FURSA nchini COMORO: Mfanya biashara, soma hapa

Ni

Ni hatari hebu tudadavulie hapo? Nna jamaa yangu kaenda Comoro kuuza dawa za nguvu za kiume anasema kuna wateja sana coz wacomoro wanaoa wanawake wengi..Toka aondoke 2014 sijasikia tena kutoka kwake labda na yeye ametekwa na mwanamke wa kingazija
uongo wakomoro hawaoi wake wengi tatizo zinaa ni nyingi
 
comores ni sehemu nzuri ya biashara ila uwe tu muangalifu
hata uwe na mamillion ya hela utatembea wakati unaotaka hakuna uhalifu
usumbufu uliopo ni utoaji wa mzigo bandarini proses ni nyingi ila kuna watu wanaweza kukusaidia
 
Tatizo la comores
Restaurent (migahawa) hutopata vyakula kama vile Tanzania kariakoo
Vyakula vingi ni vitu vikavu muhogo wa kuchoma, ndizi za kukaanga, mashelisheli ya kukaanga na kuchoma. Mapapatiko ya kuku, mishikaki . nyama wenyewe inatoka brazil ishakaa mda sana kwenye friza
Ila kuna restaurent moja moroni inaitwa nassib hapo ndio utapata chips kuku pilau vinywaji bei juu
 
Kama ni mlaji wa pweza utafaidi maana wao hawali pweza ila utajipikia mwenyeo
Wanapenda sana mziki mchukue kiba au blue au mbosso au chibu au mr Nice utapiga hela sana
 
Fursa nzuri sana kwa wafanya biashara.....Ingekua na muendeleza katika nchi zenye fursa zaidi nakubwa kuliko comoro yenye idadi ndogo ya watu uchumi mdogo tuekeeni bussiness trip nchi kama Sweden UAE nk
Umeona kwa jicho la mbali sana mkuu.
Comoro ni sawa na Unguja tu.
 
tahadhari kwa mwenye kwenda kufanya biashara comores
usije onja penzi la kingazija utapoteza mali yote hurudi na kitu tushawachangia watu nauli ya kurudi
Kwa hyo mkuu unamaanisha wanawake wa Ngazija ni watundu Kama wale wa Tanga?
 
tahadhari kwa mwenye kwenda kufanya biashara comores
usije onja penzi la kingazija utapoteza mali yote hurudi na kitu tushawachangia watu nauli ya kurudi
Hivi Mkuu Moroni kuna Ambiance Club Corner Bar yao kule? Yaan sehemu naweza kiburudishaji nikaburudika nae.
Siku moja nilizunguka mji mzima nikitafuta "Za kununua" nikakosa kabisa.
 
Zipo kama club des amis kule zilmadjou na
Rose noir disco teque wee hujaonana na wenyeji tatizo
Hivi Mkuu Moroni kuna Ambiance Club Corner Bar yao kule? Yaan sehemu naweza kiburudishaji nikaburudika nae.
Siku moja nilizunguka mji mzima nikitafuta "Za kununua" nikakosa kabisa.
 
Hv km nataka kwenda kwa ajili ya research(kwa ndege)ni mzigo gani wa biashara unaweza kua ni light alafu una soko pia ili nisi umie ktk hili swala nauli na malazi
 
Kabla hujaenda ulizia meli inaondoka mda gani dar to comores pakia mzigo mdogo ktk meli kabla siku 2 kuondoka kwa meli
Kata tiket ya ndege ondoka kabla meli kufika comores ukaisubiri meli kule ikifika tu uwepo ili utoe mzigo wako ukijisahau mzigo wako utaibiwa huko huko bandarini au . Kwa safar ya mwanzo ningekushauri upande meli hasara itapungua kuliko kuchukua ndege
 
Meli itakuchukua siku 3 kufika moroni
Ndege masaa 2 tu nauli ni 320euro + 60 euro ya visa na tax to capital city moroni itakubidi uchukue taxi ya peke yako kwa vile huna mwenyeji ni euro 10 taxi ya kushare ni euro 1 from airport to moroni capital city. Hotel euro 20 par day hizo gharama ni kubwa sana kwa mfanya biashara mdogo ila kwa mwenye kwenda kuresearch poa ushauri wasiliana na watanzania waliopo comores ili wakupokee.
 
na kwa kuongezea tu biashara ya comores ina msimu kuanzia jun july na august kwa sababu ni holiday ya wale wanaokaa ulaya huja comores kufanya maharusi yao ya mila zao hapo panakua na biashara nzuri sana hususan kwa biashara ya chakula kama vinywaji biscuit sukari ungangano basmati rice tomato paste , nazi ya unga, kanga za sare, mafuta ya kupikia , majani ya chai, hiliki, mdalasini, uzile , nk


Mkuu,asilimia ngapi ya waislamu nchini comoro?
 
Wakomoro wote ni waislam kanisa lipo moja lilijengwa na wakoloni wafaransa wanaoabudia ni wageni tu mkubwa wa kanisa la comores ni raia wa Tanzania ambaye ni dokta wa hospital ya msaada wa kanisa anaitwa dr philipo raia wa tz huyo comores ni waislam ila tu wana mila na tamaduni zao na uzungu wameufanya mwingi.
 
1. sehemu ya kufikia
2. biashara utakayo kuja nayo
3. usafirishaji utakao tumia kuja na mzigo
4. hela ya kutolea mzigo bandarini
5. sehemu ya kuuweka mzigo baada ya kuutoa bandarini
kuna changamoto nyingi saana na ukizingatia unaetoka tz ukija comores inakubidi uje na euro maana pesa ya tz haitumiki comores na tsh to euro ni hela nyingi 1euro minimum ni 2500tsh wateja wa comores wana shida zao na hata kupata mteja akanunua mzigo kwa jumla ni shida inategemea na biashara utakayo kuja nayo kiufupi kabla ya kuanza biashara nchini comoro kwanza uje kukodi room ambayo sawa na 50euro laki n 25 kwa mwezi pili utafute oda kwa wauzaji wa jumla au hata wareja reja ukifika na mzigo unaweza ukapata mkopo kutoka kwa wateja wako hadi utakapo toa mzigo ama watanzania waliopô wakusaidie kukupa hela ya kwenda kutoa mzigo na hiyo haina garantii maana hakuna uaminifu watu wamesha ibiana sana mii binafsi yangu nilimpa mtu euro 1500 aende kutoa magodoro kaenda kutoa baada ya kuuza hata hakuniaga kachukua ndege kaondoka kaja zake tz
na wa tz waliopo huko baadhi yao hujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya bangi na unga huzuga kwa kuuza vitunguu ili tu wasijulikane binafsi yangu nisha mpokea mgeni kwa kumsaidia akalala kwangu nikamuuliza umekuja na biashara gani akanambia nimekuja na choclate madwa ya kulevya hayo cjui yanaitwaje nilimuhurumia nikampa hifadhi lakini nikampa wiki moja tu aondoke nilichukua riski kubwa ila nilimuhurumia kwasababu tu ni mtanzania kuna mambo mengi visiwani comores na biashara ni nzuri maana hela yao ni kubwa kuliko shillingi ya tz ila yataka ukakamavu wa hali ya juu kama una suali lolote nitafute nitakupa ushauri mii nilikua na duka la jumla ila mzigo tulikua tunatoa dubai direct
Nakufuta mkuu, inbox me thy number
 
Back
Top Bottom