Gamboshi

Rayvanny wa jamiiForums

Senior Member
Apr 7, 2023
132
347
1704373105808.jpg

JINA LA STORY: GAMBOSHI
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 01

Whatsapp No.: +255687409189
call/Text:+255687409189

*
GAMBOSHI
(Malkia Wa Wachawi.)
**

...Ilkuwa ni jioni tulivu mida ya saa kumi na mbili abiria wa basi liendalo mikoani katika nchi ya Tanzania ikiwa kama usafiri uliozoeleka zaidi kutoka mkoa mmoja hadi mwingine. Abiria wale walikua wamekaa kwenye basi zuri lililokua likifanya safari zake kutoka Dar es salaam kwenda mikoa ya kanda ya ziwa, baadhi yao wakiwa wamesinzia na wengine wakiwa wanaangalia runinga iliyokuwemo ndani ya basi lile, dereva alikuwa akiendesha kwa umakini mkubwa huku kwa nje kukionekana miti mikubwa na minene kama ya kwenye msitu. Kwa kupitia kioo cha mbele (windshield) kulionekana barabara ya lami iliyonyooka vizuri, mara ghafla akilitokea kama kivuli cha mtu mbele ya basi lile na dereva kwa uwezo na utaalamu wake wa kushika usukani alijaribu kumkwepa mtu yule bila mafanikio, dereva yule alisahau sheria ya kwanza ya udereva na kosa lile liligharimu maisha yake pamoja na uhai wa abiria aliowabeba ndani ya chombo kile cha usafiri. Gari lilipoteza uelekeo na punde si punde lilikua likibingirika pembezoni mwa barabara na kutokana na uwepo wa miti mikubwa basi lile lilijibamiza kwenye baadhi ya miti na kupelekea kuharibika vibaya sana. Kosa dogo alilofanya dereva la kutaka kunusuru uhai wa mtu mmoja ambaye alimuona mbele ya barabara lilisababisha ajali mbaya sana, baadhi ya abiria walipiga kelele za kuomba msaada kutokana na majeraha waliyoyapata na maumivu makali, lakini sauti zao zilimezwa na uwepo wa miti minene ndani ya msitu ule uliopo pembezoni mwa barabara.
Ghafla walitokea watu wa ajabu waliokua wamevaa kaniki nyeusi na vilemba vyekundu huku wakiwa wameshikilia mitungi pamoja na vibuyu vilivyozingushiwa shanga na irizi, watu wale waliokua takribani kumi na tano, nywele zao zilikua ndefu na zilizokua zimepakwa matope, kucha zao zilikua chafu na ndefu huku wakiwa na macho mekundu sana, baadhi yao walikua na siraha za jadi vilivyozungushiwa irizi nyekundu huku vikichuruzika damu. watu wale wa ajabu wake kwa waume walilifuata basi lile lililokua limeanguka huku wakitembea kwa mwendo wa madaha na kuringa mithili ya mtu aliyeona chakula kitamu huku akiwa na njaa kali sana. "Mama tusaidie!" aliongea mmoja wa abiria huku akilia baada ya kuwaona wale watu wakilisogelea basi lile kwa kupoitia kioo cha nyuma ambacho kilikua kimevunjika vibaya. mtu yule ambeye mguu wake wa kuume ulikua umevunjika vibaya huku chuma kikubwa kikiwa kimeingia ndani ya bega lake la kushoto aliwaona watu wale lakini hakuweza kufanya lolote wala kunyanyuka. Baadhi ya majeruhi wengine walijitahidi kutoka kwenye basi lile lakini ghafla kilisikika kitu kizito kikitua juu ya basi lile lilolala kiubavuubavu. mtu mmoja aliyekua amekatika mguu na kwa ujasiri mkubwa alijitahidi kutoka nje ya basi lile kwa kupitia dirishani ghafla alivutwa kwa nguvu kuelekea nje na alisikika akipiga kelele kwa nguvu sana "mamaaaaaa nakufaaaaaa...." alisikika mtu yule lakini ghafla sauti yake ilianza kuzimika kama vile alikuwa akinyweshwa maji hivyo alishindwa kuongea, hii ilikua damu iliyokua ikizuia koo lake kutoa sauti hivyo kufanya damu kuingia kwenye koo la hewa. Abiria wengine waliokuwemo ndani ya basi lile lililopata ajali waliduwaa kwa hofu lakini ghafla kioo cha mbele cha basi lile kilitolewa kisha watu wale waa ajabu waliingia ndani ya basi lile na kuwanza kumpoteza mtu mmoja mmoja mmoja huku wakijaza vibuyu vyao damu zilizokua zikimiminika kutoka kwa majeruhi wa ajali ile.

kwa nje basi lile lilionekana likichezacheza huku sauti za abiria wakiomba msaada zilisikika lakini hawakua na huruma na waliendelea kuvuna damu kwa abiria mmoja mmoja mpaka waliwamaliza wote. Hawa wanataka kufanyiaa nini} ni moja ya mawazo ambayo yalikua yakizunguka vichwani mwa baadhi ya abiria. "mama tusaidie.... wachawiiii wanatumalii..." alisikika abiria mmoja ambaye hakufanikiwa kumaliza kauli yake. mara sauti ziliishilia kwa mbali....

Watu wale waliovaa kaniki walitoka ndani ya basi lile huku wakiwa na mitungi pamoja na vibuyu vyao mikononi vikiwa vinavuja damu, iliyokua ikichuruzika taratibu sana, kwa mwendo wa ajabu wachawi wale walitoka kwenye basi lile na kutokomea kwenye ule msitu uliopo pembezoni mwa ile barabara, sauti za bundi pamoja na fisi zilisikika kutokea ndani ya msitu ule huku wakilia kwa kupeana zamu, mara alitokea mtu mmoja kati ya wale wachawi huku mkono wake wa kuume alikua ameshikilia usinge mweusi uliokua umelowa damu, akiwa amepanda fisi mkubwa mwenye macho mekundu huku mdoomo wake wenye meno makubwa yakiwa yamechongoka ulimi wake ulikua nje huku akidondosha udenda kama mbwa, alipita kwa kasi karibu na basi lile na pembeni kidogo kulikua na kibao kilichoandikwa kwa herufi kubwa "KARIBU HAPA NDIO GAMBOSHI.... ghafla wachawi wale walipita kwa kasi wakimfuata yule mchawi wa kwanza ambaye alionekana kama ni mkubwa wao, damu iliyokuwemo kwenye moja ya mtungi uliokua umejaa vizuri na umepakiwa kwenye mgongo wa fisi mmoja iliruka na kumwagikia kwenye kibao kile na kuyafanya maandishi yale kuwa alama nyekundu na kutishia mtu yeyote ambaye atayasoma.
**
Upande wa pili, Akiwa amekaa kwenye meza ndogo anapata chakula cha jioni Nyangeta, binti mrembo alieumbika kisawasawa mwenye shepu nzuri na rangi inayoendana na ngozi safi laini yenye mvuto wa aina yake, nywele fupi zilizopangika vizuri kichwani huku akiwa ameweka blitch ya rangi ya kahawia ilimfanya aonekane binti wa kisasa, huku akiwa amevalia nguo za kulalia (night dress) mkononi mwake akiwa ameshikilia mnofu wa nyama ya kuku akiutafuna taratibu na kwa mbali akisikiliza mziki laini kutoka kwenye sabufa iliyomo ndani ya chumba chake ghafla simu yake aina ya samsung Galaxy S 5 Active iliita, aliisogelea na kuiangalia kwenye kioo ilikuwa imeandika Inspecta Rashid aliipokea kwa adabu na kuiweka sikioni
"Hallow afande..."
"Ndio afande,
"Sawa afande, ntakuwa tayari baada ya dakika tano"
"..... Sawa afande"alijibu kwa adabu Nyangeta huku akinyanyuka kwa haraka
na kuanza kubadili nguo pamoja na viatu. Alichukua koti kubwa kabatini na kulivaa juu huku akichukua na bunduki yake aina ya bastola burrete 9mm na kuiweka kiunoni, alifungua kabati lingine pembeni na kutoa magazine ndogo kisha akaiweka kwenye mfuko wa koti alilolivaa, mara alisikia mlio wa gari ukitokea nje, alisogea dirishani na kusogeza pazia lililopo dirishani ili kumpa uwezo wa kuchungulia nje, gari ndogo nyeusi aina ya rav4 ilipaki nje ya nyumba yake na kupiga honi,,, Nyageta alitoka nje na kufunga mlango wa nyumba yake, kwa nje kisha aliingia kwenye gari lile kisha dereva wa gari akaliondoa kwa kasi,,, ITAENDELEA

••••••••••••••••••••••••••••••••••••••

USIKOSE EPISODE: 02

©Copyright "haki zote zimehifadhiwa"
 
1704373105808.jpg

>>>>>>>EPISODE : 02<<<<<<<<<
JINA LA STORY: GAMBOSHI
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 02

Whatsapp No.: +255687409189
call/Text:+255687409189

*****
GAMBOSHI
(Malkia Wa Wachawi.)
**

**
TULIPO ISHIA,,,,,,,,,,,,
"Hallow afande..."
"Ndio afande,
"Sawa afande, ntakuwa tayari baada ya dakika tano"
"..... Sawa afande"alijibu kwa adabu Nyangeta huku akinyanyuka kwa haraka
na kuanza kubadili nguo pamoja na viatu. Alichukua koti kubwa kabatini na kulivaa juu huku akichukua na bunduki yake aina ya bastola burrete 9mm na kuiweka kiunoni, alifungua kabati lingine pembeni na kutoa magazine ndogo kisha akaiweka kwenye mfuko wa koti alilolivaa, mara alisikia mlio wa gari ukitokea nje, alisogea dirishani na kusogeza pazia lililopo dirishani ili kumpa uwezo wa kuchungulia nje, gari ndogo nyeusi aina ya rav 4 ilipaki nje ya nyumba yake na kupiga honi.., Nyangeta alitoka nje na kufunga mlango wa nyumba yake, kwa nje kisha aliingia kwenye gari lile na liliondoka kwa kasi
**
ENDELEA NAYO,,,,
Nyangeta Jacob binti wa miaka 26 ambae amefanikiwa kuhitimu mafunzo yake ya uaskari akiwa katika kitengo cha upelelezi, ndio kwanza ametimiza mwaka mmoja kazini lakini amekuwa ni mmoja ya wapelelezi wanaoaminiwa zaidi katika jeshi la polisi nchini, pamoja na mafanikio yote aliyoyapata Nyangeta hakuwahi kuwafahamu wazazi wake halisi maisha yake yote amelelewa na wazazi wa kambo ambao walimuokota akiwa na umri wa mwaka mmoja.
**
Ilikuwa ni alfajiri ya saa kumi na mbili, eneo ilipotokea ajali ile ya basi, watu kiasi wakiwa wamevalia mavazi ya kiaskari walizagaa pembeni mwa gari la kubebea wagonjwa mahututi ( ambulance) huku miili ya watu waliokufa kutokana na ajali ile ikiwa imefunikwa kwa mashuka maalum yenye rangi nyeupe, huku imepangwa barabarani. hatimae ndani ya mda mfupi baadae gari la kina Nyangeta lilifika na kupaki pembeni, Nyangeta pamoja na askari mwingine wakiwa amevalia kiraia wote wawili walishuka na kulisogelea eneo la tukio, askari mmoja aliwafuata na kuanza kuwapa taarifa za tukio
"Inspecta Nyangeta kitengo cha upelelezi" huku akionyesha kitambulisho chake Nyangeta alimwambia yule askari huku akiendelea kwenda.
"Jambo afande..." Yule askari alimpigia salute Nyangeta huku akimpisha njia.
"Nipe riport"Nyangeta alimuambia yule askari
"Abira 35 wamekutwa wamesha poteza maisha , hakuna majeruhi hata mmoja, abiria mmoja alitupwa nje yeye shingo imekatika kabisa, dereva alifariki palepale tumekuta kwenye amebanwa na sterring la basi hakuna dalili za kupasuka kwa tairi labda spidi ilikua kubwa au breki ilikatika bado mafundi wetu wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hii "alijibu askari yule aliyetambulika kwa jina la afande Bwire. Nyangeta akiwa na yule askari mpelelezi mwingine walilizunguka lile basi huku wakilichunguza huku na huko ghafla nyangeta aliona kama taswira ya mtu kupitia kwenye kioo cha basi lile lililoanguka aligeuka nyuma kwa kasi huku akiwa ameikamata bastola yake lakini hakuona mtu... Alianza kukimbia kwenda porini lakini bado hakuona mtu wala kitu chochote, askari wengine walimfuata na kumuuliza huku wakiwa na silaha zao mkononi
" hakuna kitu nilidhani nimeona mtu ananiangalia..." Alijibu Nyangeta.
Yule mpelelezi mwingine aliefahamika kwa jina la doto alimuuliza huku akimuangalia macho ya kutokumuelewa
" uko sawa nyangeta?"
"Niko poa Dotto... Sijalala vizuri toka juzi" Nyangeta alijibu
" pole kama vipi twende kituoni then tukatafute room upumzike kidogo" Dotto alijibu huku akiweka silaha yake kiunoni "... Ok poa" alijibu nyangeta, na hao waliondoka kuelekea kwenye Gari. Kumbe pale walipokuwa wamesimama kwa pembeni kulikua na mti mkubwa ambapo kwa juu kabisa kulikua na mtu ambae amevalia kaniki ya kijivu nywele zake zilikua ndefu na macho mekundu yaliyowaka kama taa mtu yule alikua amechuchumaa kwenye tawi kubwa la mti huku akiwa anawaangalia kwa umakini wakina Nyangeta pasipo wao kumuona.
**
Nyangeta pamoja na Dotto walipita karibu na kile kibao kilichoandikwa "karibu hapa ndio gamboshi" huku wakiwa ndani ya gari walilokuja nalo, kwa pembeni waliona kundi la watu wakipita na kutema mate chini karibu ya kile kibao,
" unaona wanavyofanya hawa watu?" Nyangeta alimuuliza Dotto akiwa katika hali ya kushangaa,
" mambo ya kiutamaduni haya sidhani kama inamaana yoyote" Dotto alijibu huku akiongeza spidi ya gari na kuondoka zao.
**
KITUO CHA POLISI SHINYANGA, yalisomeka maandishi makubwa yaliyopo kwenye jengo kubwa huku pembeni yakiwa yamepaki magari ya polisi aina ya defender, gari ya Akina Nyangita iliingia na kupaki karibu na mlango mkubwa wa kituo hicho, nyangeta na dotto walishuka na kuingia ndani ya kituo kile, mlangoni walipishana na msichana mrembo mwenye nywele ndefu akiwa amevaa gauni zuri sana alipita karibu ya Nyangeta huku akimuangalia na kumsalimia,
" habari afande" yule msichana alimsalimia Nyangeta
" salama tu habari za leo" alijibu nyangeta
" nzuri tu.... Kazi njema" alijibu msichana yule na kuondoka zake.
Nyangeta alimuangalia Dotto na kumuuliza, "yule amejuaje mimi ni askari?"
"Hee, hilo sio swali ... Kila mtu akikuona tu anajua wewe afande, kwani hutaki kujulikana!?" Dotto alijibu huku akitabasamu.
Waliingia ndani na kukutana na askari wawili kwenye deski wakiwa wanajadili kuhusu yule msichana aliyeondoka
"Yani yule mdada kila kukitokea ajali lazima aje sijui ana nini?" Aliongea askari wa kwanza
"Atakua mchawi yule" alijibu askari wa pili.
Wale askari walipowaona wakina Nyangeta wakiwa wamesimama, waliwakaribisha na kuwaelekeza offisi iliyoandikwa mkuu wa kituo, nyangeta na Dotto waliingia ndani ya offisi ile na kukutana na askari mmoja aliyekuwa na mwili mkubwa uliojengeka kimazoezi akiwa amevaa mavazi ya kiaskari. huku akiwa na nyota kadhaa kwenye mabega
"Afande Nyangeta karibu shinyanga..."
"Nashukuru afande Rashidi, huyu ni afande Dotto ni patner wangu..."alijibu nyangeta baada ya kupiga salute. Na kuketi kwenye viti vilivyokuwepo mbele yao.
" afande nafikiri mmefika eneo la tukio?" Afande Rashid alimuuliza Nyangeta huku akifunua faili lililokuwepo mezani kwake.
" ndio afande" alijibu nyangeta kwa makini
"Sasa kwenye hii kesi tumefuatilia kronometa iliyokuwemo ndani ya basi ilirekodi spidi 80 kilometa kwa saa, sasa ajali iliyotokea pamoja na kioo cha mbele kutoka kabisa inaonekana kabisa kuna jambo jingine zaidi ya ajali ya kawaida" alielezea afande Rashidi
"Na kitu cha kustaajabisha zaidi eneo lilelie hii ni ajali ya nne ndani ya miezi miwili, pia watu wote wamefariki na pia kwa ripoti za madaktari maiti zote zimekutwa zimekauka damu., hii ndio imetufanya tuombe msaada wa kiupelelezi kutoka makao makuu na wametupa nyie..."
Natumai mtafanikiwa kuupata undani wa chanzo cha hizi ajali" alimalizia afande Rashid huku akimkabidhi Nyangeta faili la kesi na kusimama, "twendeni nikawaonyeshe ofisi zenu," aliongezea afande Rashidi, wote walinyanyuka na kuelekea nje ya offisi ya Afande Rashid, walikwenda moja kwa moja kwenye offisi nyingine na kuingia walikuta viti pamoja na meza, kompyuta pamoja na kabati dogo la chuma. Nyangeta aliingia na kuweka faili mezani, aliketi kwenye kiti aligundua kwa pembeni kulikua na kikaratasi kidogo kilichokunjwa alikiokota na kukifungua na kukuta maandishi yaliyosomeka, "NYANGETA ILE SIO AJALI YA KAWAIDA, WANAKUWINDA WEWE WAKUUE KABLA HUJAFAHAMU HAKI ZAKO. UKITAKA KUJUA UKWELI NJOO KONA YA MBUYU SAA SITA PEKE YAKO" .

Nyangeta alistuka na kuangalia dirishani alimuona mtu akikimbia, alitoka mbio pasipo kuaga na kukidondiosha kile kikaratasi bila kuwaambia chochote afande Dotto na Afande rashidi, Afande Dotto alikiokota kile kikaratasi na alishangaa kuona hakijaandikwa chochote alishangaa na kuanza kumfuata Nyangeta nje.

Inspecta Nyangeta alirudi ndani huku akikutana na inspecta Dotto pamoja na inspecta Rashid wakiwa mlangoni wakimuangalia,
"Nyangeta vipi mbona sikuelewi?" Aliuliza Dotto,
"Dah mi mwenyewe hata sijui nini kinaendelea" alijibu Nyangeta
Wakiwa wamesimama Nyangeta alimpokonya Dotto kikaratasi kile chenye ujumbe ambacho Dotto alikishikilia mkononi, Nyangeta alikiangalia na kuona hakina maandishi yoyote,
" haa.. Hii karatasi uliisoma pale ulipoiokota?" Nyangeta alimuuliza Dotto kwa hamaki,
"Ningesoma nini wakati haina maandishi yoyote?!?" Alimjibu huku akimshangaa, wakiwa wamesimama Inspector Rashidi aliawaaga na kuondoka zake kuelekea offisini kwake, wakiwa bado wapo kimya wamesimama alipita askari mmoja, Nyangeta alimfuata na kumgusa begani,
"Hey samahani... Afande Bire si ndio?!?" Alimuuliza yule askari huku akiwa na mashaka,
"Bwire, afande Bwire sio Bire" alijibu yule askari huku akitabasamu.
"Yes Bwire, naomba msaada wako tafadhali," nyangeta alimwambia Afande Bwire
"Msaada gani!?"Afande bwire alimjibu
"We ni mwenyeji huku?"
"Aah sio sana"
" kuna sehehemu sijui unapafahamu?"
"Sehemu gani"
"Panaitwa KONA YA MBUYU, unapafahamu"
Afande Bwire alimuangalia usoni na kutabasamu, " kona ya Mbuyu kila mtu anapafahamu,"
" unaweza kunipeleka?"
"...eeenh, bad news, madam pale sio pakwenda, hapafai kama unataka kwenda pale lazima uwe umeaga kwenu hakuna mtu anaesogea pale" Afande bwire alijibu huku akiwa na hofu
"Yani madam kitu ninachoweza kukusaidia labda nikuelekeze ila usiende tafadhali watu wanaenda yale maeneo huwa hawarudi" aliongezea Afande Bwire
"Usijali nielekeze tu inatosha" alijibu Nyangeta
"Haya sawa..." Afande Bwire alijibu huku akichuka kalamu na karatasi na kumchorea ramani na kumpatia.
Dotto alikuwa pembeni akimuangalia mwisho akaamua kumuuliza
"Umemaliza?... Haya twende maana mi njaa inauma alafu nimechoka balaa unajua huku mbali sana" Dotto alimwambia nyangeta huku akitoka nje, Nyangeta alimfuata huku akikunja kile kikaratasi cha ramani na kuweka kwenye mfuko wa koti alilovaa, waliingia kwenye Gari yao na kuondoka kituoni pale.,,,ITAENDELEA
**

••••••••••••••••••••••••••••••••••••••

USIKOSE EPISODE: 03
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••

©Copyright "haki zote zimehifadhiwa"
 
©Copyright "haki zote zimehifadhiwa" at the same time cover ya story yako umeweka Brand name na logo ya Marvel Studios, Be serious....
 
1704373105808.jpg

>>>>>>EPISODE : 03<<<<<<<<<
JINA LA STORY: GAMBOSHI
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 03
Whatsapp No.: call/Text:+255687409189
Email ; afrobongotz@gmail.com

*************************************
Previously on GAMBOSHI...
**************************************
NYANGETA BINTI WA MIAKA 26, MPELELZI ALIYEBOBEA KATIKA UPELELEZI AMEJIKUTA AKIWA MJINI SHINYANGA KUPELELEZA AJALI ZA AJABU AJABU AMBAZO ZINATOKEA MARA KWA MARA KATIKA KIJIJI CHA GAMBOSHI NA KUJIKUTA AKIINGIA KWENYE ULIMWENGU MPYA AMBAO YEYE HAKUUFAHAMU KABISA NA ANAGUNDUA KUWA GAMBOSHI NI ZAIDI YA KIJIJI CHA KAWAIDA GAMBOSHI NI ZAIDI YA MACHO YANAVYOWEZA KUONA...

TULIPOISHIA,,,,,,,,,
"Umemaliza?... Haya twende maana mi njaa inauma alafu nimechoka balaa unajua huku mbali sana" Dotto alimwambia nyangeta huku akitoka nje, Nyangeta alimfuata huku akikunja kile kikaratasi cha ramani na kuweka kwenye mfuko wa koti alilovaa, waliingia kwenye Gari yao na kuondoka kituoni pale.

»»»»»»»»»»»»««««««««««««»»
Episode 03
««««««««««»»»»»»»»»»»»»»»»

SASA ENDELEA,,,,,
Nyangeta alikuwa amejilaza pasipo kupata usingizi kwenye kitanda cha hotel moja nzuri mjini shinyanga, akiwa ni mwenye mawazo mazito aliwaza ni kitu gani kiliendelea, Aliwaza kile kikaratasi alichokikuta offisini ni kweli au alikua anaota? baada ya kukosa majibu kwa muda wa kama masaa mawili, aliamua kuamka na kuchukua simu yake, alitazama muda na kuona imeandika 23:15 (saa tano na robo usiku) aliamka na kuvaa viatu kisha alichukua bunduki yake chini ya mto uliopo kitandani, ila wakati anataka kutoka alisikia sauti za miguu kama mtu alikua akitembea nje karibu na dirisha la chumba alicholala, Nyangeta alinyata taratibu na kusogea kwenye lile dirisha akiwa ameshika bunduki yake mkononi, alijaribu kuchungulia nje lakini hakuona kitu wala mtu yeyote, aliangalia kwa makini lakini alimuona mlinzi wa hotel ile akiwa amelala kwenye kiti huku bunduki yake aina ya gobole ikiwa pembeni.

Nyangeta alirudishia pazia lake na kutoka nje ya chumba kile aliufunga mlango kwa nje na kutembea hatua kadhaa kwenda kwenye mlango uliopo karibu na chumba chake alitaka kugonga lakini alisita na kugeuza kisha akaondoka zake kuelekea nje ya hoteli ile, wakati anatoka, mlango ule aliosita kugonga ulifunguliwa kidogo na Inspecta Dotto alitoka na kumtazama nyangeta akiwa anatoka nje.
Nyangeta alitoka nje na kumuaga mlinzi ambaye alimfungulia geti na Nyangeta alitoka nje ya geti.

Kwa nje kidogo karibu na barabara ya lami kulikua na taxii kama nane hivi zikiwa zimapaki na madereva wakiwa wamekaa kwa pembeni wakiwa wanazungumza mara dereva mmoja alikurupuka baada ya kumuona Nyangeta na kuanza kumkimbilia,
“hey ma-mdogo tuwahi?” ilisikika sauti ya dereva taxi yule aliyekua akimwambia Nyangeta ambaye ametoka nje ya geti la hoteli,
“yap njoo fasta” alijibu nyangeta huku akivuka barabara kuifuata ile taxi. Yule dereva taxi alimfungulia mlango nyangeta kisha alizunguka upande wa dereva na kuingia kisha kuwasha gari.

“club gani ant?”aliuliza Yule dereva taxi huku akianza kuondoa gari taratibu
“mhmh…hapana siendi club” alijibu nyangeta akitabasamu huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa ile karatasi ya ramani,
“mpaka hapa shi- ngapi?" Aliongezea nyangeta huku akimpa kile kikaratasi Dereva taxi
“hee…!!!” alihamaki Yule dereva taxi huku akikanyaga breki kwa ghafla.
“ma –mdogo, unauhakika unataka kwenda hapa?”
“ samahani unaitwa nani?” aliuliza nyangeta
“Hamis…jina langu linaendana nini na kwenda hapo?” aliuliza Yule dereva akionekana kupagawa,
“sikia Hamisi, elfu ishirini hii hapa ukinifikisha, laki moja kama utaweza kunisubiri mpaka nikimaliza kilichonipeleka tukifika usishuke wala usizime gari. Unasemaje?” aliuliza Nyangeta huku akitoa noti mbili za elfu kumi kumi.
“mmmhhh…mtihani kwelikweli!, haya
Funga mkanda” aliongea dereva Taxi huku akipokea ile pesa. Kutokana na hali ngumu ya maisha haswa kwa mtu mwenye familia ambayo inakutegemea kama Dereva Taxi Hamisi, ambaye mpaka kwa wakati huo alikua amepata abiria mmoja tu tokea asubuhi, ilimuwia vigumu kukataa pesa zile, haswa ukizingatia sehemu yenyewe haikuwa mbali sana japo alifahamu fika kuwa eneo lile lilikuwa linatisha, uwezekano wa kupata laki moja kwa safari moja tu ulimpa moyo na kuamua kujitosa huku akiamini kesho yake watoto wake pamoja na mkewe wataweza kupata kula vizuri na kumlipia ada mwanae mkubwa ambaye alikuwa amerudishwa nyumbani kwa ajili ya kukosa ada.

“sasa Ant tuelewane kitu kimoja, tukifika nakusubiri kwa nusu saa tu baada ya hapo hela yangu unanipa sawa? Hata nikiondoka” aliuliza Dereva Taxi huku akiweka gia na kuondoa gari kwa mwendo wa kawaida.
“nop, ukinisubiri, ukanirudisha mpaka hapa ntakupa pesa yako…by the way, ukiniacha ntakupa vipi pesa yako?” aliongea Nyangeta huku akimuangalia usoni dereva taxi
“ok sawa, wewe unajua jina langu,wewe je unaitwa nani mwenzangu?”
“Nyangeta, ila rafiki zangu hupenda kuniita Neema”
“ok… Neema, natamani mwisho wa siku niseme nashukuru kukufahamu ila daah! Sijui itakuaje mpaka mwisho wa hii safari!"
“usiogope” alijibu nyangeta huku akijiweka sawa, na gari ikiwa inakatiza mitaa ya mji wa shinyanga na kuelekea nje kidogo ya mji.

******

Nje kidogo ya mji wa shinyanga, katikati ya kijiji cha Gamboshi kulikua na kijimsitu kidogo chenye mti wa mbuyu mkubwa sana ambao umetenganisha barabara mbili za vumbi huku kwa nyuma ya mti ule kukiwa na makaburi ya zamani sana, inasemekana makaburi yale yalikuwepo hata kabla ya ukoloni, hakuna aliyejua historia kamili ya makaburi yale.

Jitihada za kujaribu kuhamisha makaburi yale zilishindikana kutokana na kila makaburi yale yakitolewa kesho yake yanarudi kama yalivyokuwepo hivyo wanakijiji wa eneo hilo waliamua kuachana na eneo hilo wakiamini ni eneo ambalo hutumiwa kama makao makuu ya wachawi, pia ilisemekana uchawi ndio ulizaliwa pale.

******
Umbali kama wa mita 100 kutoka ulipo mti ule, dereva Taxi Hamis alisimamisha gari na alimgeukia Nyangeta
“umeona hii barabara nyoosha moja kwa moja umefika unapotaka kwenda mimi sisogei zaidi ya hapa”
“Hivi Hamisi upo serious? Huoni hilo giza na hapa ni msituni na hili giza unataka niende peke angu?” alijibu Nyangeta huku akiangalia nje kupitia dirisha la gari
“we mama!! Unataka roho yangu au? Nimekwambia siendi zaidi ya hapa” Hamisi alijibu kwa nyodo
“vipi nikikuongezea 20, kwenye ile tulioongea?” aliongea nyangeta kwa upole huku akitoa tena noti mbili za elfu kumi kumi.
“dah!… hela hizi zitakuua hamis” Hamisi alijiambia mwenyewe huku akijaribu kuwasha gari, gari iliwaka lakini kabla hajaweka gia mara kishindo kidogo kilisikika kutokea upande wa nyuma wa gari na gari ilizima palepale. Hamisi alijaribu kuwasha ila gari halikuwaka, kila akiwasha haliwakuwaka
“ohoooo… nilijua tu… pesa si nzuri!!!” alilalamika hamisi huku akiendelea kung’ang’ana kuliwasha gari.
Nyangeta alifungua mlango wa gari, na ghafla dereva taxi alimdaka mkono kabla hajatoka "ant,,, sehemu salama zaidi ni ndani ya gari siyo nje" hamisi alimwambia nyangeta kwa hofu "usijali nilijiadaa" Nyangeta alijibu huku akitoa bunduki yake na kuikoki "sawa lakini kuwa makini" alijibu hamisi huku akimuachia mkono nyangeta kwa msisitizo na hofu.,,, ITAENDELEA

USIKOSE EPISODE 04 "KESHO"

©Copyright "haki zote zimehifadhiwa"
 
View attachment 2864014

Copyright "haki zote zimehifadhiwa"
mkuu tuongezee hata kamoja tu plz
 
1704373105808.jpg

>>>>>>EPISODE : 04<<<<<<<<<
JINA LA STORY: GAMBOSHI
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 04

Whatsapp
call/Text:+255687409189
(Audio version ya story coming soon)

*************************************
Previously on GAMBOSHI...
**********************************
Ilipoishia,,,,,,,,,,
ghafla dereva taxi alimdaka mkono kabla hajatoka
“ant …sehemu salama zaidi ni ndani ya Gari sio nje!” Hamisi alimwambia Nyangeta kwa hofu
“ usijali nilijiandaa” Nyangeta alijibu huku akitoa bunduki yake na kuikoki.
“Kuwa makini" alijibu hamisi huku akimuachia

»»»»»»»»»»»»««««««««««««»»
Episode 04
««««««««««»»»»»»»»»»»»»»»»
.
SASA ENDELEA,,,,,
Nyangeta alitoka nje na kuzunguka nyuma ya gari na hakukuta kitu chochote, alisogea kwa pembeni kulikua na kichaka kidogo aliangalia huku akiwa amenyoosha bunduki yake sawasawa kuelekea kichaka kile mara alitokea mbwa mdogo aliye konda na kubweka
“kwema huko?” aliuliza Hamisi kutokea ndani ya gari
“kwema tu hakuna kitu ni mbwa”alijibu Nyangeta akiweka bunduki yake na kuanza kurudi kwenye gari.
"unauhakika ni mbwa kweli!!?" aliuliza Hamisi swali ambalo lilimfanya nyangeta kutabasamu na kuanza kurudi kwenye gari
“ sasa wacha mimi niende kwa mguu wewe rekebisha gari, ntakukuta hapa” nyangeta alimwambia hamisi kupitia dirisha huku akiangalia saa yake ya mkononi.
“saa 00:22 (saa sita usiku na dakika ishirini na mbili), hakikisha umefunga vioo na milango yote. Una tochi uniazime?” aliongezea Nyangeta
“ yes hii hapa” alijibu Hamisi huku akiangalia mbele kwenye dashboard alitoa tochi na kumpatia Nyangeta
“asante, una silaha yoyote humu?” aliuliza nyangeta
“usijali nilijiandaa” hamisi alijibu huku akimuonyesha irizi kubwa iliyoko kiunoni mwake
“mmmhhh… haya sawa nikichelewa zaidi ya nusu saa ondoka” Nyangeta alijibu akionekana kustaajabishwa na Irizi ile.

Nyangeta aligeuka na kuanza kuifuata barabara ile ya vumbi akimuacha dereva taxi hamisi akiendelea kujaribu kuliwasha lile gari.
Baada ya kama mwendo wa dakika tano Nyangeta aliuona mti Mkubwa wa mbuyu alisogea taratibu kwa umakini mkubwa akiwa na bunduki yake pamoja na tochi, ghafla alisikIa “chakachaka” pembeni kwenye kichaka kidogo kama mita tano kutoka karibu na mti ule, aliangalia vizuri juu ya mti ule aliona mtu akiwa na macho mekundu yanayo ng’aa sana alinyoosha bunduki yake huku akijaribu kumuongelesha mtu Yule

“jitokeze mwenyewe, hapa nina silaha nitakupiga risasi” aliongea Nyangeta kwa ujasiri huku
Akiwa ameelekeza bunduki yake juu ya mti ule, kwa upande ule wa makaburi, ilitoka sauti ya muungurumo kama wa fisi aliyekasirika
“gggrrrrrrrr” ilisikika sauti ile, wakati huohuo Nyangeta alisikia ile sauti ya pale kichakani inaongezeka sauti na kile kichaka kilitikisika kwa fujo,
Yule mtu aliyepo juu ya mti nayeye alianza kushuka taratibu kumsogelea, nyangeta akiwa bado anajiuliza nini cha kufanya ghafla alisikia kitu kikipita nyuma yake kwa kasi ya ajabu, na hakusita aligeuka kwa kasi na kufyatua risasi nne mfululizo.

ah – pah – pah – pah” ilisikika milio ya risasi, kabla Nyangeta hajaangalia vizuri alipigwa na kitu kizito kwenye kisogo na alianguka palepale na kupoteza faham.

Akiwa na tochi pamoja na bunduki yake aina ya Bastola 9mm, inspecta Dotto ambaye alikua anaifuatilia kwa nyuma Taxi aliyopanda Nyangeta, umbali wa kama mita hamsini kutoka ilipopaki ile taxi, alishuka taratibu na kuifuata Taxi ile kwa umakini huku akistaajabu kuona mlango wa dereva umefunguliwa.
Aliisogelea taratibu na kuona ipo kimya na hakukua na dalili yoyote ya uwepo wa uhai wa binadamu yeyote, alisogea karibu kabisa na kioo cha mbele kwa upande wa abiria na kumulika ndani kwa kutumia tochi yake lakini hakuona mtu yoyote ndani, kwa kupitia dirishani pale aliona mlango wa dereva ukiwa wazi kwa upande wa pili, alizunguka upande ule wa dereva lakini hakuona kitu chochote, alimulika huku na huko ila hakuona mtu yoyote, alitoa simu yake na kujaribu kumpigia Nyangeta, lakini simu haikuita wala kujibu chochote, kutokana na kutokuwepo na mtandao mzuri eneo lile, akiwa anaendelea kuhangaika kupiga simu ghafla alihamaki huku akitazama chini aliona miburuzo kama mtu alikuwa akivutwa kwa kulazimishwa, miburuzo ile ilienda moja kwa moja mpaka kwenye kichaka kidogo pembezoni mwa barabara, Inspecta Dotto aliishika bunduki yake mujarab na kuanza kuifuatilia miburuzo ile mpaka kule kichakani, umbali si mrefu sana kutoka kwenye ile barabara alianza kuona damu ikiwa imetapakaa chini huku nyingine ikiendelea kuchuruzika taratibu na kumdondokea begani kutokea kwenye mti uliokuwepo pembeni, kabla hajamulika juu ya ule mti, mwili wa dereva taxi Hamisi ulianguka kutoka kwenye ule mti ukiwa umeraruliwa vibaya maeneo ya shingoni na kifuani!,
Inspecta Dotto alirudi nyuma hatua mbili kwa hofu huku akishilia bastola yake kisawasawa, kwa ujasiri wa kiaskari, aliusogelea ule mwili na kuugeuza kwa mguu na aliuona mwili wa dereva taxi Hamisi ukiwa mkono mmoja umeshikilia Irizi kubwa iliyokatika kutoka kiunoni, na mkono mwingine akiwa ameshika noti zake mbili za elfu kumikumi zikiwa zimejaa damu. Akiwa anaendelea kuupekua pekua mwili ule, ghafla alisikia "pah - pah - pah - pah" milio ya risasi ikitokea katikati ya pori lile kwenye giza totoro.
Inspecta Dotto alisimama na kushikilia bunduki yake kwa ujasiri, lakini kabla hajapiga hatua, lahaulaa!!!, Dereva taxi Hamisi alikurupuka na kumdaka mguu,
"WACHAWI, kimbi.... Ki-ki-mbia...kim..." Ni maneno aliyotoa dereva taxi Hamisi kabla ya kuanguka chini na kukata roho palepale,,,ITAENDELEA

USIKOSE EPISODE YA 05

©Copyright "haki zote zimehifadhiwa"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom