Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

CHANZO: TBC1

Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.

Bora hata limefungiwa, linataka kulitumbukiza Taifa katika machafuko hili gazeti, mbona Magazeti mrngine hayafungiwi?
 
Haya sasa nategemea serikali imuajiri kubenea aongoze tiss kwa kuwa ameweza kugundua vitu ambavyo usalama wa taifa wameshindwa kuvigundua, gazeti letu tunaliamini tunalikubali, tunalisubiri
 
Safi sana.ni hatua nzuri na mhm tuliyokuwa tunaitegemea japo imechelewa sana
 
Kwa hili serikali haiwezi tena kudai kuwa inafuata utawala wa demokrasia na sheria. Kama wana-dispute habari yoyote iliyoandikwa kwenye gazeti la mwanahalisi kwa nini wasiende mahakamani? Ni nani anayeamua habari fulani ni ya uchochezi au la? Nini maana ya uchochezi? Na watanzania wana akili na utashi wa kujua uchochezi au mpaka serikali iwatafunie habari? Hii inaharibu credibility ya serikali.
 
Serikari Dhaifu inafungia magazeti haiwezi kuwakamata na kuwapeleka kotini wabunge wala rushwa na wahujumu na wafanyabiashara ya mafuta wanao honga wabunge wamtimue waziri na katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Haisaaidi kulifungia mwanahalisi wangemfukuza kazi Afande kova alie amua kuwadanganya watanzania kama hawana akili, Hii ni aibu nyingine kwa ccm
 
Mwamelifungia Mwanahalisi na siyo Kubenea.....Aluta continue......Mumefungia chombo huru kilichofanya uchunguzi ambao umefunika tume ya kova
 
[h=6]Gazeti la mwanahalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana kutokana na habari zake za uchochez.
Source:dira ya mchana tbc1![/h]
 
Machafuko kamwe hayatasababishwa na Mwanahalisi bali hii Serikali dhalimu ndiyo channzo cha machafuko yote nchini. Kwa kutoshughlikia ufisadi unaoimaliza nchi na pia kuwadhulumu wafanyakazi katika sekta mbali mbali nchini ujira ambao wanastahili.

Bora hata limefungiwa, linataka kulitumbukiza Taifa katika machafuko hili gazeti, mbona Magazeti mrngine hayafungiwi?
 
Magazeti mengine yaanzie hapo mwanahalisi lilipoishia,tunataka magazeti yaandelee kuandika ukweli....yakifungiwa yote then safari ya kwenda magogoni itakuwa imekamilika
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom