
--------------------------------------
YAH:- KUJIVUA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO NA KUTOSHIRIKI SIASA.
----------------------------------------
Mimi Mchange Habibu Mchange, Leo Jumaamosi tarehe 10.12.2016, ninaujuza umma wa Watanzania, Rafiki zangu, ndugu na jamaa.

Kwamba kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikijihusisha na harakati za kisiasa, awali nikiwa mwanachama wa Chadema na baadae ACT WAZALENDO.

Kwamba katika Chama cha ACT WAZALENDO nimepata heshima ya kuwa kiongozi mwandamizi kama katibu wa Mipango na Mikakati na baadae Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika secretarieti ya Chama hicho.

Na Kwamba tangu kujiunga kwangu na Chama hicho nimekuwa mjumbe wa kamati kuu, mjumbe wa Halimashauri kuu na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Chama.

Kwa moyo mkunjufu kabisa, na kwa mapenzi mema na taifa langu.

Ninathibitisha Kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali zinazonitaka nitoe fursa na huduma Sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa.

Kwa mantiki hiyo basi, kuanzia Leo hii, nitaiomba jamii katika yote nitakayofanya inione nimefanya kama Mchange huru asiye mwanachama wa Chama chochote cha siasa.

Ninaomba uamuzi wangu huu uheshimiwe na kamwe nisihusishwe na aina yoyote ya siasa bali utanzania wangu.

Ningeweza kufanya uamuzi wangu huu kimya kimya, lakini kwa hatua niliyoifikia na ili kuweka kumbukumbu sawia ni budi niutoe kwa umma.

Ninafahamu kuwa kuwa mwanachama wa Chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba, lakini nimeamua kuihifadhi haki yangu hiyo kwa sasa Mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.

Ninawatakia kila la heri waliokuwa wanachama wenzangu wa ACT WAZALENDO katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa Chama hicho.

Kujiondoa kwangu kushiriki katika siasa kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya Chama hicho.

Tafadhali ichukueni hii kama chachu ya kuwafanya mfikie malengo mahsusi kwa wakati muafaka bila kurudi nyuma.

Msivunjike moyo, msirumbane, pendaneni,heshimianeni na shikamaneni ili mfikie lengo

Sasa nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na swahiba. zaidi mtanzania mwenzenu. Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa.

Kwa wanachama wa vyama vinginevyo kama CHADEMA, CUF, CCM, ADA TADEA na kadharika, nitaendelea kuwa rafiki mwema kwenu, jirani na ndugu wa kweli kama au pengine zaidi ya ilivyokuwa hapo awali.

Ninawatakia heri wanasiasa wote wa vyama vyote hapa nchini.

Ninawaomba radhi wote niliowahi kuwakosea, kuwa kwaza ama kuwafanya wajisikie vibaya kutokana na matendo yangu, maandishi yangu Misimamo yangu, matamshi yangu ama na mwenendo wangu wa kisiasa kwa kipindi chote nilichokuwa mwanachama wa vyama vya siasa hapa nchini.

Ninaahidi kuendelea kuwa mtanzania Mtiifu mwenye mapenzi mema kwa taifa langu huku nikiwatakia heri wanachama wapenzi na viongozi wa vyama vyote vya siasa.

Itoshe tu kufahamika Kwamba Mimi Habibu Mchange, kwa sasa si mwanachama, mpenzi wala mshabiki wa Chama chochote cha siasa.

Zaidi, Ninawaomba radhi watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine nitakuwa nimewakwaza kutokana na uamuzi wangu huu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wasalaam
Habibu Mchange,
0762178678.
Morogoro Tanzania

Once a traitor; Always a Traitor. Good riddance
 
tangu uanze mfumo wa vyama vingi hapa tz,nimeona mpinzani wa kweli na mwenye msimamo ambaye anaweza kusoma alama za nyakati ni Freeman Mbowe wengine wote waganga njaa tu,minyoo yakianza kuuma utumbo hawawezi stahimil ukame
 
ZiTTo Zuberi Kabwe aliwadanganya vijana wengi wakaikacha CDM wakitegemea iyumbe na akapewa Fedha kuanzisha ACT karibia na Uchaguzi mkuu Maskini wameangukia Pua ACT wazalendo maana maana walipata Mbunge mmoja tu amabe ni yeye Zitto kwa mantiki hiyo Chama kitajiendeshaje kwa ruzuku ya Mbunge mmoja? Kigoma yote imerudi CCM baada ya Zitto na ACT yake kuzigawa kura za upinzani?
My Take to ZZK "Better Late Than Never" Rudi CDM kwani Nyota yako IPO kule ulipolelewa na Am Sure 2020 Ungeng'aa sana km ungekua CDM
 
Back
Top Bottom