GEORGE BUSH in TANZANIA (pictures only thread)

Ina maana Bush alikuja na gari lake, kwani sisi hatuna magari? hiyo sasa mbona ni dharau hiyo au?

FMES,

Bush au rais wa USA huwa anaenda na magari yake pamoja na kila kitu popote anapoenda.

Nimeshaona mara zote hata kwa hapa Europe anakuja na gari yake pamoja na ya wasaidizi wake wote. Wakimaliza, wanayapakia na kuondoka nayo.

Hata wakati wa Clinton ilikuwa hivyo hivyo.
 
Moshe Dayan,

Mkuu, wenyeji wenyewe hawajui Bush yuko wapi na wala hawana muda wa kufahamu. Hakuna mtalii anayekwenda nchi kwa sababu aliwahi sikia Bush kaenda..
Kifupi huu ujio wa Bush tunautukuza sisi wenyewe kwa fikra za malaya aliyepata mzungu pale Jolly club!...Anachofikiria yeye ni dollar tu bila kufikiria kwamba hata huyo mzungu anaweza kuwa na Ukimwi..
Mwisho, jiulize mzungu anayenunua mapenzi na malaya hivi nani mwenye kufaidi mahuasiano hayo. Je, hayo mabusu na vishindo vya vinyaji ni kielelezo cha mapenzi ya kweli?...
Hivyo basi ikiwa sisi tunampokea Bush kwa akili za malaya, well and good lakini kama tunafikiria mapenzi na fadhila tu bila kuvua chupi zetu mkuu tumepotea..

samahani ni ukumbi wa picha, duh!

Mkandara,

Hayo mawazo yako naona yamepitwa na wakati na hayatusaidii tena. Tanzania lazima tuwe mbele kuitangaza nchi yetu kwa njia mbalimbali kwa faida ya wananchi wetu. Kwa Bush kuja Tanzania ni advertisement kubwa kuliko yale matangazo waliyonunua CNN na kwenye vyombo vingine. Umejuaje kwamba hakuna mwananchi anayeenda kwasababu kasikia au kaona Bush kaenda Tanzania? Mimi toka jana napigiwa simu na marafiki wakisema wameona picha za Bush akiwa Tanzania na imependeza. Palipo na ukweli lazima tukubali, vinginevyo tutakuwa ni watu wa kulaumu tu kwenye kila kitu.

Hapo Wazungu ndio walipotuzidi, penye interest wanaficha ubaya wao mwingine wowote.

Mimi simpendi Bush lakini naunga mkono ziara hii kwasababu ina faida kwa Watanzania mbalimbali.

Kama nchi, hatuna cha kupoteza kwenye ziara yake, labda kama kuna mikataba ya siri ambayo wengine hatuijui.

Dunia ya leo ili mambo yako yafanikiwe lazima ukubali kushirikiana na hawa wakubwa wa dunia. Muhimu tu ni kupima je faida ni kubwa kuliko hasara? Kama faida ni kubwa basi inabidi tuchangamkie tenda.
 
Wanabodi hivi kweli tukiwafuata wananchi wa Kusini uwaambie ya kuwa ziara ya Bush aina maana wakati wana uhakika wa kujengewa barabara ya Tunduru hadi Songea watakuelewa ? Barabara hii itawezesha bandari ya Mtwara kutumiwa kikamilifu, hivyo mikoa hii hatimaye itaweza kukua kiuchumi !
 
Mtanzania,

Siku Kissinger, alipokuja bongo in the 70s, nilikuwepo pale Airport, Kissninger alikuja na magari yake waziri wetu wa nje alikuwa Kaduma, ambaye alikataa kata kata kua Kissinger ni lazima apande gari letu, baada ya mabishano ya muda, secret service walilichukua gari letu na kutokomea nalo ndani ya ndege yao, baadaye wakalirudisha na hatimaye Kissinger na Kaduma kupanda pamoja,

Sasa nilifikiri ile tabia bado inaendelea, ya kuwagomea kama Kaduma, kumbe tulishakubali yaishe? Basi viongozi wa zamani walikuwa imara sana!
 
Mtanzania,
Labda nikufahamishe kuwa nimewahi fanya kazi ya kutangaza vitu kama hivi...Hivyo nafahamu nachosema, wala tusibishane ovyo kwa sababu tu unataka bisha.
Tanzania ktk dunia ya kujitangaza ni Zero na hakika bado tuko nyuma sana kwa fikra kama hizi za kufikiria ati ujio wa Bush tuna promote nchi. Wao watakachoonyeshwa ni wagonjwa wa Ukimwi na Maleria walivyozidi nchini na pengine kuomba fungu kubwa ktk NGO ya mkewe... Nchi ngapi kazitembelea ambazo leo hii wewe zimekuvutia kuzitembelea.. Benin?...
Hata visiwa vidogo kama Dominican republic wana watalii kuliko sisi na hakuna kiongozi yeyote wa Marekani amewahi fika hivi karibuni..Mkuu, hizi ndoto za kufikiria ati labda tutafaidika ni kutotumia elimu tunayopewa. Elimu bora na isiyopitwa na wakati ni pale mnapoitangaza nchi kulingana na uhuru wa huu Utandawazi kwani kutembelewa na Bush ni siasa tupu. Aliwahi kuja Jimmy Carter na Clinton uliona tofauti ya ongezeko la Utalii ama nchi yetu kujulikana zaidi?.
 
Nakubaliana Tanzania tuko nyuma katika dunia ya kujitangaza ndio maana hata hatua moja kwenda mbele ni jambo zuri.

Hata kama serikali inazembea lakini kuna watu binafsi chungu nzima ambao wanaanza kuziona hizi opportunities na kuanza kuzitumia.

Nafikiri unajua kwamba kwenye advertisement, mafanikio kwa asilimia 60 yanatokana na a word of mouth.

Naona sasa ni kama tunaanza kupinga kila kitu hata mambo ambayo ni positive.

Utalii Tanzania unaongezeka na japo haitoshi lakini kila hatua ndogo ndogo inasaidia kuliko kuchukua misimamo ambayo wengine mnaitaka ambayo ki ukweli
tulishaijaribu na ikatushinda. Kwasasa afadhali tubanane huko huko kwenye dunia ya utandawazi.

Kama kuna Watanzania watapata nafuu ya malaria au kurefusha maisha kwa msaada wa USA, mimi sioni shida kabisa.

Tuache politics, kuna Watanzania wengi tu watafaidika na hii ziara ya Bush. Labda wengine tunaona hatuhitaji hii misaada na tunaweza kujitegemea, lakini tulipofika bila ya kujali nani katufikisha hapa, kuna Watanzania wenzetu wengi wanahitaji misaada, hivyo hata kama inatoka kwa adui, msaada ni msaada tu.
 
Heeeeeeeeeeeeeee!!!

Sasa naelewa kwanini Watanzania wana kawaida ya kuvunja sheria na hapo hapo wanabisha kwamba hawavunji hata kidogo..

Si mulisema hii thread ni ya picha sasa, mimi nilikuwa sichangii kwa kuwa sina picha, nilikuwa napitia tu kuona picha kama kule kwa kaka Issa Mi.. supu!!!

Nimeshuduhia Essay zizushushwa utafikiri DS 100 pale UDSM
 
Mtanzania,
Sawa mkuu mnachofanya ni kutumia Politics ktk Biashara, kosa kubwa sana. Tanzania inaendelea leo sio kwa sababu ya mahusiano ya kisiasa na Marekani bali Utandawazi na soko huria. Ujio wa Bush ni pure politics..Hii ni reality ambayo haipendezi masikioni.

Haya leteni hizo picha.
 
_44431920_bush_protest_416ap.jpg

Kwa hisani ya BBC!!
 
Mtanzania,
Sawa mkuu mnachofanya ni kutumia Politics ktk Biashara, kosa kubwa sana. Tanzania inaendelea leo sio kwa sababu ya mahusiano ya kisiasa na Marekani bali Utandawazi na soko huria. Ujio wa Bush ni pure politics..Hii ni reality ambayo haipendezi masikioni.

Haya leteni hizo picha.

mkuu mkandara, toka asubuhi niko macho nilikuwa naangalia meet the press, face the nation, cnn, foxnews, msnbc sikuona chochote kuhusu bongo, sasa hao watalii wa huku wataona vipi ahahahaha

bbcnews kidogo niliona clip 30 seconds

ahahah
 
Mkandara,

Hayo mawazo yako naona yamepitwa na wakati na hayatusaidii tena. Tanzania lazima tuwe mbele kuitangaza nchi yetu kwa njia mbalimbali kwa faida ya wananchi wetu. Kwa Bush kuja Tanzania ni advertisement kubwa kuliko yale matangazo waliyonunua CNN na kwenye vyombo vingine. Umejuaje kwamba hakuna mwananchi anayeenda kwasababu kasikia au kaona Bush kaenda Tanzania? Mimi toka jana napigiwa simu na marafiki wakisema wameona picha za Bush akiwa Tanzania na imependeza. Palipo na ukweli lazima tukubali, vinginevyo tutakuwa ni watu wa kulaumu tu kwenye kila kitu.

Hapo Wazungu ndio walipotuzidi, penye interest wanaficha ubaya wao mwingine wowote.

Mimi simpendi Bush lakini naunga mkono ziara hii kwasababu ina faida kwa Watanzania mbalimbali.

Kama nchi, hatuna cha kupoteza kwenye ziara yake, labda kama kuna mikataba ya siri ambayo wengine hatuijui.

Dunia ya leo ili mambo yako yafanikiwe lazima ukubali kushirikiana na hawa wakubwa wa dunia. Muhimu tu ni kupima je faida ni kubwa kuliko hasara? Kama faida ni kubwa basi inabidi tuchangamkie tenda.

Mimi nakuombea kwa Mwenyeezi Mungu akupe uhai uione siku ambayo utasema "laiti tusingemualika". Na kwa speed ya dunia ya sasa wala si muda mrefu, tutakumbushana humu humu JF. InshaAllah.
 
Wanabodi hivi kweli tukiwafuata wananchi wa Kusini uwaambie ya kuwa ziara ya Bush aina maana wakati wana uhakika wa kujengewa barabara ya Tunduru hadi Songea watakuelewa ? Barabara hii itawezesha bandari ya Mtwara kutumiwa kikamilifu, hivyo mikoa hii hatimaye itaweza kukua kiuchumi !

Eeeh Rufiji wee, hiyo inakuja at a price labda siyo waMerekani.
 
Rufiji,
Hivi Marekani wasingeweza jenga bila Bush kuja Bongo?....
Mbona JK kafika US mara tatu kidogo na mkataba huo haukuwepo ama zinatoka mfukoni mwake!..Je, wanachotaka in return ni kitu gani maanake isije kuwa tunauza haki ya mafuta yaliyokwisha patikana ktk ghuba za Zanzibar na kusini kwa barabara tatu..
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoreza Rice akiwasalimia wananchi alipoingia Ikulu Dar jana. Alikuwa na mvuto wa kipekee sijui kwakuwa ni bomba ama kwakuwa ni black?

Wakuu wa nchi mzee wa Mpanda, Mizengo na hata wa Pemba Dr Shein walishuhudia.

Bush akimwaga neno kwa waandishi wa habari.

wageni waalikwa wa kimarekani wakifuatilia shughuli.

Askari wa Marekani akipita na mbwa ili kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni salama kwa wazee kuingia.

Ma FBI wakilinda gari la Bush, Cadillac One ilipowasiri mlango wa Nyuma wa Ikulu!

Hapa ndio waliwekwa wataalamu wakiwa na madarubini yao sijui yalikuwa na uwezo wa kuona Dar nzima ama kung'amua magaidi, sijui!

Cheki mshikaji yuko juu ya paa la Ikulu na nguo nyeusi lazima aliungua sana na jua maana msimu huu Dar si inajulikana kwa joto!

Jamaa wakiwa na mizigo yao tayari kwa ajili ya kuimarisha ulinzi!

Rais Kikwete akiingia na mgeni wake katika lango la Nyuma la Ikulu na kulakiwa na watanzania waliofurika huko.

Bush akashindwa kujizuia akaanza kugawa mikono kwa kila mmoja aliyeweza kumshika.

Walifurahi sana na kila mmoja alijaribu kumfikia!

Baadae wakatoka pamoja kwa ajili ya kukutana na waandishi.

Walisaini pia Millenium Challenge Compact Agreement ambapo Tanzania itapata dola kibao kwa ajili ya kuondoa umaskini kwa kuboresha miundombinu na mawasiliano. Msaada huo mkubwa kuliko yote kutolewa na Marekani.

Mke wa Wziri Mkuu, Tunu Pinda akiwa na wake wa marais wastaafu, mama Sitti Mwinyi na mama Anna Mkapa jana wakati wa shughuli ya mafirst ladies! Ameshaingia kundini.

Mama Bush anashangaa zawadi ya kibongo, tumezidi kwa ukarimu jamani!

Hili ni tenge alilopiga first lady wetu leo alipokuwa na shughuli na mke wa Bush Karimjeee wakati wazee wanatia saini mambo makubwa zaidi.

Jamani sijui mtu akiwa mpya ndio inakuwa hivi hebu cheki Mama Pinda akiwa ameduwaa huku Mama Mwanamwema Shein akizungumza na Mama Siti kwa upande wa pili mama Mkapa akiwa na Mama Lowassa! Kama wamemtenga? Hii appearance ya kwanza kwa mama Lowassa tokea matatizo ya Bungeni.
 
Tz Pride,
Wala usifikirie kukianzisha na mimi!... mawazo yako ya kufungashiwa, mtumwa wa akili wee!
Mullah Omar na Bush wote wajinga tu...

Wewe ni nani? si ni raia kama wengine tu humu JF? mbona unaanza kutishia watu? Wewe endelea kumchukia Bush kwani wako watu wengi tu ambao wanaichukia Marekani tangia tumboni mwa mama zao
 
Back
Top Bottom