Graduate, mshahara chini ya milioni moja usifanye kazi

we si ndo unasemaga upo kwa CAG?
470,000tsh x12month=5,640,000 kwa mwaka
5,640,000x3 yrs= Tsh16,920,000

sasa hiv una gar 2=20,000,000
Nyumba mbili (MODERN) assume @Tsh 50,000,000=100,000,000 tsh
viwanja 3@ 4000,000 =12,000,000 tshs
madogo 3 shule @ 1,500,000=4,500,00/yrx3=13,500,000

Total Matumizi 145,500,000 wakati kipato halali ni 16,920,000 tu

NB..hii haihusu
1.michepuko
2.chakula nyumban
3.chakula kazin
4.mafuta kwenye gar
5.service za kar
6.road lecensi ya magay 2
7.bill za umeme na maji
8.mavazi
9.michango kanisan/msikitin kama ni muumun
10. pombe
11. kusaidia ndugu na wazazi
12.nk

aisee hebu tuambie manake mhhhhhhhh
hii "inji" ina watu wake.
Mkuu hii JF ogopa kama ukoma!!
 
Vijana hawajui kuwa kupa uzoefu ni bora zaidi ya kupata mshahara mkubwa mwanzoni. Ukipata uzoefu wa kazi unauhakika wa kuitwa kufanya interview sehemu mbalimbali unazoomba na kuongeza wigo wa kuajiriwa. Lakini ukisubili upate kazi yenye mshahara mkubwa utasubili sana bila hata kuitwa kwenye interview. Interviews zina vigezo vitatu muhimu 1. uhusiano na nafasi iliyotangazwa (relevance) 2: Ufaulu wako na 3: uzoefu. Ukiwa na hivyo vitatu uko mbele ya wenzako. Ndio kuna bahati lakini sio kila mtu ana bahati ndio maana ikaitwa bahati. Kuna watu tulianza na kazi bila malipo lakini baada ya kauzoefu ka miezi 6 tu tukaanza hata kuringa kwenda kwenye interview zingine maana zilikua ama nyingi au tayari tumepata kazi ya kuwesha kuishi na kubadili mboga. Kwa dunia ya sasa kuitwa kwenye interview ni hatua ya juu kabisa kupata kazi. Kama unaomba kazi na hata interview huitwi utamaliza viatu kuzunguka. Muda mwingine inabidi uwe na cha kuja kuwahadithia wanao. Stori nzuri kwa wanao ni jinsi ulivyosota kufika pale wanakapokuona. Tusipende kuanzia kwenye matawi. Unataka mshahara mkubwa, umejiandaeje kuitwa kwenye kazi au interview ya watu watano tu kati ya waombaji elfu kumi?
 
"Nkimaliza zangu Chuo ntaaplai zangu kazi Voda, ntalipwa milioni 3.5/mwezi, ntajibana zangu kila mwezi natumia laki5 tu, izo 3m naifaZi benki, baada ya miezi mi3 nanunua gari la 9m/=, nkishakua na gari basi 3m ya mwezi unaofatia napanga nyumba ya laki mbili na amsini kwa mwezi, 3m inayofatia nanunua fenicha, kwanza adi apo ntakuwa nshatimiza miezi 6 kazini, adi apo naruhusiwa kukopa, nakopa zangu 10m/= afu natafuta kiwanja cha 6m tu, si ntakuwa nakatwa 1m/= za mkopo kila mwezi, izo 4m nafungua kabishara, bado ntakuwa nabakia na 2m/= /mwezi baada ya makato ya mkopo, izo 2m zinatosha kila mwezi kupandisha tofali, Mungu jaalia kabla Jakaya ajatoka madaLakani, nna mjengo, gari na kijibiashara changu pale Mwenge.
.
Mliosoma vyuo naamini mmewahi kuwa na muono huo mkiwa chuoni, huu muono unapangika fresh sana, huitaji hata Kalkyuleta, hii kwa kizungu inaitwa "Theory", wahisani wetu Watu wa Marekani wanaitaga "PLAN A". Maliza chuo sasa uje mtaani, utakutana na kitu kwa kizungu inaitwa "Implimentesheni", ndo neno "PLAN B" linapokujaga, plan B kuielezea ni ngumu labda nitunge sentensi fupi huyo kijana apo juu atayoituma akitoka zake Job, of kozi mwezi wake wa 10 job: "Mwana shwari, leo nmetoka mapema mwana ila sina hata ela ya Bajaj, mwana unawezakuwa na efamsini ya karibu Mkuu nmalizie ngwe, ntakurudishia mwisho wa mwezi mshahara ukitoka, sijasteblaizi bado mwana!"
umeua mkuu. Chuoni raha sana, plan A acha tu kumbe wengi wanakuwaga hivi.

Tuwasameheni tu na wao ndo wakati wao wa kutengeneza plan A. Wakija kitaa watakumbana na plan B yenyewe ni automatic haitengenezwagi unajikuta tu unayo una implement
 
Nimesoma uzi na comments zote ,
Vijana wabadilike wasidhani mtaani ni nchi ya asili na maziwa tu

Nakumbuka jamaa angu na mawazo yake ya kununua fortuner, TV inch 55
Dah nakumbuka sana, nakumbuka sana hyo moment na jamma angu


Chuo cha kweli ni Street University .


Aise mambo ni magumu sana. Hatuwatishi ila jipangeni kwa mtaa, tunawakaribisha.
 
Tatizo vijana wanafanya kusoma kwa assumption,

Mi nimebahatika kipindi fulani kufanya kazi taasisi Moja ya fedha ambapo watumishi mbali mbali walipitisha mshahara pale, nilipokuwa nachungulia kiasi wanachopata wengine niliwazid two times niliamini kwamba kumbe usijari unapata kiasi gani , we angalia hicho kiasi unakutumiaje,

Kwanza kupata kazi ukiwa huna kazi ni vigumu,.mpaka wengine huomba kujitolea kupata experience, Sembuse upewe laki 8
 
Mdogo wangu, kwanza pole kwa hiyo shida unapata, na pili pole kwa waliochangia uzi wako vibaya nimesikitika kuona wengine badala ya kukupa ushauri ndo kwanza wanakejili sana. ila hilo ni jambo la kawaida katika jamvi hili.

1.Mchango wangu ni kwamba, wazo ulilo nalo la kujiajiri ni zuli sana. biashara yoyote kabla ya mtaji inaitaji kuwepo kwa wazo. sasa wewe kwa hili tihali umepiga hatua.
2.Hatua ya pili kwa kuwa umewaza kujiajiri, anza kufikiria ni biashara gan ungependa kuifanya, then angalia kama una kamtaji kabiashara hiyo au la.
3.Kama utagundua bado mazingira ya kuacha kazi hayaruhusu mfano hauna hela ya kuanzia, usiache kazi ghafla, vumilia kwanza, tunza hela kidogo kidogo.pia wazo la aina ya biashara unayo taka kuifanya, unaweza wakati unavumilia unaweza kuwaona wajasiliamali walio kwisha ifanya na ukajifunza zaidi.

*Ki ukweli msharaha wa lak 7 ni mwingi ila kwa hali ya maisha ya sasa ni mdogo mno hata kufika million 1 bado ni mdogo sana ndugu yangu. usione wengine wanashabikia tu nahisi hawajaingia katika maisha ya kuwa na majukum! mimi nilfanya kazi sana baada ya kuona mambo hayaendi ndipo nilipata wazo kama lako. na siku nina hacha kazi wengi walinipa siku za matazamio kuona nitakavyo shindwa maisha. Namshukuru Mungu hakuniacha na ninafurahia sana kwamba baadhi ya walio niacheka Leo hii nime waajiri mimi!

Angalia mchanganuo huu. Mtu anaye lipwa msharaha wa million moja, lazima atakatwa kodi ya kichwa isiyo pungua 200,000! unaweza kupata uhakika TRA watakwambia. ukisha katwa lak2 zitabaki lak 8,makato ya mafao ya uzeeni na mengine kama bina ya afya na ya vyama vya wafanyakazi, vyote havipungui lak 150,000!. Baada ya apo utabakia na lak 650,000. labda tuseme ndo take home. ukipanga nyumba ndogo sana yaani vyumba 2 na sebur, lazi kodi isipungu 100,000 kwa mwezi. zitabaki 550,000. Nauli kila siku kwenda na kurudi kazini magar mawili kwa mwezi si chini ya 50,000. zitabaki 500,000. chakula chako kazini cha bei ya mama lishe 1,500 had 2,000 kwa mwezi pia haitapungua 50,000. zitabaki 450,000. Bili ya maji na umeme wa luku, kwa mwezi hasa luku haitapungua 30,000. zitabaki 420,000
kwa kuwa unafamilia mke/mme na watoto, kwa siku gharama ya chini kabisha haitapungua elf10 mchana na join, hivyo 10,000 x 30 = 300,000. zitabaki 120,000. kama una TV utatakiwa kulipia king'amuzi cha bei ya chini 10,000. zitabaki 110,000. Gunia la mkaa ndogo kwa sasa si chini ya sh 12,000,ges si chini ya tshs 40,000 kwa mwezi,hivyo mkaa au ges kwa bei ya chini si chini ya 30,000 kwa mwezi. zitabaki 70,000. vocha ya cm yako kwa mwezi kama umejibana sana si chini ya 10,000 kwa mwezi. zitabaki 60,000. watoto wanaitaji nauli kwenda shule na kurudi, kwa mwezi si chini ya shs 20,000. zitabaki 40,000. kama wewe ni mkiristo hiyo hela ya mshahara wako unatakiwa uitolee fungu la kumi kanisani ambalo halitapungua 80,000. zitabakia 0 na kudaiwa 40,000!!!

MAENDELEO
1.Mdogo wangu ebu jiulize kwa mtaji huu wewe ni lini utanunua kiwanja chako kwa bei hata ya chini ya miloni 2? badala yake utaishia kuomba mkopo benk kwa dhamana ya ajira na hivyo utakuwa unakatwa kila mwezi ili kulipia mkopo wa kiwanja.
2.Je katika hali hii utakuwa na ndoto ya kununua ka gari hata kale kanakoitwa stalet? sidhani
3. Je, utakuwa na ndoto ya watoto wako wapate Elimu bora hasa kama ilivyo kwa sasa elimu iko juu?
4.Je kama wewe unatokea mikoani, utakuwa na wazo la kwenda kuona wazee na mkeo/pamoja wakati hela hakuna.
katika mchanganuo wangu sijaweka emagency mfano mke au watoto wameumwa , kaja mgen nyumbani n.k
**NDUGU YANGU WAZO LAKO NI ZURI SANA SONGA MBELE UTAPIGA HATUA TU NA MUNGU AKUSAIDIE. AMINA
Uhalisia wa maisha ni tofauti sana na watu wawazavyo
 
Leo nilikuwa nimeongozana na vijana flani kutokea wizara ya elimu kama unaenda chuo cha usimamizi wa fedha/makumbusho ya taifa.

Walikua mbele yangu kidogo ila nilikuwa nasikia mazungumzo yao (inaonyesha ni wanafunzi wa IFM). Mwenzao ukawa anawambia wenzake kua yeye kama akigraduate mshahara anaotaka ni kuanzia milioni moja chini ya hapo hafanyi kazi. Tena akawa anashangaa kusikia eti graduate analipwa laki 6.

Akasema vinginevyo ataenda jeshini maana huko graduate analipwa milioni 1.5. Wenzake pia wakawa wanamuunga mkono bila hiyo hela bora waache kazi.

Inaonekana vijana wakiwa mashuleni wanadanganyana sana, wanapeana matumaini makubwa ambapo wakija mtaani wakakuta hali ni tofauti wanaishia kuwa wezi na uuzaji wa dawa za kulevya. Malizeni shule muje mkutane na mshahara wa laki 2 na digrii zenu ndio mtakoma.

Acheni kudanganyana, mtaani hakuko hivyo.
😂 😂 😂 😂 😂
 
we si ndo unasemaga upo kwa CAG?
470,000tsh x12month=5,640,000 kwa mwaka
5,640,000x3 yrs= Tsh16,920,000

sasa hiv una gar 2=20,000,000
Nyumba mbili (MODERN) assume @Tsh 50,000,000=100,000,000 tsh
viwanja 3@ 4000,000 =12,000,000 tshs
madogo 3 shule @ 1,500,000=4,500,00/yrx3=13,500,000

Total Matumizi 145,500,000 wakati kipato halali ni 16,920,000 tu

NB..hii haihusu
1.michepuko
2.chakula nyumban
3.chakula kazin
4.mafuta kwenye gar
5.service za kar
6.road lecensi ya magay 2
7.bill za umeme na maji
8.mavazi
9.michango kanisan/msikitin kama ni muumun
10. pombe
11. kusaidia ndugu na wazazi
12.nk

aisee hebu tuambie manake mhhhhhhhh
hii "inji" ina watu wake.
😂 😂 😂 😂 aiseee
 
watu waache kukatisha tamaa wenzao,na maisha haya nakwambia hayana fomula,nani anajua kama Mwigulu angekuwa hivi.kikubwa ni kukaza tu na malengo ya mbele.Mimi nina 3yrs kazini.net salary kabla ya july ilikuwa 470,000 plus posho posho za hapa na pale na network ya Makamanda walionizidi uwezo,within 2yrs a hv 2 modern houses,2 cars worth 20m,3 plots na madogo wa3 shule 1.5m each!ujasiliamali kama kawa.kazi ni msingi hata wa kuiacha na kufanya ishu zingine.sasa kazi hii imenijengea msingi,after 3yrs ntaiacha niingie kwny business ambayo itakuwa imezaliwa na kazi
mkuu ndoto ya kuendeleza business ilifanikiwa?
 
Wadau eeh.. najua wengi wetu humu ni waajiriwa ama sekta ya umma ama binafsi. Mi ni mmoja wapo wa hao waajiriwa na sijafikisha mwaka mmoja kwenye ajira yangu ila kwa kweli kwa hali ilivo sasa naona nimeshaichukia hii kazi kwa sababu zifuatazo
1) Huu mshahara wa laki saba saba unanchosha akili hasa ukizingatia i spent roughly 15 hours kwa ajili ya hii kazi, kuanzia kuamka asubuhi mpaka kulala jioni yaani nishida. Na nikichek actual savings per day its about 14000 TZS nikifikiria hii kitu kila siku napata headache. Yaani wadau ingawa mi ndo kwanza mbichi kwenye soko la ajira na mdogo pia kwa umri ila ki ukweli sasa napanga mipango ya kujiajiri maana naona hii kazi sitamaliza mwaka.

Ila nafurahia hii hali maana ndo inanipa majibu sahihi ya nini maana ya kujiajiri. Mwanzoni nlikua nachukulia mzaha kujiajiri ila sasa nimeona kijiajiri ni kitu gani haswa.

Najua baadhi ya members watanikejeli ila kwa kweli kama mtu una akili ya kuwa na maendeleo makubwa kwa maana ya makubwa, hizi ajira za laki sita, saba ,nane, tisa.. ni kupoteza muda haki ya mama.

Hii ni kwa wale wenye maono kama ya kwangu, ila kwa wengine ambao washaridhika na hizo laki sita saba naomba usipite kwenye huu uzi maana mi sitaki kumfrustrate mtu yeyote kwenye huu ujana ambao ni maji ya moto ila tukumbuke tu "FAINALI UZEENI" na kama vijana wa kileo tutazipa kumbato hizi ajira za laki sita saba haki ya mama 'FAINALI YA UZEENI' itakua ligi ya BUNDESLIGA badala ya mechi moja ya mchangani
💯 📌📌📌
 
Walikua watajua..wengine majina ya degree yanawachanganya..wakina kukutana na kishahara ya laki3 ndo akili itafanya kazi
 
Leo nilikuwa nimeongozana na vijana flani kutokea wizara ya elimu kama unaenda chuo cha usimamizi wa fedha/makumbusho ya taifa.

Walikua mbele yangu kidogo ila nilikuwa nasikia mazungumzo yao (inaonyesha ni wanafunzi wa IFM). Mwenzao ukawa anawambia wenzake kua yeye kama akigraduate mshahara anaotaka ni kuanzia milioni moja chini ya hapo hafanyi kazi. Tena akawa anashangaa kusikia eti graduate analipwa laki 6.

Akasema vinginevyo ataenda jeshini maana huko graduate analipwa milioni 1.5. Wenzake pia wakawa wanamuunga mkono bila hiyo hela bora waache kazi.

Inaonekana vijana wakiwa mashuleni wanadanganyana sana, wanapeana matumaini makubwa ambapo wakija mtaani wakakuta hali ni tofauti wanaishia kuwa wezi na uuzaji wa dawa za kulevya. Malizeni shule muje mkutane na mshahara wa laki 2 na digrii zenu ndio mtakoma.

Acheni kudanganyana, mtaani hakuko hivyo.
Ndio ndio 🤣
 
Back
Top Bottom