Gration Mukoba au Wilfred Lwakatare?

Kuna majimbo mawili mkoani Kagera la BK-mjini na BK vijijini ambayo hayastaili kuwa chini ya CCM lakini kwakuwa wagombea wa CCM wanatumia pesa na vitisho kwa wananchi mfano Kagasheki na Jason Rweikiza inakuwa ngumu kuwatoa.
Wapiga kula wananjaa sanaa anayetoa pesa ndo anapata kula.
 
ni nini kinamwangusha uyu bwana sisi vijana wake uku tumuimarishe kwa kumsaidia kutatua mapungufu yake
Mkuu uchaguzi wa mwaka jana unajua mpaka wakati wa kupiga kura watu wa kagasheki na kagasheki mwenyewe walishapita nyumba kwa nyumba mara ngapi? Walikuwa hawachoki kuja mlango kwako kukubembeleza uwape kura! Wakati kagasheki ameshazungukia nyumba kwa nyumba zaidi ya mara 2 Lwakatare haonekani! Anategemea mikutano ya hadhara! Nakumbuka ilifika mahali wazee wa kihaya wakawa wanasema urais Slaa lakini ubunge ni kagasheki! Binafsi nilijaribu kuwa challenge baadhi ya wazee wakaniambia Kagasheki na watu wake tunawaona majumbani mwetu lakini huyo Lwakatare haonekani!! Watu wa Lwakatare walianza kupita nyumba kwa nyumba dk za lala salama Kagasheki ameshafunga kazi!! Lwakatare hana watu wazuri wa kusimamia kampeni zake na hilo daima litam cost,anapaswa kujipanga sana kuanzia kwa kampeni meneja na timu nzima! lwakatare anapendwa sana anapaswa kuwa active kule hata kipindi hiki sio mpaka uchaguzi unapokaribia maana uzuri bukoba una issue kibao na watu wanamwamko mkubwa wa mabadiliko tatizo Chadema haina watu makini kule kumobilize watu!
 
Bkb ni wanamadiliko si bongolala cku zote. cdm kupoteza majimbo ya bkb ni udhaifu wao wa kujiorganize tu na kuwa watu wazuri wanaofatilia mbinu zote za upambanaji.
 
Ni kweli Lwakatare ni mpiganaji asiyechoka, namkumbuka vizur wakati nikiwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya CUF wilaya ya kinondoni yeye akiwa naibu katibu mkuu bara, alivyojitolea kwa hali na mali kupigania maslahi ya wanyonge, hata ndani ya CDM amedhihirisha alivyo kamanda hodari, wanabukoba wasirudie tena kosa, Mkoba yupo kwa ajili ya kutafuta shilingi za kuweka kwenye mkoba wake
 
ni nini kinamwangusha uyu bwana sisi vijana wake uku tumuimarishe kwa kumsaidia kutatua mapungufu yake

CUF...hii ndiyo factor kubwa ya lwakatare kushindwa mwaka jana. Kagasheki aliingia mkataba na CUF kuhakikisha anawapigia kampeni upande wa madiwani na yeye watampa kura zote za ubunge japo za uraisi hawaku-mpromise na ndiyo maana BUKOBA pamoja na kutoa mbunge wa CCM, lakini JK alibwagwa na Dk. Slaa .

That is what happened..keep in mind kwamba kabla ya Lwakatare kwenda CDM, CUF ilikuwa na nguvu nyingi pale...so ile division ndio ilimnyima kura Lwakatare, otherwise angeshinda kwani kama unakumbuka mwaka 2005 alimuacha kwa kura chache sana hadi ikahisiwa kuwa kagasheki ameiba kura. Ila mwaka jana alishinda ki-ulaini sana na kwa margin nzuri tu ya kura.
 
hivi mkuu lile sanamu la mayunga bado lipo hapo bukoba?wamerikarabati?wale nyuki wa kwenye lile sanamu ni noma.walitushambulia siku ya kampeni ya rwakatare.tulitoka kumfanyia kampeni katoma tulipofika buyekela polisi wakatuzuia kuingia mjini pale stand kwa maandamano sisi tukaforce kipindi hicho tukiwa cuf.walitutawanya kwa mabomu ya machozi tukakimbilia pale mayunga tukakuta nyuki wamechachamaa.ilikuwa ni noumer stasahau.mia

Sasa hivi umehamia Chadema nini ?
 
hivi mkuu lile sanamu la mayunga bado lipo hapo bukoba?wamerikarabati?wale nyuki wa kwenye lile sanamu ni noma.walitushambulia siku ya kampeni ya rwakatare.tulitoka kumfanyia kampeni katoma tulipofika buyekela polisi wakatuzuia kuingia mjini pale stand kwa maandamano sisi tukaforce kipindi hicho tukiwa cuf.walitutawanya kwa mabomu ya machozi tukakimbilia pale mayunga tukakuta nyuki wamechachamaa.ilikuwa ni noumer stasahau.mia

sanamu lipo ila limeboka kichwa cha bunduki,umenikumbusha police walikuja kuzuia ghasia kashai bila mabomu ya machozi jamaa wakaanza kuimba 'tunataka bomu..tunaka bomu..tunataka bomu..basi ikabidi police wayafuate mabomu tena mengi ya kutosha.tukatupiwa ya
kumwaga,nakumbuka moja lilidondoka dirishani hom usiku wa manane yaan balaa tupu..
 
Back
Top Bottom