Naomba kumuuliza Mh. Waziri Mkuu aibu hii ya shule zetu za msingi kukosa madawati na watoto wetu kusoma wakiwa wamekaa chini itakwisha lini?
Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 01/02/2010 ukurasa wa 8 kuna habari isemayo "UKEREWE YAHITAJI MIL. 713/= KUTENGENEZA MADAWATI"
Taarifa hiyo inaendelea kuonyesha kuwa jumla ya shilingi milioni 713.8 zinahitajika kutengeneza madawati 23,700 ili kutosheleza mahitaji katika shule zote za msingi 117 zilizopo wilayani Ukerewe. Habari hiyo inaeleza zaidi kuwa, kati ya wanafunzi wote 78,281 wa shule za msingi wilayani Ukerewe, wanafunzi wapatao 42,400 (53.5%)wanakaa chini. Kwa maneno mengine ni kuwa katika kila wanafunzi 100 wa shule za msingi wilayani ukerewe wanafunzi 54 wanasoma wakiwa wamekaa chini. Natumaini hali ya Ukerewe inawakilisha hali halisi ya shule zetu za msingi hapa nchini. Kwa mantiki hiyo, karibu wanafunzi milioni 5 wanasoma wakiwa wamekaa chini hapa nchini katika shule zetu za msingi.
Mh Waziri Mkuu bajeti ya Ofisi yako kwa mwaka huu wa fedha pekee (2009/2010) ni zaidi ya shilingi trillioni 2.63.
Tunaomba sana aibu hii ifikie mwisho na tuwe wakweli na waungwana katika matumizi yetu na pia tufanye kila njia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuwawezesha watoto wetu kusoma katika mazingira yanayojali utu wa mwanadamu.