Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 918
1.
Wapendwa nijuzeni, huko ndani kuna nini?
Tangu zama nilidhani, huko ndiko utamuni,
ni punde nimebaini, si kutamu asilani,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
2.
Kiumbe huyu makini, hakomi kurandaranda,
Amfumapo mwandani, huparamia kitanda,
Kasiye kama tufani, hutupia mbali mkanda,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
3.
Na kazi anayo mwenzi, miguno na mashauzi,
Ka kufumbata konzi, kiumbe utamuenzi,
kwini ataitwa manzi, kingi ataitwa mwanzi,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
4.
mwanzi ukitiwa pake, pumzi huenda mrama,
yatisha hayo makeke, vigori hupata homa,
eti imefika mwake, ya nini tena hujuma?
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
5.
Ikishaingia mwake, ndipo huanza hujuma,
Mithili ya mrusha teke, kiumbe hurudi nyuma,
achomoa mwanzi wake, si haki bali dhuluma,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
6.
ikiwa ndani kutamu, vipi mwanzi usidumu,
Upatemaliza hamu, na kiumbe ajikimu,
faidi hiyo karamu, manzi asijelaumu,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
7.
Kama ndani kuchungu, kwa nini asibaki nje?
Heri kuchapwa virungu, ndani katu usionje,
Wasikupate machangu, peponi mbuga uchanje,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
8.
Kuingia na kutoka, ndo mchezo wa kikubwa!
Mwapata vipi mizuka, hata kukacha ubwabwa?
Na mwisho wake mwachoka, hamkomi nyie wakubwa!
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
9.
Naleta kwenu wazo, siku zote mfurahi,
Mtaimaliza mizozo, yale mambo ya kuwahi,
Mtakipata kitulizo, kama wenzenu wa Bahi,
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
10.
Ukiingia sitoke, ukitoka siingie!
Yako ashiki ufyeke, na mwandani uringie,
Vigori wasiteseke,maisha wafurahie!
Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni
nawatakia tafakari njema ya fumbo hili na weekend njema
mbarikiwe sana wapendwa,
Glory to God!