Fursa usafirishaji wa bidhaa kwenda visiwa vya Comoro

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
5,024
12,784
Biashara ya usafirishaji wa bidhaa Kati ya Tanzania kwenda visiwa vya Comoro umeendelea kuwa changamoto kutokana na uchache wa Vyombo na baadhi ya vyombo kutokidhi uwezo wa speed na uhitaji wa Mzigo kufika haraka.

Mizigo inayotoka Tanzania kwenda Comoro ni Vyakula, Vinywaji,vifaa vya ujenzi,vifaa vya Umeme na mifugo kama Mbuzi,kondoo na Ng'ombe.Meli chache utumia wastani wa siku 2 Katika safari ya kutoka Dar kwenda Comoro nyingi hutumia mpaka siku 4. Changamoto inakuwa ni kuharibika Kwa mizigo ambayo ni mazao ya Shambani na mifugo hufariki. Kukosekana Kwa meli maalumu ya kubeba wanyama(Livestock Carrier) mifugo hubebwa kwenye meli za Kawaida na kuwekewa vyumba(partition) za mbao kama kwenye maroli, hii husababisha mifugo mingi kufariki kwenye upepo mkali na mawimbi makali na zikatumia muda mwingi safarini.

Hivyo ni fursa Kwa wawekezaji wazawa au wabia kuwekeza kwenye usafiri wa majini, sababu mzunguko wa biashara ni Mkubwa Meli ikitoka Dar kwenda Comoro hukodiwa Kwa wastani wa kuanzia million 45, ikifika Comoro inarudi Mtwara utapata Cement ya Kwenda Zanzibar Kwa Bei ya elfu 2 Kwa mfuko mmoja. Baada ya kufika Zanzibar utasubiri oda ya mizigo ya kuja Dar ambayo vitu vya madukani hivyo mapato ya Mtwara na Zanzibar yanatumika kama gharama za Mafuta,kulipa wafanyakazi na kulipa gharama za Bandari.
 
Hi boati inayokod8wa mil 45 ni usawa upi uzito ?
 
Back
Top Bottom