Gerala Hando wa Clouds Radio anajipendekeza kwa JK na CCM

Nimeacha kusoma hii thread yako pale tu uliposema Gelard Hando ni mmoja wa Watangazaji wenye heshima kubwa!! hizi ni pumba tupu unazotuletea hapa.

umenena vyema mkuu, nashindwa kuelewa hii heshima inatoka wapi na kwa jambo lipi hasa.
 
umepotoka tena umekosea! Ni mtangazaj gan clous ana hesima? Wote kuanzia wamilik wake ni makuad na makada wa ccm....pia clous ni chombo cha propaganda kimia kmia..mfno walmfanyia brthdy part Jk kwa ku2mia mamilion ya pesa. Wakat kuna matatzo kbao mfano, yatma,watt wa mtaan,wagonjwa. nazan umensoma..pia sizan kama kuna mtangazaj mwenye heshma clous, wenye dgree ata wat3 hawafk
 
Kuna faida gani ya kutumia raslimali kubwa kujenga barabara halafu wanasiasa wachache wa CCM kutumia maelfu ya malori yao kuvivunja kutokana na kuiua reli zilizopo hapa nchini kuuawa kimkakati? Kuhusu daraja la Kigamboni hoja hapa ni kwanini Serikali hii isimamie utoroshwaji nje wa dhahabu yetu takriabini ya kais cha Bilioni 10 kila iwiki halafu iwapore wafanyakazi mafao yao na kuzitumia kujenga daraja hilo?

kweli huwezi kumridhisha kila mtu ktk hii dunia
hata kama madarakani kingekuwa ni chama changu mimi nadhani wapo wanafamilia ambao wasingeniunga mkono,maana ulicho kiandika hakiakisi na mada husika
 
JK ni msanii hyo barabara ya bmoyo msata hiajakamilika kabisa, kipande kilichobaki kina madaraja nane mm nimepita mwezi uliopita. na thae most expensive part kwny road construction ni madarja. Hando ni radio broadcaster na hana taaluma ya uandishi wa habari, kazi yake kulewa pombe na malaya pale stereo bar kndoni. He's very unethical
 
Hivi mtu asipokuwa na degree hana heshima au haheshimiki?????
 
Kuna tofauti ya broadcaster na presenter.. Hao waclouds ni mapresenter wameingia hapo kuptia mashndano wenyewe wanaita presenter star search hvyo usimlaumu ndio uwezo wake huo he z nt professional
 
jana katika kipindi cha power breakfast kinachorushwa hewani na clouds radio mtangazaji gerald hando alikuwa akijipendekeza kwa jk na na ccm kwa kuwamwagia sifa kibao kwa miradi mbali mbali ya barabara zinazojengwa na kuwekwa mawe ya msingi hususan barabara ya bagamoyo-msata na mradi wa mabasi yanayoenda kasi.kilichonishangaza ni kitendo cha mtangazaji mwenye heshima kubwa kama yeye kujipendekeza kiasi kile ilhali ni wazi kuwa miradi kama hii ni "long overdue". Ilitakiwa serikali amabyo iko makini kuwa na "urban master plan" kupima viwanja katika surburbs zote za majiji yote ya nchi hii (maeneo yaliyoko pembzoni mwa jiji) kujenga miundo mbinu kama vile barabara za lami ikiwemo "flyovers" ,mtandao wa maji safi na maji taka na mtandao wa nishati ya umeme kabla ya kuruhusu wananchi kuanza ujenzi wa makazi katika maeneo hayo na kuhamia huko.kitendo cha serikali ya ccm kushindwa kufanya hayo mapema ni udhaifu mkubwa na ndio unaopelekea majiji yote katika nchi hii kukubwa na msongamano wa magari, watu kukosa maji safi ya bomba ilihali nchi hii ina vyanzo mbali mbali vya maji ikiwemo mito, maziwa na maji yaliyo ardhini na watu kukosa nishati ya umeme ilihali nchi hii imejhaaliwa vyanzo mbalimbali vya nishati hiyo ikiwemo maporomoko ya mji. Gesi, maka ya mawe, uranium na petroli. Ni ajabu sana kuona mtangazaji mweny heshima kubwa najipendekeza katika kidogo kinachofanyika tena kutokana na msukumo wa wapinzani. Na kidogo hicho hakina uwianao na raslimali za nchi hii zinzoporwa. Ni dhahiri kuwa kama serikali ya ccm na mkapa na jk wangekuwa makini matatizo ya miundo mbinu ya barabara, maji safi ya na nishati ya umeme nchi nzima sasa yangekuwa historia katika utawala wa miaka 20 ya mkapa na jk ni kutokana na ccm na watawala kufahamu kuwa wapo wapumbavu kama akina gerald hando katika nafasi nyeti za uelimishaji wa umma ndio maana wanafanya sherehe kubwa za uwekaji majiwe ya msingi mapya kabla ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara ambayo ilikuwemo katika bajeti ya 2011/12 amabpo wizara ya ujenzi ilipatiwa 40% tu ya fedha ilizotengewa na wakandarasi wa miradi mbali mbali ya barabara kulazimika kusimamisha kazi hizo na kuidai serikali fedha zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Kwa mtindo huu wa serikali ya ccm na jk kushindwa kufikisha fedha zilizotengwa kwa wizara husika tuna uhakika gani kuwa miradi hii inayowekewa mawe ya msingi sasa itakamilika ipasavyo? Ni kutokana na utaratibu huo ndio maana barabara ta bagamoyo-masata aliyoisifia gerala hando imefunguliwa pasipo kukamilika madaraja, haijawekewa alama za barabara na miundo mbinu mingine kuwezesha barabara kuweza kukabidhiwa. Nilitegemea investigative reporter kama anavyojiita gerald hando kujiuliza na kutafiti iweje barabara hii ikafunguliwe kabala ya kukamilika badala ya kutupigia propaganda katika redio. Nilitegemea mwandishi wa mwenye heshima kubwa kama gerald handio na kituo bora cha redio kama clouds kiwaelimishe wananchi hususan vijana kinachojidai ndio wateja wake wakuu kuhusu athari za ufisadi wa kutumia fedha fedha za pensheni za uzeeni wa wafanyakazi kujenga barabara ya kigamboni badala ya dhababu zetu za kiasi cha bilioni 10 kwa wiki zinazooporwa na wazungu kwa ruhusa ya ccm
yani cdm mnahangaika kila kukicha kupinga kila kitu serikali ya ccm inachokifanya???... Kazi mnayo wenzeni wanatekeleza ahadi ninyi mnaendelea kupinga..ikifika 2015 ccm wanasema tumefanya vs cdm tutafanya .
 
Lakini wadau,inamaana hizo barabara bado tunaona hazina msaada kwa taifa letu?
Sina chama,ila ni vyema tukawa wepesi kukubali kile kizuri kinachofanywa na serikali,kuwa upinzani sio kupinga kila jambo,
swali je barabara hizo zinazojengwa huko dsm hazitakuwa na msaada kwa taifa letu? Na vipi kuhusu lile daraja la kigamboni?
Kikawaida huwa hivi
leo ccm ipo madarakani,kila lifanywalo tutaliona si lolote,kesho chama kingine kitakuwa madarakani na tutasema na kuona hivyo hovyo.sasa waswahili wanasema huwezi kumlidhisha kila mtu ktk hii dunuia,mfano mzuri ni ktk familia tutokazo,hatuwezi kuwaridhisha wanafamilia wote,utafanya jema lakini baadhi ya wanafamilia wataona ni baya na wengine wataona ni jema
tuwe wepesi kukubali kwa yale tuonayo ni mema kwa taifa letu

Engineer Mtolera,
Ningetegemea kuwa katika fani yako ungekuwa ni mtu mwenye picha nzuri ya mambo jinsi yanavyotendeka ovyo, Lazima ujue kuwa serikali tumeipa dhamana ya kusimamia rasilimali zetu kwa uaminifu na umakini. Kufanya wajibu wake sio favour, Ni kodi zetu kwanini kusifia?Na tunatarajia return kubwa kutokana na kodi zetu, na siyo kubabaisha halafu mnasifia kitu gani?!! Ni miraadi mingapi inafanywa chini ya kiwango? Barabara ya Mbagala leo hii inarudiwa, kosa ni la nani? Nyinyi kama mainjinia mnatusaliti sana kwa tamaa ya Pesa!!:frusty:
Lazima kila mtu afanye wajibu wake kwa uaminifu mkubwa.
 
Watu wana maneno na wivu kama wanawake kupinga kila zuri la mwenzao. Jukwaani pamenuka hata hoja iwe nzuri ikionekana inapongeza govt inapingwa au mmelipwa na cdm coz huu ni zaidi ya ujinga.
 
Gerala Hando?? mhh ngonja ni google kama kuna mtangazaji mwenye jina hili pale Clouds
 
Hivi hii awamu ya nne kuna barabara gani ya maana amabyo iliianza na sasa imeshakamilika . Kwa mfano awamu ya tatu walianza na dar-mwz na wakatoka ikiwa imebaki vipande vichache vya kumalizia ambavyo awamu ya nne imechukuwa miaka yote mitano ya mwanzo kuvimalizia. Tatizo la awamu ya nne hawana vipaumbele walivyoviweka na kuhakikisha vinatekelezwa wanaibuka tu kila kona wakizinduazindua tu lakini hakuna kinachokamilika. Halafu barabara zingine ni purely misaada ambayo hakuna hata centi ya serikali pale kwa hiyo hamna cha kujisifia pale. Awamu ya tatu waliamua kutenga kiasi fulani kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya barabara and it worked very well! Hawa wa awamu ya nne wanataka kufanya mambo kiujanjaujanja tu kitu ambacho haitasaidia! Lazima wakubali kuachana na matumizi mabaya ya kaodi za umma ndipo wataweza kufanya kitu substantial otherwise wataishia tu kuzindua na kufungua miradi ambayo haijakamilika wakidhani watu watadanganyika!
 
Back
Top Bottom