FURSA nchini COMORO: Mfanya biashara, soma hapa

Tanki

JF-Expert Member
Apr 7, 2013
493
193
Huenda unafanya biashara na raia wa Comoro au ulijaribu ila ukakutana na changamoto za hapa na pale. Au pengine ulikuwa unatamani kufanya biashara aidha kuuza au kununua bidhaa kutoka Comoro. Kuwa na amani, suluhisho limepatikana.

Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na ubalozi wa Comoro nchini Tanzania wakishirikiana na UCCIA na Coso Marketing & PR solution LTD wanakuletea FURSA wewe mfanya biashara.

Ni Fursa ya kuweza kufanya biashara nchini Comoro.

UTAKUTANISHWA na wafanya biashara wakubwa , wadogo , na wa kati wa kuaminika kabisa wa nchi ya Comoro.

Hii ni USO kwa USO, tunatoka Tanzania, tunafunga safari hadi Comoro.

Note : KABLA YA SIKU YA SAFARI KUTAKUWA NA SEMINA MAALUM KWA WAFANYA BIASHARA ITAKAYOFANYIKA KWENYE UBALOZI WA COMORO.

Usikubali kupitwa na hii.

TANUA WIGO wa BIASHARA YAKO.

Kwa mawasiliano
Contact :
0684771367
Email :
coso@communicationsolution.co.tz
FB_IMG_15587745836934428.jpeg
 
Huenda unafanya biashara na raia wa Comoro au ulijaribu ila ukakutana na changamoto za hapa na pale. Au pengine ulikuwa unatamani kufanya biashara aidha kuuza au kununua bidhaa kutoka Comoro. Kuwa na amani, suluhisho limepatikana. )

Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na ubalozi wa Comoro nchini Tanzania wakishirikiana na UCCIA na Coso Marketing & PR solution LTD wanakuletea FURSA wewe mfanya biashara.

Ni Fulsa ya kuweza kufanya biashara nchini Comoro.

UTAKUTANISHWA na wafanya biashara wakubwa , wadogo , na wa kati wa kuaminika kabisa wa nchi ya Comoro.

Hii ni USO kwa USO, tunatoka Tanzania, tunafunga safari hadi Comoro.

Note : KABLA YA SIKU YA SAFARI KUTAKUWA NA SEMINA MAALUM KWA WAFANYA BIASHARA ITAKAYOFANYIKA KWENYE UBALOZI WA COMORO.

Usikubali kupitwa na hii.

TANUA WIGO wa BIASHARA YAKO.

Kwa mawasiliano
Contact :
0684771367
Email :
coso@communicationsolution.co.tzView attachment 1107977
Fursa nzuri sana kwa wafanya biashara.....Ingekua na muendeleza katika nchi zenye fursa zaidi nakubwa kuliko comoro yenye idadi ndogo ya watu uchumi mdogo tuekeeni bussiness trip nchi kama Sweden UAE nk
 
Mi huwa napata shida sana kuweka tofauti kati ya Comoro na Morroco

BTW all the best kwa watakaoparticipate
 
Mi huwa napata shida sana kuweka tofauti kati ya Comoro na Morroco

BTW all the best kwa watakaoparticipate
Tofauti ipo hata kiuandishi (Jokes dear).
Morroco ipo kaskazini mwa bara la Afrika wakati Comoro ipo kusini mashariki mwa Afrika.
 
Comoro kikubwa kama ni masuala ya biashara ya vyakula comoro unapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanachopkipenda wale wanachagua vyakula mnooo usije ukajichanganya ukapeleka kitu tofautui na wanavyopenda utajuta

Mfano kuna aina ya magimbi huwa hawapendi kama mjuavyo yapo ya aina mbili

Viazi mbatata wanapenda ila kuna vya aina yake ndo wanapenda zaidi

Ni wezi narudia ni Wezi kamwe usimwamini mcomoro narudia hawakawii kukuzunguka chap so akili kichwani na unapomuamini

Malazi ni gharama hata chakula pia ila penda ku hangout na watz wenzako utakaowakuta kule utapata mbinu za kuminimize cost ya kuish kule

Mzigo kabla haujaupeleka hakikisha umepata taarifa sahihi usije kulia

Pesa zipo kule hawapendi kufanya kazi ila pesa wanazo kutoka kwa ndugu zao waliopo nje
 
Ooh asante mkuu..halafu hicho kingine ndo waarabu?

Hapana, sio waarabu kwa mambo mengi kiutamaduni wacomoro aka Wangazija wamefanana sana na wazanzibari, waliwahi kutawaliwa na wafaransa na ndio maana idadi kubwa ya wacomoro wapo ufaransa na wengi wanaongea kifaransa.
 
Sawa.naulizia hicho kingine(morroco)
Ndo wana asili ya uarabu?

Hao wengine (Morocco) ni waarabu si unamkumbuka Mfalme Mohammed VI na mke wake Pricess Lalla Salma walivyokuja Tz? hao ni waarabu ingawa hawamo katika Jumuiya ya nchi za kiarabu GCC
 
1. sehemu ya kufikia
2. biashara utakayo kuja nayo
3. usafirishaji utakao tumia kuja na mzigo
4. hela ya kutolea mzigo bandarini
5. sehemu ya kuuweka mzigo baada ya kuutoa bandarini
kuna changamoto nyingi saana na ukizingatia unaetoka tz ukija comores inakubidi uje na euro maana pesa ya tz haitumiki comores na tsh to euro ni hela nyingi 1euro minimum ni 2500tsh wateja wa comores wana shida zao na hata kupata mteja akanunua mzigo kwa jumla ni shida inategemea na biashara utakayo kuja nayo kiufupi kabla ya kuanza biashara nchini comoro kwanza uje kukodi room ambayo sawa na 50euro laki n 25 kwa mwezi pili utafute oda kwa wauzaji wa jumla au hata wareja reja ukifika na mzigo unaweza ukapata mkopo kutoka kwa wateja wako hadi utakapo toa mzigo ama watanzania waliopô wakusaidie kukupa hela ya kwenda kutoa mzigo na hiyo haina garantii maana hakuna uaminifu watu wamesha ibiana sana mii binafsi yangu nilimpa mtu euro 1500 aende kutoa magodoro kaenda kutoa baada ya kuuza hata hakuniaga kachukua ndege kaondoka kaja zake tz
na wa tz waliopo huko baadhi yao hujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya bangi na unga huzuga kwa kuuza vitunguu ili tu wasijulikane binafsi yangu nisha mpokea mgeni kwa kumsaidia akalala kwangu nikamuuliza umekuja na biashara gani akanambia nimekuja na choclate madwa ya kulevya hayo cjui yanaitwaje nilimuhurumia nikampa hifadhi lakini nikampa wiki moja tu aondoke nilichukua riski kubwa ila nilimuhurumia kwasababu tu ni mtanzania kuna mambo mengi visiwani comores na biashara ni nzuri maana hela yao ni kubwa kuliko shillingi ya tz ila yataka ukakamavu wa hali ya juu kama una suali lolote nitafute nitakupa ushauri mii nilikua na duka la jumla ila mzigo tulikua tunatoa dubai direct
 
na kwa kuongezea tu biashara ya comores ina msimu kuanzia jun july na august kwa sababu ni holiday ya wale wanaokaa ulaya huja comores kufanya maharusi yao ya mila zao hapo panakua na biashara nzuri sana hususan kwa biashara ya chakula kama vinywaji biscuit sukari ungangano basmati rice tomato paste , nazi ya unga, kanga za sare, mafuta ya kupikia , majani ya chai, hiliki, mdalasini, uzile , nk
 
Vipi mtu kupata passport ya kule na kuingia ulaya ni kazi?
 
Back
Top Bottom