Ganzi ya CCM kwa sasa haisaidii taifa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Chama tawala cha CCM ni kama wamepigwa ganzi. Kwa mazoea mabaya ya miaka michache iliyopita wamepigwa ganzi kwenye haya

1. Hawawezi tena kuja na hoja za muhimu wakati wenzao wapinzani wanatoa hoja za muhimu sana bila kujibiwa.
2. Tabia ya kusingizia fujo za upinzani ili watumie Polisi haziugwi mkono tena na Watanzania ambao kwasasa wameelimika zaidi
3. Kuita wapinzani makada wa mabeberu nayo imepitwa na wakati na badala yake tumeona wapinzani wameaminika zaidi wakati huu wa bandari. Haieezekani tena zile hoja za kusema wanatumiwa na mabepari!
3. Kitendo cha Raisi Samia kumfukuza kazi mkuu wa wilaya huko mtwara ambaye alibasilisha pesa za maendeleo kwasababu tu hiyo sehemu iliyopangiwa pesa ilikuwa ya upinzani. Raisi Samia alisema “ kwani wenyewe sio Watanzania?”. Hivyo zile mbinu za kunyima maendeleo na kusingizia ni ya chama na sio ya serikali haina mshiko.
4. Raisi Samia kusema magari ya CCM yatumike serikalini kwasababu chama ndiyo chenye madaraka kuna vigogo wa CCM hawaupendi huu utamaduni mpya.
5. Kitendo cha wananchi wa kanda ya zima kumpa Mbowe changamoto za maeneo yao kama vile ndiye waziri mkuu nayo inaonyesha sasa wananchi wanaongeza uaminifu zaidi kwa wapinzani.

CCM lazima ibadilishe utamaduni wao na tatizo kubwa mbinu za zamani hazitaweza kufanya kazi kwa sasa kwa sababu hizi

1. Teknologia ya sasa hakuna siri tena kuanzia mikataba, makusanyo ya kodi na hata matumizi ya pesa.
2. Raisi Samia pamoja na mambo mengi yaliyosemwa ni mwazi sana kuliko chama chake. Anajali nchi kuliko chama. Kuruhusu kusemwa kumeonyesha uvumilivu na ganzi kali kwa machawa ambao hawana hoja badala yake ni kusifia tu.
3.wapinzani wameweza kutumia teknologia vizuri kuliko CCM
4. Watanzania wakati wa tozo waligundua umuhimu na uchungu wa kodi.
5. CCM hawajajua jinsi ya kuwatumia diaspora wa Tanzania ambao wanasaidia sana kwenye hoja za kimkataba na kimataifa. Raisi ameona hilo lakini bado watendaji wake wanafanya kazi kwa mazoea na kwa sasa wana ganzi

Ganzi hii wengi wamekuwa kama hawajui la kufanya. Ushauri kama hoja za upinzani ni nzuri zichukuweni ubishi pekee haisaidii taifa.
 
Inakuwaga hivi hivi kipindi cha harakati, lakini kuja kufikia uchaguzi, upinzani ndio unaingia ganzi, kufunga, kufungua... CCM kidedea!.
Hizi ganzi ni ganzi za kupita tuu, muda muafaka wa uchaguzi ukifika, CCM ni ile ile na sio hii CCM Ganzi!.
P
 
P,

Hii ganzi ya sasa kwa CCM sio nzuri sana maana kuna hoja kubwa sana za kitaifa .
1. Mikataba mikubwa
2. Uchumi sasa wazazi wangu walikuja US mwezi wa saba Tanzania kumbe hakuna US $ !
3. Katiba na wasikokuwa waangalifu hili litaleta taabu.
 
Inakuwaga hivi hivi kipindi cha harakati, lakini kuja kufikia uchaguzi, upinzani ndio unaingia ganzi, kufunga, kufungua... CCM kidedea!.
Hizi ganzi ni ganzi za kupita tuu, muda muafaka wa uchaguzi ukifika, CCM ni ile ile na sio hii CCM Ganzi!.
P
Kaka Paulo hivi ukitokea umejifungia kwenye kachumba mko wawili tu na Yesu akakuuliza 'Paulo hebu niangalie usoni unijibu, UCHAGUZI WA TANZANIA CCM HUWA INASHINDA KIHALALI AU WANATUMIA NGUVU NA UBABE KUSHINDA' utamjibuje kaka.
 
Inakuwaga hivi hivi kipindi cha harakati, lakini kuja kufikia uchaguzi, upinzani ndio unaingia ganzi, kufunga, kufungua... CCM kidedea!.
Hizi ganzi ni ganzi za kupita tuu, muda muafaka wa uchaguzi ukifika, CCM ni ile ile na sio hii CCM Ganzi!.
P
P,huwa kule ni uchafuzi mwanzo mwisho,najua huwezi kusema,huenda hata wewe ungekuwa mjengoni huu leo🤸🤸🏃🏃
 
Chama tawala cha CCM ni kama wamepigwa ganzi. Kwa mazoea mabaya ya miaka michache iliyopita wamepigwa ganzi kwenye haya

1. Hawawezi tena kuja na hoja za muhimu wakati wenzao wapinzani wanatoa hoja za muhimu sana bila kujibiwa.
2. Tabia ya kusingizia fujo za upinzani ili watumie Polisi haziugwi mkono tena na Watanzania ambao kwasasa wameelimika zaidi
3. Kuita wapinzani makada wa mabeberu nayo imepitwa na wakati na badala yake tumeona wapinzani wameaminika zaidi wakati huu wa bandari. Haieezekani tena zile hoja za kusema wanatumiwa na mabepari!
3. Kitendo cha Raisi Samia kumfukuza kazi mkuu wa wilaya huko mtwara ambaye alibasilisha pesa za maendeleo kwasababu tu hiyo sehemu iliyopangiwa pesa ilikuwa ya upinzani. Raisi Samia alisema “ kwani wenyewe sio Watanzania?”. Hivyo zile mbinu za kunyima maendeleo na kusingizia ni ya chama na sio ya serikali haina mshiko.
4. Raisi Samia kusema magari ya CCM yatumike serikalini kwasababu chama ndiyo chenye madaraka kuna vigogo wa CCM hawaupendi huu utamaduni mpya.
5. Kitendo cha wananchi wa kanda ya zima kumpa Mbowe changamoto za maeneo yao kama vile ndiye waziri mkuu nayo inaonyesha sasa wananchi wanaongeza uaminifu zaidi kwa wapinzani.

CCM lazima ibadilishe utamaduni wao na tatizo kubwa mbinu za zamani hazitaweza kufanya kazi kwa sasa kwa sababu hizi

1. Teknologia ya sasa hakuna siri tena kuanzia mikataba, makusanyo ya kodi na hata matumizi ya pesa.
2. Raisi Samia pamoja na mambo mengi yaliyosemwa ni mwazi sana kuliko chama chake. Anajali nchi kuliko chama. Kuruhusu kusemwa kumeonyesha uvumilivu na ganzi kali kwa machawa ambao hawana hoja badala yake ni kusifia tu.
3.wapinzani wameweza kutumia teknologia vizuri kuliko CCM
4. Watanzania wakati wa tozo waligundua umuhimu na uchungu wa kodi.
5. CCM hawajajua jinsi ya kuwatumia diaspora wa Tanzania ambao wanasaidia sana kwenye hoja za kimkataba na kimataifa. Raisi ameona hilo lakini bado watendaji wake wanafanya kazi kwa mazoea na kwa sasa wana ganzi

Ganzi hii wengi wamekuwa kama hawajui la kufanya. Ushauri kama hoja za upinzani ni nzuri zichukuweni ubishi pekee haisaidii taifa.
Ganzi hii wengi wamekuwa kama hawajui la kufanya. Ushauri kama hoja za upinzani ni nzuri zichukuweni ubishi pekee haisaidii taifa.
869bd07e67e29c35d24b6d4892fd3015.jpg
 
Back
Top Bottom