Gazeti la Uhuru ladai CHADEMA wananunua shahada za kupigia kura Igunga kwa noti feki

He, ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni. Uhuru wanajihisi ni gazeti credible na wanadhani watu watalichukulia serious?
 
I agree with you. This newspaper enjoys the same status as Tanzania Daima na Mtanzania or Rai. They are all propaganda tools!

Hapana hapana hapana napingana na wewe..... mimi sikubaliani na wewe kufananisha hii takataka na magazeti ambayo nayasoma na kuona ukweli ndani yake. Gazeti kumilikiwa na mwanachama yeyote wa chama cha siasa sio lazima liwe propaganda tool..... umepotoka!

Hata hivyo mie sijawahi kusoma Uhuru kwa miaka kama 20 hivi au hata zaidi........ Nawashangaa sana wanaolisoma gazeti hilo maana hata nikipita kwenye vibanda vya magazeti macho yangu hayaangalii hata vichwa vya habari kwenye gazeti hilo.. Poleni mnaosoma takataka hizo.
 
Yaani CCM wanajisahau mpaka wanaona kununua shahada ni biashara halali na kosa ni kutumia noti bandia tu!? Kweli magamba ni nouma!

Kwa CCM kununua shahada ni jambo la kawaida, kutumia noti bandia ndo jambo geni....
 
  • Thanks
Reactions: SMU
ha ha ha ha haaaaaa kweli nimeamini magamba wameshikwa pabaya igunga... its just a matter of time


RIP ccm
 
Hilo gazeti halisomwi na watu. Bora habari hiyo wangeiandika kwenye toilet paper kuliko kwenye gazeti hilo.
 
Habari nzuri sana hii, hawa si ndio waliosema kelele za mlango hazimkoseshi usingizi mwenye nyumba, mara oooh vyama vya upinzani ni vya msimu, vinaibuka tu wakati wa uchaguzi na bada ya hapo vinapotea, sasa wamekuwa suprised jinsi chadema wanavyowapeleka speed, toka uchaguzi wa 2010 mpaka leo non-stop. watatumia kila njia wawezayo ili kujaribu kuokoa jimbo ambalo hata hivyo hawatalipata, msisitizo wangu kwa wana igunga ni kulinda kura zao at any cost. Hebu onesheni mfano, chadema watakula jimbo mojamoja mpaka yaishe yote.
 
Hivi kwanini Uhuru wasitafute Waandishi wa habari waliandikie habari! Hivi kuna mtu anayeweza kukubaliana na ujinga kama huu! Hivi kununua shahada kwa noti bandia ni kujijenga au kujibomoa! Lakini kwakuwa wanatumia Masaburi kufikiri ndio maana wanaweza kufikiri kwamba wanaweza kuuza ujinga wao na ukakubalika na watu.

Ni gazeti takataka

Magamba yanajilainisha ili yatoke vizuri
 
Kwanza tujiulize gazeti hilo ni la nani ? jibu ni la Ccm. Hao wanajaribu kuwachanganya watu akili, kampeni ya uchaguzi Igunga
iendelee kwa kuwaelimisha watu zaidi na zaidi kuhusu madhara ya Ccm na vyama pandikizi vya Ccm. Habari za gazeti uhuru ni
za kuzipuuza, na kuelekeza mawazo bora zaidi kwa wananchi na mpaka kwa wale wa vijijini na kwa njia mnayoitumia CDM
kuwaelimisha kwa lugha ya kisukuma mpaka na vikongwe sasa hivi wanatambua kama ni nani anayesabisha wao na watanzania
wote kuwa maskini wa kutupwa, ilo ni jambo zuri sana na lisilokuwa na mfano wake kwa CDM. Na mashambulizi yaendelee
nchi nzima ya aina yake mpaka kieleweka na ukombozi hupo jirani sana, kwani dhairi uwezo wa kuongoza nchi chini ya CDM ni
mkubwa sana na wa kuleta maendeleo kwa haraka. Hilo gazeti la uhuru bado lipo kwenye propaganda za Lenin ambazo
zimeshapitwa na wakati za kuwaacha watanzania wanakula ngumi.
 
Gazeti la chama tawala CCM la Uhuru la leo 20/09/2011 limeandika kuwa CHADEMA wanatumia noti bandia kununua shahada za kupigia kura toka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali huko Igunga.

Isije ikawa ni ku-counter yale yaliyowapata CCM kwa mabalozi na makada wao kukamatwa na wakiorodhesha najina na namba za shahada ili kuwarubuni wapiga kura na hatimae kushinda kimazingaombwe kama walivyozoea.
Ni heri CCM wanatumia pesa halali!
 
Gazeti la chama tawala CCM la Uhuru la leo 20/09/2011 limeandika kuwa CHADEMA wanatumia noti bandia kununua shahada za kupigia kura toka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali huko Igunga.<br />
<br />
Isije ikawa ni ku-counter yale yaliyowapata CCM kwa mabalozi na makada wao kukamatwa na wakiorodhesha najina na namba za shahada ili kuwarubuni wapiga kura na hatimae kushinda kimazingaombwe kama walivyozoea.
<br />
<br />
pambafu zao magamba,mbinu za kitoto kabisa, bahati yao jeshi la polisi mali yao..
 
gazeti la chama tawala ccm la uhuru la leo 20/09/2011 limeandika kuwa chadema wanatumia noti bandia kununua shahada za kupigia kura toka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali huko igunga.

Isije ikawa ni ku-counter yale yaliyowapata ccm kwa mabalozi na makada wao kukamatwa na wakiorodhesha najina na namba za shahada ili kuwarubuni wapiga kura na hatimae kushinda kimazingaombwe kama walivyozoea.


hili gazeti huwa linatolewa nakala moja tu likisha somwa redioni wanalirudisha ku-recycle
 
Hilo gazeti linaandikwa na wehu,nadhani noti bandia ndo swala tete kuliko hilo la kununua shahada kwani ccm wamawazoesha watanzania wenye njaa zao kufanya hivyo
 
Hilo gazeti hata kama lingekuwa linatolewa bure kama vile vjarida vya duka la game nsingelisoma.. Na kama unataka kupata degedege ya ukubwani soma hilo gazeti.
 
UHURU.....duuuh hivi kuna watu bado wanasoma hilo gazeti????
Vidingi vevyewe nna wasiwasi kama bado vinasoma hiyo takataka. Halina hadhi hata ya kufungia maandaz labda kujisafishia nnya kwa wale wanaojihelp vichakani
 
Sasa polisi na usalama wa Taifa wanafanya nini Igunga kama kuna noti feki mtaani? Hii inaonyesha kuwa polisi hawajui kufanya shughuli zao wakati CCM ina ushahidi kuwa kuna noti feki zinatumiwa na CHADEMA.
CCM wanaweza kufukiri kuwa hapa wanawapiga bao Chadema lakini hawajui wanajipiga bao wenyewe kwa kudhalilisha taasisi inayoendeshwa na serikali inayotokana na chama chake. Chama kinajua kuwa kuna noti feki Igunga lakini taasisi inayosimamia ulinzi na usalama haina taarifa hiyo. Uzoba mwingine hapa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom