General Tyre: Is it a slow death to a once an East Africa Giant??

ngongo...........karibu sana JF.........

.......taarifa maridadi kabisa.......Dahh!.....Shelukindo.......!!!
 
Nyumbu,

Devendra Lohani alimwoa miss Nepal wa mwaka 2005 na si mnenguaji, miss Nepal wa mwaka 2005 kashajifungua na mtoto wake anaitwa Arusha tena anauraia wa Tanzania.

Rev.Kishoka,

General Tyre Amerika iliuzwa kwa Continental Ujerumani mwaka 2000.Hata kiwanda mama cha General Tyre USA share kubwa inamilikiwa na Continental wajerumani.

Ngongo,

Rose Soloka aliondoka na computer yenye kumbukumbu muhimu za GTEA jambo hili tumeshalipeleka ofisi ya mkuu wa Arusha kwa ufuatiliaji. Vile vile taarifa zake za ufisadi tumeshazipeleka TIB ingawa majibu ya manaja mwajiri hayaonyeshi wako makini.

Mkuu Ngongo, sina ubishi kwamba unajua mambo mengi ya GTEA tafadhali tushirikiane kuhakikisha wale wote walioshiriki kuiangamiza GTEA wanashughulikiwa no matter where they go.

Majibu ya ofisa wa TIB haya hapa,

Ndg. George Kabonde

TIB imepokea barua pepe (e-mail) kutoka kwako inayohusu kichwa cha habari hapo juu.


Kwa kuwa e-mail hii ina tuhuma za wizi na ubadhirifu wa mali ya Umma juu ya mfanyakazi wetu Rose Soloka, vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma, TIB imeona ni vema kulifanyia kazi suala hili.


Hivyo basi, uongozi wa TIB unaomba kufahamu unapatikana wapi au namba yako ya simu ili uweze kuwasiliana nawe kwani, tunaamini kuwa ushirikiano wako utaisaidia sana Benki kuendelea na uchunguzi kuhusiana na suala hili ili hatua zinazofaa zichukuliwe mara moja.


Tunategemea utawasiliana nasi mara utakapopata e-mail hii.


Tunatanguliza shukrani.



Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu.

Tanzania Investment Bank Ltd.
P. O. Box 9373
Dar es salaam
Tel: 2110511
Mob: 0786 056560
 
Kabonde,saafi sana kumbe mwenzangu umetoka katika ule ugonjwa wa kulalamika tu, umefuatilia mpaka TIB.

Nimefinywa sikio na wadau wenzangu eti Soloka kapewa assignment ya kulifuta deni la Sumbawanga Agricultural And Animal Food {SAAFI} inayomilikiwa na Mzindakaya, huyu mama anaweza nadhani hata hizi fedha za EPA atawaonyesha namna ya kuzitafuna.
 
Devendra Lohani anatoka katika ukoo wa kifalme Nepal, alikwenda Marekani kwa ajili ya masomo lakini pia alikimbia vita vilivyokuwa vikiendelea nchini Nepal kwasababu kulikuwa na sheria iliyowalazimisha vijana kujiunga na jeshi ili kupambana na wapinga utawala wa kifalme wa Maoist.

Devendra Lohani alitumia fedha nyingi za GTEA {pamoja na fedha za mkopo wa NSSF $10,000,000} kumsaidia mfalme Gyanendra wa Nepal {Hindu kingdom} dhidi ya Maoist lakini hatimaye walifanikiwa kumaliza utawala wa kifalme may 2008.

Mwaka 2004 vijana 23 wa kinepal waliletwa Tanzania na mfalme Gyanendra kwaajili ya kupata mafunzo ya kijeshi TMA – Monduli, Rtd lt col Muro alipewa jukumu na Devendra kuandaa utaratibu wa kuwaingiza chuoni Monduli.

Kulikuwa na kila dalili ya mpango kushindwa kwasababu vijana wa kinepal hawakuwa wanajua lugha ya kiingereza pia taratibu za kiserekali hazikufuatwa kabisa, mipango ya kuwapatia ajira hapa Tanzania ikafanyika kwa kuwachomeka kwenye department mbali mbali GTEA na wengine wakapelekwa Clock Tower service center na Tanzanite One Mining kwa kazi za kuziba pancha na ulinzi respectively.

Wafanyakazi wa GTEA waliona ajira zao ziko mashakani wakaamua kutoa taarifa Uhamiaji, napenda kuwapongeza hawa jamaa wa uhamiaji kwa kazi nzuri kwasababu baada ya kupata taarifa wanepal walirejeshwa kwao baada ya muda mfupi lakini wanepal waliopelekwa Mererani {Tanzanite One Mining} mpaka leo wapo wanafanyakazi ya ulinzi.

Devendra Lohani aliwahi kututamkia wafanyakazi muda si mrefu Nepal ingefungua ubalozi Tanzania na yeye angekuwa balozi ,kwamaneno yake mwenyewe alitoa msaada kwa mfalme Gyanendra kwa matazamio ya kupewa ubalozi.

Inashangaza mtu wa aina ya Devendra Lohani pamoja na uovu wote mpaka leo anapata wapi uwezo wa kufanya mawasiliano na ofisi ya waziri mkuu,waziri wa fedha,waziri wa biashara, viwanda na masoko,ina maana idara ya usalama wa taifa imelala!

Usalama wa taifa inavyoonekana kazi yao ni ulinzi wa viongozi tu, ni vizuri usalama wa taifa wakaona umuhimu wa kulinda uchumi wetu pia kwasababu kufungwa kwa kiwanda cha General Tyre kumeambatana na athari kubwa kiuchumi.

Hakuna ubishi kwamba General Tyre ilikuwa ikilipa kodi VAT 150 milioni kwa mwezi, direct employment 400, indirect employment 1500, tumepoteza soko la matairi Kenya, Somalia, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi na Malawi
 
Mkuu Ngongo, huyu Lt Col Muro ni yule tyre dealer wa GTEA ana kampuni inayokwenda kwa jina la G-INVESTMENT ama ni mtu mwingine.

Lt Col Muro ni kati ya wale askari waliotaka kumpindua Mwl Nyerere, hili ni kundi la maofisa jeshi hasa kutoka kanda ya kaskazini waliondolewa jeshi na kupatiwa kazi nyingine. Capt Mushi alipachikwa Fiber Board Arusha, Col Metili - huyu alipewa Mkonge Tanga.
 
Mwaka 2002 General Tyre ilisimamisha uzalishaji wa tubes kwa kisingizio cha kupunguza gharama kubwa za uzalishaji ingawa hakuna mfanyakazi aliyepungwa kazi, kitengo cha uzalishaji wa tubes kilikuwa na wafanyakazi zaidi ya 25.

Tubes za General Tyre zilikuwa zinasifika kwa uimara na ubora hata watumiaji wa matairi ya nje walipendelea kutimia tubes za General Tyre. D Lohani na Managing Director wa G-Investment rtd Lt Col Muro waliagiza tubes kutoka Apollo ya India kwa kutumia nembo na specification ya General Tyre. General Tyre ilitumika kuagiza na kulipa kodi, kuuza kwa kutumia mtandao wake mkubwa {branches} kisha faida iliyopatikana ilirejeshwa G-Investment.

Wana JF mtashangaa haya mambo yaliwekana vipi kufanyika? General Tyre kama nilivyosema mwanzo haikufanyiwa ukaguzi kwa miaka minne, pia haikuwa na mkaguzi wa ndani {Chief Internal Auditor} kwa zaidi ya miaka kumi na mbili.
 
Mwenyekiti wa bodi mheshimiwa Shelukindo na wanabodi wenzake hawakuona umuhimu wa mkaguzi wa ndani.
 
Mheshimiwa sana W Shelukindo karejeshewa uwenyekiti wa bodi ya General Tyre pamoja na kuvurunda kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na saba.

Ikumbukwe W Shelukindo alilazimika kujiuzulu uwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi General Tyre kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake, hali iliyosababisha kiwanda kufungwa, wafanyakazi kulipwa mishahara na hazina [wizara ya fedha] pasipo kufanyakazi,madeni makubwa yasiyoweza kulipika [NSSF, EXIM BANK, CONTINENTAL, GENERAL TYRE].

Wakuu nchi yetu ina watu zaidi milioni 36 na ushe wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha, hakuna mantiki kwa watu aina ya Shelukindo kuharibu alafu kuendelea kurundikiwa majukumu waliyoshindwa kuyatekeleza.
Chini ya uongozi wa Shelukindo General Tyre hakufanyiwa audit kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka huu 2008. Mwaka 2005 Shelukindo walipata mkopo wa $10 million kwa ajili ya ku-modernise kiwanda [kununua mashine za kisasa] kitu ambacho hakikufanyika kabisa.

Chini ya uongozi wake Shelukindo alishiriki kuuza mali [asset] zote za General Tyre [Nyumba tatu zilizoko uzunguni "Serengeti Road"] Arusha, [Godown lililoko Nyerere road] Dar es salaam na Malori ya kubeba mizigo.

Mamlaka ya uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ni ya rais, lakini habari tulizonazo ni kwamba mheshimiwa Mizengo Pinda ndiye aliyeshinikiza Shelukindo kuendelea na wadhifa wa mwenyekiti wa bodi.
 
Morani,

Hicho kiwanda kimeachwa kife kwa maslahi ya wanasiasa wetu, walikibinafsisha kwa Continental Tyre ambao walikigeuza kuwa godown kinyume na mkataba wa uwekezaji huo, na serikali inajua kuwa kiwanda hakizalishi lakini kwa sababu binafsi za baadhi ya wanasiasa wetu wanataka kife.

Wafanyakazi wanasema kuwa kiwanda kikifanya kazi mara moja kinaweza kulipa mishahara ya wafanyakazi na gharama za uendeshaji kwa miezi 3.

Nakuthibitishia na muulize mwenye magari madogo ya tani 1 na chini ya hapo atakuambia jinsi ambavyo tairi za General ni Hot cake! Lakini Serikali imeamua kuachia kiwanda kife na wafanyakazi hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu sasa na miezi michache ilopita Menejiment ya Genral Tyre imeanza kuuza mali za kiwanda (magodown) zilizopo Dar
 
kama ni kweli kinachoua GT ni tamaa ya viongozi basi ni balaa....tamaa na rushwa za viongozi wetu zina cost ajira na maisha ya watu zaidi ya 1000...ni aibu kweli kweli na hao wakurugenzi wanaishi mitaani na wananchi? nchi yenye rushwa na wezi haiwezi kuendelea hata watu wafanye kazi kwa bidii usiku na mchana,ndio maana kiongozi mzuri ni yule anayesimamia justice & fairness kwa wananchi wake!
 
Well,

Actually the last time I was there ni three months ago.I used to spend my sundays there playing football na wazee wa UN untill someday huyo Mhindi tells us there plans to build a hotel hapo so we should move. Wazee wengi wakagomba then we just had to move.

I think it has been inoperative for so long until wakaamua kudai wako bankrupt!
 
Wakati wazee wailiyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki wanaendelea kusotea malipo yao,wafanyakazi wa General Tyre {ea} Ltd wanaendelea kulipwa na hazina {wizara ya fedha} kwa kukaa nyumbani bila kufanyakazi.

Wizara ya fedha ilianza kuwalipa wafanyakazi wa General Tyre kuanzia January 2008,haijulikani mpango huu utaendelea hadi mwaka gani.wengi wawafanyakazi hawapendi hali hii iendelee badala yake wanataka kiwanda kipatiwe fedha za kununulia malighafi ili waweze kurudi kazini na kuendelea na ujenzi wa taifa.

Watanzania wote tunajua kwamba uzalishaji ulisamamishwa miaka minne iliyopita kwasababu mbalimbali ambazo wakuu wengine wameshazieleza kwa mapana na marefu, ajabu ni kwamba huu mpango wa hazina kuwalipa wafanyakazi ulipofahamika kwa baadhi ya managers waliamua kujiongeazea mishahara maradufu.

Managers walikuwa wakilipwa mishahara kati ya tsh 1.3 milioni mpaka 1.5 milioni kwa mwezi lakini baada ya hazina kuanza kulipa miashahara managers walilipwa tsh 3.5 milioni kwa mwezi. Kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji mashirika ya umma kupanda kwa mishahara lazima kuambatane na baraka za bodi ya wakurugenzi.

Swali ambalo limeendelea kuumiza akili yangu kama bodi ilitoa baraka za ongezeko la mishahara na wakati huohuo inaomba msaada kwa serekali kwa ukosefu wa fedha za uendeshaji!.

Naomba kuwasilisha jamvini.
 
Mafisadi waliochota hela ya NSSF US $ 10 milioni walisuka aka kampango hazina ili kuwanyamazisha wafanyakazi. Inawezakana wakaendelea kulipwa mishahara mpaka mwaka 2010.

Bodi ilibariki ongezeko la mishahara kwasababu waliofia baadhi ya mameneja wangeweza kutoa siri na kuvuruga mpango wao wa kujiuzia General Tyre kwa bei ya nyanya.
 
Meneja mkuu wa General Tyre (EA) Ltd, Devendra Lohani ametoroka nchi baada ya kupata habari rafiki yake mpendwa Basil Pesambili Mramba kawekwa ndani na kwa ujumla hali za mafisadi si shwari tena Tanzania.

Bwana Lohani alitakiwa kurejea Tanzania kutokea Nepal, India na Ujerumani alikokwenda kwa ajili ya mapumziko tangu 13/09/2008 lakini mpaka leo ajarudi na amesitisha mawasiliano baina yake na General Tyre.
 
Wizara ya fedha imewalipa wafanyakazi wa General Tyre malimbikizo ya mishahara ya miezi mitano (kuanzia mwezi Sept. 2008 mpaka Jan. 2009). Miongoni mwa wafanyakazi waliolipwa miashara ni pamoja na wale waliostaafu,waliokufa na walioajiriwa na makampuni mengine.

Katika hali inayoosha wizara ya fedha inashindwa kusimamia vizuri fedha za walipa kodi hapakuwa na uhakiki madhubuti kwatambua wafanyakazi halali wa General Tyre.

Ikumbukwe pia baadhi ya managers walijipandishia mishahara mara baada ya kupata fununu kwamba wizara ya fedha ingechukua jukumu la kulia mishahara.

Mpaka sasa wizara ya fedha imeshatumia kiasi cha tsh 1.5 bilioni kwaajili ya mishahara ya wafanyakazi wa General Tyre na hajulikani lini zoezi hili litamalizika pia hajulikani lini serekali itaamua kuwekeza katika kiwanda chake ili uzalishaji wa matairi na tubes uanze na kuepukana na mzigo wa kulipa mishahara wafanyakazi wasiofanyakazi.

Naomba kuwasilisha.
 
Lakini nadhani kwa mtindo huu wa kuibua hizi kashfa zinazousiana na mali ya umma tutafika mahali mambo yatakaa sawa. Kwani ni mali zetu na hela zetu, unapoona jambo lolote linalohusiana na matumizi mabaya ya mali ya umma, ufujaji, wizi ni vizuri tukapiga kelele. kwa umoja wetu tutasikikika tu. Hata kuku wakiwa elfu kumi wakikukimbiza utaogopa, lakini si mmoja.

Inauma kwa kweli mshenzi anatoka Nepal anakuja kula mali zetu kiasi hiki. Na huyu shelukindo ndio yule mbunge? kama ni yeye hili linatosha kumuondoa kwenye Uwenyekiti huo wa Bodi na bodi nzima ivunjwe, na hata kwenye ubunge kama yupo kwe nye tume yeyote ile wamtoe tu.

Nchi tutaijenga tu, kama tutaendelea kuwa makini kwenye kutazama mali zetu kwa umakini.

Naamini tutafika tu kunakopataka.

Kila safari ndefu uanzia hatua moja.
 
Ni kweli kiwanda kimefungwa na umeme umekatwa. Wafanyakazi bado hawajaachiwa kazi na bado wanalipwa ingawa hupita miezi kadhaa kabla ya kulipwa. Hivi karibuni tu Genaral Tyre wameuza godown lao huko Dar (ilikuwa Sept au Okt) na wakafnikiwa kupunguza deni la mishahara ya wafanayakazi.

Ukweli ni kuwa General imeuawa na serikali ina mkono. Iliingia ubia na Kamuni ya Continental AG ya Ujerumani na Menejimenti ya Continental wakaleta Wahindi wao ambao walikigeuza kiwanda cha Genaral Tyre kuwa godown!

Tair chapa General ni kiboko kwa matairi yanyuzi hasa kwa magari yasiyozidi tani moja (Landrover, Landcruisers na salooo), kwa matairi hayo YANA/Firestone wanaachwa mbali mno. Yaani ikitokea Genaral wanaanza uzalishaji na kumwaga tairi zao za magari nliyotaja YANA hataweza kushindana kabisa lakini kama ujuavyo nadhani kuna mkono wa mafisadi ili General isifanye kazi kuwafaidisha wenye viwanda (au waagizaji matairi) vya India, China na YAna (Kenya) kwa kupata chochote.

Kuna wakati Genaral Tyre waliomba mkopo wa mil. 700 kutoka kwa C. Gachuma wa Nyanza Bottlers wakazlisha matairi (ingawa aliyepewa haki ya kuyauza ni Gachuma tu), angalau matairi yalionekana mtaani nayakanunuliwa. Sijui baada ya hapo waligombana vipi.
 
i hope this will be given the attention it deserves.it looks like in the heat of the ballali issue this ufisadi will get ignored.if followed up i can assure you it will shed light on the big mfisadi - mramba.and shelukindo needs to be invistigated as well. General tyre has been his goose that lays the golden eggs. We need to recruit " a firing sqad " to deal with the situation in tz.

lets try the same way jerry of ghana did, by applying the firing sguard; kwani imekuwa fudisho kiasi kwamba uchaguzi wao ni mfano africa
 
Wizara ya fedha inaendelea kumlipa mshahara wa tsh 30 milion kwa mwezi meneja kuu wa General Tyre bwana Devendra Lohani ambaye amegoma kurudi Tanzania kwa kuhofia kukamatwa na kuhojiwa na vyombo vya dola kwa kuifilisi General Tyre.

Bwana Devendra Lohani aliletwa nchi na Continetal ya Ujerumani ambao pia waliwajibika kumlipa mshahara laikini Continental ujerumani walimfukuza kazi Devendra Lohani mara baada ya kubaini uendeshaji mbovu mwaka 2007. Mwenyekiti wa bodi na wajumbe wote wa bodi waliamua kumwajiri bwana Devendra kinyume na ushauri wa Continental ujerumani waliotaka mtanzania mzawa aajiriwe ili kupunguza gharama kubwa za kumwajiri mgeni. Uamuzi wa bodi kumwajiri bwana Devendra Lohani umeendelea kuliletea taifa hasara kubwa kwasababu mpaka sasa wizara ya fedha imeshamlipa tsh360,000,000/= bila kufanyakazi pia ikumbukwe bwana Devendra ni muhusika mkuu kwenye sakata la kuifilisi General Tyre.

Bwana Devendra Lohani kwa sasa ameajiriwa na kiwanda cha kutengeneza matairi India Appolo. Appolo ya India nao walihusika sana kuhijumu General tyre kwa kuchukua kinyemela specification za utengenezaji wa Tubes baada ya uzalishaji wa tubes kusimamishwa kuzalishwa.
 
Back
Top Bottom