General Tyre: Is it a slow death to a once an East Africa Giant??

Kweli hii ni nchi ya machinga. nadhani hata zile ajira milioni 1 alizoahidi mkuu ni za kimachinga na sio endelevu. ndio maana alikimbizia mamilioni huko nmb na kwenye sacos watu wakaanzishe magenge na viduka.

Viwanda kama hivyo kimoja kina uwezo wa kazalisha ajira 50 elfu direct na indirect. hata kale kauchumi kake alikosoma hakamsaidii. hatuwekezi kwenye viwanda wala kilimo sasa sijui nini nguzo yetu!!!

inauma sana kuona kila kukicha ni hatua mbili nyuma, sijui tutaishia kutumbukia wapi
 
Msumari wa mwisho wapigiliwa jeneza la General Tyre

  • Ni kilio na kusaga meno kwa wafanyakazi 317
  • Serikali yakatisha rasmi ajira zao

MWAKA 2003 mmoja wa wafanyakazi vijana wa kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre East Africa Ltd cha Arusha alifichua tuhuma za ufisadi mkubwa uliokuwa ukifanywa na menejimenti ya kiwanda hicho kwa kuwaeleza baadhi ya wafanyakazi wenzake.

Mfanyakazi huyo hakuishia kueleza wenzake tu, lakini pia alichukua hatua za kuvujisha habari hizo katika vyombo kadhaa vya habari; lengo likiwa ni kuiamsha bodi ya wakurugenzi na serikali ambayo ndiyo yenye hisa nyingi katika kampuni hiyo kuhusu ufisadi huo.

Ufisadi huo uliokuwa unatishia ustawi na uhai wa kiwanda hicho ulikuwa unafanywa na meneja wake, Deven Lohan - raia wa Nepal kwa kushirikiana na wakuu wa idara mbalimbali ambao ni wazawa.

Vyombo kadhaa viliripoti habari za ufisadi katika kiwanda hicho lakini kwa mwamko kidogo wa serikali yetu; hakuna hatua za maana zilizochukuliwa huku Wizara ya Viwanda na Biashara, ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Waziri Basil Mramba (Awamu ya Tatu), ikikalia mada hayo bila kuyachunguza.

Hata hivyo, pamoja na kuonyesha uzalendo wake, mfanyakazi huyo hakupata kuungwa mkono na wenzake katika kufichua ufisadi huo, na badala yake baadhi walimchongea kwa wakubwa ambao nao walichukua mara moja hatua za kumfukuza kazi.

Wafanyakazi hao walimwona mwenzao kama mtu msumbufu na vijana wa sasa ambao wanakosa nidhamu katika sehemu za kazi wenye tabia za kujaribu kuhoji kila jambo. Hata hivyo, jambo ambalo wafanyakazi hao hawakulijua ni kwamba ufisadi huo ungekuja kuwa "gharika" katika maIisha yao ya baadaye.

Baada ya kuachishwa kazi, mfanyakazi huyo alipata kazi katika moja ya makampuni ya simu za mkononi mkoani Arusha, na hadi leo bado anaendelea kufanya kazi na kampuni hiyo.

Lakini miaka mitano (mwaka 2007) baadaye, ufisadi huo mkubwa ulisababisha kiwanda hicho kusitisha uzalishaji na wafanyakazi wakawa wanalipwa mishahara bila kuzalisha chochote kwa miezi sita hadi mwaka 2008 kiwanda kilipofungwa kabisa.

Kiwanda hicho kilifungwa baada ya kushindwa kuagiza mali ghafi ya kutengeneza matairi, kukatiwa umeme na maji na wafanyakazi walipelekwa likizo isiyokuwa na malipo.

Tuhuma za ufisadi zilizokuwa zimeibuliwa kuhusu meneja huyo ni kutumia fedha za mkopo wa Shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa matumizi mengine badala ya kufufua kiwanda hicho kwa kuongeza uzalishaji.

Baada ya kiwanda kupata fedha hizo huku kikidhaminiwa na serikali, menejimenti ilipa kiasi cha fedha kwa madeni waliyokuwa wanadaiwa lakini kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 3.5 zinaelezwa kutumika bila vielelezo vyovyote.

Imeelezwa kuwa meneja huyo alitumia fedha nyingi kwa matumizi binafsi yakiwemo ya kuwaleta ndugu zake kutoka Nepal na mmoja wa wana wa mfalme wa nchi hiyo kutembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro, Serengeti na Manyara kwa gharama za kiwanda hicho!

Aidha, kiasi kingine cha fedha kilitumika kwa sherehe za kidini zilizofanywa na meneja huyo katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam.

Meneja huyo kabla ya kuondoka nchini na kurudi kwao pia aliuza nyumba nne za kampuni zilizokuwa katika eneo la Corridor katika manispaa ya Arusha kwa bei ya kutupa; huku moja akijiuzia mwenyewe kwa kwa kiasi cha Shilingi milioni 100.

Wakati Meneja huyo akifanya vitendo hivyo, ambavyo kwa ujumla vilionekana kama hujuma, wakuu wa idara nao hawakuwa nyuma katika "udokozi"; kwani inaelezwa kuwa kila moja katika idara yake alifuja kiasi alichoweza wakitumia mwanya wa udhaifu wa menejimenti.

Baadhi wanadaiwa kuiba vipuri mbalimbali vya mashine za kuzalisha matairi na wakati mwingine wakinunua vipuri feki ambavyo vilishindwa kufikia viwangi vinavyotakiwa.

Kufuatia mlolongo huo wa matukio ya ufisadi uliochukua zaidi ya miaka mitano sasa, wafanyakazi hao wapatao 317 wamekumbwa na hali ya hofu, mashaka na wasiwasi baada ya serikali kukatisha ghafla mikataba yao ya ajira kuanzia wiki iliyopita; huku wakiwa hawajalipwa mishahara kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uamuzi huo wa kusitisha ajira za wafanyakazi hao ambao umekuja ghafla na bila kutarajiwa ulitangazwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk.Shaban Mwijaki wakati alipofanya mkutano na wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao wamepewa notisi ya kulipwa mshahara wa mwezi mmoja pamoja na mafao yao yatakayolipwa na serikali ambayo ndiyo yenye hisa nyingi katika kiwanda hicho.

Serikali inamiliki hisa karibu asilimia 80 za kiwanda hicho wakati kiasi cha hisa kilichobakia kinamilikiwa na kampuni ya Continental ya nchini Marekani.

Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi, mafao ya serikali kwa mujibu wa sheria ni kidogo sana, na kuna uwezekano hakuna mfanyakazi atakayelipwa zaidi ya shilingi milioni 2 bila kujali muda ambao mfanyakazi husika amefanya kazi.

"Kuna waliofanya kazi miaka 17 wanaambullia Shilingi 700,000 na wengine milioni 1.2….sasa hapo utaona ni kwa kiwango gani wafanyakazi wanapata hofu ya maisha watakaporudi mitaani", alisema mmojawao mwishoni mwa wiki.

"Kwa kweli wafanyakazi wote wamepata hofu hasa wengi ambao tuna umri mkubwa ambao si rahisi kupata ajira serikalini na hata makampuni binafsi tunaweza kumudu gharama za maisha wakati hatujalipwa mafao ya maana", aliongeza mfanyakazi huyo.

Wafanyakazi hao wanadai kuwa wao hawahusiki na ubadhirifu huo na hatua zilizochukuliwa na serikali ni sawa na kuwapa adhabu kwa makosa ambayo hawakutenda.

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi (TUICO), tawi la kiwanda hicho, Lukio Tulule alikataa kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu na sheria inayotumiwa na serikali kulipa mafao kwa wafanyakazi hao kwa madai kuwa jambo hilo limemfanya achanganyikiwe.

"Ndugu yangu, sielewi chochote naomba uniache tu suala hilo limenichanganya sana….nipigie simu Jumatatu nitakuwa nimepitia nyaraka zilizopo na nitajua utaratibu uliotumika kulipa mafao yetu", alisema.

Akizungumzia hatua ya kukatisha ajira za wafanyakazi hao, Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kutokana na ukweli kuwa kwa sasa kiwanda hicho hakiwezi tena kuzalisha matairi hadi hapo serikali itakapopata mbia mwingine.

"Kutokana na kiwanda kuwa na madeni makubwa na ufisadi uliofanywa na menejimenti, serikali imeona ni vyema kiwanda hiki kikafungwa kwanza na wafanyakazi kulipwa mafao yao wakati tukijipanga upya kutafuta hatua za kuchukua", alisema.

Kufungwa kwa kiwanda hicho kunahitimisha kuwepo kwa viwanda vya umma katika mkoa wa Arusha vilivyokuwa vimeanzishwa katika miaka ya 70 na 80 na ambavyo karibu vyote vilikuwa vimebinafsishwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu kwa wawekezaji mbalimbali, lakini vingine vikiwa vimetelekezwa na kubakia magofu.

Viwanda hivyo, ambavyo viliufanya mkoa wa Arusha kuwa ni mkoa wa pili kwa kuwa na uchumi mzuri baada ya Dar es Salaam, ni pamoja na kiwanda cha bia, kiwanda cha madawa ya binadamu cha TPA, kiwanda cha kusindika nafaka cha NMC, Baby Food, kiwanda cha nguo cha Kiltex, kiwanda cha sabuni cha EMCO na kiwanda cha mbao cha Fibreboard.


Source: Raiamwema.


Hii habari kwa kiasi kikubwa imejaa uzushi.

Kijana anayezungumziwa kwamba alifichua ufisadi uliokuwa ukifanywa na managemant ya GT kwa kuwaeleza wafanyakazi wenzake na baade vyomba vya habari si za kweli hata kidogo tena zimejaa ubabaishaji na uvivu wa hali ya juu kwa mwandishi wa habari hii. Gazeti la Raiamwema linapaswa kuwaomba radhi wasomaji wake kwa kuandika habari pasipo kufanya utafiti wa kutosha.

Kwa sisi tuliowahi kufanyakazi GT uliposoma hii habari tulijua moja kwa moja kijana anayezungumziwa anaitwa Antony Mhandiki.

Kilichomwonda A Mhandiki si kwasababa alifichua ufisadi uliokuwa ukifanywa na managemant ya General Tyre bali kugombea ulaji baina yake yeye na L Mgoyo [Purchasing Manager]

Bwana A Mhandiki alikuwa Ag Marketing Manager kuanzia mwaka 2004 mpaka alipoondolewa mwaka 2007. Kama mkuu wa division ya masoko Bwana Mhandiki alihusika na uhagizaji wa vifaa vya promotion [t-shirt, kofia,key holder na vifaa vya michezo] kupitia idara ya ununuzi [Purchasing]. Kampuni ya Zizou ilipata tender ya kuleta vifaa vyote vyenye thamani ya zaidi ya tsh 250 milioni,ugomvi wa Bwana Mhandiki na Bwana Mgoyo ulisababishwa na kutokugawana kwa usawa 10% na mgawo wa fedha za vifaa ambavyo kampuni ya Zizou hawakuweza kusupply.

Bwana Leonard Mgoyo alitumia vyema fursa iliyokuwepo wakati huo, vyombo vya habari hasa gazeti la RAI na baadaye Mwahalisi yalikuwa yakitoa habari za ufisadi uliokuwa ukifanywa na Bwana D Lohani.

Bwana L Mgoyo kwa uchungu wa kunyimwa ulaji alikwenda kujengea hoja kuu mbili kwa manaja mkuu aliyeanza kulemewa na kashfa za ufisadi.

[1] Kwakuwa Bwana A Mhandiki aliwahi kufanyakazi katika gazeti la Daily news ni rahisi kwake kujuana na wanahabari na kuwa yeye anahusika na uvujaji wa habari zilizokuwa zikihihusisha General Tyre na ufisadi.

[2] Gazeti la RAI wakati huo lilikuwa na wanahabari wengi wahaya/wanaotoka mkoa mmoja na Bwana A Mhandiki.

Hoja hizi mbili zilisababisha Bwana A Mhandiki kuachishwa kazi General Tyre, ingawa manaja mkuu alikuja kukiri baadae alifanya kosa kubwa kumwachisha A Mhandiki kazi kwasababu bado habari za ufisadi ziliendelea kutoka kwenye vyombo vya habari.

Najua waandishi wa habari wa gazeti la Raiamwema wanatembelea sana hapa jamvini itakuwa jambo la maana kama mtaweza kuirekebisha habari mliyoitoa bila kuifanyia utafiti wa kutosha. Tuliokuwa tunazitoa habari za ufisadi tuko bado hatujafa tena tunafahamiana sana. A Mhandiki alikuwa ni sehemu ya viongozi waliosababisha General Tyre ikafikia hapo ilipo.

Naomba kuwasilisha.
 
Viwanda hivyo, ambavyo viliufanya mkoa wa Arusha kuwa ni mkoa wa pili kwa kuwa na uchumi mzuri baada ya Dar es Salaam, ni pamoja na kiwanda cha bia, kiwanda cha madawa ya binadamu cha TPA, kiwanda cha kusindika nafaka cha NMC, Baby Food, kiwanda cha nguo cha Kiltex, kiwanda cha sabuni cha EMCO na kiwanda cha mbao cha Fibreboard.

They are all either in ICU or dead completely.
 
Serekali imekamilisha zoezi la kuwalipa wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza magurudumu mwishoni mwa wiki.Mara baada ya serakali kumaliza zoezi la kulipa wafanyakazi mafao na madeni ilianza mara moja zoezi la usahili[interview] wa mamaeneja wote ambao serekali kupitia naibu katibu mkuu Dr Mjaka ilikiri managemant ilitafuna tsh 3.4 bilioni.

Serekali kupitia mkurugenzi wa viwanda Bibi Pallangyo imetoa ajira ya mwaka mmoja kwa Bwana L Mgoyo[Purchasing Manager],Bwana P Mwetta[Sales & Marketing Manager],Bwana TT Mnzava[Factory Manager},R Mangowi[Export Manager].Managers wote watakuwa wanalipwa tsh 1,200,000/= kwa mwezi kwa kukaa nyumbani.Wizara ya viwanda biashara na masoko pia imetoa ajira kwa wafanyakazi wengine kumi wa ngazi za chini kwa mshahara wa tsh 500,000/ kwa mwezi ambao pia hawatakuwa na kazi za kufanya zaidi ya kukaa nyumbani.

Jambo kubwa la kushangaza ni kwamba serekali kupitia naibu katibu mkuu Dr Mjaka ilisema wazi managemant ilihusika na manunuzi hewa ya malighafi na matumizi mengine mengi yalikoso viabatanisho.Mhusika mkuu wa manunuzi yote ya General Tyre ni Bwana Leornad Mgoyo,lakini serekali hiyo hiyo badala ya kumfikisha mahakamani inakuja kumpatia ajira kwa kazi ambazo haziko.

Bibi Pallangyo pia anahusika kuipatia kinyemela kampuni ya ulinzi ya Full Time Security inayomilikiwa na Prof Kapuya mkataba wa kulinda GTEA LTD bila kufuata taratibu.
 
General Tyre been dead and buried, what are you talking about "slow death"?
 
Wadau,

Nipo Arusha kwa mwezi sasa, but I could not believe when i saw what remains of what used to be GENERAL TYRE, nilipata kusikia CEO alikuwa raia wa Kenya, then kiwanda kikahujumiwa, mpaka kimefikia hapo, ninacho shindwa kuelewa, how can we let such a sabotage take place in our land,where was the national intelligence agency?

Hii inauma sana wadau, nasikia uchungu sana nikipita maeneo yale, sasa tunanunua YANA ya Kenya, tunakuza uchumi wao, pls any one with more info naomba, it hurts a lot guys!
 
Wadau,

Nipo Arusha kwa mwezi sasa, but I could not believe when i saw what remains of what used to be GENERAL TYRE, nilipata kusikia CEO alikuwa raia wa Kenya, then kiwanda kikahujumiwa, mpaka kimefikia hapo, ninacho shindwa kuelewa, how can we let such a sabotage take place in our land,where was the national intelligence agency?

Hii inauma sana wadau, nasikia uchungu sana nikipita maeneo yale, sasa tunanunua YANA ya Kenya, tunakuza uchumi wao, pls any one with more info naomba, it hurts a lot guys!

pole sana aisee.............ndio maana tupo hapa tunawapigia kelele hawa MAFISADI na majambazi CCM.........ipo siku!
 
Wadau, nipo arusha kwa mwezi sasa,but i couldnot believe when i saw what remains of what used to be GENERAL TYRE,niripata kusikia CEO alikuwa raia wa kenya,then kiwanda kikahujumiwa,mpaka kimefikia hapo,ninacho shindwa kuelewa,how can we let such a sabotage take place in our land,where was the national intelligence agency,?hii inauma sana wadau,nasikia uchungu sana nikipita maeneo yale,sasa tunanunua yana ya kenya,tunakuza uchumi wao,pls any one with more info naomba,it hurts a lot guys


Usalama wa Taifa wapo busy ndugu yangu hawawezi kuhangaika na masuala ya Viwanda nchini wakati unafahamu fika kwamba nchi hii ni ya vyama vingi hivyo kuna uwezekano watu wakawa wana mipango ya kukiangusha chama kilichopo madarakani. Lazima tuwekeze katika eneo hilo
 
Mbona umeuliza General Tyre tu? Hotel 77 je? Fiber boards, KILTEX na mengine kibao tumenyamaza tu.

Hii nchi inakera nadhani mwisho umekaribia
 
Do we have it at all? No!
Have you heard of MOSSAD? We need to learn from that one!

Yes we have them na kazi yao ni kudhibiti vyama vya upinzani.

Before learning to MOSSAD lazima kuichakachua kikamilifu hii tuliyonayo. Haina uwezo wowote wa ki-intelijensia, bora mara mia hata mgambo wa America (sherrif)
 
Lowasa/GM alitaka hiyo kiwanda so alichofanya ni kukifilisi kionekane kinarun kwa hasara ili baadae wakinunue na waendelee na business its so sad lakini CEO hakuwa mkenye nadhani ni mhindi mmoja hivi ambaye pia ameuza sana nyumba za Generaltyre na magari kauza sana tu then akaishia zake..
 
Tatizo ni katiba.....maana TISS hawajui wanatakiwa kufanya nini wala kuwajibika kwa nani..
 
Wadau, nipo arusha kwa mwezi sasa,but i couldnot believe when i saw what remains of what used to be GENERAL TYRE,niripata kusikia CEO alikuwa raia wa kenya,then kiwanda kikahujumiwa,mpaka kimefikia hapo,ninacho shindwa kuelewa,how can we let such a sabotage take place in our land,where was the national intelligence agency,?hii inauma sana wadau,nasikia uchungu sana nikipita maeneo yale,sasa tunanunua yana ya kenya,tunakuza uchumi wao,pls any one with more info naomba,it hurts a lot guys

Heshima kwako Juan Manuel,

Mkuu suala la General Tyre limeshajadiliwa kwa kirefu sana hapa jamvini kama sijakosea thread ilianzishwa na Morani 75 mwaka 2008.Binafsi nilitoa ufafanuzi usiokuwa na mashaka kwasababu niliwahi kufanyakazi pale idara ya Accounts.

Labda nikupatie nondo kwa ufupi sana kama utahitaji maelezo marefu na mapana tafuta hiyo thread ya Morani 75.

General Tyre (EA) Ltd ilianzishwa miaka 70s na Mwl JK Nyerere kufuatia ziara alioifanya nchini Marekani.Kiwanda kilikuwa kijengwe Dar lakini Mwl alikuwa na sera ya kuwekeza viwanda mikoa mbali mbali ya Tanzania bahati nzuri kiwanda kikajengwa Arusha.Marekani walijenga Tanzania kwakuwa walikuwa wanaigia kwenye teknolojia mpya ya tairi ilivyo mitambo ya zamani ililetwa Tanzania.

Serekali ya Tanzania ilikuwa na hisa ya asilimia 76 na General Tyre Amerika asilimia 24.General Tyre marekani walikuwa na wajibu wa kuhakikisha wanaleta technology hivyo Chief Executive Officer,Finance Manager na Factory manager ilikuwa ni lazima watoke Marekani,Tanzania ilikuwa na nafasi moja tu ngazi ya management nayi ni Human Resource Manager.Mwenyekiti wa Board ya wakurugenzi na wajumbe nadhani saba walikuwa watanzania.

General Tyre Amerika ilikumbwa na matatizo ya kifedha kwenye miaka ya 80s ililazimika kuuza viwanda vyake vyote duniani kwa continental ya ujerumani General Tyre Tanzania nayo haikusalimika ikaangukia mikononi mwa Continetal Ujerumani.

Continental ilimleta Chief Executive Officer wake Muhindi [Nepal] mwenye uraia wa marekani Bwana Devendrah Lohani bila kuuma uma maneno kaburi la General Tyre likawa limechimbwa.Lohani aliikuta General Tyre katika hali nzuri [Stock,Cash flow,Debtors & Assets] kwa kushirikiana na mwenyekiti wa bodi Bwana Shelukindo na baadhi ya managers wazalendo Assets ziliuzwa hovyo fedha zilizopatikana badala ya kusaidia kampuni zikawafaidisha zaidi manager hasa Lohani.Hali ya General Tyre kufikia mwaka 2004 ikawa mbaya kiasi cha kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi wake na madeni ya creditors yakawa yanazidi kila kukicha.

Mwaka 2005 CEO D Lohani kwa ushirikiano na Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba walifanikisha mpango wa mkopo wa us 10 milioni [Tsh 14.5 bilioni]kutoka NSSF kwaajili ya kumodernise kiwanda [ununuzi wa mashine za kisasa] na nusu ya fedha kulipa madeni ya benk zilizokuwa zikiidai General Tyre.Fedha zilipopatikana badala ya kununua mitambo mipya na ya kisasa zikaliwa mitambo ya zamani ikapakwa rangi.Muda wa kurejesha mkopo ulipofika General Tyre haikuwa na uwezo wa kurejesha hata senti moja mbaya zaidi haikuwa na sifa tena za kupata mkopo mwingine kutoka bank yoyote.
 
Wadau,

Nipo Arusha kwa mwezi sasa, but I could not believe when i saw what remains of what used to be GENERAL TYRE, nilipata kusikia CEO alikuwa raia wa Kenya, then kiwanda kikahujumiwa, mpaka kimefikia hapo, ninacho shindwa kuelewa, how can we let such a sabotage take place in our land,where was the national intelligence agency?

Hii inauma sana wadau, nasikia uchungu sana nikipita maeneo yale, sasa tunanunua YANA ya Kenya, tunakuza uchumi wao, pls any one with more info naomba, it hurts a lot guys!

Ukiona manyoya ujue keshaliwa huyo!!!
 
Mossad is responsible for intelligence collection and covert operations including targeted killings and paramilitary activities beyond Israel's borders, bringing Jews to Israel from countries where official Aliyah agencies are forbidden, and protecting Jewish communities worldwide.

Zimbabwe
The Mossad secretly evacuated Zimbabewan Jews out of the country due to fears of persecution by the Zimbabwean government, which was allied with the Palestine Liberation Organization and Libya. The Mossad infiltrated the Zimbabwean government's Central Intelligence Organization, in response to the supply of plutonium from the Congo via Zimbabwe to North Korea, Syria, and Iran
Intro hapa
What about TISS? Who is it protecting?
 
Back
Top Bottom