Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

Tunashangaa nini ni jambo lililotegemewa gazeti limejiachia uhuru kupita kiasi hayo ndio matokeo yake.
 
halafu kuna bandiko moja walilituma hapa usiku wa manane eebwana lilikuwa babu kubwa cha ajabu sasa uzi umewekwa wametoa mpaka picha ya Ramadhani ighondi anayehusika na utekaji wa ulimboka mpaka namba za simu za wote waliohusika na mida waliyokuwa wanapigiana lilikua noma aisee sema MODS walijua ule ni utata wakalitoa fasta ila nilibahatika na mimi kulipitia usiku huo na kucoment asbh likawa ukituma comment unaambiwa huna access na hii makitu. duh ial kubenea ni noma aisee.

Duuh, gfsonwin, JF noma! Yaani ukijifanya hawakujui utajulikana mpaka ushangae na roho yako,lol!
 
Last edited by a moderator:
wewe ndio mwenye chuki na uislam kama umekasirika nenda mahakamani kama walivyofanya TCRA.

sio kila mtu mwenye kichwa kikubwa kama wewe ana akili wengine kumejaa au maji au kamasi tu!! mimi kusema redio inachochea uhasama wa kidini nina chuki na uslamu??wewe kanusha kwa point kuwa redio Imani haichagizi harakati za udini na kuutukana ukristo! umesikia wapi redio au gazeti la kikristo likiutaja uislamu? nitajie moja!!
 
limefungiwa kwa mda usiojulikana? mmh! kubenea afanye mpango wa kusajili jingine.
 
Kubenea hana ukweli wowote, yeye ni mchonganishi na mzushi, na kama uko karibu nae mwambie hivyo hivyo na wananchi wanajua hivyo

Uzuri kila mwananchi anaamua anavyojua yeye. Kuanza kusema watu wengine hapa inawezekana tukawa tunajisemea wenyewe.
 
Si kweli, kuandika ukweli kuhusu yaliyomsibu Dr Ulimboka si kuipeleka nchi pabaya. Hii Serikali dhalimu ambayo sasa imeamua kufanya mauaji dhidi ya raia wake kwa kudai kuboreshwa kwa ujira wao na pia mazingira ya kazi ndio inaipeleka nchi pabaya.

Watanzania tumuogope sana mtu anaechochea chuki na fitna katika nchi yetu.ni hatari sana kwa ustawi wa jamii iliyostaarabika.mwanahalisi ilikuwa inaipeleka nchi kubaya.
 
Kufungia gazeti hakuisaidii serikali hii dhalimu ambayo inafanya madudu na ufisadi wa kutisha huku wananchi wakibaki na umaskini wa kutupwa,mapambano yanaendelea na kwa sasa kuna njia nyingi tu za kufikisha ujumbe kwa wananchi na wakaelewa serikali yao inavyoboronga.
 
Mungu ibariki tanzania,mungu lisambaratishe mwanahalisi na wafuasi wake wanaopandikiza na kueneza chuki na uongo mioyoni mwa watanzania.aaaimen
 
Iliwishajulikana pindi data zikitolewa kuna mtu atasema gazeti lifungiwe.

Serikali lazima ikubali kwamba kwa sasa "investigatve journalism" ndio inashika kasi na zile zama za "chequebook journalism" kama alivyowahi kusema mzee John Malecela zimepitwa na wakati.

Uandishi wa habari za uchunguzi unachukua muda na unahitaji mambo muhimu wakiwemo vyanzo vya habari husika na uadilifu wa hali ya juu. Pia ni katika kutimiza maadili ya uandishi kwamba jamii inapashwa habari, inaburudishwa na inamulikwa.

Sasa mpiganaji Kubenea na gazeti lake wamekosa nini kumulika suala la Dr Ulimboka?

Uvivu wa kufikiri wa baadhi ya watanzania ndio unavyofanya jambo la Dr Ulimboka liende taratibu na mpiganaji Kubenea anajaribu kuaninisha wazi mambo yaliyotokea ambayo yanahusiana na ukandamizaji.
 
Kuna tetesi kuwa gazeti lililoko mstari wa mbele kufichua maovu mbalimbali ya serikali, na ambalo kwa sasa lililoshikia bango kufichua njama na mbinu za watesi wa Dr. Ulimboka, sasa huenda likafungiwa.
Hii ni baada ya kutaja kuwa kinara wa idara ya usalama wa taifa ndio aliye ratibu na kusuka njama za utesi huo.
Pia Mwanahalisi lilichapisha namba za simu na majina ya maafisa usalama waliohusika na mateso na utekaji wa Dr. Ulimboka
 
Back
Top Bottom