Gavana wa Benki Kuu kukimbia maswali ya waandishi kunatoa tafsiri gani?

Yaani kodi na uchumi hazina uhusiano? Kama anajua kodi tu na yeye ni Gavana wa Benki kuu basi ni kilaza mtupu, ataangamiza uchumi na hiyo benki yanyewe inaopumulia oxgen ya ICU
Ni mtaalamu wa sheria ya kodi na siyo kodi. Ndo madhara ya kutoheshimu taaluma. Huwezi mchukua mwanasheria akawa gavana wa benki kuu.
 
yaaani prof.mzima anakimbia wanahabari dah...hii kali ya mwaka ila msukuma hakukosea kabisa kuna prof.wengi ni vimeo,,bora darasa la saba anaeza kuelezea jambo akaeweka

You know what? Hawa ndo Mapro-FEDHA wa Magufuli. Kichwani hakuna kitu wanachosubiri ni MAELEKEZO YA JIWE ndiyo watoe matamko au kujibu hoja za Media.

Kinachoonekana hapa ni kwamba huyu Gavana aliogopa kujibu Maswali ya Wana-media kwa hofu kwamba katika maswali hayo angeliweza KUJICHANGANYA na kujibu ukweli na uhalisia wa HALI YA DOLARI na UCHUMI wa nchi kitu ambacho JIWE HATAKI KUKISIKIA na matokeo yake ungelisikia leo GAVANA KATUMBULIWA...!!!
 
Sasa kulikuwa na haja gani kuitisha press conference kama uliowaita hawaruhusiwi kupata ufafanuzi wa ulichokisema?!
Si angekwenda tu studio za TBC akasoma taarifa yake?!
Kawapotezea tu waandishi wa habari muda wao.
 
Hahahaaa nimecheka sana hiyo clip sijaiona ila najaribu kujenga picha jinsi alivyoyeya huku waandishi wakimsindikiza na vimaneno chinichini.

Waandishi wengine kimykimya wakisema" huyu nae boya tu"
nimeitafuta hyo clip mpaka sasa sijaipata sjui iko wapi
 
Hahahaha! gavana karara mbere, waandishi nao walikuja na majibu yao mfukoni gavana ni msomi kawasoma akaona isiwe tabu. au alijisahau akajua yeye ni Gavana wa County maswli ya fweza yatamzingua akala kona ile anafika oficn anajikuta ye ndo gavana wa hela.
Usomi au ujuha mtupu.Uproff Tz ni sawa na comedian
 
Mkuu waandishi wa habari wanatisha wewe!! Ndio wanaokukuza au kukuangusha. Unapaswa kuwa makini ukikutana nao. Huenda hili lionakosekana kwa profesori.
 
Bruh yu a dem genius....man from Jamaica, nah Babylon system, man yu a fire.....burn dem in de name of jah rastafarai, de most high
Kuna msemo maarufu wa kilatini unasema “horror vacui”. Aristotle ndiye anayetajwa kuusema awali.

Kiingereza wanasema "nature abhors a vacuum". Asili haipendi ombwe.

Yani ukiondoa hewa kwenye chombo, ubaki na ombwe,ukiachia hicho chombo wazi kitajaa kitu tu, kama si hewa basi maji, chochote kilicho karibu kitachukua nafasi ya ombwe.

Katika "Information Theory" napo kuna kitu kama hicho. Habari ya kweli isipotolewa, kukawa kuna ombwe la habari, kila mwenye kuweza kujitungia habari yake, atajitungia na kuisambaza.

Ndiyo maana wenzetu walioendelea katika mambo ya habari, wanafanya press conferences zinajibu maswali kirefu.

Wanatoa version yao ya habari, iwe ya uongo au ukweli hilo ni jambo lingine.

Ukikataa kujibu maswali ya waandishi na wananchi, maana yake umekataa kuelezea version yako ya mambo, ukikataa kuelezea version yako ya mambo, umekubali version yoyote nyingine isambae.

Gavana, kwa kukataa kujibu maswali, ameacha maswali yale yaendelee kuwepo na kujibiwa kwa speculations zozote zitakazoendelea kuwepo.
 
Taarifa ya msomi,wakili,Gavana wa benki Kuu juu ya operation ya kudhibiti maduka ya fedha za kigeni kwa kutumia jeshi imeacha maswali mengi na madhara makubwa kwa uchumi wetu.Hata IDD Amin alianza hivi kidogokidogo akawa anakibalika na vikundi vya watu wachache wenye maslahi.
Taarifa ya BOT ya kurasa NNE imeshindwa kujibu maswali kama ifuatavyo, kama ni operation ya sita hizo tano za awali ni maduka mangapi likiuka masharti na kufungwa au watendaji wangapi walikamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani?. Je tangu lini vitengo vya ukaguzi na uchunguzi vikafanya kazi chini ya ulinzi wa jeshi au polisi maana ukagizi ni goal,objective oriented or terms of references set na unachukua muda with scope set.
 
Hivi profesa si mtu aliyebobea? Sasa anawakimbia wanafunzi wake tena? Bombii nyumbii vipi wa kunyumbi?
 
Magu anawaweka wasaidizi wake katika wakati mgumu sana. Msomi nguli unaonekana kama hujawahi kalia kiti cha darasani. Duuuh!
 
Kuna msemo maarufu wa kilatini unasema “horror vacui”. Aristotle ndiye anayetajwa kuusema awali.

Kiingereza wanasema "nature abhors a vacuum". Asili haipendi ombwe.

Yani ukiondoa hewa kwenye chombo, ubaki na ombwe,ukiachia hicho chombo wazi kitajaa kitu tu, kama si hewa basi maji, chochote kilicho karibu kitachukua nafasi ya ombwe.

Katika "Information Theory" napo kuna kitu kama hicho. Habari ya kweli isipotolewa, kukawa kuna ombwe la habari, kila mwenye kuweza kujitungia habari yake, atajitungia na kuisambaza.

Ndiyo maana wenzetu walioendelea katika mambo ya habari, wanafanya press conferences zinajibu maswali kirefu.

Wanatoa version yao ya habari, iwe ya uongo au ukweli hilo ni jambo lingine.

Ukikataa kujibu maswali ya waandishi na wananchi, maana yake umekataa kuelezea version yako ya mambo, ukikataa kuelezea version yako ya mambo, umekubali version yoyote nyingine isambae.

Gavana, kwa kukataa kujibu maswali, ameacha maswali yale yaendelee kuwepo na kujibiwa kwa speculations zozote zitakazoendelea kuwepo.
Huku ukihoji sana mwisho wake unaambiwa umetumwa maana mtu anakosa jibu la kushawishi anaishia kusema umetumwa ama unaambiwa sio mzalendo...btw nimependa nondo zako natamani kama wangekuwa wanasoma japokuwa wanajua wanapaswa kufanya nini tatizo tu kile wanachofanya hakipo kwenye mpango kazi wao ama wamepewa amri na mamlaka za juu na hawajapewa nafasi ya kukiangalia kwa jicho la undani kabla ya kukifanya hivyo wanaitisha press conference kama formalities kuonyesha serikali huwa inatoa taarifa kwa waandishi wa habari
 
Mheshimiwa Lissu aliwahi kuita taarifa fulani iliyoandaliwa na maprofesa kumfurahisha mkuu wa nchi "Professorial rubish". Sasa sijui kama sababu ni haya yanayotokea sasa. Wataalamu wameweka taaluma pembeni, wapo kukidhi matakwa ya watawala
 
Back
Top Bottom