Gharama nyumba ya Gavana halali - Utouh

Mujuni2

Senior Member
Jun 11, 2008
142
3
Haya wakuu pamoja focus ni uchaguzi na hili nalo limo,Huko nyuma gazeti la Mwananchi liliripoti habari tofauti sasa nani mkweli? au ndio kulindana kumeanza?

Source: Nipashe 2010/8/6

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ametetea gharama za ujenzi wa nyumba mbili za Gavana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilizofikia Sh. bilioni tatu, na kusema Watanzania hawapaswi kushangazwa na hali hiyo.
Pia Utoah ametetea ujenzi wa majengo pacha ya BoT, kwa madai kuwa yanakidhi matumizi ya muda mrefu.
Utouh alisema pamoja na thamani hiyo kuonekana kubwa, lakini kama nyumba hizo zitauzwa hivi sasa kwa bei ya soko, thamani yake itafikia Sh bilioni 5.7.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa wadau wa ukaguzi wa hesabu ulioandaliwa na ofisi yake.
Alisema uchunguzi uliofanywa na ofisi yake ulibaini kwamba hapakuwa na matumizi mabaya katika ujenzi wa nyumba hizo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Alisema umaskini wa Watanzania hauwezi kusababisha nyumba za viongozi zikajengwa kwa viwango vya chini na kuongeza kuwa, kuna Watanzania ambao wana nyumba zinazozidi thamani ya nyumba hizo.
Utouh alisema nyumba hizo zina manufaa kwa umma kutokana na ukweli kwamba si mali binafsi, hivyo zitaendelea kumilikiwa na serikali na zitatumiwa na magavana na manaibu wao kwa miaka yote.
“Zile nyumba sio za watu binafsi, wanaokaa mle ni watumishi wa serikali na mtu yeyote anayeteuliwa kuwa na wadhifa wa ugavana au naibu gavana ataishi mle, ina maana, mnataka kwa kuwa nchi ni maskini viongozi waishi kwenye vijumba vibovu,” alihoji.
Aliongeza: “Hata majengo pacha ya BoT, watu waliyashupalia wakidai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma, hivi mnataka kila baada ya miaka kumi tujenge majengo ya Benki Kuu?
“Kwani mnadhani yale majengo ni ya Gavana, yale majengo ni ya Watanzania hivyo hakuna kibaya kilichofanyika kuyajenga na yamejengwa kwa matumizi ya muda mrefu,” alisema.
Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) aliyemaliza muda wake, Zitto Kabwe, alisema Gavana ni mtu mkubwa anayeshikilia uchumi wa nchi, hivyo anapaswa kuishi sehemu yenye usalama zaidi.
Alisema kulikuwa na ulazima wa kujenga nyumba za viwango hivyo, kwa kuwa makazi aliyokuwa amepangiwa yaliligharimu taifa fedha nyingi. Zitto alisema gharama iliyokuwa ikitumika kulipia pango la gavana kwa miaka miwili linafikia kiasi kilichotumika kujengea nyumba hizo.
 
Haya wakuu pamoja focus ni uchaguzi na hili nalo limo,Huko nyuma gazeti la Mwananchi liliripoti habari tofauti sasa nani mkweli? au ndio kulindana kumeanza?

Source: Nipashe 2010/8/6

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ametetea gharama za ujenzi wa nyumba mbili za Gavana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilizofikia Sh. bilioni tatu, na kusema Watanzania hawapaswi kushangazwa na hali hiyo.
Pia Utoah ametetea ujenzi wa majengo pacha ya BoT, kwa madai kuwa yanakidhi matumizi ya muda mrefu.
Utouh alisema pamoja na thamani hiyo kuonekana kubwa, lakini kama nyumba hizo zitauzwa hivi sasa kwa bei ya soko, thamani yake itafikia Sh bilioni 5.7.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa wadau wa ukaguzi wa hesabu ulioandaliwa na ofisi yake.
Alisema uchunguzi uliofanywa na ofisi yake ulibaini kwamba hapakuwa na matumizi mabaya katika ujenzi wa nyumba hizo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Alisema umaskini wa Watanzania hauwezi kusababisha nyumba za viongozi zikajengwa kwa viwango vya chini na kuongeza kuwa, kuna Watanzania ambao wana nyumba zinazozidi thamani ya nyumba hizo.
Utouh alisema nyumba hizo zina manufaa kwa umma kutokana na ukweli kwamba si mali binafsi, hivyo zitaendelea kumilikiwa na serikali na zitatumiwa na magavana na manaibu wao kwa miaka yote.
"Zile nyumba sio za watu binafsi, wanaokaa mle ni watumishi wa serikali na mtu yeyote anayeteuliwa kuwa na wadhifa wa ugavana au naibu gavana ataishi mle, ina maana, mnataka kwa kuwa nchi ni maskini viongozi waishi kwenye vijumba vibovu," alihoji.
Aliongeza: "Hata majengo pacha ya BoT, watu waliyashupalia wakidai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma, hivi mnataka kila baada ya miaka kumi tujenge majengo ya Benki Kuu?
"Kwani mnadhani yale majengo ni ya Gavana, yale majengo ni ya Watanzania hivyo hakuna kibaya kilichofanyika kuyajenga na yamejengwa kwa matumizi ya muda mrefu," alisema.
Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) aliyemaliza muda wake, Zitto Kabwe, alisema Gavana ni mtu mkubwa anayeshikilia uchumi wa nchi, hivyo anapaswa kuishi sehemu yenye usalama zaidi.
Alisema kulikuwa na ulazima wa kujenga nyumba za viwango hivyo, kwa kuwa makazi aliyokuwa amepangiwa yaliligharimu taifa fedha nyingi. Zitto alisema gharama iliyokuwa ikitumika kulipia pango la gavana kwa miaka miwili linafikia kiasi kilichotumika kujengea nyumba hizo.

Kuna thread nyengine inazungumzia hili jambo mujuni. Moderators ingekuwa vema hii thread ikaunganishwa na ile nyengine please.
 
Nimekupata Mdondoaji ila thread ikiwa ndefu sana inapotesa flow ndio maana time after time inatakiwa iwe refreshed with a different title..!
 
Ben Berbanke wa USA na Melvyn King wa UK ukiniambia wanashikiria uchumi wa nchi zao nitakubali.
Lakini msaani Gavana wa Tz ,among the poorest countries in the world ,ambae yuko kulinda ufisadi wa serikali na chama is a big joke.

Bora aogelee kwenye swimming pool tu
 
Back
Top Bottom