Wanahabari wadai kudhalilishwa na Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa mambo ya Nje. Mobeto na Shilole wapewa nafasi za Waandishi

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Kwa miaka 19 ya uzoefu kwenye uandishi wa habari leo (Julai 17,2023), nimekutana na jambo ambalo nisipopaza sauti nitakuwa sijaitendea haki taaluma yangu, nafasi yangu kama kiongozi wa taasisi ya habari ya MISA TANZANIA, Mhariri na mwandishi wa habari wa muda mrefu.

Leo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilialika wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kwenye mkutano wa Waziri, Dk. Stergomena Tax, tuliitika wito kwa kufika kwenye ukumbi wa Mwalimu JNCC saa nne kamili, lakini bahati mbaya alifika baada ya saa tano unusu, alituomba radhi kwa kuchelewa kutokana na majukumu mengi aliyonayo.Hili halikuwa tatizo.

Lengo la mkutano ni waandishi wa habari kuujulisha umma kuhusu ujio wa Rais wa Hungary, Katalin Novak mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki kuhusu raslimali watu utakaofanyika nchini Julai 25 na 26, mwaka huu.

Kilichonishtua na kunisukuma kuandika haya ni muda mfupi kabla ya kiongozi huyo kufika alitokea Ofisa mmoja aliomba wahariri na waandishi kukaa nafasi za mbele kwa kuwa Waziri amekaribia kufika, tulitii wito na kwenda kukaa mbele.

Muda mfupi tuliona idadi wasanii kadhaa kama kumi wakiingia kwenye chumba hicho, haraka ofisa mmoja alitufuata kututaka tupishe nafasi hizo kwa kuwa zilikuwa maalum kwa ajili ya wageni ‘maalum’ wa Waziri,tulipisha.

Kilichoshangaza ni kwamba wote tuliitwa kama waandishi wa habari na wale wageni maalum walitambulishwa kama waandishi wa ‘kisasa’ nasi tulitambulishwa kama waandishi wa ‘zamani’, na walipewa nafasi maalum kwa ajili ya kumsikiliza waziri na kuuliza maswali pamoja nasi wa ‘zamani’ kuuliza maswali.

Taaluma hii inatambuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, 2016 na huwezi kufanya majukumu ya habari kama hujasoma kwa kiwango cha Diploma, lakini leo hii wasanii na influencer wanaitwa kwenye mkutano wa waandishi na kutambuliwa kama waandishi wa ‘kisasa’ na wale waandishi wenye taaluma yao wanapaswa kupisha ‘wageni maalum’ ‘waandishi wa kisasa’

Ni muhimu kuandika haya ili Serikali, Wizara na Taasisi nyingine zikajua tofauti kati ya mwandishi wa habari na mtu mwenye wafuatiliaji wengi kwenye mitandao ya kijamii aliyeamua kutumia ukurasa wake kwa madhumuni tofauti, haipendezi kabisa kuishusha hadhi taaluma yetu kiasi hiki, tena kwa Wizara yenye watu ambao wamewahi kufanyakazi ya uandishi wa habari sio kwa ‘kujipenyeza’ tu bali kwa kusoma darasani kwa ngazi tofauti tofauti.

Tabia hii ikiachwa hivi maana yake leo ni kuruhusu kuendelea kuitukanisha na kuidharaulisha taaluma ya habari nchini, ambayo inaonekana kila mtu anaweza kufanya, HILI HALIKUBALIKI.

Napendekeza Serikali ambayo ndiyo inayosimamia wa sheria iliyotungwa na Bunge, ilinde sheria kwa wivu mkubwa, pia lazima kutofautisha mkutano wa waandishi wa habari na mkutano wa wasanii na influencer.

Mara kadhaa waandishi wa habari wamekuwa wakitupiwa lawama ya kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwasababu baadhi ya watu wanshindwa kutofautisha na kuona wote ni waandishi wa habari, na kama hili linaanza kufanywa na mamlaka maana yake ni kuhalalisha ‘kusigina’ Sheria iliyopitishwa na Bunge.

Salome Kitomari-Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Mhariri na Mwandishi wa Habari.
 
Kwa miaka 19 ya uzoefu kwenye uandishi wa habari leo (Julai 17,2023), nimekutana na jambo ambalo nisipopaza sauti nitakuwa sijaitendea haki taaluma yangu....
Waandishi wa habari mmejitakia wenyewe Kwa yanayotokea Kwa kuwa mmeendekeza 'uchawa'...mlichofanyiwa na wizara hiyo ni 'sahihi' kwani 'mmejidharaaulisha wenyewe..
 
Kwa miaka 19 ya uzoefu kwenye uandishi wa habari leo (Julai 17,2023), nimekutana na jambo ambalo nisipopaza sauti nitakuwa sijaitendea haki taaluma yangu, nafasi yangu kama kiongozi wa taasisi ya habari ya MISA TANZANIA, Mhariri na mwandishi wa habari wa muda mrefu...
Nawajua waandishi wa enzi za Rai Nguvu ya Hoja, Raia Mwema, Mawio, Mwanahalisi n.k enzi hizo kabla hayajachakachuliwa. Kwa sasa bongo hakuna waandishi wa habari kuna machawa so walicho wafanyia ni haki yenu tena wangewapiga na virungu
 
Wizara ‘isidhalilishe’ taaluma ya habari

Kwa miaka 19 ya uzoefu kwenye uandishi wa habari leo (Julai 17,2023), nimekutana na jambo ambalo nisipopaza sauti nitakuwa sijaitendea haki taaluma yangu, nafasi yangu kama kiongozi wa taasisi ya habari ya MISA TANZANIA, Mhariri na mwandishi wa habari wa muda mrefu.

Leo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilialika wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kwenye mkutano wa Waziri, Dk. Stergomena Tax, tuliitika wito kwa kufika kwenye ukumbi wa Mwalimu JNCC saa nne kamili, lakini bahati mbaya alifika baada ya saa tano unusu, alituomba radhi kwa kuchelewa kutokana na majukumu mengi aliyonayo.Hili halikuwa tatizo.

Lengo la mkutano ni waandishi wa habari kuujulisha umma kuhusu ujio wa Rais wa Hungary, Katalin Novak mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki kuhusu raslimali watu utakaofanyika nchini Julai 25 na 26, mwaka huu.

Kilichonishtua na kunisukuma kuandika haya ni muda mfupi kabla ya kiongozi huyo kufika alitokea Ofisa mmoja aliomba wahariri na waandishi kukaa nafasi za mbele kwa kuwa Waziri amekaribia kufika, tulitii wito na kwenda kukaa mbele.

Muda mfupi tuliona idadi wasanii kadhaa kama kumi wakiingia kwenye chumba hicho, haraka ofisa mmoja alitufuata kututaka tupishe nafasi hizo kwa kuwa zilikuwa maalum kwa ajili ya wageni ‘maalum’ wa Waziri,tulipisha.

Kilichoshangaza ni kwamba wote tuliitwa kama waandishi wa habari na wale wageni maalum walitambulishwa kama waandishi wa ‘kisasa’ nasi tulitambulishwa kama waandishi wa ‘zamani’, na walipewa nafasi maalum kwa ajili ya kumsikiliza waziri na kuuliza maswali pamoja nasi wa ‘zamani’ kuuliza maswali.

Taaluma hii inatambuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, 2016 na huwezi kufanya majukumu ya habari kama hujasoma kwa kiwango cha Diploma, lakini leo hii wasanii na influencer wanaitwa kwenye mkutano wa waandishi na kutambuliwa kama waandishi wa ‘kisasa’ na wale waandishi wenye taaluma yao wanapaswa kupisha ‘wageni maalum’ ‘waandishi wa kisasa’

Ni muhimu kuandika haya ili Serikali, Wizara na Taasisi nyingine zikajua tofauti kati ya mwandishi wa habari na mtu mwenye wafuatiliaji wengi kwenye mitandao ya kijamii aliyeamua kutumia ukurasa wake kwa madhumuni tofauti, haipendezi kabisa kuishusha hadhi taaluma yetu kiasi hiki, tena kwa Wizara yenye watu ambao wamewahi kufanyakazi ya uandishi wa habari sio kwa ‘kujipenyeza’ tu bali kwa kusoma darasani kwa ngazi tofauti tofauti.

Tabia hii ikiachwa hivi maana yake leo ni kuruhusu kuendelea kuitukanisha na kuidharaulisha taaluma ya habari nchini, ambayo inaonekana kila mtu anaweza kufanya, HILI HALIKUBALIKI.

Napendekeza Serikali ambayo ndiyo inayosimamia wa sheria iliyotungwa na Bunge, ilinde sheria kwa wivu mkubwa, pia lazima kutofautisha mkutano wa waandishi wa habari na mkutano wa wasanii na influencer.

Mara kadhaa waandishi wa habari wamekuwa wakitupiwa lawama ya kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwasababu baadhi ya watu wanshindwa kutofautisha na kuona wote ni waandishi wa habari, na kama hili linaanza kufanywa na mamlaka maana yake ni kuhalalisha ‘kusigina’ Sheria iliyopitishwa na Bunge.

Salome Kitomari-Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Mhariri na Mwandishi wa Habari.
 
Kwa miaka 19 ya uzoefu kwenye uandishi wa habari leo (Julai 17,2023), nimekutana na jambo ambalo nisipopaza sauti nitakuwa sijaitendea haki taaluma yangu, nafasi yangu kama kiongozi wa taasisi ya Habari.
Nimekulewa vizuri sana,Asante kwa ufafanu.Juzi Dr slaa alipowashukia wana Habari nilijiliza maswali mengi bila majibu leo umenifungua macho,vizuri jamii ikatofautisha machawa na waandishi wa Habari sio kila anayeandioa Habari ni mwandishi wa Habari.
 
Pole sana, lkn huu ndio uhalisia utakao takiwa kuukubali na kuuishi kuanzia leo na Milele. Hifadhi hii comment yangu. Iko hivi,

1. Kwanza pingezi, kila ninapokuta post yako naona taaluma, weledi, uzalendo viko pamoja.

2. Umetumia taalumu yako kuitendea haki tasnia ya habari,

3. Unachokifanya hakina mlaji katika jamii pana. Wanasiasa na viongozi wetu wa kileo wanahitaji jamii pana. Sasa Lulu na Shilole wakipost jambo katika dk 5 limeonwa na watu 100,000. Wewe ukipost katika siku 2 limeonwa na watu 1000. Unadhani mwanasiasa ataona nani wa maana kati yako na Lulu?

4. Mabadiliko ya kidemografia, kuongezeka na kupanuka kwa vionjo vya binadamu. Kula page unapita unapata vyote. Umbea, ngono, habari, etc hapo utawakuta wengi.

Ushauri. Miaka mi5 ijayo taifa litakuwa la kijinga. Andikeni ujinga mtapata kuheshimika
 
Waandishi wa habari lazima mdharaulike maana mmezidi kujikomba. Kila mara mnapewa kuandika mambo ya kuipamba serikali na bado mnajichekesha tu.

Na sasa vyombo vyenu vimepoteza mvuto, na hao waliowapotezea mvuto ndio hao wanawakejeli kwa kuwaita waandishi wa kizamani.
 
Back
Top Bottom