Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Wizara ya fedha inaendelea kumlipa mshahara wa tsh 30 milion kwa mwezi meneja kuu wa General Tyre bwana Devendra Lohani ambaye amegoma kurudi Tanzania kwa kuhofia kukamatwa na kuhojiwa na vyombo vya dola kwa kuifilisi General Tyre.
Bwana Devendra Lohani aliletwa nchi na Continetal ya Ujerumani ambao pia waliwajibika kumlipa mshahara laikini Continental ujerumani walimfukuza kazi Devendra Lohani mara baada ya kubaini uendeshaji mbovu mwaka 2007. Mwenyekiti wa bodi na wajumbe wote wa bodi waliamua kumwajiri bwana Devendra kinyume na ushauri wa Continental ujerumani waliotaka mtanzania mzawa aajiriwe ili kupunguza gharama kubwa za kumwajiri mgeni. Uamuzi wa bodi kumwajiri bwana Devendra Lohani umeendelea kuliletea taifa hasara kubwa kwasababu mpaka sasa wizara ya fedha imeshamlipa tsh360,000,000/= bila kufanyakazi pia ikumbukwe bwana Devendra ni muhusika mkuu kwenye sakata la kuifilisi General Tyre.
Bwana Devendra Lohani kwa sasa ameajiriwa na kiwanda cha kutengeneza matairi India Appolo. Appolo ya India nao walihusika sana kuhijumu General tyre kwa kuchukua kinyemela specification za utengenezaji wa Tubes baada ya uzalishaji wa tubes kusimamishwa kuzalishwa.
Hizi ni tuhuma kubwa Ngogo. Ni vema ukaanika data hapa JF si wajua Wakulu huchota evidences hapa? Kama ni kweli basi naamini huo mshahara unagawanywa kwa wajumbe wa Bodi ya Genaral Tyre na Wizara ya Fedha maana mwenye akili timamu hawezi kufanya hivyo.
Hata hivyo uwezekano huo upo si imeandikwa RUSHWA HUPOFUSHA MACHO!