Fumbo: Huko Ndani Kuna Nini?

Ukitaka faulu Ms J, tambua love sio kusudi,
Ukitaka jibu kamili, elewa ngono ndio kusudi,
ndani nje kama laana, ukute wala sio lake kusudi,
ila tu zake tamaa, yamfanya onekana na kusudi.

Kiumbe majibu hana, bure utajikondesha,
waweza mjua hasa, na bado akakuendesha,
kama ndani arudi, basi tambua wamkosha,
kama nje atabaki, huna budi ni kujiondosha.

karibu tena ADii, wazo lako mwanana,
najua hukusudii, japo wakolea hina,
hisi zangu hurudii, fumbo lifanya fumbana,
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!

fumbo si la ndoa, poswa wala kuposa,
wote mmetia doa, na jibu mmelikosa,
msichoke kuchokoa, punde jubu tanusa,
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!

wengine wanisabahi, bila majibu kutoa,
leo ninawastahi, kesho nitawaumbua,
nangoja wazo sahihi, kama karanga chambua,
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!

sioni hata wakongwe, wapi mekimbilia,
au wataka wahongwe, jukwaa kulirudia?
kama vipi walengwe, huko wakojichimbia
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!
 
Hiyo wife material unavyoikazania hebu tupe darasa ndo wapoje hao wasije kuwa waloimbwa na ace hood.
@mis jud
ntarud ngoja nkaumize ndonga ila always home sweet home na our homes is where our heart is and always kwa wanaume our heart is somewhere between legs. MWANZI PAHALA PAKE LOH.

nimekusoma mkuu, bold nimenakili,
wanena yalo makuu, japo ni kwa ubahili,
fumbua ukae juu, kwa mwanzi we mkali,,
tupe walau nukuu, hata ikiwa mithali,

hapo bitwini dhe legs, ndipo palipo na jibu,
mwataka za nini kiss, hadi mwageuka bubu,
zaenda wapi stress, bila ya hata kutubu,
tupe walau nukuu, hata ikiwa mithali,
 
nimekusoma mkuu, bold nimenakili,
wanena yalo makuu, japo ni kwa ubahili,
fumbua ukae juu, kwa mwanzi we mkali,,
tupe walau nukuu, hata ikiwa mithali,

hapo bitwini dhe legs, ndipo palipo na jibu,
mwataka za nini kiss, hadi mwageuka bubu,
zaenda wapi stress, bila ya hata kutubu,
tupe walau nukuu, hata ikiwa mithali,

JF kuna vipaji, hongereni!
 
Ukitaka faulu Ms J, tambua love sio kusudi,
Ukitaka jibu kamili, elewa ngono ndio kusudi,
ndani nje kama laana, ukute wala sio lake kusudi,
ila tu zake tamaa, yamfanya onekana na kusudi.


Kiumbe majibu hana, bure utajikondesha,
waweza mjua hasa, na bado akakuendesha,
kama ndani arudi, basi tambua wamkosha,
kama nje atabaki, huna budi ni kujiondosha.

Yaani mkielewa hili kwahakika wala hamtajikondesha......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom