Fundraising for JF Development. Tusifanye politics bila vitendo

Wazo lako zuri ikiwa na maana ya kuwafikia wengi pamoja na watu wa Nyamuswa na Nyamwaga pia kwa sababu pale internet hata ya simu ni issue. Ila kwa mtazamo wangu, yapo magazeti ambayo yana mawazo sawa tu na wengi humu JF, sio kusema kwamba kuongeza gazei jingine la mtazamo sawa tunakosea, ila nadhani kama tukiweza kuitangaza ikiwa hapa kwenye net, it will serve the same purpose. Pia kuwekeza kwenye gazeti yapo mengi ya kutegemea faida e.t.c kwa sababu tayari ni investment kitu ambacho kinaweza kuleta finger - pointing.
Otherwise a good idea na I support.
 
Kwa muda mrefu sasa Jamii Forums imeshajulikana na sifa kemkem imepata. Lakini kwa kiasi kikubwa inajulikana sana kwa wasomi na wachache wenye uelewa wa masuala ya internet.

Kwa utafiti nilioufanya japo sio rasmi, nimegundua kuwa tunapokaa sehemu na kuanza kuongea mambo mbalimbali, tunaombwa source, na kila tunapotaja Jamii Forums, wengi na ambao tunawapigania hushangaa na wengine hutaka waione hiyo jamii forum wakidhani kuwa ni gazeti. Sasa ndo nikapata wazo kuwa kazi nzuri tunayoifanya kuipigania nchi yetu, si vibaya na walengwa wakalijua hili. Hivyo mawazo yangu ni kuwa viranja waandae Business Plan nzuri ikiwa na lengo la kuanzisha gazeti. Baadae tukijua gharama za kuanzisha hilo gazeti, kila mwana JF mwenye moyo atajua achangie kiasi gani kwa ajili ya kufanya kitu fulani.

Gazeti hili la Jamii Forums litasomwa kwanza na sisi wadau na ndio itakuwa njia mojawapo ya kuichangia JF kwa njia rahisi. Sio mbaya gazeti hili hata likitoka mara moja kwa wiki. Wananchi watajua ukweli na harakati zote tunazozifanya. Hii kwa mawazo yangu najua itasaidia sana. Mapambano tunayoyafanya humu yanaonwa na wachache ukisema uanzishe movement wenye taarifa ni wachache.

Naomba niwasilishe kwa wadau na mniambie imekaaje hii. Nasubiri comments.

Samahani sana sikusoma hii post yako mapema. Ila nimegundua kuwa kwa vile wewe ni mgeni hapa huenda hufahamu kuwa tulikuwa na effort ta namna hiyo, yaani kuchapisha majumuisho ya mijadala yetu kwenye vijitabu. Wazo hilo lilianza tangu mwaka 2007 wakati tungali tunajulikana kama JamboForums, na nakumbuka nilikuwa nimejitoilea kuhakiki mijadala inayohusu Katiba (tulishalijadili hilo siku nyingi sana hapa). Baada ya forum hii kuwa active sana katika kuibua kashfa mbalimbali zikiwemo za Richmond na EPA, kulitokea hujuma iliyosababisha JamboForums kufa, na kuanza upya kama JamiiForums unayoijua leo. Transformation ile iliendana na forum kupata wanachama wengi sama kwa kasi kubwa na mada zikawa ni nyingi sana zenye kubadilika kwa kasi ya mwanga. Majumuisho hayo yalisababisha iwe ni vigumu sana kuzihakikii post zote za hapa JF.

Wazo linalowezekana ni kuwa na publication volume moja ya JF ikijumuisha mada zote kwa kipindi kichaojulikana, kwa mfano miezi minne ( mara tatu kwa mwaka) au miezi sita (mara mbili kwa mwaka) hasa kwa vile mada nyingine huchukua muda kuzi-exhaust.

La kuongezea pia ni kuwa kulikuwa na T-shirt za JamboForums kama hii kwenye picha zilizokuwa zimetayarishwa kwa ajili ya fundraising lakini zikasihiwa kutolewa bure kwa wanachama. Wiki hii nimegundua kuwa kuna T-shirt nyingine za Jamii Forums zitatoka. Jitahidi unune nyingi uzigawe kwa mashabiki na watu wengine waisojua kiunga hiki ili nao waweze kuvutiwa na kujiunga.

IMG_20110218_235331.jpg
 
Poa mkuu lakini, likiwepo moja kama Mwanahalisi si mbaya. Tusikate tamaa. Sio lazima kila mjadala uonekane , makala zitatumwa nzuri tu.
 
Kwa muda mrefu sasa Jamii Forums imeshajulikana na sifa kemkem imepata. Lakini kwa kiasi kikubwa inajulikana sana kwa wasomi na wachache wenye uelewa wa masuala ya internet.

Kwa utafiti nilioufanya japo sio rasmi, nimegundua kuwa tunapokaa sehemu na kuanza kuongea mambo mbalimbali, tunaombwa source, na kila tunapotaja Jamii Forums, wengi na ambao tunawapigania hushangaa na wengine hutaka waione hiyo jamii forum wakidhani kuwa ni gazeti. Sasa ndo nikapata wazo kuwa kazi nzuri tunayoifanya kuipigania nchi yetu, si vibaya na walengwa wakalijua hili. Hivyo mawazo yangu ni kuwa viranja waandae Business Plan nzuri ikiwa na lengo la kuanzisha gazeti. Baadae tukijua gharama za kuanzisha hilo gazeti, kila mwana JF mwenye moyo atajua achangie kiasi gani kwa ajili ya kufanya kitu fulani.

Gazeti hili la Jamii Forums litasomwa kwanza na sisi wadau na ndio itakuwa njia mojawapo ya kuichangia JF kwa njia rahisi. Sio mbaya gazeti hili hata likitoka mara moja kwa wiki. Wananchi watajua ukweli na harakati zote tunazozifanya. Hii kwa mawazo yangu najua itasaidia sana. Mapambano tunayoyafanya humu yanaonwa na wachache ukisema uanzishe movement wenye taarifa ni wachache.

Naomba niwasilishe kwa wadau na mniambie imekaaje hii. Nasubiri comments.

kWA jinsi waheshimiwa wanavyochukia JF sidhani kama litapata registration na hata likipata litapigwa Ban fasta itakapogusa kunako.
 
Hapo ni vema sana, watajua nini tunazungumza hata wabunge wetu wenyewe hawaijui technology hii,

Naomba kuunga hoja
 
Ni wazo zuri sana kwa malengo ya kuelimisha jamii msakabadi wa serikali yetu na madudu yake pamoja na mambo ya kijamii

nakubaliana na wazo na kushauri kuwepo na limited shares kwa JF members na msiogope maana inawezekana kabisa

Big up uliyetoa ushauri huu
 
JF haiwezi kuwa huru ikiwa printed, ila kinachowezekana ni kutengeza e-book CD ,na kuzisambaza bure kwa wananchi,and if posible ziweze hata kuplay ktk deck za dvd za kawaida.

Serikali na sheria ya vyombo vya habari italifunga hilo gazeti,hakutakuwa na uhuru wa editor atabanwa na sheria,
wana JF walio nje ya nchi, wenye uraia wa Nchi zingine wanaweza kufanya hivyo na kuliprint China, then linaingizwa in TZ, either kwa njia za panya, au kwa njia halali.

So we can have Jamii Forums lnc. registered in USA, then print content inaaandiliwa na kuwa emailed kwa printer in China, then tunai-ship bongo, gharama ni ndogo mmno kuliko hata kuprint in Tz.

Magazeti mengi makubwa yanakuwa printed in China siku hizi
 
Back
Top Bottom