Fundraising for JF Development. Tusifanye politics bila vitendo

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Kwa muda mrefu sasa Jamii Forums imeshajulikana na sifa kemkem imepata. Lakini kwa kiasi kikubwa inajulikana sana kwa wasomi na wachache wenye uelewa wa masuala ya internet.

Kwa utafiti nilioufanya japo sio rasmi, nimegundua kuwa tunapokaa sehemu na kuanza kuongea mambo mbalimbali, tunaombwa source, na kila tunapotaja Jamii Forums, wengi na ambao tunawapigania hushangaa na wengine hutaka waione hiyo jamii forum wakidhani kuwa ni gazeti. Sasa ndo nikapata wazo kuwa kazi nzuri tunayoifanya kuipigania nchi yetu, si vibaya na walengwa wakalijua hili. Hivyo mawazo yangu ni kuwa viranja waandae Business Plan nzuri ikiwa na lengo la kuanzisha gazeti. Baadae tukijua gharama za kuanzisha hilo gazeti, kila mwana JF mwenye moyo atajua achangie kiasi gani kwa ajili ya kufanya kitu fulani.

Gazeti hili la Jamii Forums litasomwa kwanza na sisi wadau na ndio itakuwa njia mojawapo ya kuichangia JF kwa njia rahisi. Sio mbaya gazeti hili hata likitoka mara moja kwa wiki. Wananchi watajua ukweli na harakati zote tunazozifanya. Hii kwa mawazo yangu najua itasaidia sana. Mapambano tunayoyafanya humu yanaonwa na wachache ukisema uanzishe movement wenye taarifa ni wachache.

Naomba niwasilishe kwa wadau na mniambie imekaaje hii. Nasubiri comments.
 
wamiliki wa gazeti watakuwa nani...? JF au JF members....?
 
we cannot re-invent the wheel, Tayari yapo magazeti yanapigania maskahi ya taifa. Kwanini tusiwekeze nguvu zetu huko? Na namna nzuri ya kuwekeza nguvu zeti ni kuhakikisha kila mmoij awetu ananunua nakala yake kila wiki. ][/SIZE]
 
Sauti ya wengi ikitoka kwa kupitia source mbalimbali inasound vizuri. Pia unaposema we-cannot unamaanisha wewe na nani?
 
Wazo lako ni zuri naunga mkono hoja, ukiangalia jumla ya members wa jamii forums ni kama 32,000 tu Tanzania nzima ambayo ina wakazi milioni arobaini.

Kwa takwimu hizi ni vigumu watu kuelewa nini kinajadiliwa humu ndani juu ya mustakabali wa maisha na taifa kwa ujumla. Si kila mtu mwenye uwezo/nafasi ya kutumia mtandao sehemu kubwa ya Tanzania haijafikiwa na huduma hii, hivyo basi njia rahisi ya kuieneza JF ni kupitia gazeti ambalo ni rahisi kufikiwa/kusomwa na kila mtanzania.

Ningependa kuona jambo hili linaungwa mkono na wadau wengine humu ndani.
 
avatar28647_3.gif

senene
 
Nahukuru kama umeliona hilo kwa sasa registered members wa JF ni

Registered Members: 31,661
 
Kwa muda mrefu sasa Jamii Forums imeshajulikana na sifa kemkem imepata. Lakini kwa kiasi kikubwa inajulikana sana kwa wasomi na wachache wenye uelewa wa masuala ya internet. Kwa utafiti nilioufanya japo sio rasmi, nimegundua kuwa tunapokaa sehemu na kuanza kuongea mambo mbalimbali, tunaombwa source, na kila tunapotaja Jamii Forums, wengi na ambao tunawapigania hushangaa na wengine hutaka waione hiyo jamii forum wakidhani kuwa ni gazeti. Sasa ndo nikapata wazo kuwa kazi nzuri tunayoifanya kuipigania nchi yetu, si vibaya na walengwa wakalijua hili. Hivyo mawazo yangu ni kuwa viranja waandae Business Plan nzuri ikiwa na lengo la kuanzisha gazeti. Baadae tukijua gharama za kuanzisha hilo gazeti, kila mwana JF mwenye moyo atajua achangie kiasi gani kwa ajili ya kufanya kitu fulani.

Gazeti hili la jamii forums litasomwa kwanza na sisi wadau na ndio itakuwa njia mojawapo ya kuichangia JF kwa njia rahisi. Sio mbaya gazeti hili hata likitoka mara moja kwa wiki. Wananchi watajua ukweli na harakati zote tunazozifanya. Hii kwa mawazo yangu najua itasaidia sana. Mapambano tunayoyafanya humu yanaonwa na wachache ukisema uanzishe movement wenye taarifa ni wachache. Naomba niwasilishe kwa wadau na mniambie imekaaje hii. Nasubiri comments.

wazo zuri.

kama Mwana Halisi.
 
Wazo zuri.

Basi toa mapendekezo ya muundo wa gazeti ilo. Je,mawazo na maoni ya wanaJF yatawekwaje kwenye ilo gazeti? Pia JF ina sub forums nyingi,sasa ilo gazeti litakuaje ili kuhakikisha mawazo na maoni kutoka kwenye hizo sub forums yanakua considered?
 
we cannot re-invent the wheel, Tayari yapo magazeti yanapigania maskahi ya taifa. Kwanini tusiwekeze nguvu zetu huko? Na namna nzuri ya kuwekeza nguvu zeti ni kuhakikisha kila mmoij awetu ananunua nakala yake kila wiki. ][/SIZE]
kwa mtazamo huu... tungeishia kuwa na gazeti la uhuru, daily news, kiongozi na mfanyakazi

sijui tungesoma wapi rai, mwanahalisi, citizen nk.
 
Ni wazo zuri ila litakuwa more appealing kama michango hiyo itapatikana kwa kununua hisa yaani lets Jamii forum float shares! ila ziwe limited maana mtu kama RA anaweza akainunua jamii Forums na ku-dictate vitu gani viwekwe humu! tukala goli za ugoko :wink2:!
 
Back
Top Bottom