Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Kama Tanzania ingekuwa kama Arusha basi ,Nchi ingekuwa mbali

Martin! Kuna miji yenye upinzani mkali zaidi ya Arusha. Mfano ni Musoma mjini. CCM ina viti 2, CUF 2 na CDM 9 wakati Arusha CCM 9, TLP 1 na CDM 9. Arusha pia wapo fit lakini nadhani makali ya upinzani sasa ni nchi nzima
 
Kwanza kabisa Kamanda Lema nakushukuru kwa maneno mazito uliyoyaandika hapo juu, kiukweli najua unapitia wakati mgumu sana katika maisha yako ya ubunge hapo Arusha mjini lakini umeendelea kujipa moyo katika kuwapigania wanyonge lakini kubwa kabisa umekuwa ukimtanguliza na kumtumainia mungu kama nguzo yako katika mapambano haya hatari kabisa. Naomba ninukuu baadhi ya maneno yako; " kazi ya siasa tunayoifanya ni kazi ya hatari sana lakini tumeamua kujitolea maisha yetu, ikumbukwe kuwa hata sisi tunapenda kufurahia maisha yetu na hata kupata fursa ya kuwaona wajukuu zetu lakini tumekuwa tukisema ukweli kiasi cha hata kumtuhumu amiri jeshi mkuu kuwa ni mdini kitu ambacho sio rahisi kufanya hivyo kama huna ushahidi wa kutosha >>> nasisitiza ushahidi wangu sitapeleka tena uchochoroni"
Aidha uone mungu alivyo wa jabu kwa kukupa mke ambaye anakushauri na kukutia moyo katika mambo magumu yanayokupata, kamanda unatakiwa kumtunza sana Neema Lema maana huyo mama ni msaada mkubwa kwako. Unapomuongelea mama Lema kwa uchache nakumbuka jinsi makachero walivyovamia kwako usiku wa manane pamoja na mambo mengine wakitaka kuichukua simu yako iliyokuwa na ushahidi msg uliyotumiwa wa Mhe. RC ili wafute msg hiyo haraka mama akajiongeza na kuichimbia kwenye pampers ya mtoto wako mchanga!! Polisi walipiga upekuzi nyumba nzima wasijue simu iko wapi!! >>> hao ndio wanawake sharp na wanaojiongeza, ukiwa mke wa kamanda na wewe lazima unakuwa na uasili wa ukamanda.
Mwisho nakubaliana na kauli yako kuwa: "Giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ ............. Kweli viongozi wa Chadema wanapitia kipindi kigumu lakini mungu atawaepusha na mipango yote mibaya na dharimu dhidi yenu kwa sababu nchi yetu hii msema ukweli ndio anayeonekana mbaya.

Msikatishwe tamaa makamanda tutaishi hata kwa mkate na maji lakini safari yetu ya kuitafuta 2015 ifikie.
 
Nalazimika kubadilisha Signature yangu niliyoipenda kuanzia saa hii kwa heshima yako G.Lema,Neema Lema
na wapambanaji wa Arusha wote,Nasema "Mungu awabariki sana"
 
Asante sana mpiganaji wewe kweli ni jembe hapo Arusha na umeonyesha upendo kwa wapiga kura wako,

Ila bana hujaweka hata mstari mmoja wa kutushukuru na sie tuliokuwa tunapiga debe tukitokea huku Nyakahanga, Geita, Buseresere, Manyovu, Godegode, etc?

Mwisho nakuomba 2015 kaweke kambi kwa kajitu fulani kamo Bungeni ni kafupi hivi kanakuwaga na maneno ya nyodo sana kakikaa pale mbele ya Bunge na nafikiri kanatokea Mpwapwa hivi

Lema Mungu akubariki sana na akupe pia maisha marefu wewe na familia yako. Kwa jina la Mungu Baba, Bwana Yesu na Roho Mtakatifu akulinde sawa na maneno yake kwamba akugusaye wewe na familia yako awe anaigusa mboni ya jicho la Mungu, Mungu amshugulikie mwenyewe.

 
1002316_555828297812696_2004089766_n.jpg
hapa tunazungumzia a town mkuu co mtwara
 
...It only seems impossible until its done - So said Kamaradi Madiba.

Arusha you showed its Possible, its done. Viva Chadema.
 
Nimejifunza kitu kwa wake wa makamanda wa CDM,kile nilikiona kwa Joyce Kiria,nakiona pia
kwa Neema Lema. You are my role model"
 
#LEMA
Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Ujumbe Murua, asante sana
 
Maneno mazito na ya
busara.Pia Spirit ya Neema Lema ni ya kuigwa na wenzi wa wanasiasa
wapenda mabadiliko.

Mkuu Ben Saanane, hii inatuthihirishia ule usemi wa kiingereza unaosema "Behind any successful man there is woman" so Lema is not different. God bless you all.
 
Last edited by a moderator:
Lema, you real inspired me to become strong and self determined. I real appreciate your hard work your such an amazing leader that tanzania should fill proud off, keep going don't hesitate despite all setbacks, cause our liberty is on your figure tips big up may god bless you ubundantly
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Asante sana GJL; ni kweli tumshukuru Mungu kwaa kila jambo, napendekeza kwamba tofauti na mkutano wa kisiasa wa kuwashukuru wanawa Arusha kwa kusimama imara kuushinda udhalimu wa CCM na serikali yake kama uliouelezea vizuri sana katika waraka wako; nakuomba taratibu zifanywe ili wana wa Arusha tufanye ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa pamoja; katika tarehe na siku tofauti na mkutano wa kisiasa; tuwakaribishe ndugu zetu wote wapenda amani na mabadiliko na maisha bora kwa watanzania wote bila kujali itikadi; dini wala kabila; ili tusali pamoja na kumshukuru Mungu kwa wema na neema zake kama alivyodhihirisha katika uchaguzi wa madiwani juzi jumapili.

NAWASILISHA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom