Fursa: Gharama Halisi za Kuanzisha Radio ya Jamii (Community Radio)

Radio Producer

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
724
295
Heshima kwenu wadau!

Leo napenda kuelezea kwa kina gharama na mambo muhimu kuhusu radio jamii. Natumaini nitajihidi kuelezea angalau kwa asilimia tisini hivi.

1. Radio Jamii (Community Radio): Umiliki
Ni radio ambazo humilikiwa na jamii husika. Ni radio zenye lengo la kusaidia jamii husika kupiga mbele katika maendeleo.

Mara nyingi radio hizi zinaweza kumilikiwa na wanajamii wenyewe, taasisi au mtu binafsi kupitia taasisi, hatua za kuomba leseni ya radio jamii ni sawa na hatua za kuomba leseni kwa radio zingine.

2. Covarage (Eneo linalotakiwa radio isikike)
Kwa mujibu wa TCRA, radio jamii zinaruhusiwa kutumia kifaa cha kurushia matangazo (Transmitter kisichozidi Watts 500. Kitalaamu Watts hizi 500 zinaweza kurusha matangazo kwa umbali wa kilomita 50, ground level, sana sana inategemeana na eneo kuna zingine huenda mbali zaidi hata kilomita 200 kwa Watts hizohizo.

3. Jinsi ya kujiendesha kimapato.
Kwa mujibu wa TCRA radio hizi siyo za kibiashara na kwamba kiuhalisia kabisa haziruhusiwi kupokea matangazo ya biashara japo kwa bongo bado hilo halijatekelezeka. Sasa zinawezaje kujiendesha hizi radio? Nifuatilie:-

Radio Jamii nzuri ni ile yenye msingi ulioanzishwa na ASASI au kampuni isiyotengeneza faida (Limited by guarantee) kwa mantiki hiyo radio hii itakuwa na sura ya kwamba iko chini ya taasisi husika. Sasa basi kujiendesha kwa hii radio kunatokana na projects grants. Namaanisha ruzuku kutoka mashirika mbalimbali. Yaani kuna mashirika mengi saaaaaaaana yana pesa za wazi kwa taasisi kama hizi za media, unachotakiwa ni kuwa staff angalau watatu vichwa wanaoweza kuandika proposal za nguvu pamoja na kusimamia miradi kwa ufasaha hakika utashangaa.

Kuna radio moja hapa nchini hawapokei matangazo ni radio jamii na wanalipa vizuri sana staff wake, wanatumia mfumo huu. Yaani wao unakuta kwa mwaka wana project 3 kwa mpingo moja ina milioni 400, nyingine milion 100 na nyingi million 700, kwa kweli zinawatoa sana.

Pia unatakiwa kuwa na network nzuri na mashirika na kimataifa, UNESCO ni moja ya shirika linalosaidia sana radio jamii hapa nchini, kwa sana. Kuna BBC Media Action, UNCEF, UNDP, Balozi za nchi za Ulaya, n.k

Nadhani nimetoa picha halisi ya namna nzuri ya jinsi radio jamii zinavyojiendesha.

Lakini pia upande wa Matangazo unaweza kuendelea kupokea pokea, na kma aukiwa sehemu nzuri ambayo haina ushindani sana unaweza kuwa unapata hata mpaka milioni 20 kwa mwezi.

4. Gharama halisi sasa za kuanzisha radio hii ya jamii.

i. Usajili TCRA
Application Fee ni Tshs 1,700,000/=
Gharama zingine nikulipia Frequncy kila mwaka Tshs 1,700,000/=
Gharama za kuandikiwa maandiko ya kusubmit TCRA sisi tunafanya Tshs 1,500,000/=
Jumla suala la usajli TCRA= Tshs 4,900,000/=
ii. Gharama za vifaa.
Kampuni yetu inapackages za vifaa mbalimbali kwa order. Package ya bei rahisi kabisa ikiwa full ni hii hapa:-

Kleio Gold Package consisting of:-
1. Studio and Transmitter!
  • Behringer X1204 12 channel audio mixer,
  • Numark MP103 CD/MP3 player,
  • 1 x Behringer XM8500 dynamic microphone.
  • 1 x Behringer C1 condenser microphone,
  • 2 x table mic stands and 2x 6m mic cables,
  • DELL Inspiron note book computer with audio editing and play out software pre-installed,
  • AV30 powered monitor speakers (pair) and monitor speaker mute/fade control,
  • Sennheiser HD203 headphones, Alesis compressor/limiter,
  • 300W TX300 Italian FM stereo transmitter,
  • Polar 114Fm folded dipole antenna and 50m RG 213 RF cable with antenna clamp and RF cable clamps.
  • Major equipment pre-installed in a table top rack, all necessary cables provided pre-made.

2. Studio Production
Behringer X1204 12 channel audio mixer,
Numark MP103 CD/MP3 player,
1 x Behringer XM8500 dynamic microphone.
1 x Behringer C1 condenser microphone,
2 x table mic stands and 2x 6m mic cables,
DELL Inspiron note book computer with audio editing and play out software pre-installed,
AV30 powered monitor speakers (pair) and monitor speaker mute/fade control,
Sennheiser HD203 headphones

iii. STL-Studio Transmitter Link
  • RVR STL 5W complete with transmitter, receiver, 2x 9dB Yagi antennas and 2x 20m low loss cables terminated.

JUMLA KUU YA BEI YA VIFAA HIVI PAMOJA NA KUSAFIRISHA MPAKA DAR ES SALAM AIRPORT NI TSHS 35, 618, 520/=

IV. Gharama za Customs Airport.
Vifaa vya radio vinamsamaha na pia kama ni taasisi unaweza kuomba msahama wa kodi lakini sipowezekana gharama halisi ni hizi hapa:-

Import duty 25% = 35, 618, 520 x 25%= 8,904,630/=
VAT 18% = 35, 618, 520 x 18% = 6,411,340/=
Agent Fee Tshs 300,000/=

Jumla ya Gharama za customs zote ni Tshs 15, 615, 970/=

Kwa hiyo jumla kuu ya vifaa vyote, transmitter, antenna, STL na vifaa vinatosha studio mbili onair na production mpaka vinakufikia kwako hapo ulipo ni Tshs 51, 234, 490/=

iii. Gharama za kujenga mnara wa mita 40.
Tshs 8,000,000/=

iv. Gharama za kukufungia mitambo na kutoa mafunzo completely.
Tshs 3,000,000/=

v. Gharama za kukodi jengo la studiona kuirekebisha kuwa katika hadhi ya studio na furnitures tukadirie Tshs 3,000,000/=


SO JUMLA KUU MPAKA UNAMILIKI RADIO HII INAGHARIMU TSHS 70,134, 490/=

NB: Ukitaka kuanzisha ya biashara unaongeza Transmitter tu angalau ifike Watts 1000, hii inaweza ongeza pesa kidogo kama m10 hivi.

Kwa huduma hizi wasiliana nasisi:-

Radio Consult LTD
Jengo la Sekta ya Chai (RSTGA), Nanenane Mbeya.
P O Box 2213.

Website: radiot
Email: consultancy@radiotz.com
Facebook: https://www.facebook.com/radiotz?ref_type=bookmark
au kwa PM.

Nawashukuru wadau wote!

Moj ya kazi zetu
DSC00446.JPG
 
nasikia frequency tanzania zimeisha je ni kweli? naomba unisaidie na mchanganuo wa redio ya biashara

Dar es salaam ndiyo zimeisha. Huku mikoani bado. Radio ya biashara we ongeza hata m 15 tu kwenye huo mchanganuo mambo yanaenda sawa.
 
Asante sana kwa ufafanuzi mkuu natumai umekata kiu ya wadau waliotaka kujua abc kuhusu hilo.
 
Back
Top Bottom