Gari za umeme pasua kichwa gharama za uendeshaji

Habari wapendwa. Ni wazi dunia inapigana kuhakikisha gari za umeme ndio zinatawala kwa hoja ya kuwa rafiki na mazingira. Licha ya yote bado hizi gari ni changamoto hasa inapopata damage.
Tuchukue mfano kesi ya hivi karibuni huko Vancouver, mmiliki wa Hyundai Ioniq 5 ya mwaka 2022 alipata ajali iliyopelekea cover plate ya battery pack kubonyea na kuharibu battery lakini body haikuwa hata na mchubuko. Gari hii thamani yake ni $41,245 mpaka $55,745 ikiwa mpya lakini Bill ya kubadilisha betrii alipewa $60,000. Aliporipoti katika shirika la bima la ICBC(Insurance Corporation of British Columbia) waliiandika gari kama haitengenezeki kwa sababu matengenezo yamezidi thamani ya gari.
Professor mmoja huko Marekani anasema, " hizi gari watu wanazinunua bila kujua ukweki lakini thamani ya battery pekee ni 30% ya bei ya gari, kwamba kama utatoa milioni 100 basi battery ikifa andaa milioni 30+ au zaidi kwani huenda ukaambiwa ubadili na battery management system. Watu mliowahi kununua injini za gari za mafuta nazani mtaelewa hapa kwenye battery na engine kipi nafuu.
Tukiangalia Tesla Cyber truck baytery yake inauzwa $20,000 lakini bado kuna battery la $16000 linajulikana kama range extender au reserve. Jumla ya battery pekee ni $36,000 zaidi ya milioni 80 za kitanzania na unatakiwa baada ya miaka 10 hadi 20 ubadili battery kulingana na matumizi yako.
Hitimisho: Hizi gari sizioni Afrika leo wala kesho kutwa.
Things do change...
Hata simu za mkononi zilipoingia zilikuwa aghali.....
Ngoja tumsubiri Mchina
 
Kuna prius ambayo.battery yake ni 2.5 mil
Prius kama una maana ya Toyota Prius ni hybrid, inatumia motor ya battery na engine ya petroli. Battery kwa motor ya umeme ni kubwa kuliko battery za kawaida na ni ghali ila siyo sawa na batteries za electric cars.
 
Unazungumzia kuponda tu, ila hakuna anaekas na gari miaka kumi hata la mafuta likiwa zima, lazima litahitaji heavy matengenezo.

Kumbuka pia kuna gari cheap nyingi tu za umeme sasa, wachina wanaleta gari za $15k za umeme, and with time price ya battery itashuka sana bei.
Tesla ndio wanaonekana kuwa speed katika kuboresha teknolojia ya betrii na kwa makadilio mpaka 2030 watakuwa bafo hawawezi kukidhi mahitaji ya gari zao wenyewe, bado hawaja crack the secret to dry cathode coating so usitegemee gharama kushuka hivi karibuni.
 
Nchi za ulaya na US ni kawaida sana matengenezo ya gari kuwa gharama kubwa, hasa US, unakuta hata hizi crown athlete za 2005 mfano (sina uhakika kama US wanatumia athlete, ni mfano natoa kwa hizi cheap vehicles), gari pendwa za vijana matengenezo ya kawaida ni $5000 au zaidi, ndio maana US watu wanatupa sana gari na watu wengi tu wanaokota gari, mtu anaona ya nini kutumia gharama hii yote bora anunue used mpya 😂, imebidi nijicheke eti used mpya.

Hio $5000 au $7000 ya matengenezo bongo unapata chuma nzuri tu kwa dalali wa instagram au mtaani.

Usitizame tu gharama ya battery utakayokuja badili miaka 20 baadae, je ume calculate inaokoa gharama kiasi gani kwa kutotumia mafuta huo muda wote?

Cha mwisho ni teknolojia mpya imeingia, lazima itakuwa ghali, lakini soon hizo gari na vifaa vyake itakuwa gharama nafuu sana, ni kama upepo wa simu smart zilipoingia au flat screen TV, lakini hivi sasa hizo flat TV hadi wauza alkasusu mujarab huku mtaani unakuta wamewafungia wateja kutazama taarifa ya habari.

Kwa makadirio 2030 kwa sababu companies nyingi zimetangaza kuacha kutengeneza combustion engines, kuna uwezekano hizi gari za umeme tutaanza kuziona mtaani kwa wingi. Am sure.
Sisi huku Tanzania tunaosubiri used itakuaje? Haya magari ni mayai Tu sioni faida yake zaidi ya siasa Tu za wazungu za kukataa kutumia petroleum.
Kama ni mazingira kuna viwanda,mitambo ya kuchimba madini na vifaa vingine ambayo vinasababisha uharibifu wa mazingira

Magari ya kifala Sana haya sioni faida zake, gari haina mlio hata Ile vibe ya engine ikinguruma husikii Kwa kifupi haya magari ni baiskeli tu
 
Tesla ndio wanaonekana kuwa speed katika kuboresha teknolojia ya betrii na kwa makadilio mpaka 2030 watakuwa bafo hawawezi kukidhi mahitaji ya gari zao wenyewe, bado hawaja crack the secret to dry cathode coating so usitegemee gharama kushuka hivi karibuni.
Nimeona mwezi uliopita Tesla wamezindua pick up Yao ya Kwanza inaitwa cyber truck ina Sura mbaya kwelikweli
 
Kanunue gari za kichina za umeme bei nafuu.

Sio Kila gari ni la Kila mtu!

Wewe kama unaona Dolla 30,000 Kwa betri ni kubwa Kuna wengine hiyo ni bei ya konyagi tu!

Ukiona bidhaa kwako ni ghali jua wewe sio mteja mlengwa
 
Running cost ya EV ni ndogo kuliko ICE kwa muda mrefu.

Future ni Hybrid na EV.
Angalia hii model ya Tesla na engine halisi ya ICE sidhani kama dunia IPO sahihi kuingia kwenye ulimwengu wa EV,s
1000058288.jpg
 
Sisi huku Tanzania tunaosubiri used itakuaje? Haya magari ni mayai Tu sioni faida yake zaidi ya siasa Tu za wazungu za kukataa kutumia petroleum.
Kama ni mazingira kuna viwanda,mitambo ya kuchimba madini na vifaa vingine ambayo vinasababisha uharibifu wa mazingira

Magari ya kifala Sana haya sioni faida zake, gari haina mlio hata Ile vibe ya engine ikinguruma husikii Kwa kifupi haya magari ni baiskeli tu
Ndio maendeleo mkuu,
 
Habari wapendwa. Ni wazi dunia inapigana kuhakikisha gari za umeme ndio zinatawala kwa hoja ya kuwa rafiki na mazingira. Licha ya yote bado hizi gari ni changamoto hasa inapopata damage.

Tuchukue mfano kesi ya hivi karibuni huko Vancouver, mmiliki wa Hyundai Ioniq 5 ya mwaka 2022 alipata ajali iliyopelekea cover plate ya battery pack kubonyea na kuharibu battery lakini body haikuwa hata na mchubuko.

Gari hii thamani yake ni $41,245 mpaka $55,745 ikiwa mpya lakini Bill ya kubadilisha betrii alipewa $60,000. Aliporipoti katika shirika la bima la ICBC(Insurance Corporation of British Columbia) waliiandika gari kama haitengenezeki kwa sababu matengenezo yamezidi thamani ya gari.

Professor mmoja huko Marekani anasema, " hizi gari watu wanazinunua bila kujua ukweki lakini thamani ya battery pekee ni 30% ya bei ya gari, kwamba kama utatoa milioni 100 basi battery ikifa andaa milioni 30+ au zaidi kwani huenda ukaambiwa ubadili na battery management system. Watu mliowahi kununua injini za gari za mafuta nadhani mtaelewa hapa kwenye battery na engine kipi nafuu.

Tukiangalia Tesla Cyber truck baytery yake inauzwa $20,000 lakini bado kuna battery la $16000 linajulikana kama range extender au reserve. Jumla ya battery pekee ni $36,000 zaidi ya milioni 80 za kitanzania na unatakiwa baada ya miaka 10 hadi 20 ubadili battery kulingana na matumizi yako.

Hitimisho: Hizi gari sizioni Afrika leo wala kesho kutwa.
Sometimes hata hiyo miaka haifiki nishaona watu wanalalamika sana
 
Wapi huko wanauza battery ya prius kwa 2.5m mzee tukanunue maaana nmetoka kumfungia mteja wangu hata week haijapita kwa 4m tena hapo baada ya kupunguziwa toka 4.3m
Maisha yetu ya kibongo tunayajua wenyewe pamoja tunamiliki magari lkn sio muda wote utaweka full tank kuna kipindi huwa naweka ya BUKU 20-30 tena mara nyingi nafanya hivi..ingawa wadau wanasema kuwa magari ya umeme hayana gharama za uendeshaji bado nakataa ebu fikiria 4.3 milioni Kwaajili ya battery Tu.
 
Back
Top Bottom