Habibu Mchange aikacha ACT-wazalendo na kuachana na siasa

Naanza kuamini maneno ya kada mmoja, "ningepata nafasi ya kumshauri zito kabwe ningemwambia atulie kabisa asihangaike kuhama Chadema kwani kutokana na mafanikio makubwa aliyopata kama kijana, ni kilele cha mafanikio ambacho watu/wanasiasa wengi wanatamani kufikia lakini wameshindwa , hivyo awe makini sana na maamuzi yake ambayo yanaonyesha wazi Kuna msukumo ndani yake wa uroho wa madaraka, atulie katika nafasi yake mafanikio zaidi yanakuja" sasa nimeelewa alimaanisha nini kwa kuwa naona mbele kinachofuata Kuna kila dalili za anguko la ACT, sikuhizi hatuwasikii wakubwa wa Chama hiki kabisa especially Prof. Nimekubali kweli usitukane mamba kabla.......
 
Njaa na uroho wa madaraka ndio unaofanya watu wafikiri kuanzisha vyama vya kisiasa na kijamii eg churches) ili awe mwenyekiti au mchungaji aendelee kuheshimiwa , kipindi kama hiki wapiga dili wamebanwa koo wataachana na siasa sana maana wengi Walikuwa wanaachana na shughuli za kitaaluma eg Dr, pr , mwl , eng naye kukimbilia siasa
 
Hiki chama kilianzishwa kwa malengo ya watu sasa malengo yao yamefika mwisho na waliwatumia wasaliti mwisho Wa usaliti ni kusalitiana haya sasa atabaki zitto Na ubunge wake sasa rasmi chama kitabaki kigoma tu
Wale waliokuwa wanawafadhili wanaogopa rungu la Magufuli lisiwashukie kwa ufisadi wao.

Tutajua 2020 wapinzani wa kweli ni wapi.
 
huwa nawaza kuutangazia umma au jamii maamuzi yako binafsi ni kiashiria kuwa saikolojia ya mtu huyo is disturbed! wazungu wanaita "cry for help" sorry ni mtazamo wangu tu, si umetutangazia umma!
mtu yeyote anaetangaza hivi, maana yake anaweka lable kwenye title yake, anaua soo kwanza,
kumbuka kujenga siasa juu ya dhambi ya usaliti haiwezi kusimama,

kuna hii ebu fungua na kisha soma hapa
___________________________________
RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE
___________________________________
 
Hiki chama kilianzishwa kwa malengo ya watu sasa malengo yao yamefika mwisho na waliwatumia wasaliti mwisho Wa usaliti ni kusalitiana haya sasa atabaki zitto Na ubunge wake sasa rasmi chama kitabaki kigoma tu
siyo " kigoma tu"
bali. " kigoma mjini tu"
 
Kama ambavyo huna haya kufuatana na FISADI LOWASSA, siku akienda ACT-WAZALENDO utakuwa naye huko. Wewe hakuwa CCM bali ulikuwa kwa LOWASSA na hata leo hauko CHADEMA bali kwa LOWASSA, hiyo ndiyo njaa kuu, ya kumlamba mtu viatu
unalia nini?
 
Duh nakumbuka alivyoinanga chadema pale mbagala mkutano wa ACT hadi zito akamwambia apunguze kiherehere alimtukana Lowasa hadi aibu...
Afie mbeleeee huko
 
Wajukuu zangu nyie......eeh
Mimi babu yenu.............eeh
Sina nguvu tena.............eeh
Ya kuua simba...............eeh

Lile nguli la matusi la ACT lililokuwa likitukana viongozi wa vyama upinzani esp Chadema leo limetundika daruga. Limesalimu amri lenyewe na kuachana na siasa.

Wajukuu zangu kama mnakumbuka niliwai kuandika post humu ya kumtaka kijana huyu amuombe radhi Mhe Lowasa kwa matusi yake aliyomtukana pale mbagala zakhem otherwise hatma yake ya kisiasa itakuwa tete. Leo imejidhihirisha sasa kwenye siasa ameaga rasmi hatutakuwa naye tena na tutamiss matusi yake.

Ila mjukuu wangu huyu kwa matusi tu namvulia kofia alikuwa akikunanga lazima uombe poo.
 
Dah jinsi alivyokuwa bingwa wa mitusi bora atulie tu. Labda itamsaidia akirudi atakuwa na busara kidogo.
 
Wasaliti wote watajipukutisha wenywewe. Wazalendo wakweli wanaimarisha upinzani na si kuumega. Sisi CCM tunazidi kupaa tu. Kutafunana kwenu ni nafuu kwetu. Wasalimie Morogoro. Kibaha umehama? Na bado?
 
Kwa mujibu ya magazeti ya leo kuna taarifa aliyekuwa kada mkubwa wa CHADEMA aliyehamia ACT amekiacha chama hicho kichanga.Haijajulikana kama amejiunga na chama gani, huyu amekuwa kada wa pili kukihama chama hiki baada ya Machali.Mwenye taarifa zaidi atujuze .
 
Kwa mujibu ya magazeti ya leo kuna taarifa aliyekuwa kada mkubwa wa CHADEMA aliyehamia ACT amekiacha chama hicho kichanga.Haijajulikana kama amejiunga na chama gani, huyu amekuwa kada wa pili kukihama chama hiki baada ya Machali.Mwenye taarifa zaidi atujuze .
Ha ha ha alienda kwenye chama cha msimu!
 
Back
Top Bottom