Gazeti la Nipashe lifungiwe baada ya Serikali kuchunguza habari hii

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,837
Gazeti la Nipashe liliandika kwa kichwa cha habari kikubwa kuwa Watoto wafundishwa kulawitiana shuleni

Watu wengi walishtuka lakini mimi Nilishikwa na wasiwasi kuhusu ukweli wa hii habari hasa ukizingatia gazeti hili lilikuwa nalijua kwa kuandika habari kwa mtindo wa "sensationalism", kwa wasiojua maana ni kuandika kichwa cha habari kwa lengo la kuleta mshtuko ambao hauendani na ukweli wa habari yenyewe ili kuvutia wasomaji kununua gazeti au kubonyeza "link"

Ila nikanunua gazeti lenyewe ili kuona ipoje, kama wasiwasi wangu ulivyonituma nikakuta ni sensationalism Ile ile

Habari yenyewe inaelezwa kuwa ni mzazi alikuwa akimsimulia mwandishi kuwa alimuona mtoto wake akifundishana na mtoto wa jirani vitendo vya kulawitiana, mzazi huyo akashtuka na kumbana mtoto huyo amuelezee alijuaje hayo mambo, ndio mtoto akamsimulia kuwa wanafundishwa shuleni
Na shuleni wanafundishwa jinsi ya kutumia vilainishi na ili wasiumizane na wanafunzi wakubwa wa darasa la saba ndio huwalawiti wanafunzi wa madarasa ya chini

Sasa hii ni habari yenye chain ndefu ya kusimuliana ambayo inaifanya kuwa na uwezekano mkubwa kuwa ya uwongo au ya kutiwa chumvi,

Yaani mtu A (mtoto) alimsimulia mtu B (mzazi) kisha mzazi ndio akasimulia mtu C (mwandishi)

Swali langu ni je, kwa nini mwandishi baada ya kupata tip ya habari kubwa na ya kushtua hivyo kwa nini asingefanya uchunguzi, kwa kuhoji wanafunzi wengine kadhaa wa shule hiyo au hata kutuma undercover (jasusi) shuleni hapo ili kupata ukweli wenyewe?

Mbona ilikuwa kazi rahisi sana, badala yake ni kukimbilia kuandika tu ili kuuza gazeti..

Haya ndio maadili ya waandishi wetu?

Nasubiri majibu ya serikali, natumaini hayatamaliza mwezi
 
Gazeti la Nipashe liliandika kwa kichwa cha habari kikubwa kuwa Watoto wafundishwa kulawitiana shuleni

Mbona ilikuwa kazi rahisi sana, badala yake ni kukimbilia kuandika tu ili kuuza gazeti..

Haya ndio maadili ya waandishi wetu?

Nasubiri majibu ya serikali, natumaini hayatamaliza mwezi
Haya endelea kusubiri majibu ya serikali.
P
 
Subiri nikiingia desktop nitajutumia clip ya watoto wa primary wanashitakiana wanavyo lawitiàna. Hapa sitaweka nitakutumià inbox
 
sijui, ngja niitoe kwenye simu niiweka hapa inbox for the few selected
Watoto wanakaa na watu wengi ambao wanaweza kuwafundisha huo ujinga, au wametazama kwenye simu za wazazi wao video za porn

Sasa gazeti kukurupuka moja kwa moja bila uchunguzi na kusema wanafundishwa shuleni sio sawa
 
Habari yenyewe inaelezwa kuwa ni mzazi alikuwa akimsimulia mwandishi kuwa alimuona mtoto wake akifundishana na mtoto wa jirani vitendo vya kulawitiana, mzazi huyo akashtuka na kumbana mtoto huyo amuelezee alijuaje hayo mambo, ndio mtoto akamsimulia kuwa wanafundishwa shuleni
Na shuleni wanafundishwa jinsi ya kutumia vilainishi na ili wasiumizane na wanafunzi wakubwa wa darasa la saba ndio huwalawiti wanafunzi wa madarasa ya chini
Mbona hata BBC waliitoa hii habari
 
Ulitaka Nipashe wakuwekee picha watoto wanavyopakana vilainishi?

Nipashe wameweka mhitasari tu ni jukumu ya la serikali kufuatilia Kwa undani...

Jana Tu serikali imetangaza kufuatilia vitabu vya msaada vinavyopotosha maadili ya kifamilia...

Serikali inajua Sana huu upuuzi sema ile misaada tunayopewa inaambatana na mashariti ya kutokemea haya mambo.
 
Soma hoja yote,usikurupuke

Gazeti kuandika habari ya kushtua kwa maneno ya kusikia kutoka kwa mtoto ni ukosefu mkubwa wa weledi
 
Hata Mimi nimeifatilia hiyo habari lakini haikuwa kama kichwa cha habari kilivyo. Kiki ni kubwa ila habari yenyewe inaonekana haijanyooka sana
 
Back
Top Bottom