Gari yenye injini ya d4

Memory

Senior Member
Jun 29, 2011
106
37
Jamani naomba kuuliza kama gari kama Toyota corona Premior au Verossa yenye injini ya D4 kama ina matatizo katika uendeshaji. nataka nijue kama iko safi kwa matumizi.
 
Jamani naomba kuuliza kama gari kama Toyota corona Premior au Verossa yenye injini ya D4 kama ina matatizo katika uendeshaji. nataka nijue kama iko safi kwa matumizi.

Mkuu RAV4 new model zote pamoja na na Ma-VX injini zake ni D4 na unajua kuwa magari haya yote ni ghali. Kwa mantiki hiyo nategemea kuwa injini za D4 zitakuwa bomba kabisa.
 
Tatizo la D4 ni utunzaji,inabidi uwe unafanya services mara kwa mara,pia epuka mafuta ya mtaani haya ya kwenye vidumu vya lita 5,nunua mafuta yenye quality yasiyochakachuliwa!!
 
Hahahahaa!!
D4 ina matatizo, na toyota walikubali kwamba zina matatio.
Tatizo lake ni pump, seal zinakufa na ona switch flani ni noma ikifa! Lazima kuweka mpya na sio ya taiwan.
Kama unaweza kuziepuka, do so for your own good.
 
Ahsanteni jamani maana haya magari ukikurupuka unaweza ukachukia gari maisha yako yote lakini kumbe hukufanya analysis nzuri wakati wa kununua.
 
Ahsanteni jamani maana haya magari ukikurupuka unaweza ukachukia gari maisha yako yote lakini kumbe hukufanya analysis nzuri wakati wa kununua.

Si unakumbuka msemo wa fid Q? "Anayewauzia wasanii magari anaitwa nani? Maana wanatumia mda mwingi gereji kuliko barabarani?"
 
Back
Top Bottom