GARI KUVIBRATE IKIFIKA SPEED 80 NA KUENDELEA

thehunk

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
527
221
JAMIIFORUM,
NAJUA HUMU KUNA WAJUZI WENGI HIVYO NAAMINI NITAPATA MSAADA,GARI YANGU AINA YA TOYOTA CROWN ILIGONGA JIWE NA KUPINDISHA PROPELA,TANGU SIKU HIYO IMEKUWA NA TATIZO LA KU VIBRATE IKIFIKA SPEED 80 NA KUENDELEA.
JE HILO NDIO LINAWEZA KUWA TATIZO MANA NIMEPELEKA KWA FUNDI HAPA MTAANI ANASEMA KWA JINSI ILIVYOGONGA WALA SIO TATIZO . NAOMBA MSAADA WENU KABLA YA KUPELEKA KWA MAFUNDI WENGINE
 
Hiyo gari ni kanyaga twende?(Automatic)
au ni mwanaume kazini?(Manual)
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Ni kitu gani hasa kinachotetemeka, gari zima au usukani? Nilienda safari siku chache zilizopita, kila nikifika mwendokasi wa 100-110kph, usukani unatetemeka sana, nikifika 120kph, unatulia. Baada ya kufika, nili Google, nikaona wanashauri kufanya wheel balancing, siku 5 kabla ya safari nilifunga tairi zote mpya. Nilipoenda kwenye wheel balancing, matairi yote yalikuwa out of balance. Baada ya kurekebishwa, nilifika hadi 140kph bila kuhisi mtetemo wowote ule kwenye usukani. Zingatia hilo pia. Endapo ungekuwa ukipunguza mwendo ndio unasikia mtetemo, hiyo ingekuwa kuna shida kwenye calipers.
 
JAMIIFORUM,
NAJUA HUMU KUNA WAJUZI WENGI HIVYO NAAMINI NITAPATA MSAADA,GARI YANGU AINA YA TOYOTA CROWN ILIGONGA JIWE NA KUPINDISHA PROPELA,TANGU SIKU HIYO IMEKUWA NA TATIZO LA KU VIBRATE IKIFIKA SPEED 80 NA KUENDELEA.
JE HILO NDIO LINAWEZA KUWA TATIZO MANA NIMEPELEKA KWA FUNDI HAPA MTAANI ANASEMA KWA JINSI ILIVYOGONGA WALA SIO TATIZO . NAOMBA MSAADA WENU KABLA YA KUPELEKA KWA MAFUNDI WENGINE
Tatizo umeshalijua, badilisha iyo PROPELA
 
Matatizo yote yanayohusiana na ballance pamoja na aligment huanza taratibu.

sababu huwa ni kuisha kwa tie-road hand, bush, au boll joints au king-pin kwa magari makubwa.

Hii ni tofauti sana na alichokieleza mleta mada.

"Gari iligonga jiwe" tuanzie hapa kwanza.

Mkuu ipeleke car wash ipandishe juu angalia kama kuna mkono wowote unaoshika hab za matairi huenda umepinda kdg (ni shida)

Angalia propeller ulilokuwa na wasi wasi nalo. Kama linaonyesha kugongwa hata kidg (ni shida sana)
ni simpo tu. Unalitoa unapeleka engineering linapimwa alignment. Itakuwa poa.

Ukikuta kuna mkono wowote umegongwa usifanye chochote, wapelekee watu wa ballance & alignment. Itakuwa poa"

Mb. Propeller hunyooshwa na lace mashine, ukilinyoosha kienjeji imekula kwako!
 
Sababu nyingine yaweza kuwa adjust ya coilovers na mibush yetu ya kienyeji tunayoweka kubust mashine isikwangue ukishaiweka hiyo nakuhakikishia ukifika spidi ya juu usukani unatetema kama unaopareti mashine ya sindiria...dawa yake hapo kama umeadjust coilovers zirudishe usawa wa mwanzo na kama ulibust kwa mibush itoe halafu leta mrejesho.au laah kama upo mwenge dar nipm kwa msaada zaidi
 
1 Wheel balance au Alignment.
2 Tairi limefanya kuvimba unahitaji jipya.
3 Tie rod
4 Break pad au rotor zinaisha hii kama ukikanyaga break na kufanya vibration.
5 Inawezekana ulipo gonga rim imepinda.
Angalia hayo matano peleka kwenye gereji za uhakika achana na mtaani wataiharibu gari yako.


Ndukiiiii ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ
 
Back
Top Bottom