"Giving money abroad to Africa - It has to stop"

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
I am sick of the adverts and appeals to give money to Africa. Over the last thirty years, the money given out would probably rival a middle income country, and you would think by now they'd have found solutions to their problems.

Whilst I know it's a shame, it's time to close the bank. Nothing is happening at all in those countries, and any progress that has happened and has been through small investements.

We're struggling in the UK at the moment. Children are going hungry here. What's happening abroad is not. Charity begins at home.

Wadau hii nimeikuta kwenye forum ya Uk wanajadiliana......

Wachangiaji wengi wamelaani pesa zao zinapelekwa Africa...
Na Waafrica hawaheshimu haki za msingi za Binaadamu
 
Wanataka 'haki' gani za kibinadamu tena hawa wazungu?? Kama kuwa MASHOGA na kupumuliwa visogoni tumeshakubali, wanataka tufanyeje tena???
 
Ni kweli kabisa. Haki za binadamu kwa Tanzania hazipo.....

Polices%20In%20Iringa%20beats%20Daudi%20Mangosi%20before%20his%20death.jpg
Slaawife.jpg


Kama huna macho basi wewe CCM imekupa ukipofu.....
 
Kuna kaukweli kwa mbali, a lot of money to Africa inamilikiwa na watu wachache sana!
 
Mimi nadhani wako right! tena ikibidi wahisani wote wakatishe kabisa hiyo misaada, sasa nchi kama Tanzania imeanza kupokea misaada toka kwa wahisani miaka nenda rudi sasa, lakini mafanikio yako wapi?!, watu ndiyo wanazidi kunywa maji machafu yasiyo salama kutoka kwenye vidimbwi. hebu fikiria listi hii. UK, EU; UN, World Bank + Wajapan na Wachina wote hao wanatoa misaada kwa Nchi za kiafrika. baada ya kumaliza hapo, jumlisha hiyo misaada na Kodi inazopata SJMTZ( Misaada + Kodi ), yaani unaweza kuchanganyikiwa. Fedha zinatoka USWISS kisha zinarudi tena huko huko USWISS.
 
Wanantoa misaada frika ambako viongozi wa nchi na extended families zao wanaishi kama mbinguni kuwazidi wale wa Ulaya zaidi ya mara mia!!
 
Wameshatuchoka! Enough is enough, kwanza viongozi wengi wa Afrika wanapokea misaada kutoka G8 na kuwaambia wananchi tumepewa msaada let say 5m $, zinasomwa tu kwenye media na wanaendelea na umaskini wao, while ule msaada unaenda ktk a/c zao USWISI.
 
Kama ingekuwa ni kupiga kura ningekuwa wa kwanza kusupport kutopewa misaada,
 
misaada imezidi,nashauri misaada tusipewe ili tuwe na akili ya kujenga siyo kila bajet kutegemea wahisani ndio maana wanatupa masharti magumu,na inakuwa rahis kuingia mkenge kwenye kusaini nao mikataba,nashauri wasitupe misaada
 
Wanantoa misaada frika ambako viongozi wa nchi na extended families zao wanaishi kama mbinguni kuwazidi wale wa Ulaya zaidi ya mara mia!!

Kweli kabisa Kichuguu, ubinafsi ndio unaotutafuna. viongozi wa Afrika ni wabinafsi sana, wanafikiria tu maisha yao na watoto zao. majumba na magari ya kifahali ili mradi tu waonekane miungu mtu. kunatakiwa kuanzishwe kampeni ya kukataa hii misaada especial ''From the People of America'', sababu ndio iliyotufanya tuwe na hali hii ya umaskini kwa sera ya utegemezi, kwani sisi tunashindwa kuwalisha hao Wamarekani??!!, uwezo tunao, Tanzania ni moja kati ya nchi tajiri sana duniani, kuna all kind of resources + manpower, misaada haitatusaidia zaidi ya kutuangamiza. Misaada ndio functional material ya Neo-colonialism, inakufanya usiifikirie kesho, inakufanya usiumize kichwa , inakufanya ubweteke! Kiufupi ni kwamba tu misaada hii inaua Generation ya kesho, tunaandaa generation ambayo inategemea kuishi kupitia kwa wahisani, generation isiyopenda kufikiria, generation ya Wavivu. Aid to Tanzania must be stopped!
 
'Misaada' inayoletwa ni sehemu ndogo tu ya kiasi ambacho kimetolewa hapo awali. Wengi katika nchi zinazotoa hiyo misaada wanafaidi sana kutokana na misaada hiyo na hawataacha kutuma misaada kwa sababu ,kwa kufanya hivyo, na wao watakosa. Hao wanaolalamikia misaada ni wananchi wa kawaida ambao hawamo katika mfumo huo na hawajui jinsi unavyofanya kazi.
 
Wadau hii nimeikuta kwenye forum ya Uk wanajadiliana......

Wachangiaji wengi wamelaani pesa zao zinapelekwa Africa...
Na Waafrica hawaheshimu haki za msingi za Binaadamu

Hurricane Katrina na hii sandy wamarekani wako slow kusaidia.ngojea itokee Kama ile ya Haiti maana hiyo misaada wamarekani ilivyopelekwa.michelle Obama John Edward bill Clinton yaani watu walishuka Huko.i guess wanapenda kusifiwa nje ya nchi .mimi naona UN inakula pesa Za waafrica zaidi
 
nyie mnaita misaada bt ni misaada kweli? nyie mnaona afrika ni bara maskini so inabidi lisaidiwe bt mnasahau hao hao wazungu wanaotupa misaada makampuni yao yote yako huku kuanzia oil, gas and other minerals, wanajua wananchi wao wanakuja huku for holidays kila mwaka...sasa wasipotoa misaada it could affect hata na watu wao...clinton ana biashara africa, george bush ana biashara africa, tony blair ana biashara africa...nyie mnafikiri mnasaidiwa tu hivi hivi? hao wanaoandika hiz articles ni wale wazungu mbumbumbu hawajui kua viongozi wao wanatoa misaada kwa sbabu na wao wanapata kitu in return sio bure bure
 
Hili neno msaada sidhanii kweli kama linatekeleza msaada isipokuwa wanatoa chao na sisi tunatoa chetu.Kwanini wasijitolee kutoa elimu ambao ni msaada mkubwa tunaohitaji ili kukuza uchumi wetu bila ya msaada.Au kwanini wasitujengee barabara na miundo mbinu mingine ambayo ni msaada mkubwa tunayohitajia.Wanajua Tanzania kuna shida ya umeme kwahiyo wanafurahia kuja kuwekeza.Wazungu ni watu wajanja sana wanatuchukulisha pesa kutoka IMF halafu halafu tunabakia na deni lisilo isha huku linaongezeka kwa kulipa riba kubwa hamuoni kama wanafaidika kutoka Africa.Africa ni kama reserve ya uchumi wao wakiishiwa utaona jinsi wanavotoa hiyo misaada.Bara la ulaya hivi sasa lipo hoi kiuchumi.Wanachi hawana kazi mpaka wengine wanajiua.Coment kama hizo nimeziona nyingi sana tena zingine ni za kibaguzi kabisa kuhusu nchi za kiafrica.
 
Wasilalamike kamwe! walitutoa porini kwanini? tulikuwa hatujui hela, wala hatuvai nguo, tulikuwa tunakula nyama na kushushia na maziwa. Wabebe mzigo wao hadi hapo tutakapo waambia tunaweza maisha waliotufundisha. Tena wasitukumbushie kwamba walituchukuwa watumwa. blali fulus!
 
Wasilalamike kamwe! walitutoa porini kwanini? tulikuwa hatujui hela, wala hatuvai nguo, tulikuwa tunakula nyama na kushushia na maziwa. Wabebe mzigo wao hadi hapo tutakapo waambia tunaweza maisha waliotufundisha. Tena wasitukumbushie kwamba walituchukuwa watumwa. blali fulus!

Umenena jambo zito mwaya...
 
Back
Top Bottom