Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Viongozi Waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wapo katika maandalizi ya kufanya Ziara kabla ya mwishoni mwa mwaka huu 2018 kwenda katika Nchi za Ulaya zikiwemo Ujerumani na Scandinavia, pamoja na Marekani, ikiwemo Bunge la Congress kwa lengo la kuomba msaada dhidi ya masuala ya kisiasa na hali yao dhidi ya Serikali.
Viongozi hao wanakwenda kudai kuwa, wanaonewa, hawana haki dhidi ya Nchi yao, wananchi na wabunge wao. Vilevile, watalalamikia juu ya Ukanda Imani was demokrasia ndani ya Nchi. Aidha, watalalamikia juu ya vitisho na usalama wa uongozi wao, nafasi zao na mwenendo wa uchaguzi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Je, CHADEMA wakienda huko watapata nafasi ya kuongea kwenye Bunge la Congress? Endapo wataipata hiyo nafasi, nini athari zake kwa Siasa za Tanzania hasa kuelekea 2020. Je, Marekani atataka kutulima tena kwenye misaada? Je, unadhani Magufuli anaweza kuogopa ghadhabu za Marekani, Ujerumani na Scandinavia (Norway, Sweden, Finland, Denmark na Iceland)? Je, Norway (Statoil/Equinor) na Nchi nyingine yanakotokea Makampuni ya gesi, wanatuvizia baada ya mwenendo wa kobe katika makubaliano ya kujenga LNG nchini?