KUTOKA: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi

mose

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
284
232
Habarini Wote.

Nimepata kufanya Utungaji wenye kufungamana na mawaidha yajayo na mada mbalimbali katika Jukwaa hili Jamii -- kwa faragha.

Mapenzi yangu yamekuwa ni kwamba kama hali bado haijaandaliwa ama umma haujajiandaa, si vema kufunua na kubayanisha mambo ama mashauri fulani juu ya Wanajamii, Mifumo na Dini.

Ninaridhika sasa ya kwamba, ndani ya hili jukwaa kizazi sahihi cha wanamafikara kimeshawasili...

Ninafarijika na kuazimia sasa kushiriki mawaidha ambayo awali niliyafanya kwa ajili watu wenye fikra huru -- japo niliowaandikia hapo nyuma si kuwa niliwategemea hasa kunielewa, ila kuwatumia wale kama vigezo vya kuandaa matanuko wa mashauri, uono na upeo kubayanisha mambo. Kwa kuwa wapendwa wangu hasa ni wale walio ni wadadisi, wachunguzi, wenye kiu ya kuhama kutoka kwenye 'Utumwa wa Kiakili' kuelekea kwenye uwanda wa ahadi--Uhuru katika dimensha zote za mwili, akili na roho...

Kwa wale wote wanaojijua ndani yao kuna ujasiri na wito wa kutoka, safari hii imeshaanza...

Tutaelekezana, kutaamulisha, kupashana, kufundishana, kufundwanishana n.k kusudi hakika ya Taifa Jipya la watu -- watu walio Wapya kwa Mioyo na Dhamira katika kuongozea kuliko bora zaidi iweze kutimia.

Ninawahakikishia uwezo wa kusonga kwenye kheri upo, na mambo makubwa sana yanatungojea safarini... Kwa kuwa safari hii ni safari ya ajabu, maana zawadi yake ni ulimwengu wote kuutwaa... Anga si kikomo...

Niwatake na kuwasihi enyi kizazi cha mitazamo huru na wazi zaidi kwa kheri na jaala njema zaidi, msikatishwe tamaa na lolote kulingana na hapa tulipo kwa kufananisha na kule tunakotamania...

Tuelekezana yote kwa lugha ambayo wote tunaifahamu vizuri -- Kiswahili, tutazungumza yote kuhusu 'Nishati' hadi 'Wakti'... Tutahandisi mambo na mitambo ya kuweza kuyafanya hata makuu--kimawasiliano na uchukuzi... Tufanya namna mpya kuvuna nishati, na tutasafiri hata nje ya sayari yetu ya dunia kwa namna moja hata nyingine... Haijalishi hili litatimia ndani ya miaka 80 - 100 ijayo-- ila ninawahakikishia sehemu ya hizi jitahada zitakuwa hapa hapa kwenye hii ardhi yetu tuuitayo Tanzania kwa leo na Afrika kwa kesho... Kwa kuwa roho ya ushindi huu tayari ipo miongoni mwetu, na kazi ni kwetu...

Msihofu miongoni mwetu ni nani atatuongoza... Zama hizi si zakuongozana. Kwa kuwa tupo katika zama ambazo Uongozi ni Kuchagua na Kujichagulia. Kila mtu kwa nafsi yake yampasa kuamua, ikibidi kuunganisha nguvu zetu kwa ajili ya jambo lolote la kheri ya pamoja, tutajaunda namna ya taasisi zisizoongozwa na 'siasa' za utaratibu ila 'itifaki' sahihi na uelewa kamili juu ya jambo liwalo lolote.

Na sasa nilete kwenu, mashauri anuai -- mapana na marefu juu ya kile ninachokifananisha na kumbukumbu la vitabu vitano vya Musa -- Pentauki, kwa maana ili kufika ustawi na staarabu mpya mambo kama yale yale yaliyosadifiwa kwenye vitabu hivi vya mapokeo yatahusika kwetu sote... Japo huu inakuja kuwa kile ambacho Francis Bacon alikitaja kuwa ni 'Instauration of Knowledge' katika kuielekea 'Atlantisi Mpya'...

Ni wakati wa kuyaupisha mafundisho na maarifa ya zamani...

+++++++++

Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi seh. I
5 Septemba 2011 saa 12:15 Asubuhi
Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi

(Iliandikwa kwa rafiki kama mchango wa mawazo na kwa uchochezi wa fikra)

Pendo lililobarikiwa dada MwKT,

Siku kadhaa nyuma ulileta habari jukwaani juu ya ‘Kuanzishwa kwa “un-women” – kaeni mkao wa kula’ katika jukwaa la siasa.

Nilipendezwa na habari hii na hasa kwa kuzingatia mapenzi yangu juu ya mabadiliko yenye kuleta kheri katika jamii niishiyo na ulimwengu kwa ujumla. Ni jambo lenye kupendeza kutambua harakati za watu mbali mbali na kujaribu kuunganisha maono ama kufanya fikra tunduizi.

Amko la wanaharakati katika kutunga na kupelekea taasisi kama chombo chenye kuongezea kwenye ushawishi, utendaji chini ya mamlaka, mifumo na utekelezaji wa mipango ama maelekezo; linavutia wote walio na dalili za kuamkia huko kimwelekeo wa fikra na imani lakini pia zaweza kuvuta ukosoaji wa kiudhanifu—yaani juu ya dhahania ya mpango mzima vile kusema, filosofia ama asili ya mwongozo wake na misingi ya ustawishi wa jitihada.

Kwanza kabisa nitambue ‘unene’ na uzito wa michakato uliopo katika vyombo vya kimataifa na utengeneaji wake. Itifaki zake ni namna ya mifano yenye kufafanua mifumo na taratibu katika kuratibu matukio kulingana na makutano ya watu na michakato. Na hivi nitambue msuko wa chombo kama namna ya mipaka na mamlaka juu ya mambo yake na tena kwa muktadha wa kufanyika kwake.

Ujio wa chombo hichi kwako umekusukuma kupenda kuwaatarifu wanajamii wenzako; maana yake: uwezekano wa fursa mbali mbali--ajira, na mipango ya maendeleo. Na vile vile umepata kusema : hivyo havitaweza kuja kwenye sahani ya dhahabu… Kisha ukazungumza juu ya ‘nafasi za juu’… Halafu ukataja mjumuisho wa mataifa na hivi kuonesha kutambua msukumo wa nguvu ya uwezo na ushawishi kulingana na sehemu watu watokayo kmf Amerika ya Kati, Scandinavia na nchi nyingine za Afrika katika ugombeaji wa nafasi za kazi na labda vile vile kumaanisha vyeo vya usimamizi na utendaji pia.

Pia ukazungumza dokezo la kukabiliana na adha ya shughuli kwa kutaja umuhimu wa watarajiaji nafasi kudumu kukesha katika jitihada kwa kufuatilia kwa makini nyenendo za michakato ya uanzilishi.

Nikushukuru kwa angalizo na kushiriki habari na wenzako kama mimi na wengine.

Niliingie neno la leo kwa kutanabaisha jambo kuhusu ulimwengu wa kuona mambo kwa kiini cha usababishaji na matokeo yake.

Tumezoea kuona mipango ikipangwa na jitihada kusukwa na matokeo kuainishwa ili kuelekeza sura ya utendaji na utekelezaji. Binadamu toka zamani hadi hii leo tunaona upangiliaji wa mambo ni kama sanaa inayoweza kufanywa kamilifu ijapokuwa matokeo yake si kwamba daima huwa ni hivyo. Kuna vitu vinaweza kupangilika lakini mara kadha wa kadha mashauri juu ya watu ama jamii si yenye kupangilika na kujitosheleza bila mikingamo ama kadhia ya namna fulani kujitokeza. Labda hii tuseme inatokana na ukweli kwamba binadamu ni kiumbe chenye uwezekano wa fikra binafsi na utashi na hivyo haiwezekana kuwakundisha watu pasipo ridhaa na makubaliano na wao wenyewe kwa wakati.

Basi katika ulimwengu wa makubaliano kuna yale ya juu juu na kuna yale ya ndani. Vivyo hivo kuna kuona mambo kwa sura ya juu juu na kuona mambo katika sura ndani. Naam, vile vile kuchukulia jambo kwa sura ya nje na kuchukulia mambo kwa sura ya ndani. Uhusiano wa mambo ya ndani na yale ya nje ndiyo hujaa kuzaa uthabiti wa makubaliano na labda pia kusema, umadhubuti wa jitihada kulingana ufananikaji wa dhamira. Hata hivyo, kupo kuridhika na mambo ya nje bila kuchunguza misingi yake; na hata tena kwa namna kama hiyo; kutotambua athari za matokeo kwa kutozingatia uasili wa jambo lenyewe kwa uzima wake. Haya mawili hujitokeza hasa katika maisha ya mwanadamu kwa kutoangalia/ujisahau wake wa mashauri yaandamayo dhamira zake kwa wakati hadi wakati.

Na hivi leo ningependa kuzungumzia nafasi ya Tekinokrasia katika ustawi mpya kwa wanadamu katika zama hii mpya.

Nimechagua mchango wako toka jukwaani kujenga usuli wa shauri langu la leo kwako na kwa wadau wengine; kwa kuwa wanawake katika zama hii wanachukua sura takatifu ya michakato ya jamii na ustawi. Na hivi udadavuaji wa utata wa hali ya ustawi wa jamii unachipukia na kuanza kwa kumuelewa mwanamke na sifa ya kike ya uumbaji wote--jambo lililosahaulika katika nidhamu na uelewa wa wanadamu wa leo.

Katika hali ya juu juu shauri lako juu ya uanzishwaji wa baraza la wanawake-umoja wa mataifa, umelenga hasa fursa za ajira na labda kwa upande mwingine usiowazi ni shauku yako ya chombo hiki cha wanawake na kwa ajili ya wanawake. Kuangalia upande wa ajira-- na hapa umewakumbusha hata wanaume pia kutazamia nafasi; kulinikumbusha mashauri juu ya uchumi na siasa—na miye nikapata hamu nije kushiriki na wewe na wengine fikra tunduizi mintarafu vyombo vya jamii na nafasi yake katika kuchochea ama kuleta mabadiliko.

Jambo la kwanza ambalo halinifurahishi na vile kuniacha nikisikitika ni ukweli wa kwamba nafasi za kazi na ajira kugombaniwa na kushindaniwa. Ni ukweli mchungu na ambao mimi siupendi kabisa. Naitekeleza chuki yangu dhidi ya huo kwa kuleta fikra mbadala za jinsi ya kutokomeza sura hiyo ya mambo kwa ghadhabu ya kuwakilisha mawazo ya upeo na maarifa yangu kwa wakati. Lipo tatizo kubwa katika jamii ya leo ambalo ladumu kwa mwendelezeo ama udumishwaji wa dhana ama pia fikra ya kuwa maisha hayanabudi kustahimilishwa kwa urasmi wa ajira za kazi kwa ajili kipato kwa kutumikia chombo fulani na hata kama makusudi mazima ya hicho chombo si yenye kueleweka kwa mtu husika kujihusisha nacho—ama kupimwa/kujipima ikiwa mna dhamira bora kabisa kuwezekana ya utashi ndani ya mtu mwenye kutaka kujihusisha hicho chombo. Hili kwa leo sitazungumza sana kwa maana ni shauri linapelekea kipengele kimoja katika tatu cha kuyaleta mabadiliko kamili ya kijamii katika muktadha wa kufafanua Meritokrasia. Leo nataka kuzungumzia Tekinokrasia kwa mapana.

Dhana ya ushindani kwa lolote lile ni jinsi ya kiume ya mambo. Akili inayofikiria katika minajili hii ni namna ya akili ya kiume. Jamii inayovumilia na kudumisha mashindano ya huyu kupata na yule kukosa, ni yenye jinsia ya kiume na bila shaka inadumisha namna ya mifumo dume katika kusimama kwake.

Mchezo wa ajira ama kutafuta kipato unachezwa katika kiwanja cha uchumi na mabadilishano ya kijamii. Ikiwa mtu hatataka kuusoma uwanja kabla ya mpambano hapana shaka mtu huyu atakuja kutingwa na adha ya ujinga wake kwa kukosa maarifa ya kutosha katika kuungia mchezo. Matokeo yake katika kuuelekea mwisho wa mchezo au kadri mchezo ukiendelea--huenda yakaambatana na dosari nyingi ambazo zitajitokeza kwa sura ya kama mtu kupata hiki kwa gharama ya kukosa kile; ama kupata hili badala ya lile lililotarajiwa ama kutakwa. Basi yampasa mtu kuwa ni mwenye kujitambua ili apate kutambulika katika uwanja wowote wa jitihada chakatuzi. Na hivi aje kuvuna matokeo kwa stahiki ya nia yake katika jitihada sahihi.

Na hili linajenga hoja ya msingi katika filosofia ya Tekinokrasia. Kweli ya kwamba mtu hawezi kuunda bila ya kuwa na ramani; hawezi kuanza safari na hali hajui mapito; hawezi kukatiza kokote eti akafikiri atafika kwa kuwa tu mwenye kutimba maguu… Je, ajijua yeye ni msafiri? Je, ajua uhusiano wa hapo alipo na kule anakokwenda? Je, ajua akiba yake safari na vipindi vya kuitekeleza hiyo safari? Je, ajua jambo la muhimu katika safari ni safari yenyewe? Na je, yu ajua yeye kuwa palipo na nia daima safari hazikomi na hivi penye nia pana njia ? Na basi lilikokuu kuliko yote-- je, yeye yu ajua Nia yake ambayo ni ufunguo wa dhamira yake mwenyewe ?

Kukosa kuelewa Nia zetu hasa daima kutatuacha sisi kama watangajitangaji katika nchi za wageni. Ni kusahau tulikotoka na hivi vile vile kutokujua hasa ni wapi tunakwenda. Pilika za maisha na mahangaiko yanaweza kutia upofu wa tafsiri juu ya maana zetu za kuwa ni wenye kuishi na kuwa hai--binadamu kukosa jicho la kupima uhusiano kati ya mazingira na mambo ya nyakati--katika siti za utu wetu, uzima na busara. Kuangalia chakula, malazi na mavazi kwaweza kumtinga asione maana ipitayo yote yenye kufanyika na yeye kuhifadhika kwamo. Mtu, Dunia, Nyota na Mbingu vinautumikishi wa kimoja kwa mwenzake ; na vivyo hivyo kuonesha dalili ya fumbo la namna ya uhifadhiko kati ya vinavyoonekana basi ndani ya vile visivyoonekana.

Basi natuukague uwanja wa mchezo.

Nia ni mkuki wenye kuleta mwelekeo wa wakati na jitihada. Kutoka na Kufika ni uhifadhiko katika ulimwengu wa madhahirisho. Na hivi wakati si kitu ila tu rajisi ya mabadiliko katika utambuzi wa mtu. Bila nia hakuna badiliko na bila mwili wa madhahiriko hakuna muda wala wakati. Na vile vile pasipo na utambuzi hakuna rajisi ya wakati na wala nia yenyewe. Lakini katika namna yaajabu maisha/uzima ni uhifadhiko wa haya yote katika moja. Itokeapo namna ya utambuzi uliofanyikia katika hiyo moja lakini usijitambue uhifadhiko wake katika moja basi ndipo nia huzaliwa na wakati kuwepo.

Tutatazame mambo ya nyakati na wakati.

Mtu ni kutaniko la uzima wa mwili na karama za yasiyoonekana kwa macho ila tu kutambulika kwa ishara zake. Shani ya utu ni matokeo ya kubebea ndani hadhi ya namna bora za vitu/mambo/matendo kufanyika. Na kuna namna ya kumuona mtu kama mchakato hai miongoni mwa mambo matatu—nia, uwezo na maarifa/busara katika ishara ya sura tuiitayo ‘Uzima’ pale hayo matatu yanapotunukiwa mwili wa madhahirisho wenye kudhihirisha ‘chanzo-sababu / hisia-matendo’ ; kwa kupitia nia na uwezo katika kuhadhikisha kitendo na matokeo yake. Basi haya yakutanapo huzaa sura ya mambo iliyo ni dhana ya Muda na matukio-- vile pia kusema msongo wa wakati kulingana na tafsiri itegemeayo nuru yenye kumulika dhamira ya utambuzi katika siti ya utu wa mtu na akili/kumbukumbu. Na hivi mtu anayonafasi ndani yake yenye kuweza kudadavua mambo ya nyakati na hali pia wakati huo huo anayokurunzi isiyokamatika katika dhana yoyote ya wakati. Kurunzi hii ndiyo mwenge wa busara yake ishindayo tafsiri zote zenye mwanzo na mwisho ; inayomulika na hali yenyewe haimulikwi. Na hivi mengineyo yote kuwa tu ni vina vya tafsiri vya mambo vimvuli kwa ‘Kweli’ ya ‘Moja’ ; kufanya mukabala wa kumbukumbu.

Tutazame vimvuli vya watu na vina vya tafsiri.

Vimvuli haviishi ila tu kwa nguvu ya udhanifu wa mtu ; huhuishwa katika sura ya tafsiri yenye kujaribu kukidhi haja ya kupunguza ama kuondoa mashaka juu ya mashauri ya ustawi wa watu na makabila katika pia kufafanua utambulisho wa mambo yao ambayo kwa ujumla huitwa utamaduni na ustaarabu. Na jinsi hii, watu wa makabila ama utaifa kuwa daima katika kutafuta kujitambulisha kwa jinsi ya kutetea, kudumisha mambo yao yanayowafungamanisha ama pia kuonesha msisitizo wa mapokeo yao juu ya nchi na tawala ; kwa kuyaenzi hayo. Lakini watu pia ni wenye kujua sana dhamira zao za kimakundi zaweza kuharibiwa na hata kuharibika mapema pale zipambanapo uso kwa uso na tamaduni nje ya mizingo yao. Na hivyo binadamu katika sura ya kijamii huwa na namna ya kulinda mila, desturi na mapokeo yao yaliyo ni ishara ya utambulisho wao kwa pumzi ya nguvu ya uwezo wao.

Historia inaonesha jitihada zote za wanadamu katika muktadha huu zimezaa kuinuka na kuanguka kwa mataifa ya makabila na vipindi vya utawala kwa wale waliokamia hilo; kwa kukutana uso kwa uso na wale waliothubutu kuleta mpishano katika kupanda na kuporomoka kwa mataifa/makabila hasimu. Basi nia za chini za wanadamu zenye kutawala matendo yao ni zenye namna ya kukosa utangamano miongoni mwa mataifa na makabila na daima hutoa ahadi kubwa kubwa kwa makundi ya watu na hali katika kupita kwa wakati huleta pia majonzi, vilio, maasi na mambo yote yote yaliyokosa ubarikika.

Basi binadamu kwa jinsi hii ana nafsi mbili ; ya chini na ya juu. Ya chini ni ile yenye kuzaa makusudio yenye kuharibika upesi na hivi ni kimvuli tu cha nafsi ya kweli isiyoweza kuharibiwa wala kunajisiwa na mashauri ya mwili wa nyama wenye maradhi ya kuridhi ya kupenda kujipendezesha nafsi na kujihifadhi kwa mahodhi ya mali ama starehe za nchi/dunia na hivi mwili wa madhahirisho.

Nafsi ya juu ya mtu ni hazina kwa yale yote yasiyodhahirika na ni kioo kwa utambuzi wa mawezekano yaliyoko katika nyakati zote na fumbo kuu la imani kwa mtu. Ikiwa 'Mungu' ni dhana yenye kuwakilisha moja na moja na moja katika moja ; basi ndani ya mtu kuna daraja-mbegu ambalo ni lenye kuweza kusemwa mtu na mungu ni moja pia katika muktadha wake. Na nuru ya ufahamu wa mtu ndiyo muujiza mkuu kuliko wote wa dhahirisho la Uzima katika ‘mwili wa madhahirisho’ na ‘pasipo udhahirisho’ vile vile. Lakini mwanadamu akiwa ni mwenye kulewa sana na mvinyo wa fahari za mwili wenye kuharibika ; huishi kupenda kudumisha kimvuli cha nafsi yenye kufa na kutotambua namna ya fahari yake isiyojua mauti wala kuzaliwa—Ukweli juu ya ‘uzima wa milele’. Na hivi anguko la mwanadamu ni dhana ya mwanadamu kujitambulisha na mwili wenye kufuata sheria ya mauti na adha zake zote na hivyo kuuona ulimwengu katika jicho la namna hiyo. Na ndiyo katika kisomo cha leo tunaita namna hii ya jambo—‘dainetenia’ ya utambuzi ; mtu hutaka kuona kile anachopenda kuona kudumisha kile anachokidhania na kuwa kipofu wa vinginevyo vyote.

Nilipata kudokeza ya kwamba kazi niliyofanya kusanifu USANISI WA UJASIRIAMALI WA KIJAMII, Oganam ya karne ya 21 juu ya njia ya tatu-- ni mkamilisho wa kujumuisha kazi za Pythagoras, Yesu na Buddha katika kuwakilisha sura halisi ya mabadiliko ya kiustaarabu tunayoyaingia. Basi kwa jinsi hii Pythagoras ni kiungo kati ya Ufahamu kwa mujibu wa Yesu kuelekeza mafundisho; na kujaribu kwake kuwasilisha namna ya uelewa wa maumbile ; yeye pia ni kiungo katika kukutanisha maelekezo ya Yesu na yale ya Buddha ambayo yote kwa pamoja ndiyo mhimili wa fahari ya zama hizi katika ustawi na neema. Na hili halina budi kufafanuliwa kwa maelezo zaidi. Na tena si katika mrengo wa kiordhodoksi ila sayansi halisi ya ukweli wa mambo. Kwa kuwa mimi si muumin wa dini yoyote ya kimapokeo na wala sipendekezi kwa mtu yeyote usadikifu wowote iwe wa 'Mungu' ama mambo yajayo/yaliyopita/yaendeleyo kwa jicho la upofu wa fikra ya udhanifu na hofu. Usadikifu ni kasumba na hadhi ya sifa dumazi--haimtii binadamu heshima ya ‘kweli’ ya utu ila tu kimvuli chake.

Kwa kuwa kutokana na Pythagoras ninazungumza mambo ya nyakati na utangamano wa vitu/mambo kihadhi na pia ukiasi wa namna yake katika msuko ya yote yanayoonekana na yale yasiyoonekana. Na hivi Pythagoras anawakilisha Wakati na mshahibiano wake na mtiririko wa madhahirisho, Yesu anawakilisha Tekinokrasia na Buddha anawakilisha Meritokrasia ; lakini mwenye kuvitanganamisha vyote hivi ni Pythagoras.

Na sasa basi nimtambulishe Yesu kama mtu aliyeyajua haya kwa kutangulia na kujaribu kuleta msogezo wa dhana na pia fikra miaka kadhaa iliyopita ; takribani kipindi cha zama moja toka leo—kadri tuzisomapo tabia za mabadiliko ya watu kimakundi na mnyambuliko wa hadhi na ustaarabu wao ; twazigawanya hizo katika vipindi tuvitajavyo kama zama.

Basi Yesu alijua dhahiri jitihada zake zilikuwa ni kipindi cha matayarisho lakini matunda yake halisi ama kusema musimu wa kuchanua ni zama moja mbele katika mwendo wa hatua za mabadiliko ya kiustaarabu na hadhi ya utabia kwa wanadamu. Lakini tena katika utambuzi ndani ya daraja-mbegu ; fahari yake kamili yeye alipata kuiita ni ‘Ufalme wa Mbingu’, ni vile kutamka bayana kuwa upo karibu na hapa na vile pia kusema upo ndani ya mtu na labda tu akizaliwa mara ya pili si kwa jinsi ya mwili wala kiakili na wala kihisia za mwili bali kwa jinsi ya ‘roho wa uzima’-- huwa moja na huo na hivyo kuwa ni ‘Mfalme’. Kwa kuwa wakati si kitu katika roho wa uzima ijapohali hili ni shauri gumu kuenea katika uelewa wa kawaida wa mtu asiyetaamulika, aiishiye katika uwanda wa nchi ya vimvuli, ila tu kuelekezwa yeye kwa namna ya picha za vielezi vyenye funguo za kuleta ishara ya ukweli wenyewe ulivyo.

Basi kabla ya kuyadadavua mashauri ya ontolojia kwa mujibu wa Yesu tuikague kazi yake kulingana na kumbukumbu zilizopo na mapokeo. Yeye ni mtu mwenye kukumbukwa kwa kulingania ‘Ufalme Mpya’, pia kusihi umma kuwa tayari kuupokea ‘Ufalme’. Alikuwa ni muasi wa sheria na desturi na huku akisisitiza kuzikamilisha hizo kwa Sheria Mpya. Alipata kukiri kiulaini tu kuwa yeye ni ‘mwana wa mungu’ na vile kusisitiza pia kuwa mtu yeyote kwenye kuzaliwa tena kwa jinsi ya roho hufanyika ‘mwana wa mungu’. Pia alitamka bayana kwa kukumbushia, kusema binadamu ni ‘miungu’; wana wa aliye Juu (katika Mbingu). Aliponda dhana ya watu kutaka ishara ili kujiridhisha usadikifu juu ya karama za kimamlaka ya wadhifa/ukiongozi mkuu kutarajiwa ama unabii mkubwa--akikwepa kuridhisha watu na siasa zao. Lakini hapo hapo ikitaarifika kufanya ‘miujiza’ ya wenye kuwa ‘viziwi’ kusikia, wenye ‘upofu’ kuona, walio ‘bubu’ kuzungumza, Kuzungumza na ‘vipepo’ vyenye kuendesha Pepo na dhoruba za mawimbi ya bahari nahivyo ‘vipepo’ kumsikia na kuitika kwa kutuliza tafrani… Yote hayo kukimbia sifa za kiuanadamu ila tu kuitikia hitaji la wakati.

Shughuli ya Yesu ilikuwa na mwanzo wa upacha na binamu yake aliyeitwa Yohana. Machache hujulikana kuhusu Yohana katika mapokeo ya vitabu kama vile pia kukosekana kwa simulizi la maisha ya Yesu kati ya miaka 12 na mpaka kuja kukutana na Yohana akiwa na umri wa kama miaka 28 katika ile shughuli isiyofafanuliwa kinagaubaga ya ‘Kubatiza’ ambayo alikuwa akitenda binamu yake huyo katika ukingo wa mto Yordani.

Labda ikiwa shughuli ya Yohana ingehifadhika kwa kina katika kumbukumbu za simulizi za kimaandishi, ‘ukweli wa ishara’ ya tendo lenyewe la ubatizo ingeng’amuliwa vema na uhusiano wa shughuli za hao wote wawili mbele za umma kufahamika vema.

Basi kulingana na simulizi mbadala toka kwenye kumbukumbu la matendo yote ndani ya nyakati inatupasa kutafuta majibu. Upo ujuzi wa kuona matukio katika ‘kitabu cha uzima’ na ambapo yeyote aweza kuzisoma kumbukumbu za mambo yaliyotangulia kwa vipeo vyote vya taarifa: picha, maneno, harufu, hisia n.k… Basi nitumie msaada wa Levi Dowling , aliyepenyezea kiufahamu ndani penye ‘Akasha’—mahala pa kumbu kumbu zote, kuwakilisha ujaziliazi wa simulizi kosekanifu.

Nimepata kutafsiri kazi ya Levi na hii hapa ni nukuu nyakuzi:

SURA 7

Arkelausi atawala mamlaka. Mariamu na Elizabeti pamoja na wana wao wapo Soani na wafundishwa na Elihu na Salome. Somo la Utangulizi la Elihu. Asimulia juu ya mfasiri.

Mwana wa Herode, Arkelausi, alitawala mamlaka yote katika Yerusalemu. Alikuwa ni mbinafsi, Mfalme mkatili, aliwaua wale wote wasiompa heshima yeye. 2 Aliita barazani wote wenye hekima zaidi juu ya watu na kuwauliza kuhusu mtoto mchanga mwenye kudaiwa kustahiki kiti cha ufalme wake. 3 Baraza likasema kwamba wote wawili Yohana na Yesu walikuwa wameshakufa; basi na yeye akaridhishwa. 4 Sasa Yosefu, Maria na Wana wao walikuwa chini katika Soani, na Yohana alikuwa na mama yake katika vilima vya Yudea. 5 Elihu na Salome wakawatuma wajumbe kuharakisha kuwatafuta Elizabeti na Yohana. Waliwapata nao wakawaleta wao Soani. 6 Sasa, Mariamu na Elizabeti walikuwa wakistaajabia sana kwa sababu ya kukombolewa kwao. 7 Elihu akasema, si ajabu, hakuna matokeo tu; kanuni hutawala kuendesha matukio yote. 8 Kutokea nyakati za nyuma sana ilishapangwa kwamba mtalikuja kuwa nasi, na katika shule hii yenye kutunzwa kusudio safi ili kufundishwa. 9 Elihu na Salome wakawachukua Mariamu na Elizabeti nje kwenye ua takatifu karibu na pale ambako wao walikuwa na desturi kufundisha. 10 Elihu akawaambia Mariamu na Elizabeti, mwaweza kujionelea furaha ninyi wenyewe mmebarikiwa mara tatu, kwa kuwa ninyi ni mama wateule wa wana walioahadiwa kipindi kirefu, 11 Wao ambao ilivyopangwa kuwekewa mkono kuja kuweka mwamba mgumu imara msingi jiwe wa uhakika ambao juu yake hekalu la mtu kamilifu litasimama--hekalu ambalo halitaweza kamwe kubomolewa. 12 Twauhesabu wakati kwa mizunguko ya zama za vipindi, na lango kwa kila zama twasema akilini ya kuwa ni jiwe la maili katika safari ya kundi la watu wa sifa ya namna moja. 13 Zama zimepita; lango kuelekea kwenye zama ingine lafunguka wazi katika kugusa kwa wakati. Hii ni zama ya maandalizi ya nafsi roho, ufalme wa Imanueli, wa Mungu katika mtu; 14 Na hawa, wana wenu, watakuwa ni wa kwanza kueleza habari, na kuhubiri injili ya mapenzi mema kwa watu, na amani duniani. 15 Kazi kubwa ni yao; kwa kuwa watu wa miili ya nyama hawataki Nuru, wao walipenda giza, na pale ambapo nuru yang'ara gizani wao hawaitambui. 16 Twawaita hawa wana, Wafunuaji wa mwanga; lakini inawapasa kuwa na nuru kabla ya wao kuweza kufunua nuru. 17 Na yawalazimu kuwafundisha wana wenu, na kuzitia moto nafsi-roho zao kwa upendo na msisimko mtakatifu, na kuwafanya wao kuwa macho fahamuni na mpango wao mahsusi kwa wana za watu. 18 Wafundisheni kwamba Mungu na Mwanadamu ni moja; ila kwamba kupitia mawazo ya mwili wa nyama na maneno na matendo, mwanadamu hujirarua mwenyewe mbali na Mungu; kujishusha hadhi yeye mwenyewe. 19 Fundisheni ya kwamba Pumzi Takatifu italiwafanya wao moja tena, kurejesha hali ya kwenda kwa utangamano; 20 Kwamba hakuna chochote chenye kuweza kuwafanya moja ila Upendo; kwamba Mungu ameupenda sana ulimwengu hata kumvika mwana wake katika nyama ili kwamba mwanadamu aweze kutambua. 21 Mwokozi pekee wa ulimwengu ni upendo, na Yesu, mwana wa Mariamu, aja kudhahirisha pendo hilo kwa watu. 22 Sasa, pendo haliwezi kudhahirika mpaka njia yake iandaliwe, na hakuna chochote chenye kuweza kuivunjilia mbali miamba na kuangusha chini vilima vilivyo kwea juu sana na kujazia juu mabonde, na hivyo kutayarisha njia, ila usafi wa moyo. 23 Lakini usafi wa moyo katika maisha wanadamu hawatambui; na hivyo, huo, pia, waja katika mwili wa nyama. 24 Nawe Elizabeti, umebarikiwa kwa kuwa mwana wako ni Usafi wa moyo kufanyika nyama, na yeye ataifanya njia kwa Pendo. 25 Zama hii itatambua ila kidogo tu juu ya kazi ya Usafi wa Moyo na Upendo; lakini hakuna neno limepotea, kwa kuwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Mungu ingizo lafanyika kwa kila wazo, na neno, na tendo; 26 Na pale ambapo ulimwengu u tayari kupokea, lo, Mungu atamtuma mjumbe kufungua kitabu na kunakili kutoka kwenye kurasa zake zilizohifadhika patakatifu ujumbe wote wa Usafi wa Moyo na Upendo. 27 Na kisha tena kila mtu wa juu ya nchi atayasoma maneno ya uhai katika lugha ya nchi yake ya kuzaliwa, na wanadamu wataiona nuru, kutembea katika nuru na kuwa nuru. 28 Na mwanadamu tena atakuwa mmoja na Mungu.


Zama inayokwisha ni zama za ya ‘Maandalizi’ na hivi kwa imani binadamu amepata shauri la kuogelea katika ‘bahari’ ya kweli ya uzima wote akiwa kama samaki asiyebudi kuwa na kiu. Kwani lugha ya ishara na vielelezi aliyotumia Yesu ni ufundi wa kufungua pazia la mkingamo wa udhanifu dhidi ya ‘Kweli’ na uchukuliaji wa hadhi ya matendo katika kumwandaa mtu na upokeaji wa ‘busara’ ya ‘roho wa uzima’ kama Yesu alivyoijua na yeye kujulikana katika hiyo. Na hivi kila mtu aweza kufunguka kwa kadri ya stahiki yake kwa wakati na hali kielelezi kikiwa vilele. Na vile vile kuthibitisha jinsi binadamu awezavyo kujifunza kwa kushirikisha ubongo wenye kutenda kazi kwa kutumia picha za mfano na mashauri yenye mantiki/changanuzi; na Yesu alikuwa muepesishaji wa mawasiliano ya ndani ya mtu katika kuchochea utambuzi wa kiroho.

Mapokeo ya mafundisho ya Yesu yameleta mkondo wa imani na taasisi za dini. Ni ushawishi na msukumo wa vitendo ndivyo vilivyozaa mwongozo katika sura ya dini na mtapanyiko wake wa madhehebu. Kwa kuwa fikra na hisia-kutenda zikinogeshwa kwa itikadi huweza kusimamisha utaasisi wa watu na msukumo wa ushawishi. Na hivi twaweza kutazama finomena ya dini kama Ukristo ulivyo kuwa ni kama chombo tu chenye mfano wa utumikivu wa mwanadamu katika kufanikisha kazi fulani. Lakini la msingi ni kuelewa utaasisi ni kitu gani na ‘Kweli Halisi’ ni kitu gani. Taasisi ni ubunifu wa mwanadamu ; ‘Kweli’ haina ushirika wa moja kwa moja na utaasisi ingawaje utaasisi waweza kutengeneza mazingira ya ‘Kweli’ kumea katika wanataasisi husika. Hili hutazamwa na kupimwa kwa ‘matunda’ ya taasisi yenyewe.

Taasisi ni kifungo cha kufungamanisha na itikadi na ushawishi; Kweli haina mipaka na ni hadhi ya mbegu ya yote yenye kufanyika na kudhahirika. Dhana vile vile ni kitu chenye sura ya ukikomo na hivi haewezi kuwa ‘Kweli’. Dhana ni chembe katika mwili wa ufikirifu katika daraja la mawasiliano, ubunifu na uchukuliaji wa tambuko akilini. Lakini dhana si stawishi la yote na kwa jinsi ya mote katika uchukuaji wa nafasi. Dhana, mawazo na fikra vyaweza kuandikwa na kuwasilishwa lakini daima vitafaa kwa akili na utambuzi wa namna yake. Na hivi hakuna neno la maandishi ama maandiko linaloweza kuwa 'Kweli' ila tu kimvuli cha tafsiri. Ni tafsiri ya mwanadamu na kwa jinsi ya mwanadamu. Kweli haikamatiki kwa mawasiliano na ndio maana hata kama miujiza ilitendwa na Yesu, ‘Kweli’ ilibaki ni fumbo la Imani kwa watu wenyewe. Na hadi hii leo ‘Kweli’ ipo karibu sana na mwanadamu lakini yeye haitambui na hivi yeye kutafuta maana ya maisha yake kwa kufukuzia kimvuli cha muuakisiko wa hofu zake yeye mwenyewe na ujinga wa kukosa utambuzi wa kiroho na hivyo kuamini katika mamlaka ya wale wenye ushawishi wa namna za ishara za nje. Kwa kuwa ‘Kweli’ hujulikana kwa jinsi ya ‘Rohoni’.

Basi nilete maneno ya Paulo wa Tarso kama ‘msikirifu’--mystic wa namna yake katika mkondo wa mapokeo ya mafundisho ya Yesu na ndiye busara yake inaunganisha ‘Tertium Organum’ ya PD Ouspensky na Oganam ya karne ya 21 juu ya njia ya Tatu ninayoitayarisha mimi. Nayeye anataarifika kupata kusema hivi :

Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii wanaobatilika; bali wanena hekima ya mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangalijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu; lakini, kama iliyoandikwa,

Mambo ambayo jicho halikuyaona wala masikio halikuyasikia,

(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)

Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyondani yake? Vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena si kwa maneno yanayoyanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya roho. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yanajulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote na wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, Ni nani aliyefahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Tafsiri hii kwa Kiswahili ni yenye kujaribu sana kwani kuna maneno yalikosa tafsiri ya moja kwa moja. Na hivi nilete ya kiingereza cha zamani kukoreza maana; ile iliyokuwa kabla ya hisani ya Mfalme James wa Uingereza katika kufadhili kazi tafsiri na uhakiki na nakala za kiingereza zilizotangulia katika jitihada zake za kuhifadhi mapokeo ya vitabu vya dini ya kikristo:

We speak the hidden mystical Wisdom of God, which God ordained before the World unto our Glory; Which none of the Princes of this World knew; For had they known it, they would not have crucified the Lord of Glory. But, as it is written, Eye hath not seen, nor Ear heard, neither hath it entered into the Heart of man to conceive the Things which God hath prepared for them that Love him. But God hath revealed them unto us by His Spirit: For the Spirit searcheth all Things, yea, the deep Things of God. For what Man knoweth the Things of a Man, save the Spirit of a Man which is in him? Even so the Things of God knoweth no Man, but the Spirit of God. Now we have received, not the Spirit of this World, but the Spirit which is of God; that we might know the Things that are freely given us of God. Which Things also we speak, not in the Words which Man's Wisdom teacheth, but which the Holy Ghost teacheth; comparing Spiritual Things with Spiritual. But the natural Man receiveth not the Things of the Spirit of God: For they are Foolishness unto him; neither can he know them, because they are Spiritually discerned. But he that is Spiritual judgeth, or discerneth all Things. “For who knowth the mind of the Lord so as to instruct him?” But we have the mind of Christ.

Nimependa kutumia nukuu nyakuzi iliyopata kutumika katika siku za Jacob Boehm wa Ujerumani miaka ya karne ya 16 na 17 kwa kuwa na yeye alikuwa ni msikirifu wa siku za karibuni aliyepata kufumbua kwa watu siri za mambo ya kiroho, naam kama ilivyopata kuwa na Dionysius, askofu wa kwanza wa jimbo la Athens-- maarufu kwa kazi yake ya Theologia Mystica, siku za nyuma zaidi; na meister Eckhart wa Ujerumani katika karne ya 14.

Shauri la ‘Jinsi ya rohoni’ ni kuzungumzia ginosia ya nafsi, ya kuwa mtu ‘hujua’ si kwa kutaarifiwa bali kwa ‘uzoefu’ wa kupitia hali ya utambuzi wa 'Moja' kati ya nafsi yake ya chini na nafsi yake ya juu. Nimeongeza neno katika msamiati wa Kiswahili ‘Usikirifu’ kukidhi tafsiri ya moja kwa moja ya neno ‘Mysticism’. Katika hali ya kawaida binadamu huwa wamependelea mambo ya mitaala ya ‘usadikifu’ na imani na hivi kusema mambo ya kiordhodoksi. Lakini mambo ya kiordhodoksi hufaa kwa watu wasiotambua shauri lipitalo unafsi wa kawaida wa mtu na wao kupendelea uhifadhina wa fikra na mawazo katika muktadha wa Theolojia na matendo ya kimapokeo. Na ndiyo hayo huja kuleta madhehebu na mgawanyiko wa taasisi za kiimani kwa mirengo ya kiitikadi za kutukuza na kuendeleza utaratibu wao.

Paulo alikuwa anajua umuhimu wa kuunganisha nguvu katika pilika na jitihada za kusambaza mafunzo ya imani na ujuzi wa kufungamanisha watu. Hii ni moja azma ya zama inayokwisha katika kuchochea watu kukaa pamoja katika namna za imani. Na hivi Paulo alijua fika Yesu ni kielelezo cha kuwaunganisha watu katika mashauri ya itikadi na hivi ndio maana alikuwa anaweza kuzungumza kuhusu uhusiano wa wanataasisi na Yesu ama ghafla akahamia kwenye elekezo mbadala la Kristo kama ‘Kweli’ ya ‘Roho wa Uzima’ katika Nia ya kudharihisha fahari ya Mbingu katika maisha ya Watu. Na ndivyo hivi kwa nini alikuwa mjuzi wa kubomoa hoja za mapokeo ya kiordhodoksi kama vile dhana ya kutokuwa na hukumu dhidi ya watu wenye ‘kuishi’ katika Kristo, maelekezi ya kushinda ‘mauti’ na ‘dhambi—uasi wa sheria za staha ya kiroho na dhana ya dosari ya moja kwa moja’ haya mawili katika muktadha wa kutambua Ufahamu wa Kristo ndani ya mtu mwenyewe. Kwa kuwa Paulo alikuwa ni msikirifu na tena mwenye kukiri uwezo na Ufahamu ndani yake wenye kupita fahamu za mwili kwa jinsi ya kiroho—mwili wa Kristo.

Na hivi kuna mahali anasema hivi:

Hata imekuwa, sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya ; ya kale yamepita ; tazama ! yamekuwa mapya. Lakini vyote pia vyatoka na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake katika Kristo ; naye alitupa huduma ya upatanisho ; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao ; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

Neno la upatanisho ndivyo Pythagoras alipata kufundisha miaka mingi kabla ya Yesu juu ya uhusiano kati ulimwengu wa LOGOS na NECESSITY ; ulimwengu wa Neno lenye Nguvu na ulimwengu wa Utumikishi wa Mwili wa madhahiriko. Na hivi dhana ya Kristo ni yenye kufafanisha maana mbadala kati ya ‘Kristo’ na ‘Neno la Uzima’. Kinyume na ulimwengu wa kiordhodoksi, watu huchukulia maandishi ama maandiko kama ndiyo ‘neno la uzima’... Hii ni tafsiri ya vimvuli vya unafsi wao wenyewe.

Lakini jinsi ambayo Neno la Uzima huhifadhi na kustahimilisha yote ndiyo safari ya haja ya Pythagoras kutafuta kueleza ‘Muziki’ wa utangamano wa yote yaliyopata kudhahirika. Kristo—Neno la Uzima, ni ramani na uweza wa nguvu utaokutanisha ulimwengu uliodhahirika na upasipo dhahiriko katika kutaniko liitwalo WAKATI. Na hivi Pythagoras aliliita Neno hili ni SHERIA. Kwani kila kitu hufanyika ndani ya kanuni zake. Kutokujua daraja la kanuni ni kuishi katika dhambi na mpotoko lakini kuzaliwa katika Kristo ni kukomboka na kuishi zaidi kuzidia mbali ulimwengu wa vipimo iwe vya nyakati, umbali, upana wa uso, na hata ujazo. Na kwa hivi kufaa kusema neno liko kote na pote ; hakuna palipo na dhahiriko pasipo neno—vitu vyote vimefanyika katika neno. Mbingu huhifadhi vyote vilivyodhahirika lakini yenyewe hahihifadhiki na kitu chochote cha mfano. Na hivi Neno ni kiungo cha upatanishi wa mambo ya ulimwengu wa madhahirisho-Mtu, Dunia, Nyota na Mbingu. Naye Paulo huyazungumza haya anapomulika juu ya fahari ya mwili wa nyama, fahari ya miili ya nyota—uharibika na usipouharibika. Dhana ya Mauti na Ufufuko ambayo ni ontolojia ya Kristo katika Yesu pia.

Na hivi tutazame alichofundisha Yesu kwa msaada wa kumbu kumbu ya Levi :

Sura 115

Yesu afundisha kando ya Bahari. Asimulia kielezi cha mpanzi. Asema ni kwanini yeye afundisha kwa vielezi. Aelezea kwa mapana kielezi cha mpanzi. Asimulia kielelezi cha ngano na magugu nyasi.

NA Yesu akasimama kando ya bahari na kufundisha; makundi ya watu wakabanana naye na yeye akaenda katika mtumbwi ulio karibu na kusogea mbali kidogo na ukingo wa maji, na halafu akazungumza katika lugha ya vielezi; yeye akasema, 2 Tazameni, mpanzi alichukua mbegu na kwenda shambani kupanda. 3 Kwa mikono yenye kutoa kwa moyo alizitapanya mbegu na nyingine zikaangukia kwenye udongo mgumu ambao watu wamefanya, 4 Na muda si mrefu zilikanyagwa chini na miguu ya watu wengine; na ndege wakaja chini na kuzibeba na kuruka nazo mbali. 5 Mbegu nyingine zikaangukia katia ardhi yenye mwamba ambako kulikuwa na udongo kidogo; zikakua na muda si mrefu majani yakajitokeza na kuonesha dalili njema; 6 lakini basi hakukuwa na kina katika udongo, na hakuna nafasi ya kulishwa toka mizizini, na katika joto la mchana yakanyauka na kufa. 7 Nyingine zilianguka kwenye vichaka vya majani, na kukosa udongo wa kukulia nazo zikawa zimepotea; 8 Lakini mbegu nyingine zilipata makazi katika udongo mzuri na wenye rutuba na kukua haraka, na katika kipindi cha mavuno ikakutwa kwamba mingine ilizaa na kuleta mara mia, mingine sitini, mingine thelathini. 9 Wale wenye masikio ya kusikia waweza kusikia; na wale wenye mioyo ya kuelewa waweza kuelewa. 10 Sasa, wafuasi wake walikuwa kando yake ndani ya mtumbwi, na Tomaso akauliza, ni kwanini wazungumza katika lugha ya vielezi? 11 Na Yesu akasema, maneno yangu, kama maneno ya kila mkuu, ni yenye maana mbili kwa wakati mmoja. 12 Kwa nyie wenye kujua lugha ya nafsi-roho, maneno yangu yana maana iliyo ya kuzama ndani sana kwa watu wengine kumaizi. 13 Maana ingine ya kile nikisemacho ni kile makundi yote ya watu waweza kuelewa; maneno haya ni chakula kwao; mafikara ya ndani ni chakula kwa ajili yenu. 14 Acheni kila mmoja wenu kuunyosha mkono na kuchukua chakula ambacho yu tayari kukipokea. 15 Na halafu alizungumza ili kwamba wote waweze kusikia; yeye akasema, sikieni maana ya kielezi: 16 Watu wasikia maneno yangu na kutoyaelewa, na halafu nafsi yao ya kimwili yakwapua mbali mbegu, na wala dalili ya roho ya uzima kutokea. 17 Hii ni mbegu ambayo yaanguka ndani ya mapito ya watu. 18 Na wengine wayasikia maneno ya uzima, na kwa uchangamfu wa jazba kuyapokea yote; waonekana kumaizi kweli na dalili njema; 19 Lakini matatizo yaja; kuvunjika moyo kuinuka; hakuna kina katika mafikara; dhamira zao njema zakauka na kufa. 20 Hizi ni mbegu ambazo zilianguka kwenye ardhi ngumu. 21 Na wengine wasikia maneno ya ukweli na kuonekana kujua thamani ya kustahili kwake; lakini kupenda starehe, heshima, utajiri wa mali na umaarufu wa jina kuijaza ardhi yote; mbegu hazipaji mahitaji yake nazo zapotea. 22 Hizi ni mbegu ambazo zilianguka katikati ya vichaka vya majani na miiba. 23 Lakini wengine wasikia maneno ya ukweli na kumaizi vema; wao wazama vizuri katika nafsi-roho zao; waishi maisha matakatifu na ulimwengu wote wabarikiwa. 24 Hizi ni mbegu ambazo ziliangukia kwenye udongo wenye rutuba, ambayo ilileta matunda kwa ujazi. 25 Enyi watu wa Galilaya, mpate kuangalia jinsi msikiavyo na jinsi mpandavyo mashamba yenu; kwani ikiwa mwapuuzia matoleo ya siku hii, mpanzi aweza asije tena kwenu katika zama hii ama katika zama ingine ijayo. 26 Halafu Yesu asema kielezi; yeye akasema: 27 Basi ufalme nauweza kuufananisha na shamba ambalo mtu alipanda mbegu bora; 28 Lakini wakati amelala muovu akaenda na kupanda kujaza kote mbegu za magugu; halafu akaenda zake. 29 Udongo ulikuwa ni mzuri, na hivyo ngano na magugu nyasi vikakua; na watumishi alipoona magugu miongoni mwa ngano, walimpata mmiliki wa shamba na kusema, Mtu mwovu mmoja amepanda mbegu za magugu nyasi. 32 Watumishi wakasema, Je, tuende na kung'oa hadi mizizi manyasi ya magugu na kuyachoma motoni? 33 Mmiliki akasema, Hapana, hivyo haitakuwa vyema. Ngano na magugu nyasi vyakua karibu karibu pamoja udongoni, na wakati mkivuta manyasi mtaiharibu ngano. 34 Hivyo tutaziacha zote kukua pamoja mpaka wakati wa mavuno. Halafu kwa wavunaji nitasema, 35 Enendeni na kukusanya magugu na kuyafungia pamoja na kuyachoma motoni, na mkusanye ngano yote katika maghala yangu. 36 Aliposema haya, akaondoka kwenye mtubwi na kwenda juu kwenye nyumba, na wafuasi wake wakamfuata.


Sura 116

Wakristuni wapo nyumbani kwa Filipo. Yesu atafsiri kielezi cha ngano na magugu nyasi. Aelezea kwa mapana ufunukaji wa ufalme kwa vielezi: mbegu bora; kukua kwa mti; chachu; hazina iliyofichika. Aenda mlimani kusali.

Wakristuni walikuwapo nyumbani kwa Filipo na Petro akasema kwa Yesu, Bwana, utatuelezea maana ya vielezi ulivyotuambia leo? Na hasa kile kuhusu ngano na magugu nyasi? 2 Na Yesu akasema, Ufalme wa Mungu ni umbili; una namna ya sura ya nje na ile ya ndani. 3 Kama vile uonekanavyo kwa watu hufanyika kwa namna ya watu, ya wale ambao wamefanya ukirifu katika jina la Kristu. 4 Kwa sababu mbali mbali watu mbali mbali wajazana kuubana ufalme huu wa nnje wa Mungu wetu. 5 Ufalme wa ndani ni ufalme wa roho-nafsi, ufalme wa waliosafi katika moyo. 6 Ufalme wa nje naweza kuelezea vema kwa mapana katika vielezi. Tazameni, kwani nimewaona ninyi mkizitupa nyavu zenu baharini, 7 Na wakati mlipozivutia ndani, lo, zilikuwa zimejaa kwa kila namna ya samaki, wengine wazuri, wengine wabaya, wengine wakubwa, wengine wadogo; na nimewaona ninyi mkiwabakiza wazuri na kuwatupa mbali wabaya. 8 Ufalme huu wa nje ni nyavu, na kila namna ya mwanadamu hushikwa; lakini katika siku ya kuchagua wabaya wote watatupwa, na wazuri kutuzwa. 9 Sikieni, basi, maana ya kielezi cha ngano na magugu nyasi: 10 Mpanzi ni mwana wa mtu; shamba ni ulimwengu; mbegu nzuri ni watoto wa nuru; magugu nyasi, watoto wa giza; adui ni nafsi ya kimwili; siku ya mavuno, ni mwishoni mwa kufunga zama; mvunaji ni mjumbe wa Mungu. 11 siku ya malipo*[Pia siku ya hukumu] itakuja kwa kila mtu; halafu kutakuwa na magugu nyasi kukusanyika pamoja, na kutupiwa katika moto na kuchomwa. 12 Halafu wema kung'aa kuwaka mbele kama majua katika ufalme wa roho-nafsi. 13 Na Filipo akasema, Je, yawabidi wanaume kwa wanawake kuteswa katika moto kwa sababu hawakuipata njia ya uzima? 14 Na Yesu akasema, Moto wasafisha. Wakimiya*[Watu washughuliakao na kubadili sifa za tabia za vitu kwa kanuni za uelewa wake] hutupa motoni malighafi ya chuma chuma na kushikilia kuichuja kila namna ya mabaki ya yasiyotakiwa. 15 Mali ghafi ya chuma chuma yenye kuonekana kutokuwa na manufaa kuwa imetafunwa na moto; lakini si hata chembe ya dhahabu yapotea. 16 Hakuna mtu ambaye ndani yake hana dhahabu ambayo haiwezi kuharibikika. Vitu viovu vya watu vyote vyatafunwa katika moto; dhahabu yabakia. 17 Ufalme wa kindani wa roho-nafsi naweza kuuelezea katika vielezi: 18 Mwana wa mtu aenda mbele na kutawanya mbegu za kweli; Mungu azimwagia vizuri udongo maji; mbegu yaonesha uhai na kukua; kwanza yaja majani, na halafu mashuke; na halafu masikio, na halafu ngano tupu katika masikio. 19 Mavuno yaja na lo, mvunaji abeba mavuno yaliyoiva hadi katika maghala ya Bwana. 20 Tena, ufalme wa roho-nafsi ni kama mbegu ndogo ambayo watu waweza kupanda katika udongo wenye rutuba. 21 ( Maelfu yake kwa kiasi pungufu tu kwa uzito wa shekeli moja.) 22 Mbegu ndogo yaanza kukua; yasukuma kupenya katika udongo, na baada ya miaka ya kukua kwake waja kuwa ni mti mkubwa na ndege watulia katika matawi yake yenye majani na watuwapata hifadhi katika kimvuli kukingwa na Jua na matufani. 23 Tena, ile kweli, hali ya roho ya ufalme wa roho-nafsi, ni kama vipande vya unga wa kukandwa uliotiwa chachu ambayo mwanamke huufunikia katika kipimo, tatu, na katika muda kidogo wote waumuka. 24 Tena, ufalme wa roho-nafsi ni kama hazina iliyofichwa shambani ambako mtu huipata, na moja kwa moja aenda njia yake na kuuza vyote alivyonavyo na kununua lile shamba. 25 Yesu aliposema yote hivi alikwenda peke yake katikati ya vilima palipo ni karibu na kusali.


Sura 120

Nikodemasi yupo kalamuni. Amuuliza Yesu, Je, dini ya kristuni haiwezi kuletwa mbele kwa mafanikio zaidi kwa kutengeneza upya huduma ya Kiyahudi? Yesu ajibu katika namna ya kinyume na atoa sababu. Yesu amponya mwanamke mwenye matatizo ya kuvuja damu. Amponya binti Yairo. Apotea watu wanapolitaka kumuabudu.

SASA, Nikodemasi, ambaye hapo mwanzo alikuja kwa Yesu wakati wa usiku kujifunza njia ya uzima, alikuwa ni miongoni mwa wageni. 2 Na kusimama mbele yeye akasema, Raboni, ni kweli kwamba Kanuni za sheria za Kiyahudi na matendo ya Kiyahudi haviendani. 3 Ukuhani wahitaji kufanyiwa matengenezo upya; watawala yawapasa kuwa na rehema zaidi na huruma; wanasheria yawapasa kuwa na haki zaidi; watu wa wakawaida yawapasa kutokubeba mizigo kama hiyo. 4 Lakini Je, huwezi kuongezea humo ndani yake kwa matengenezo mapya na pasipo kuharibu huduma za Kiyahudi? 5 Je, huwezi kufanya kazi zako kubwa ziendane sambamba na zile za Mafarisayo na waandishi? Je, ukuhani huewezi kunufaika na filosofia yako manani? 6 Lakini Yesu akasema, Hauwezi kuutia mvinyo mpya katika vifuko vya kale, kwani utakapojisafisha kuwa bora, lo, watanuka; vifuko vya kale haviwezi kumudu nguvu ya mtanuko; hivyo hupasuka, na mvinyo wote wapotea. 7 Watu hawatii viraka nguo iliyochakaa kwa kipande cha nguo mpya, ambayo haiwezi kustahimili msokoto wa nyuzi, mdhaifu kwa uzee, na halafu mtatuko mkubwa zaidi watokea. 8 Mvinyo wa zamani waweza kuhifadhiwa katika vifuko vya zamani; lakini mvinyo mpya wavitaka vyombo vipya vya kuhifadhia. 9 Hii kweli-ya-roho niiletayo kwa kizazi hiki ni mpya, na ikiwa tutaiweka katika vifuko vya zamani vya namna za Kiyahudi, lo, utapotea. 10 Ni lazima utanuke; vibebeo vya zamani haviwezi kustahimili na hivyo vingalipasuka. 11 Tazameni ufalme wa Kristu! Ni wenye umri sawa na Mungu mwenyewe, na wakati ni mpya kama vile jua la asubuhi; wenyewe tu ndio uwezao kubeba ndani yake kweli ya Mungu. 12 Na alivyokuwa akizungumza mtawala wa sinagogu, Yairo kwa jina, akaingia na kuinamisha kichwa miguuni pa Yesu na kusema, 13 Mkuu wangu, sikia ombi langu! Mwanangu ni mgonjwa sana, ninahofu atakufa; lakini hili nalijua ya kwamba ikiwa utakuja na kuzungumza Neno mwana wangu ataishi. 14 (Alikuwa ni mtoto wake wa pekee, binti wa miaka kumi na miwili.) 15 Na Yesu hakungoja; alitoka na yule mtu, na watu wengi wakawafuata wao. 16 Na walipokuwa wakienda mwanamke aliyekuwa akiugua ugonjwa wa kuvuja damu kwa miaka mingi, amekuwa akijaribiwa kutibiwa na waganga toka mbali na karibu, na wote walikuwa wamesema, hawezi kuishi, akainuka kutoka kitandani mwake na kukimbia njiani Yesu alivyokuwa akipita. 17 Na yeye alisema ndani, ikiwa nitagusa vazi lake, basi najua nitakuwa ni mzima. 19 Na Yesu akasikia kama vile nguvu za uponyoji zimemtoka, na kuzungumza kwa makundi, yeye akasema, 20 Ni nani amegusa koti langu? 21 Na Petro akasema, Hakuna mtu anayeweza kusema; makundi yamekubana bana; idadi ya watu waweza kuwa wamekugusa koti lako. 22 Lakini Yesu akasema, Mtu mmoja kwa imani, kwa fikara la kuponya, amegusa koti langu, kwani kipawa cha uweza wa uponyaji kimetoka toka kwangu. 23 Na mwanamke akajua ya kwamba alichokifanya kimejulikana, yeye akaja na kupiga magoti miguuni pa Yesu na kusema yote. 24 Na Yesu akasema, Imani yako imekufanya uwe mzima, enenda zako kwa amani. 25 Sasa, alipokuwa akizungumza, matumishi kutoka nyumba ya Yairo akaja na kusema, Mkuu wangu, Yairo, usimsumbue Bwana kuja; mtoto wako kafariki. 26 Lakini Yesu akasema, Yairo, mtu wa imani, usiruhusu imani yako kutetereka katika wasaa huu wa majaribu. 27 Hicho ni kitu gani ambacho mtumishi kakisema? Eti, mtoto kafariki? Lo, kifo ni nini? 28 Ni kuondoka kwa nafsi-roho kutoka katika nyumba ya mwili wa nyama. 29 Mtu ni mkuu wa nafsi-roho na wa nyumba yake. Mtu anapoinuka toka kwenye mashaka na hofu, lo, yeye aweza kuitakasa nyumba yake tupu na kuwarejesha wapangaji tena. 30 Basi akimchukua pamoja naye Petro, James na Yohana, Yairo na mama wa mtoto, alikwenda kwenye chumba cha aliyekufa. 31 Na milango ilipowafungia makundi nje, yeye akazungumza maneno ambayo nafsi-roho yaweza kuelewa, na halafu alimchukua mwanamwali mikononi na kusema, 32 Talith cumi, mtoto, inuka juu! Nafsi-roho ya mwanamwali ikarudi na yeye akainuka na kuomba chakula. 33 Na watu wote wa mji wakastaajabu, na wengi wangalitaka kumuabudu Yesu kama Mungu. 34 Lakini, kama vile jinamizi la usiku, yeye alipotea na kwenda zake.

Yesu alitumia vielelezi vyenye kufananisha utaratibu wa maisha na mazingira katika kufafanua shauri lake la Kristo na Ufalme. Maisha kama milki ya fahari ya Kristo katika mpinduko wa sura ; toka umilele na kuwa umuda ; yeye alizungumza kupambanua Mambo ya Nyakati na Msuko wa hali na Hadhi.

Kwake yeye maisha ya mwanadamu ni makutano ya jinsi ya kanuni za mwili wa nyama na hivi ndivyo kusema himaya nzima ya ulimwengu wa madhahiriko ; na vile pia, chembe mbegu ya ufahamu kwa ukweli wenye kupita yote yenye ukomo wa hali—pale mwanadamu ahusishwavyo kiuzima wake na utambuzi. Katika hali ya kawaida huweza kusemwa kwamba binadamu ana macho mawili ; moja ni lenye kuona mambo kwa kanuni za vipimo, kadri, ukiasi na kupelekea ujengaji wa hoja/fikra ; na hali jingine ni lenye kutazama hadhi ya mambo kwa wakati pasipo kujenga hoja. Basi husemwa pia jicho moja lenye kuona kwa hoja za tafsiri ndilo mkingamo wa kutambua Ufalme wa Mbingu uliopo hapa na sasa. Na ndivyo hivi kwa nini--lugha ya picha ama vielezi ni ufundi wa kuzunguka hoja na hali vile vile kuonesha hadhi ya mchukuo wa sura kwa jinsi yake na hata namna ya hali endelevu ya jambo. Na hivi pia kusema binadamu hataingia katika ‘Ufalme wa Mbingu’ hadi tu Macho yake mawili yawe Moja—kusudi apate kukirimika kwa ‘Busara’ ya Roho wa Uzima na hivi kujua hata mambo ya Kina katika ile Moja. Kuachana la lile moja jicho lenye kumponza kutoufikia ‘Ufalme’ angali likimpatia yeye namna ya utumikivu baina yake na viumbe vya dunia na mazingira yake kulingana na hisia zake na fikra za utanabaishaji... Na hivi tena Kristu ndiyo ile Njia, na Kweli, na Uzima—Neno la Uzima wote na namna ya kuipata ile Nia ya kung’amua mashauri ama maarifa juu ya yote na kote. Hakuna mwenye kuweza kuingia Ufalme wa Mbingu ila tu kwa kufanyika moja na Kristu. Kristu--jicho lenye kuona kote na kutambua yote na hali hilo halitambuliwi na mtu ila tu katika yule mtu aliyezaliwa mara ya pili katika Nuru iingaziayo kote ; kumfanya huyo mtu kuwa mwana wa Nuru. Asiyekuwa katika hii nuru kuwa ni mwana wa giza na mtu aiishiye katika nchi ya kimvuli na vina vya tafsiri kwa jinsi ya fahamu za mwili wa nyama na kwa hekima ya mambo ya kimwili.

Na hapa ndipo penye hekima ya Neno lenyewe, aliye na macho na aone, aliye na masikio naasikiye.



Oganam ya Karne ya 21 juu ya Njia ya Tatu inajengwa juu ya shauri lenye kuelekea katika Jicho lenye kuona kote na kwa nia yake ya ung’amuzi.



Jitihada za mtu kuitafuta ‘Kweli’ kusudi aje kuisimamisha heshima ya utu wake ndiyo hasa hutajwa ni ‘Kuuleta Ufalme’. Ufalme huletwa kwa matendo yenye kheri kwa kadri ya Nia ya mtu aliyekirimika kuyajua yaliyo katika hazina ya Mbingu. Mwanadamu si mkamilifu wa kutunukiwa shani ya ubora usioharibika mpaka apate kufahamu ufundi wa kujenga hekalu lake ambamo ajifunza staha ya ‘kuabudu katika roho na Kweli’.


Basi lipo jiwe liliokataliwa na Waashi wa Dunia hii ya nchi ya watu wenye kuishi kwenye vimvuli na hali ndilo jiwe kuu la pembezoni kukamilisha Hekalu lisilobomokeka na kile hasa kitovu cha ‘Ufalme’ ulio ni ule uhuru wenye kumweka mtu huru kweli kweli. Na Jicho la Tatu ndilo jicho ambamo ‘mbili hufanyika moja’ kwa wakati wowote na mtu kufanyika Moja na ‘Kweli’ ili kuuendea ustawi na ustaarabu mpya—mpangiko wa ulimwengu mpya.

Tekinokrasia ni ujenzi ; ni ujenzi kwa mujibu kwa picha na kanuni zenye kukirimika kheri. Yesu alionesha hizo ramani za ‘Mpango Mzima’ lakini matokeo ya shughuli yake yalibashirika hata kwa wenye busara wa siku hizo ; kuwa zama yake itatambua japo kidogo tu shauri lake juu ya huduma yake kuu na mshughuliko wake. Kwa kuwa kizingiti kikuu ni mlemeo wa ujinga wa fahamu za mwili na mazoea ya mapokeo na kiutamaduni wa kufikiwa. Kosekano la usafi wa dhamira katika moyo wa wanadamu wenye kuruhusu maarifa yenye kubatilisha utaasisi na mapokeo ya kale na kusimamisha mambo mapya.

Zama yake Yesu inakatikia na hii hapa sasa zama mpya ikisogea karibu kabisa. Wanadamu wote wa siku ya leo wanataharuki migogoro mikubwa ya kiustawi na mapokeo ; vile vile mitafaruku ya kisiasa, machafuko na hata mapigano. Mahodhi ya kiuchumi kwa mataifa na udororaji wa ‘ukuaji’ wake. Na katika kutazama Utaasisi wa taaluma za mambo ya sayansi na pia mawasiliano na usambazaji habari ; haya mawili kuchukua nafasi ya kuonekana kana vile ndiyo shani ya ‘ukuhani mkuu’ na ‘utowashi wake’ katika kipindi hiki katika kushawishi mwelekeo wa ukubali wa watu kuamini kitu gani juu ya maisha ama wachukuliaje taarifa—kila siku. Vile vile itikadi za kiutawala zenye kufanya mamlaka katika serikali za watu hali ni zenye kupwaya shauri kuu juu uhusishaji na vile vile maridhiano kwa raia wake wote katika sura ya mikakati ya kupanga na pia katika kutekeleza mipango ya ustawi ndani ya mipaka yao.

Mihimili ya mapokeo ya dini zote zenye idadi kubwa ya watu inaanza kukosolewa na kuumbuliwa juu ya mashauri ya uchukuliaji wake wa maadili. Ukasisi wa kusisitiza utaratibu wenye kuonekana kama ni sahihi katika macho ya wanadamu na kumbe ni njia ya mauti yenye kujishindilia aibu ya unajisi wa makusudi wa nguvu za uzazi. Uimamu unaojaza fikra za uharibifu kwa minajili ya chuki-- kwa umma wa waumin wake ili kujitoa muhanga kwa mauaji ya kukusudia na hali wao wenye siyo wenye kuonesha mfano wa kufa kwanza ikiwa mashauri hayo ni yenye kujitosheleza ukweli. Haya yote kuonesha jinsi kiu ya haja ya ushawishi huweza hata kumsukuma mwanadamu kutenda upumbafu na kuhatarisha amani na maridhiano—na hilo hatimaye kumtafuna mwanadamu mwenyewe na ustawi wake.

Maelekezo yote ya wenye kheri yaliyoleta dini na ukundiko wa kiimani sasa hayanabudi kutathminiwa matunda yake na hukumu kupitishwa. Baraza la kutoa hukumu ni utashi wenye kuinukia kwenye jicho lenye kuona kote na tena la Muamuzi mmoja kwa kila mtu mwenyewe—si tena andiko lolote wala shauri la nje nje juu ya watu kwa ujumla.

Oganam ya karne ya 21 juu ya Njia ya Tatu ni kazi ya udadavuaji kwa mwanadamu mwenye kutafuta sura ya mfananio wa utatuzi kwa mambo yaonekanayo ni magumu kutafutia majawabu katika wakati huu wa mpito kuianza rasmi zama mpya.

Oganam ni chombo chenye kutumikika katika mchakato wa kazi, na hasa pale ukwamuzi unapohitajika kwa tatizo lililojitokeza. Lakini vile vile kwa jinsi yake ni wavu wenye kuchuja yatakiwayo na yasiyotakiwa kutoka baharini.

Kupokelewa kwa kazi hii ya Oganam katika jamii ya watu wote duniani ni mashauri kuwasilishwa katika siti ya Muamuzi na matokeo yake ya kufikia hukumu juu ya mashauri ni kunawa ama kujisafisha ili kuingia Zama Mpya—na hivi ni Mavuno ; kipindi cha kutaharuki pumba na uwele vikitenganika kwa pumzi ya upepo unaovuma...


...... Inaendelea....
 
Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi seh. II
5 Septemba 2011 saa 12:20 Asubuhi
Basi na tuliingie Shauri kuu.

Hoja ya msingi kutokana na itikadi ya kusema kwamba ili nchi iendelee inahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi bora ni yenye kutambua kingo nne za ustawi wa jamii lakini ikakosa hasa uthabiti wa kuthibitika ukweli wake katika muktadha wa ustahimilishaji wa maendeleo na mwongozo sahihi katika kutambua wajibu wa ‘Watu’ na ‘Viongozi’. Katika Hali Halisi, siasa na uongozi ni tu ufikirifu wa kimawazo na udhanifu katika uwanja wa mafikara na mashauri ya kujaribu kuielewa jamii na mambo yake.

Katika jitihada za kulielewa hili tuanze na kupambanua mwenendo wa jamii zilizoanza na makundi ya watu wasio na namna ya utengeneaji mpana ila tu maisha rahisi kujipatia mahitaji muhimu ya kimaisha kama chakula kwa shughuli kama za uwindaji na kutangatanga, uokotaji wa matunda na matumizi ya mazao ya kuchimbuliwa ardhini nk ; kuzizungumzia hizo dhidi ya zile zilizokuja kuendelea na kuanza kujishughulisha na mambo ya kutulia sehemu moja na kuchanganya baadhi ya nyenendo zile zilizotangulia pamoja na shughuli zingine mpya mfano kama kilimo, ufugaji, sanaa za mikono na utengenezaji vitu vya kutumika katika maisha ya kila siku.

Kusonga mbali kuzidi yote hayo mawili tunatazama muungano wa kaya za jamii zenye kubobea kwenye shughuli za aina yake na kuanza kufanya ziada za mazalisho yake ikilinganishwa na muktadha wa mipaka yake midogo midogo ya kujisimamisha juu ya nchi na hivi kuja kuibuka kwa utaratibu wa mabadilishano na mahusiano katika sura iliyopana zaidi na zingine kutoka mbali.

Mabadilishano na mahususiano ndiyo kipengele cha kwanza cha jamii ambacho kipimo cha usawa katika muktadha wa ulinganifu wa hitaji na upatikaji ; hayo hutafuta vigezo sahihi vyenye kuridhisha pande mbili zinazokutana uso kwa uso. Na hili pia linazaa shauri juu ya jambo lenye kuitwa ni uchumi. Uchumi katika jinsi ya kufafanuliwa maana yake kutokana na lugha ya kiyunani huelezwa ni uendeshaji wa mambo yenye kuhusika na mahitaji ya nyumba ama kaya ‘oikonomia’. Ni muhimu kabisa kutambua sana chimbuko halisi la uchumi kuwa ni utoshelezaji wa mahitaji ya jamii ama kaya ya watu katika sura ya ‘kuzalisha’ na ‘kutafuna’. Kama vile nyumba ndivyo ilivyo ni mwili mkubwa wa mtu na pia kaya katika kusogeza mahitaji muhimu ya maisha mfano wa maji na chakula ; Uchumi katika sura halisi ni jambo-mama mfano wa nyumbani. Uchumi ni uvumbuzi wa mwanamke kama ilivyo kwa kilimo.

Mama kama mratibu wa mahitaji ya kaya yeye pia ni mvumbuzi na mwendelezaji wa utaratibu wa kubadilishana mazao toka sokoni, kwa kuleta na pia kupeleka, ili kuijaza na kuitia afya kaya yake. Kwa kuwa kuna nadharia moja yenye kusema shauri la kuwa, kuanza kwa shughuli ya kaya ni pale ilivyokuwa mwanaume ikimpasa kwenda kuwinda wanyama porini ; naye kumuacha mwanamke katika kukaa na watoto na kuwatunza kwa ukaribu ; basi na yeye mwanamke akaanza taratibu kugundua mimea inayolika akitofautisha na ile isiyofaa kuliwa ambayo ndiyo mbadala kwa chakula cha nyama ; na pia taratibu baadaye, kuanza mazoea ya kupanda na kuivuna mimea hiyo yenye kustahili kulisha watoto na kaya nzima na pia kupendezesha mazingira ya nyumba kwa kupanda mimea yenye maua na yenye kutoa matunda yenye kumpendeza yeye moyoni na machoni pake na ndivyo chimbuko la ujumi, hisia za kupenda kujishughulisha na mambo yapendezayo—ni ndivyo kusema mwanzo wa shughuli ya kilimo na kuendeleza makazi ya kudumu sehemu moja bila kuhama hama. Ni hekima ya Mwanamke ndiyo iliyomfundisha mwanaume kukaa sehemu moja na kuacha silika yake ya damuni ya kutanga tanga na kujihangaisha kwa chochote. Na hivi mwanamke anachokipengele muhimu katika kutambua mwanzo wa ustaarabu wa mwanadamu—huduma, biashara na ustawi.

Pale mabadilishano ya kijamii yanapopoteza ukadirifu wa namna yake ya usawa katika hayo ndipo kipeo cha kwa kwanza cha ushawishi huzaliwa. Jamii ambayo inapunjika katika mabadilishano haiwezi kukubaliana na hali ila tu kwa shinikizo ama ushawishi ulioelekezwa katika upande wake. Hapo ndipo huzaliwa makundi yenye kudumisha tofauti za stahiki na usawa na pia ndiyo mwanzo wa taasisi katika jamii. Jamii yenye kutengua usawa wa kimabadilishano ni jamii yenye ushawishi dhidi ya ingine yenye kuruhusu kushawishika kwa namna yake ; kulingana na itikadi zinazotawala pande zote mbili.

Taasisi ya msingi kabisa katika maisha ya mwanadamu ni kutaniko la mwanaume na mwanamke lenye kuzaa watoto. Baba, mama na watoto ni taasisi yenye kujifafanua shauri lake kuu juu ya namna ya sura ya mipango yake na kulirithisha kwa watoto kwa nguvu za kiushawishi ili nao wao waje kufanya hivyo hivyo. Na tendo la msingi lenye mabadilishano ya usawa katika jamii ni tendo la kujamiiana. Mwanaume kutoa mwili wake na mwanamke kuutoa mwili wake ni msukumo alioundukia mwanadamu na unamtaka yeye kuwajibika na kuthamini mazao ya hiyari yake kuyaendea mabadilishano kwa jinsi ya utangamano wake.

Taasisi ya pili iliyowazi kujitokeza katika mfanyiko wa utengeneaji wa mwanadamu na jamii huchukua sura yake katika uwanja wa mipaka ya medani za mabadilishano nje ya mwili wake ambayo ni amari ya kujifunga na mazao ya kazi zake za mkono na pia namna yeyote ya huduma ya kazi na kuwa na hiari atakapo kujifungua toka kwa hiyo ; na tena kwa ajili ya kumwachia mwingine iwe katika sura hiyo hiyo ya huduma ya kazi ama zao la kazi. Naye huyo mwingine kufanya hivyo hivyo kwa hiari yake kwa mapatano yenye maridhiano ya kukubaliana bila deni wala kinyongo. Ikiwa uso wa makutano ya mabadilishano una kuzidiana kwa upande mmoja, bila afiki la nia hiyo kwa upande mwingine, basi ukosefu wa utangamano unaoweza kuleta mvurugano wa hali ; mvurugano huo unapothibitiwa na kuwa rasmi katika kutumika hivyo hivyo—kwa sura ya chombo cha kufanya hivyo ; huo huwa ni namna ya Utaasisi wa mtu/watu.

Utaasisi kulingana na jumla ya matendo na sura mbili zinazokutana mara kwa mara katika jamii ndiyo huleta utanuzi wa kisomo cha ‘akitipu’ na ‘ukawaidishaji’. Kuja kufaa kuzungumza ya kwamba kawaida ni kama sheria. Shughuli katika jamii inaweza kutendeka kama kawaida na kumbe huku ‘mazoea’ ya kuyaingia matendo na fikara-mbegu yake ya msukumo wa matendo yaani akitipu ni mchangamano wa itikadi tawalifu na uruhusu wa mtenda au mtendewa pia wakati mwingine chini ya utaratibu unaolinda shughuli zinazokuja kuonekana ni rasmi katika nyenendo zote za maisha ya kila siku.

Ujuzi wa kulinda nyenendo za jamii katika muktadha wa hiari ama shurti ndiyo kwa wakati kumekuja kuzaa kutungaji wa sheria na usimamamizi wa utekelezaji wake. Na jamii tofauti zina historia tofauti za kufanya sheria na kuhifadhi utaratibu wa shughuli zake zinazotambuliwa na watu wenyewe katika sura ya ustawi wao.

Pale uzalishaji mazao ya kazi ulipoongezeka na kuwa mseto mpana ndipo hata sura ya madilishano iliposukuma aidha binadamu asonge mbele ama akwame juu ya suluhu ya kigezo mbadala vya mabadilishano ukidhifu wa haja.

Tunajifunza toka katika historia jinsi watu wa Mesopotamia wa zamani walipoinuka ghafla kutoka kwenye maisha ya kutanga tanga na kukusanya matunda hadi kuwa na ustaarabu mkubwa baada ya kuibuka kwa ‘miungu’ kutoka majini ambao waliwafundisha watu hao mbinu za kilimo, kisomo na matumizi ya sarafu za fedha. Vile visa vya Gilgamesh na mfalme-bahari Oannes. Wakiwafundisha kuhusu misimu na upandaji, mafunzo ya ujuzi wa kusoma na kuandika na hisabati na ujenzi. Pia kutoka huko twajifunza kuhusu mfalme Hamurabi iliyebuni na kuwakilisha taratibu za mambo ya kifedha na labda ndiko huko mambo ya ‘riba’ na ‘faida’ kuhusishwa na biashara ; yalipitishwa katika utaasisi wa watu.

Basi tulipo leo katika upana wa mambo ya ustawi wa jamii hapana tofauti na pale pa siku zile binadamu alipokwama juu ya shauri kuu la misingi ya mabadilishano. Na yeye kuazimu kutoka katika mabadilishano ya mali kwa mali hadi yale ya ‘mali-kwa-fedha-kwa-mali’ ilivyo ni jinsi ya biashara. Riba na Faida ndiyo mwendo wata hii leo mintarafu uwanja wa mabadilishano ya kijamii.

Ipo tofauti ya siku za leo na zile za zamani ambapo ‘mtaji’ mkuu wa mtu ulikuwa ni nguvu zake mwenyewe na labda na za hayawani wengine... Mapinduzi makubwa ya mbinu za kazi na uzalishaji yaani tekinolojia ; yamekuja sambamba na mapinduzi ya matumizi ya Nishati na huduma ya Maji na Afya. Matokeo yake ni sura ya uchumi tengevu wenye kuzaa ulimbikizi, mienendo ya kitamaa ya mali na fedha kama ‘nguvu ya kiuchumi’ na pia kupanuka kwa utofauti wa matunda ya ustawi kutoka mahala pamoja hadi kungine. Hili ni adha hasi ya utaratibu wa riba na faida katika biashara na mabadilishano ya hata rasilimali na bidhaa ; na pia uhodhi wa tasnia, vyombo vya mitaji katika miliki moja ; ile yenye kufanya biashara na nyingine isiyokuwa na mitaji, tasnia za kitekinolojia na maarifa ya kutosha kujikwamua. NA hivi binadamu leo anakigugumizi ; uchumi wa leo umekuwa ukizaa migogoro na udororaji. Lipo hitaji lakutafuta suluhu ya kuondoa riba na faida katika sura ya kibiashara kusudi biashara iwe ni yenye mabadilishano ya sarafu na huku matokeo yake ni yenye kuboresha pande zote mbili pasipo moja kunyonya nyingine katika muktadha uliofichika ; na vile vile kwa wale wanaohusika katika kufaidika, kujipatia nguvu za ushawishi hata kutawala wengine kwa itikadi, agenda, siasa za kimataifa na kujifanyia ‘ukuu’ wa kitaasisi kwa fimbo ya fedha na pia matokeo ya ujinga kwa wale wasioshtukia ushabiki wao mbaya kwa falsafa mbovu ya taasisi zinazowazunguka.

Jinsi hii ya mabadilishano yenye kubebea hadhi ya yote mawili fedha na fanaka ya kheri baina ya pande mbili ndiyo shauri kuu la kazi hii niliyoiandaa ya USANISI WA UJASIRIAMALI WA KIJAMII, Oganam ya karne ya 21 juu ya njia ya tatu.

Na katika kudadavua mashauri ya itikadi na itifaki za leo ; tuzikague hekima na falsafa zinazofafanua misingi ya leo na chenye kutajwa ni ‘ustaarabu’ wa mataifa ‘yaliyoendelea’.

Kumekuwepo na falsafa na mawazo mengi juu ya utawala, mamlaka na sheria, shani za kudra njema na maadili ya raia katika kuunda jamii ; na ambapo kuna wakati ulizaliwa utaratibu wa ujitengeneaji wa kijamii katika muktadha uitwao ‘Jamhuri’ yaani vile ukidhifu wa haja iliyojitokeza kwa mfano pale watu walipokuja kuanza kuwa na ustaarabu wa kudumu kukaa katika nchi moja kwa muda mrefu na hali ya kuja kukua kwa namna zake za mabadilishano ya kijamii kama uzalishajimali na biashara, elimu, utumishi na itifaki za taasisi za utaratibu, tawala, miliki na sheria.

Jamhuri ni utaratibu wa kitendo cha hali ya kuwa na watu/wanajamii wenye kujitengenezea utaratibu wa wawakilishi katika kusimamia na kutetea maslahi yao ndani ya utaifa kwa mtindo wa kuweka nafasi za madaraka na mamlaka ya sheria . Na hii shughuli ina sura mbali mbali kutokana na jamii mbalimbali zilizopata kuwepo hapa duniani. Ikidhihirisha kuinukia kwa ustaarabu na ustawi wa jamii mbali mbali na tamaduni zake ; kiwango na pia ngazi za ufahamu katika kuzaa tunda la maarifa na utumikivu vipawa vya kuongozea utendaji wa watu wenyewe.

Msisitizo wa takwa la msingi kwa hapa na sasa ni basi kujaribu kukagua ikiwa falsafa iliyopo hadi hii leo duniani je, hii ni yenye kumtosheleza mwanadamu na kumtimiliza kimwili, kiakili na kiroho ? Na ikiwa binadamu wamekuwa wakichagua sana mafikara juu ya kujichukulia kuangalia mwili na hisia zao za kila siku, kipi kimeonekana kukosekana katika ustawi wake ? Utenganisho wa dini na mamlaka kwa mfano ; je, ilikuwa ni lazima kama historia ilivyokuja kuchukua sura hapo siku za nyuma? Nafasi ya dini ni nini katika jamii; na shauri kuu la mamlaka ni kitu gani katika jamii ? Je, yatosha kusema kuwa kiongozi ni mtu mwenye madaraka katika jamii ? Jamii ni akina nani ? Je, ni zipi sifa za kiongozi zingalimpasa yeye kuwa mwenye kustahili ‘madaraka’ na ‘mamlaka’ ? Je, siasa kwa kiasi gani hukidhi ama kutosheleza kuwakilisha mawazo ya kiushawishi ya watu/wanajamii dhidi ya mifumo iliyopo katika jamii husika na hivi ufanisi wa utawala katika sura ya madaraka hufaidikaje na hizo? Je, mchakato wa mawazo na fikra za mtu mmoja mmoja zinaweza kweli kuwakilishwa vya kutosha kwa mitindo ya uwakilishi iliyopata kuwepo/iliyopo pasipo kumezwa na mengine ya ujumla jumla ? Je, jukumu la uongozi ni ukaribisho wa wazi kwa yeyote kwenye kutaka ama kujifikiri kustahili kugombea nafasi--yeye kujitosa katika kinyang’anyiro cha kutafuta kushika kiti kikuu na ili pia kufaidi kuinuiliwa na kuwa na amari ya uamuzi juu mashauri ya kiutendaji ya wanajamii wanaongozwa pamoja na wawakilishi wao ? Je, kiongozi ni mtu wa kawaida kama wengine ama ni mtu mwenye vipaji maalum vinavyokosekana kwa raia wengine ? Je, ikiwa kuna tofauti, tofauti hizo zaweza kuwa ndiyo ‘mtaji’ hasa wa kapewa siti ya utawala ama kuna lingine ? Je, liwezekanalo kwa ‘kiongozi’ lina tofauti gani na yule asiye kiongozi ; na je, ni tu uwezo na nia ya mtu ama kuna jingine kama sababu ? Je, ushawishi wa kiongozi aliyekatika hatamu ni ‘nguvu’ zake mwenyewe ama kuna misingi ya namna ya uchochezi ndani ya mzingo wa chombo chake cha uongozi yaani namna ya utaasisi ? je, taasisi zina nafasi gani katika msukumo wa mabadiliko ya jamii nzima ? Je, maendeleo ni zao la mtu/kundi la watu bila mpangilio wowote ama ni mtu/kundi la watu wenye mpangilio na ushawishi kustahili kuitwa ni taasisi yenye dira, dhima na mbinu ? Na Je, maendeleo ya mwanadamu yanapimwaje, kwa namna ya fikra zenye ukomo, kama ubunifu wa mipango na usimamizi wa miradi yenye kutazamiwa ama ni yale ‘Maono’ ya kiustawi na tena yenye kanuni zenye kuweza kuakisika kwa namna za fikra zenye kuweza kuchukua sura yeyote ili hali ni ndani ya kanuni zenyewe na hivyo kuwa mipango ndani ya mpango, visura ndani ya sura isiyo na mpaka? Kwa hivi je, kuna maarifa yeyote juu ya kuwa ‘kiongozi’ halisi katika sura kamili hasa na taratibu zake ?

Namna ya utaratibu wa miliki na tawala uliopo sehemu kubwa duniani ni utaratibu ulioendelezwa ama vile vile sahihi kusema ulioasisiwa kwa namna ya kadri mpya, wakati hadi wakati, katika sehemu ya mashariki ya kati miongoni mwa wafikirifu wa Uyunani ya zamani—katika zile zama zao ambapo vilele vya ustawi na ustaarabu vilifikiwa na tena taratibu hizo kuja kuonekana kufaa kuigwa na kuboreshwa na tawala za wengine duniani kadri wakati ulivyokuwa ukienda hadi kufikia hii leo.

Kwa kuwa utaratibu unaotawala nchi nyingi kwa sasa ni ubunifu na uchukuliaji ule ule kama ilivyofalsafika uyunani ya zamani katika kupendekeza sura ya jamii, tawala na vizazi vya watu hebu basi twende moja kwa moja kwa wafikirifu wa mwanzo na kuutazama usadifu wao katika kuelewa misingi ya utawala, maridhiano ya kuwakilishana katika maamuzi mazito, usimamizi, uundwaji wa sheria, utelekezaji wa haki, ulinzi kwa maadili mema ya jamii kwa mujibu wa sheria na michakato yake.

Wayunani katika kipindi chao cha kufikia vilele vyao vya juu vya ustaarabu, walikuwa ni watu wenye kuamini sana nguvu ya ‘fikra ya sababu’/sababu za kifikra kuelezea vitu vyote. Walichochea sana sifa za mtu kuwa na karama njema, kutukuza uzuri wa maumbo ama sifa za sanaa, ujumi na maongezi yenye mvuto katika kuleta maana dhahiri na ushawishi katika kupokeleka kwa wasikilizaji.

Wayunani waligusa vilele vya ustaarabu wao huo takriban miaka 460 KK na hivyo tunaweza kujifunza maendeleo yaliyopata kudhahirika katika maarifa/kujua kwao na pia mbinu zao za kustawisha maarifa na hekima yao kwa kipindi kile kwa kumbukumbu ya vinara wa kuchochea na kushikilia hayo.

Palikuwa na mtu anayekumbukwa hadi hii leo kama Socrates ; yeye ni mwanafalsafa anayetambulika kwa kufundisha mbinu za kuweka fikra bayana katika kuelezea jambo na kutetea hoja kwa jinsi hiyo. Njia hii yenye kujulikana kama mbinu ya Socrates iliyopokelewa na kuendelezwa na mwanafunzi wake mmoja aliyeitwa Plato.

Naye Plato alikwenda mbele kubuni namna mbalimbali za uchanganuzi wa kimantiki katika kujaribu kusimamisha falsafa yenye kukusanyia ndani yake yote juu ya maisha.

Plato ndiye mtu wa kwanza kuanzisha chuo cha maarifa alichokiita ‘Akademi’ ambapo watu wa siku zake walikwenda huko ili kuelimika na maarifa ya juu ya kipindi chao. Sehemu kubwa ya mambo yaliyokuwa yakipitisha muda katika maisha ya kila siku ya taasisi hiyo ya elimu ilikuwa na majadiliano juu ya mawazo ya mabingwa wa kupambanua masuala ya maisha na asili. Hayo yalikuwa ni mawazo kuanzia masuala ya kijamii hadi falsafa ya chimbuko la maarifa na elimu yenyewe-- yaani kuyakagua mashauri kwa epistimolojia yake. Plato kwa mfano, aliandika vitabu kadhaa katika mtindo wa mazungumzo kati ya Socrates na mwanafunzi akiwakilisha baadhi ya mashauri ya Socrates kuhusu chanzo cha maarifa na kujua. Socrates alikuwa ni mwenye kusimamia hoja ya kudai kwamba maarifa yote ya mtu si chochote hasa chenye kustahili kuitwa ni ‘kujua’ bali hayo ni tu kumbukumbu ya mtu katika kukumbukia yaliyopita akilinganisha na yanayoendelea katika akili yake. Socrates alikuwa ni mwenye kudai ‘maarifa ya kweli’ hayawezi kunakilika katika akili ya mtu yenye kutenda kazi kwa namna ya mawazo. Na hivi yote ya kufikirika kwa mawazo ni ‘kimvuli’ na bado hayajafikia hadhi ya kufaa kuitwa ni ‘maarifa’. Dhana hii ya maarifa yasiyogusika kuwa ndiyo ile ‘picha’ kamili ya yote yanayokuja kufikirika kwa mtu ndilo imekuja kuzaa ‘falsafa ya kiplato’.

Kwa miaka mingi mbele hata baada ya mashauri ya Plato kwenye kazi yake ya ‘Republic’—Jamhuri ; kwa mfano, imekuwa ikihusudiwa na wafikirifu wengi katika kutanabai ugumu wa falsafa. Kwa kuwa hata katika kipindi kabla ya Socrates kumewahi kuwa na wasikirifu katika uyunani kama mmoja mwenye kufahamika kama Herakraitasi ‘Mtata’ ambaye amewahi kuzungumza juu ya kutowezekana kwa falsafa ya kweli kuandikika kwenye namna yeyote ya maneno... Lugha ya Herakraitasi ilikuwa kwamba ulimwengu wote uliofanyika ni ‘siyo kweli’ ila tu kweli yenyewe ni jinsi ‘iliyofichika’. Kwa hivyo hata katika siku za Socrates na Plato, wanakisomo wengi walikuwa si wenye kuridhishwa na msimamio wa shauri la wasikirifu kama Herakraitasi. Wao walikuwa ni wenye kutafuta namna ya kupata kueleza yote ama njia yenye kuweza kuelekeza kwenye kufafanua yote na kuwa ‘maarifa’.

Basi Socrates alikuwa ni mwenye kujenga ushawishi wa falsafa ya jinsi ya ukanushaji, na hali kiu ya wakati ilikuwa ni kutaka shauri kinyume juu ya kutaka kuyaelewa mambo. Falsafa ya jinsi ya ukanushaji inabainisha upotofu wa tafsiri juu ya kweli ya ‘maumbo’. Falsafa hii inazungumza kuwa kinachoonekana ‘ni sicho’ ila tu ‘kisichoonekana’. Kwa jinsi hiyo kisichoonekana ndiyo ‘kweli’ na ‘daima kuwa’. Na hivi pia kulikuwa na shauri kwamba ‘maarifa’ ya kweli huja kwa jinsi ya ‘ufunuko’ uwezao kutokea kwa mtu kama vile msanii apatapo wayhi wa kazi mpya—gutu la mfano wa kazi iliyo haijafanyika.

Socrates pia katika kazi ya kitabu cha Republic anazungumza juu ya starehe ama raha kubwa mno ijayo na ‘ufunuko’... Kwa hiyo yeye hujenga hoja kuwa namna ya ‘uroda’ ndiyo wenye kuweza kuleta ‘aarifa’ na kumfanya aliyepokea hilo kuwa ni ‘Mfalme Mfilosofia’ na mtu mwenye kufaa kutawala. Na hivyo pia shauri la ‘haki’ iliyokamili katika maisha inawezekana ingawaje wengi katika kipindi chake walikuwa wakijaribu kudadavua shauri halisi mintarafu ‘haki’ katika jamii.

Kulingana na Socrates, ni kana vile alisema yule aliye ‘funukika’ ajua juu ya haki ; ila hili halikutosha kueleweka bayana miongoni mwa wanafunzi wa falsafa na labda hadi hii leo hali ni hiyo hiyo. Basi Plato akiwa ni mwanafunzi na uzao wa kisomo cha Socrates kiasi kwamba kazi zake zilikuwa ni chombo cha kufikisha ujumbe wake, alikuwa ni mwenye kuafiki shauri kuhusu mambo ya Juu—yaani Mbingu ; kuwa kwa karama zake zilizofichika, hutawala yote katika maisha ya watu na ustaarabu wao kwa kadri ya kazi yake ya Timaeus. Pia mashauri juu ya ‘nafsi-roho’ isiyokufa kwa kadri ya vitabu vya mazungumzo ya Socrates viendavyo na majina ya Phaedo na Phaedrus.

Kulingana na mashauri yake mwenyewe juu ya jamii isiyoongozwa na ‘Mfalme Mfilosofia’ ila namna tu za taratibu za kijamii na kisheria, Plato alizungumza juu ya taratibu tano za kitawala katika jamii zenye kuja kusimama kwa sura zake. Kwa mujibu wa dhana ya ‘nafsi-roho’ ilikuwako ndani ya mtu, Plato kama ilivyokuwa kwa Socrates vile vile, wote waliamini ya kuwa hiyo nafsi-roho ya mtu ndiyo huja kusimamisha vipengele vitatu vyenye kuhuisha sura ya mtu ambavyo hivyo ni fikara, takwa-hamu namatendo. Basi tasnifu ya Plato juu ya ustawi wa jamii ni yenye kuendea kutambua namna na makundi makuu matatu katika jamii—(1)wale walio ni wafanyakazi kwa zile zote kazi zenye jinsi ya uzalishajimali kama vile useremala, ujenzi, wafuga mifugo, wafanya bidhaa za biashara n.k ambao yeye aliwatafsiri hawa kuwa ni wale wenye kuwakilisha kundi lenye jinsi ya kudhahirisha ‘Hamu ya Chakula’ kwa nafsi-roho.(2) wale walio ni wenye kuilinda jamii ambao ndiyo askari wa kupambana vitani, wenye mioyo ya ujasiri na ushujaa hata kuweza kufunga safari za kufa ama kupona. Hawa aliwatafsiri kufanania kwa sehemu ya ‘Roho’ katika nafsi-roho. (3)Watawala wa vyombo vya mamlaka ambao yeye aliwalinganisha kufanana na kipengele cha ‘fikara’ kutokana na nafsi-roho. Na yeye aliona kuwa hawa ni hufanya kundi la wachache katika jamii.

Tunaweza kusema hapa kuwa kundi la kwanza ndilo lenye kufanya hitaji kutambuka na kuelekea kulitimizia haja yake katika mizunguruko ya uhitaji na upatikanaji wa mahitaji—hamu na matendo ; na hali angali kundi la pili na lile la tatu ni pacha katika kuiwakilisha mipaka ya ustawi na utaratibu katika vipindi vya vyote vya urefu wa maisha ya wanajamii kama chombo/taasisi moja.

Na hivi tuzitazame taratibu tano za kiutawala na hivi taratibu zake hasa za kuja kufanyika ama kujitokeza. Plato aliita taratibu hizi tano kwa majina yafuatayo ; na huku pia akisisitizia ushukaji chini wa kadri ya hadhi ya ubora : Aristokrasia, Timokrasia, Oligaki, Demokrasia na Dhalimu.

Kulingana na hadhi ya kufanyika kwa jinsi ya nafsi-roho, Plato alifananisha Aristokrasia na utaratibu bora kabisa ambapo wenye kutawala hutenda hivyo kwa kufuatisha fikara/hisia-matendo kama vile ‘falsafa ya kiplato’ inavyoelekeza.

Jamii ya mtu wa kiaristokrasia ni yenye kuendana na sifa ya kudumisha sababu za kifikra zinazotawala mienendo ya maisha na huamua mambo na kuyatambua kwa jinsi ya ‘neno’ ama ‘fikara la kheri’. Kufanya hivyo katika kuakisika uwianifu kati wa pande mbili mbili za mashauri na uzito wake akilini ilivyo ni busara; kama inavyoashiriwa na ‘falsafa ya Plato’ ambayo pia ni yenye kusisitiza kuzienzi karama za utuwema kama shani ya Mbingu katika mtu na ustawi wake. Na hivi katika maisha ya kila siku ya jamii yenye kuleta tunda la mtu wa jinsi ya kiaristokrasia ni yenye utaratibu wa mafunzo lukuki ya kiakili, michezo ya kimwili kwa ajili ya hadhi ya ukakamavu, kwa ajili ya wepesi na nguvu za kukamilisha vitendo kwa ufundi na pia maambukizo ya desturi njema ambazo humfunda mtu kustahili kung’amulika miongoni mwa wengine katika jamii kuwa kama ni wa nafsi-roho ya ‘dhahabu’ ; chuma bora, adimu na yenye shani. Vile vile hayo ni kusudi kumuandaa yeye apate kutambua na kulea kudra njema kwa kuzaliwa ; na kuenzi karama bora kwa nuru ya ufahamu wake wenye kupenyezea akili yake ya mambo ya kila siku.

Utakato wa jinsi ya dhahabu, humuinua muastokrasia na kumfanya yeye kuwa ni mwenye kufurahia mambo ya ustaarabu wa juu kuliko siasa zozote katika jamii. Na hivi kustahili kusemwa ‘muastokrasia halisi’ kwa wakati ; yeye yuko kuzidi ile tamaa yenye kuweza kuongoza mtu kutumia vibaya nguvu za kimamlaka. Azma yake juu ya watu ingalikuwa ni tu kudumisha karama njema kama zile ambazo yeye azijua na aweza kuziundia namna ya mifano yake ndani ya ustawi wa jamii yake pana iliyojikabidhi katika mwongozo wake.

Katika jamii yenye kutawaliwa na Aristokrasia halisi, shughuli zake za kila siku na magawanyo wa majukumu huhusisha namna fulani ya sura ya Meritokrasia pia. Hii ni kwa maana kwamba serikali hufanya kufuatilia dalili za shani ya karama za utu bora za raia wake ili kuja kuwachukua hao na kuwaweka katika utumishi unaostahili. Pia ukiwaelekeza njia watu hao katika namna ya elimu yenye kuwafaa kuvuna kudra zao za kuzaliwa zilizo ni pacha kwa kukamilishwa na karama njema. Kwani Plato ni mwenye kujenga shauri la msingi kwa kweli ya kuwa mtu mwenye nafsi-roho ya ‘dhahabu’ hawezi kuzuilika kupata kuzaliwa kokote katika jamii ya mchanganyiko wa nafsi-roho za jinsi ya ‘fedha’, ‘Shaba’ na ‘chuma’. Kama vile vile ilivyo kweli hata jinsi kinyume katika kaya ya wazazi wenye jinsi ya ‘Dhahabu’ ; aweza kuzaliwa mtoto wa jinsi ya nyingine ya nafsi-roho pia.

Jamii ya Aristokrasia kamili ni nchi ya kusadikika kwa kuwa ni nadra na labda kusema bayana hakujawahi kuwa na miliki halisi katika muktadha huo wote. Na hivi jitihada zote za kujaribu kufikiaAristokrasia ni jinsi ya watu kutafuta jibu kamili la ‘matatizo yote ya kijamii’ na huu ndiyo ulikuwa ni msingi wa falsafa kwa wanazuoni wa kiyunani. Plato kama chombo za sauti ya Socrates aliyependeka na kuheshimika kwa mashauri yake miongoni mwa chipkizi wapendao kufanya kisomo wa siku zake. Na humo ndani ya Akademi mara nyingine wakichambua mambo kutoka katika sura ya udhanifu wa ‘kamilifu ya kimawazoni’ na picha iliyokaribu na hali halisi waitambuayo katika maisha yao ya kila siku. Basi Aristokrasia hata kwa mfano wa zile tawala ambazo zimesogea karibu na utaratibu huo ; hizo ilichambulika kuonekana kuwa na mianya ya mapungufu katika ile minajili ya kuikagua na kuzungumzia kadri ya ushahibifu wa mkunjuko wa sura halisi katika jamii husika—ulio ni uadilifu wa kuendana na sura ya ukamilifu wenye kudhanika tu akilini pa mtu mmoja mmoja na hasa kwa kumtazama muastokrasia na hali ya vile katika kupita kwa wakati kuwezavyo kuleta mapokezano ya shughuli ile ile.

Hivyo hata kama pametokea ‘mtawala’ mwanafalsa wa jinsi ya kiplato ni tu katika kile kipindi chake cha ‘uongozi’ wake jamii yake yaweza kustawi hasa na kupata fanaka. Ikiwa kwa kadri uzao wake ni wenye kufanikiwa kufanania kabisa na yeye ki desturi, uwezo, kudra, karama na busara, wanaukoo wake ndiyo wenye kufaa kabisa kuwa ni warithi wa ‘uongozi’ wake kuliko wengineo wote katika jamii. Lakini pia chipkizi la kizazi chake inaweza kurithi yote mazuri kwa kadri ya utajiri na ustawi na kutotilia mkazo shauri la kutafuta karama zilizo bora kwa kipawa cha ‘fikra za sababu’ na basi Jamii hii kuja kuchocheka kushuka ubora hadi kwenye kufikia katika mabadiliko ya kiutaratibu wa tawala za kawaida. Na hali ilipata kuwa ya kwamba kuishi karibu na muastokrasia halisi ni baraka za kuweza kuwa kama yeye kuliko yeyote yule ambaye hajapata kuishi kwa karibu na yeye.

Basi pakitokea upungufu ama ukosefu wa ‘wafalme wafilosofia’ katika miliki ; adha ya kwanza ni kuondoka kwa namna ya Meritokrasia na nguvu za kisiasa kuanza kuchukua hatamu. Pale ambapo siasa zilimezwa kwa kusharabiwa na mashauri ya busara ya ‘wafalme wafilosofia’ hali huja sasa kubadilika na utawala huanza huanza kuchukua sura ya kuwakabidhi viti vya hatamu za kitawala kwa wale wenye hamu ama tamaa ya kuongoza. Na hapa ndio linaingia shauri la Timokrasia.

Plato ni mwenye kuchora picha kuwa wana wa ‘mfalme mfilosofia’ kwa ile hali ya kutotea mali na jinsi ya maisha yao ya kila siku ; siasa inaweza kuwa nje ya silika yao na hivi ili kuendelea kuonekana ni ‘viongozi’ kwa kuzaliwa na hivyo kwa wabidi wao kufanya jitihada kutetea kustahili kwao na hadhi ikiwa wanapenda heshima yao ya nje. Basi hutumia sehemu ya ushawishi wao kuzipika sura za tawala na siasa kwa kuchagua na kupanga wale wanaowataka kushika hatamu za tawala. Na mara nyingi watu wenye kuvutika sana kwenye huo mwelekeo huwa ni wale waliopata kuwa nje ya ulingo wa ndani wa ‘mfalme mfilosofia’ kama waangaliaji/walinzi wa mipaka ya kijamii na taratibu zake nyingine. Kwani wao ni wale ambao walikuwa hawawezi kuona ama kutambua ‘kudra njema’ alizopata kufanyikia ‘mfalme mfilosofia’ kwa kusudi jema la kutafuta kuiga mfano wake ; ila wao walimuona yeye kwa macho ya utajiri wa miliki na mipaka yake ; na ule ‘utawala’ juu ya mambo kama hayo ; na hivyo kwa macho ya utamanifu. Basi wao ndiyo wale wenye kuja kuleta Timokrasia kwa kugeuza utaratibu mzima wa ‘ufalme’ kuwa ni tawala, himaya na jinsi ya dola yake ya ndani pale fursa itakapojitokeza. Kwao hao wataitazama nchi kwa misingi ya nguvu za kijeshi na na upanuko wa miliki za nchi kuliko jingine lolote. Na ndiyo hawa huwa na mawazo ya vita na hata uharibifu kwa kutetea dhana ya ‘kujihami’ na ubora wa jeshi lao. Agenda na ahadi zao mbele umma itakuwa ni daima juu ya utajiri wa mali na nguvu za kihimaya dhidi ya wengine nje ya mipaka yao.

Kwa kuwa watu wa jinsi ya koo za Aristokrasia huwa ni kundi dogo katika muktadha wa mapana ya jamii yote nzima ; hao pia huwakilisha jinsi ile ya watu wachache waliofaulu kujilimbikia mali na ziada katika maisha. Kutokana na hayo wanayo nguvu ya kiushawishi na pia kiuwezashaji kuathiri michakato ya ‘wajasiriamali-siasa’ katika mifumo ya siasa na utawala. Bila shaka wao pia si wenye kusita pale wafuatwapo na mtu mwenye nia yenye kuweza kukidhi ajenda yao ya tabaka la ‘vibopa’ ama ukombaji wa mali zaidi toka kungine. Japo wao ni si wenye makelele wala makeke, uwezo wao ni wa kimya kimya kama upepo wenye nguvu nyingi uletao kelele pale tu unapogonganisha matawi na majani ya miti ama vitu vingine.

Basi pale mali na madaraka vinapofungamana na kutawala michezo yote katika uwanja wa siasa, uongozi na heshima katika jamii; pia kuna madau yanayopotea kwa azma ya kufadhili pilika na harakati za watu wa siasa na michakato ya kusimika viongozi na hivyo tutapanywa kwa mali kwa baadhi ya familia ambazo hapo mwanzo zilikuwa na utajiri. Kifuatiacho hapo ni utaratibu wa tu kwamba mgawanyiko wa matajiri na masikini ; ambapo matajiri wanachukua sura ya watu wenye kushikilia vyombo vyenye ushawishi muktadha wa uongozi na tawala ya dola. Hili ndilo hufikia kuitwa kwenye utaratibu wenye kuitwa Oligaki.

Wale watu wenye uchu wa madaraka na mali pia, huja basi kurithisha vizazi vyao dhana ya ‘mtu mali’ na tena ‘mtu mali’ huyu ni ‘sauti ya mamlaka’ ; tafuta mali uje kuwa mtawala ama tawala uje kuwa na mali na hadhi ya hapo ulipo kitabaka kuja kubadilika ; kwa kuwa ‘mtu kitu’ ; maisha ni kutafuta ‘kitu kidogo’ ama kujihusisha na siasa za kuingia madarakani moja kwa moja ama kwa kushabikia mtu mwenye kukuletea maslahi binafsi kwa mujibu wa itikadi anayosimamia kama mtu ama hata pamoja na kundi nyuma yake; hayo yote ili kujinyooshea mambo yako. Jamii nzima upande wa tabaka la ‘watawala’ katika oligaki huanza kufuatisha nyayo za kukimbizia mwendo wa mali, madaraka na pia hata rushwa. Hivyo vyote kujipenyeza kuchukua nafasi katika mifumo ya siasa, utawala na hata sheria kama sumu kwa haki za wanyonge.

Kadri ya kusonga kwa mwelekeo wa mwendo wa mali, madaraka na uchafuzi wa michakato utawala na sheria kwa mujibu mambo ya kisiasa katika mfumo ; mwishowe huleta hesabu ndogo ya wanajamii wenye kuwa na mali nyingi na pia dalili za upendeleo wa makusudi kwa tabaka lao ; na huku idadi kubwa ya watu katika dola wakiwa si wenye mali na wala sauti ya mamlaka katika sura ya ustawi mzima. Hayo yakijitokeza sambamba na usimamishwaji wa sheria zisizoendana na haki za kimsingi. Lakini wingi nao ni nguvu ikiwa nia ya uamko ikiwepo miongoni mwa kundi lake. Basi pale kundi hili wa wengi linapoamka na kudai kusikika kwa sauti yao katika muktadha mashauri kamili ya ustawi wa nchi ndipo Demokrasia hujitokeza katika kuingilia michakato ya siasa, utungwaji wa sheria, utekelezaji wa haki na stahiki juu ya nchi.

Demokrasia ni kuhusisha maamuzi ya wengi katika kubadili mifumo na taratibu kukidhi usawa wa kiustawi kusudi yale mambo kama umiliki wa mali na shughuli binafsi na kuyatawala hayo kuweze kutoa nafasi kwa wale wote wenye kupenda hivyo ; na kwa maslahi ya pamoja. Na hivi kulingana na kutokea kwake kwenye tabaka la wenye mielekeo ya kudumisha uwezo wa kimali na ‘sifa’ vile hata dhidi ya wasio na mali ; demokrasia ndio huja basi kuzaa misuguano ya kiitikadi ; kati ya wale wenye kutaka mabadiliko ya hapo hapo kwa kubayanisha itikadi na ilani kuelekea mchakato kurasmisha nafasi ya kutekeleza juhudi na wale wasiotaka mabadiliko ya moja kwa moja kwa minajili ya itikadi za kihifadhina kutafuta kinga ndani mchakato huo huo. Upande mmoja kuonesha nguvu ya mawazo mapya na ingine kujiangalia tu ustaarabu wake na kuhofia mabadiliko na kujenga hoja wakilishi.

Na ndivyo hivi Plato aliona wale waliopata upendeleo katika utaratibu wa oligaki hawawezi kufungua milango ya hazina yao kuwapa silaha wale wengi inapotokea hitaji la kupambana na vita dhidi ya maadui watokeao nje ya mipaka ya tawala yao. Kwani wao huhofia mapinduzi kutokea na hatimaye wao wenyewe kupoteza utajiri na ulinzi wa vizazi vyao ikiwa hata hao wengi walio ndani ya mipaka yao wakija kuamua kuwageuka kwa kuwakomesha. Ndivyo kusema vile pia, mwishoni pa utaratibu wa oligaki pia huwa ndiyo mwanzo wa jeshi dhaifu la ulinzi wa mipaka. Vile vile demokrasia daima huweza kuchukua sura mbili misuguano ya ndani ya jamii yenyewe ama hata vita vya wenyewe kwa mwenyewe ikiwa ufundi wa maelewano umebomoka.

Kwa siku za zamani, jeshi lilikuwa ni watu wenyewe na ujasiri wao; lakini kwa siku za sasa ; maendeleo ya ufundi na kutumika kwake yameleta hamu ya mataifa kutengeneza silaha za maangamizi sizizohitaji nguvu ya moja kwa moja ya mtu/watu ; zenye hata kutishia usalama wa dunia yote kwa kuweza kufuta na kuangamiza kabisa kizazi chote kilichopo. Pia tekinolojia imezaa hoja za mashauri ya vitisho vya usalama wa ndani wa wanajamii mbali mbali na mipaka nchi zao na kumbe hiyo ni tu agenda ya matajiri wa nchi hizo ‘kuzikuza’ hofu zao hadi kufutikisha na wengine ili iionekane watu wote ndani ya dola si salama hapo wanapoishi na hivyo ibidi siasa zichukue mwelekeo fulani wa kihifadhina katika kuongoza utendaji wa kiserikali ufahamikao kama sera za mahusiano ya nje— okiondoa zile za mambo ya ndani.

Hivyo basi siku za leo hazina ujasiri wowote hasa ila tu sarakasi za utunishaji misuli, itikadi mbovu na upumbazaji wa umma. Na katika siku za leo ‘Pesa’ inaweza kuwa ni silaha, inaweza kuwa tamu ya kupumbazia umma pia. Demokrasia inaweza kuwa ni mahubiri ya ubabe na kujitukuza ‘nguvu za kiuchumi’ na ‘siasa bora’ na huku vyombo vikuu vya tawala za kifedha kama mabenki na mifuko ya fedha ya kimataifa, biashara utengenezaji silaha na tekinolojia za kijeshi kuwa sehemu ya agenda ya siri ya tabaka la ‘vibopa’ katika muktadha ule ule wa kioligaki.

Kwa matajiri wa leo uwekezaji wao mkuu upo juu ya mipaka ya himaya zao na usalama wa ulimbikizaji wao na huku wakitumia siasa ‘kulingishiana’ mafanikio yao ya kuwekeza katika mikondo ya tekinolojia za kijeshi ambazo hufanya tasnia aghali kuliko nyingine yoyote hapa duniani kwa leo. Pia kufanya umma kusadiki kuwa hata matumizi ya hazina zake itokanayo na kodi za mapato biashara zote za kimataifa kwa sehemu kubwa kulazimu kuelekezwa katika bajeti za matumizi ya shughuli za majeshi na ulinzi kwa mwaka hadi mwaka. Na kumbe kwa utaratibu huo fedha hurudi mikononi mwao na kuwahakikishia utawala wa kudumu kwa mwendo wa kimya kimya.

Basi pale maridhiano yanapofarakana kabisa na mtafaruku wa kisiasa kukosa msaada wa kumaliza mzozo ; jamii husika inakuwa ukingoni mwa mtibuko na dalili za mapinduzi ya lazima kuzuka wakati wowote. Ikiwa mbinu yoyote ya kupindua huo ‘utawala kimvuli’ wa demokrasia iliyoshindwa itafanikiwa kumuinua mtu ama kundi la wanyemeleaji wasio na maadili ; mfano wa mfuatano wa jinsi kana : wale walioanza kujitokeza taratibu pale uastokrasia ulipoisha pumzi ya uhai, wakakosa fadhila toka kwa watimokrasia, wakaota sugu katika kuzoea dhamira mbovu ya ulimbikizaji mali na madaraka wa kioligaki, wakashtukia janja ya utungwaji na upindishwaji wa sheria katika utaratibu wa demokrasia kwa jinsi za rushwa, wakasahau upesi mazuri na mabaya yote ya taratibu zote zilizotangulia—basi wao wakikamatia viti vya utawala hawatakuwa wenye kujali watu wengine wote ila mawazo yao ya kujisikia na kulazimisha kwa wengine pasipo kujali sana wala kuangalia mbali. Ikiwa ni mtu mmoja ndiye aliyemtoa utawalani yule aliyemtangulia kumkuta—tena pasipo kuzingatia sheria na taratibu ; na kukosa kujali kabisa uhalisia wa mambo kama hayo ; basi huo ndiyo mwanzo wa taratibu ya Udhalimukushika hatamu.

Mtu mdhalimu ataigiza kwa nje ustahiki wa yale yote ya ‘ukuu’ katika taratibu zilizotangulia lakini katika sura zake hasi ; kwani yeye hatakuwa na uvumilivu na ustahimilivu kwa maana hatambui thamani ya vitu vinavyohitaji muda ili kubadilika hadhi ; na hivi yeye atakuwa ni mwenye kulazimisha sheria apendavyo, na yeye mwenye kupingana na matakwa yake kwa wakati huyo moja kwa moja ni adui yake ; atastahili adhabu yake na kadri ya ukali wa hasira zake. Jinsi yoyote ya ukaidi katika kutimiza ya matakwa yake itatibua ghadhabu ya kuwakomesha hao walioisababisha hiyo kwake na pia wale wadaku wenye kuthubutu kumchunguza udhaifu ndani ya mji wake wa ndani na mbinu zake dhalimu ikiwemo kuwajichilia mbali na hivi kuua ili kudhibiti hata kelele za ‘chura’ wote wasio na adabu na utii kwa utaratibu wake. Ukimya wa hofu wa wale waliokaribu yake utamjengea hasa kutojiamini ambako yeye atakuficha na maamuzi ya haraka haraka kwa wale wote vizabizabina wenye kutaarifika kwenda kinyume na maneno aliyoyasema ama kumsema. Naye mdhalimu katika kufikia hatua mbaya atakuwa ni mtu asiye na hata yule rafiki wa ‘kumnong’oneza’ jambo kwa faragha ; na yeye ataogopa hata kimvuli chake atokapo nje ya maskani yake na kugeuza hiyo kuwa Ngome. Naam, hata maadili ya karibu ya kiutu yeye aweza kukosa na kuja hata kufikia hatua ya kuweza kumuua baba yake mzazi na kumbaka mama yake mzazi. Mwishoni ataishia kujifungia ndani kwa hofu hadi kifo chake na ama hata kujiua mwenyewe kuliko kutoka nje ambako hana tena rafiki ili umma wenye chuki na kisasi dhidi yake kwa kuua ndugu na jamaa katika mji bila hatia na sababu zozote. Kwa maana hakuna sababu yoyote itoshayo kuua mtu kwa ‘uzito’ wa kosa la aina yoyote ikiwemo hata kuua mwingine ijapokuwa tu mwanadamu akosapo shauri la kimsingi la kuhusu kumshughulikia mwenye ‘kukosa’ ; yeye huweza kuhalalisha chochote ikiwepo kuua tena ; na basi jinsi hiyo hiyo na yeye anakaribisha kipimo hicho hicho cha kushughulikiwa akoseapo.

Na hivi vilikuwa vituko vya hata wadhalimu wa siku nyingi. Kuleta sura kinyume kabisa ya yule mtu toka kwenye mfano wa mtoto wa muastokrasia aliyekuwa akimstahi sana ‘baba-mfalme’ na kumheshimu mama yake mzazi na hata kufaa kheri ya kurithi ‘ufalme’ na miliki kwa uhuru, upendo, baraka na kutambulika sifa bora kwa wale wenye kutarajia na kuukubali mwongozo toka kwake bila hata mkataba wa maandishi.

Wadhalimu wa leo hawana tofauti na wale wa zamani , hawa huwa na tamaa ya kuingia madarakani hata kwa mtutu wa bunduki na mapinduzi ya damu, uwizi wa kura, rushwa katika taasisi za umma na hata propaganda za uchafuzi dhidi ya wale wenye kuwatangulia katika hatamu. Wenyekuja kuendeleza agenda za serikali za usiri mkubwa na ukandamizaji wa sauti za wengi na uhuru wa taarifa pia vyombo vya habari kukidhi haja yao adhimu ya kupata zamu yao ya ‘kutesa’ ; kama wale ‘wateule’ wengine waliowatangulia. Kwa vile hivi : wao wakiingia ni wenye kupenda kupora mali na hazina za nchi zao ili kuwa mahodhi yao binafsi—ambacho ndicho kitendo cha mfano wa kubaka mama zao wazazi ; wakazidhihaki taratibu zote za sheria kwa kufikia hata kutangaza wazi wazi utawala wa kudumu/maisha, kujiongozea vipindi vya kuwa madarakani na kipindi angali wakiwa madarakani au kunga’ang’ania madaraka na mamlaka kwa miaka yao yote kuishi duniani ; hii ilivyo ni kielelezo cha kumuua baba mzazi. Vile vile huwa na kupenda kurithisha nyadhifa wajumbe wa koo zao na watoto wao. Wao hawana staha kwa wazee wa siku zao na wala heshima kwa wanawake na watoto katika miliki zao kwa tabia za udanganyifu wa makusudi kabisa na hila mbele zao. Hawajali ya kesho ila tu salama yao ya matumbo na ulevi wa madaraka ; wenye kukosa karama njema kwa kuwa wamekosa staha hata kwa baba mzazi na heshima kwa mama mzazi ; na hivi hawawezi kuwa na mapenzi mema na nia njema kwa mapana ya jamii ila tu kutafuta sifa za kuficha aibu ya ujinga wao wa kukosa misingi ya utu bora usiyohitaji hatamu ili kujiridhisha ubatili wa jinsi yake. Wenye kukosa msingi wa kung’amua mielekeo ya ‘falsafa ya kiplato’ kusudi kupata kukirimika kuelewa utangamano wa uadilifu wa kiroho na matunda mema ya ustawi kwa nchi zao. Na kwa kukosa hilo kuongoza nchi kwa porojo na maarifa ya kuazima isivyobusara yao kamili.

Uchanganuzi wa Plato kupitia kazi zake za kuwakilisha namna ya mazungumzo kati ya mwalimu na mwanafunzi si tu yalikuwa ni yenye kulenga kisomo cha maadili na ujuzi wa kuyaingia mashauri ; bali pia yalikuwa yakisisitiza uhusiano usiozungumzika kati ya yale yaendeleayo kila siku katika maisha ya mwanadamu na mbingu. Ni hili ‘lisilozungumzika’ lililokuja kusahaulika mapema ama kushindwa kuendelezwa na kuachwa na ‘utata’ wake. Basi ndipo akajajitokeza mwanafunzi mmoja katika mkondo wa Plato aliyejulikana kwa jina la Aristotle. Huyu ndiye aliyekuja kufanya changamoto ya ‘kimtizamo’ dhidi ya kutozungumzika kwa mambo ya ‘kimbingu’ kwa kufanya namna ya kisomo chenye kuzungumzika na kufaa kuitwaa ni ‘maarifa’. Ndiyo iliyesisitiza kuwa vitu vyote vinaweza kuchunguzwa katika misingi midogo midogo yenye kuelekea kudadavua ugumu wa mashauri yake mapana. Na misingi hiyo midogo ni kadri ya kweli za kuonwa zinazoweza kuthibitishwa na zenyewe kuja kujumuishwa ili kuthibitisha kweli pana zaidi. Tofauti na Plato, Aristotle alikita kisomo katika ulimwengu unaonekana na huu tuliopo akiweka kando yote yasiyoonekanika. Ni hivi ndivyo ilivyozaliwa sayansi ya nchi za magharibi na maendeleo yote ya leo katika fani mbalimbali za taaluma.

Kutoka kwa Aristotle ndiyo ilizaliwa Oganam ya kwanza. Jiwe la kwanza la msingi kwa kisomo chenye manufaa katika muktadha wa sayansi. Lakini pia hapa ndipo vitu viwili vilijibainisha ; ninapenda kuvitaja hivyo kama ‘filosofia’ na ‘falsafa’. Katika lugha ya Kiswahili maneno haya mawili mara nyingi hutumika kama ni yenye maana moja ; ni mapenzi yangu yakwamba haya mawili yabainishwe na ili yaje kupelekea maana tofauti.

Falsafa ni mashauri ya kina kiudadavuaji ; ama vile vile kusema ni ufikiriaji unaoelekea kwenye chanzo chenye kuleta sababu za kimatokeo. Filosofia ni mapenzi kwa ile ‘hekima’ ambayo haikamatiki kwa macho bali tu kusudi la mtu mwenyewe kwa jinsi yake kutengeneza nafasi katika utambuzi wake ili kumfunulia utangamano katika mashauri. Neno filosofia linafanyika kwa vijineno viwili ‘filo’ na ‘sofia’. Sofia ni hekima na jinsi ya kike yenye kuweza kutangamanisha ndani yake hadhi zote mbili ya kike na ya kiume. Filo ni ‘mpenda’... Mtu mwenye kufaa kuitwa mfilosofia ni yule ambaye katika akili yake amekaa kumpokea sofia –mama wa maarifa yote kama mpenzi wake wa mwisho katika maisha.

Falsafa huleta milengo na itikadi, Hekima haijui mipaka wala mwelekeo. Falsafa ina vikomo, Hekima ni bahari isiyo na mwanzo wala mwisho. Falsafa husigana na hata kuhitalifiana wakati hata wakati, vipindi hadi vipindi ; Hekima ni ile ile leo, jana na hata kesho kukadrisha tu hadhi ya mtu mwenyewe na ufunuo wake kwa wakati.

Falsafa ni matunda ya kisomo na yale yenye kuonwa kwa jicho la ukiasi katika kushindana na adha ya ujinga ; Hekima ni shani ya nuru ya vyote vilivyoumbika na kudhahirika, kutangamanisha nuru na giza vile vile na kwa jinsi hii ujinga na werevu kuwa pande mbili muhimu katika muktadha wa maisha yote.

Hekima imejitokeza kokote na angali haikufundishwa kwa jinsi ya kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine—ikizidisha kile inachokikuta katika moyo na akili za watu. Lakini maarifa hufundishwa na kurithishwa kwa kadri ile ile ya uadilifu wa mashauri kuhamishika kihabari.

Kutoka kwenye kabila la Wanyaturu wa Singida kwa mfano ; ‘dini’ yao ya asili hufundisha mwanzo wa vyote yaani mungu ni Jua. Na mwezi ndio ulikuja kuumba vinginevyo kwa jinsi ya uwili uwili na muktadha wa kuongezeka kwake. Halafu katika kufanyika kwa ulimwengu, wao ni wenye kusema kuna watatu waliokamilisha shughuli. Mmoja alikuwa ni ‘Mfikiriaji’-Maghema, mwingine ‘Msemaji’-Mahanyana aliyebaki alikuwa ni ‘Muumbaji’-Matuunda.

Wanyaturu wakiwa kama wale watu miongoni mwa wahamiaji kutoka kaskazini ya mbali; watu wa kundi la Nilo-Hamiti kutoka Abisinia ya zamani huko wakiitwa ni Warimi na angali ndiyo kusema wapo waliobakia huko; Siku hizi nchi hiyo ni sehemu ya Ethiopia--huenda mashauri yao juu ya uumbaji ni urithi wa mafikara waliyotoka nayo mbali. Kwa kuwa haya yanafanana na hata yale kutoka Misri ya Kale na ya wale wenye kuitwa na wapagani. Kinyume na dini zote zilizokuja kujitokeza baadaye na kuzibatilisha zile za zamani kuziita za kipagani na kufanya ‘upagani’ wowote kuwa ni mbaya kwa asili ; hiyo ilikuwa ni kasumba tu. Kwa kuwa hata mashauri ya dini zingine huenda yakawa pia na mashauri mengine mengi yasiyothibitika ila tu kwa ishara na usadikifu. Basi hatuangalii mapokeo kwa minajili ya mashauri ya kifalsafa hasa ; bali twayatazama mashauri ya ndani kwa kadri yake ambapo ukweli fulani waweza kuakisika katika jinsi ya maisha yenyewe yalivyo. Tukitambua wazi wenye Hekima wamepata kujitokeza kokote na bila kukingwa kokote kutokuzaliwa.

Na hivi tunaweza kuzibainisha dini za asili na zile kuambukizwa na tamaduni za kigeni katika jamii moja kwa kutazama nguvu ya uhifadhiko wa kisomo cha mashauri yake yaani ikiwa ni kwa jinsi ya mdomo ama jinsi ya maandishi. Jinsi ya mdomo huenda sambamba na matendo ya ibada, matambiko ama vitu vingine vyenye kuwakilisha ishara ama uweza fulani juu ya ustawi wao. Binadamu wa zamani sana walienenda kwa jinsi ya maneno ya kuamishwa kwa mdomo na utaasisi wa kudumisha imani juu ya shauri lenye ‘nguvu’ kwa jinsi yoyote iliyotafsiriwa na wanajamii wenyewe dhidi ya hofu yao mwenyewe. Lakini binadamu alipogundua maandishi ya maneno aliweza kufikia kuchanganya ushawishi wa kifikra na matendo kwa namna imara zaidi kuliko ile iliyotangulia. Hii iliwezesha hata dhamira ya mwanadamu kuanza kumulikwa na kulengwa moja kwa moja katika mapokeo ya maandiko ya kiimani. Lakini maandiko yote si yenye kumuinua mtu katika ‘hekima’ kwa jinsi ya moja kwa moja. Haijapata kutokea hivyo na yumkini haitawezekana kamwe. Kwa maana hilo lingekuwa ni lenye uwezekano kungeshakuwa na jinsi ya kitabu ambacho mtu akisoma hutaamulika na yote kwa hicho—mara tu amalizapo kukisoma.

Basi na tufafanue na kujaza mapengo kulingana na ‘dini’ ya asili ya Wanyaturu(jina lililokuja kutokana na watani zao 'Wasukuma'--kutokana na umahiri wa wahamiaji hawa wa Kirimi kufuatisha nyayo za wanyama wakati wa mawindo wakisemezana 'Mughuu turu turu' kumaanisha alama za miguu/nyayo hizi hapa na tena hapa... Basi wasukuma wakawa wanawaita 'Banyaturu' na hali tena Warimi waliwaita na wao 'Anyakuma'--Watokao kaskazini) na ili kuleta utangamano kwa yale yalipata kuwakilishwa miongoni mwao. Jua ni kile kitu chenye udumivu wa milele. Mwezi ni kitu cha jinsi mbadala kwa kile chenye kuwa ni cha milele. Na hivyo mwezi unaweza kusemwa ni namna ya majira na mienendo ya vipindi vya muda na wakati. Jambo lenye kushangaza ni ukweli kwamba isingaliweza kamwe kudhanika kuwa jua ni lenye jinsi ya milele katika kuwaka kwake kwa watu wa makabila na mataifa kwa siku za zamani sana, kwa kuwa usiku na mchana lilikuwa ni fumbo lisilong’amulika siri yake itokanayo na tabia ya kuzama upande mmoja na kuibuka mwingine ; tena tofauti ya joto na baridi ya usiku. Basi shauri la Mwezi na Jua ni kielelezo cha kweli ya kiuwakati na ile ingine isiyoshikwa na wakati. Na vyote vilivyofanyika vimetokea kwenye ‘mwezi’.

Na tuyaingie mashauri kuhusu watatu.

Mfikiriaji ni 'kizio' cha uakilifu wa maarifa yote. Namna ya unafsi ni ishara kujitosheleza kwake kusikoingiliana na mengine yote. Ufikirifu ni ishara ya kuwepo kwa neno ama shauri katika ukamilifu wa jinsi yake. Ufikiriaji ni jinsi isiyo na kikomo ama hazina isiyopukutushika ya sura ya mawezekano yote ; kwa jinsi zote inavyowezekana kuwa. Lakini katika muktadha wa unafsi wa pili ni mchakato wa ‘Msemaji’. Tamko lolote ni ishara ya Nia kuwepo. Utamkaji ni uchaguzi miongoni mwa yale ya kuwekwa mwangani na yale yakubakizwa gizani ; yaani yale yenye kudhirishwa kwa jinsi ya kauli yenyewe kuacha yale ambayo hayadhihirishwi. Katika fahamu zote tano za mwanadamu zilizo ni kuona, kuonja, kunusa, kugusa na kusikia ; fahamu nne ni utambuzi wa papo kwa hapo isipokuwa kusikia. Kitendo cha kusikia ni kitendo chenye kutekelezeka kwa jinsi ya kukatisha kwa ‘umuda’. Si tu kuwa inajulikana kwa kisomo cha sayansi kuwa sauti ni mitetemo ambayo hukadirika kwa jinsi ya frikwensi ; lakini pia ndiyo kisomo cha msingi ambacho shauri ya kizio cha wakati hakina budi kusanifiwa ili kutangamanisha sifa za maumbile mengine yote katika uhusiano wake na kinachotajwa ni ‘wakati’. Na kwa hivi usemaji ni ishara ya udhahirishaji wa mwanzo na mwisho wa vyovyote vinavyopasa kuchukua sura. Basi unafsi wa tatu katika mpango mzima unafanikishwa na ‘Muumba’. Muumba ni ile nafsi inayojenga na kustawisha yote katika muktadha wa neno na mafikara mengine yote ambayo hayajatamkwa kwa nguvu ya kitu kinachoweza kufananishwa na pumzi, yaani kuleta sura ya ujazo na kujitokeza umbile. Vile vile muumba ndiye hufanya vitu vyote katika sura ya ‘neno ramani’ linalojaliwa ‘urefu wa pumzi’ kwa kile kitu chenye kudhahirika na halafu kusharabika katika usikokuwa-kwake-kitu ; na hali uumbaji daima upo.

Kwa hivyo tofauti ya Wanyaturu na Wayunani ipo katika mwili wa falsafa hasa pale tunapoingia uwanja wa mashauri na ustaarabu wa watu. Ingalikuwa miongoni mwa wanyaturu kuna jinsi ya utunzaji wa mashauri katika maandishi kama ilivyokuwa miongoni mwa Wayunani siku za Plato na Aristotle ; si ajabu katika kupita kwa wakati kwa kadri ya vizazi kadhaa jamii ya Wanyaturu ingezaa taasisi yenye ushawishi wa jinsi yake katika falsafa na filosofia pia.

Kwa kuwa ni jinsi hiyo hiyo ya jua na mwezi inaweza kufafanua mfanyiko wa mwanadamu na mambo ya nyakati. Binadamu anapokuwa katika hali ya kutotaamulika kiroho huwa ni mfano wa mtu anayeishi katika kipindi kirefu cha usiku mmoja. Mwangaza wake autumiao kung’amua ulimwengu ni nguvu ya mbalamwezi na hivi tunachoweza kukitaja kuwa ni nafsi-roho ni mfano wa mwezi ndani ya mwanadamu. Kupitia nafsi-roho binadamu husadiki majira ya mwili, na ya nchi na hata shauri la hatma ya mauti yake dhidi ya uzima wake ; na kumbe, lo, nafsi-roho yake ni tu kioo kinachoakisi nuru ya Jua ; lile jua lisilotambua mipaka ya usiku na mchana, na wala mkingamo wowote na lenye kumulika pande zote. Na hivi uzima na mauti si chochote ila tu majira ya mbegu ya utu wake katika kupandwa kwenye mwili wa madhahiriko ulio ni dunia. Siku atakapotambua mauti zake zilikuwa ni njozi matata ndiyo siku mwanadamu huyo atakuwa ameliona ‘jua la asubuhi’ na kukumbuka asili yake isiyokufa milele na ndiyo siku ya ‘ufufuo’ na kukamilisha ‘hukumu’ juu ya ujinga wa kutokutambua kweli zilizokuwa zikihifadhi jinsi yake ya uzima. Lakini mambo haya yasiyokadirika kwa kiono cha macho ni yenye kuingia kusikika na kuonwa katika moyo ya msafi yeyote na kwa jinsi yake ya kuweza kuchora picha. Na ndivyo wenye hekima miongoni mwa Wanyaturu walipata kukirimika picha pia.

Kilichokosekana haswa katika mashauri ya Plato na Aristotle katika mchepuko ni shauri jahara mintarafu ‘umuda’ na maumbile. Kuna jinsi ambavyo utangamano wa yale wenye kuonekana kwa macho na yale yasiyoonekana huweza kuja kuchukua sura fulani tanabaifu. Kama vile sayari zingukavyo Jua, Mwezi kuzunguka Dunia, Mfumo wa Jua kuwa ndani ya mzunguruko mpana zaidi... Hivyo vyote hutokea kwa utangamano wa namna yake. Mienendo ya miili hiyo yote imefanyika kwa siri zile zile ambazo uzima wa mtu na vingine vyote umefanyika.

Na hivi tuiingie kutazama mizunguko ya mwanadamu katika uzima wa milele—kama neno linalotamkika na hivi lilikwisha anza na litakuja kwisha kusharabiwa kule kule lilikotoka.

Katika kipengele chochote cha kukatizwa kutizama juu ya maisha ya mwanadamu na ustawi wake tunaiona vita yake dhidi ya ujinga na adha zake zitokenazo na huo na pia tunaona changamoto zote zijazo na ‘maarifa’ na ujuzi wa wake katika kumudu mazingira yake. Kwa kadri ya ujuzi wake wa mema na mabaya tunachunguza maadili yake mtu na nidhamu ya uadilifu kwa mashauri yenye kheri ndani ya jamii yake aishiyo. Kwa kuwa mawili haya ni bayana katika jamii yoyote na wakati wowote (1)Ustawi wa vizazi na (2) Ufunuo wenye kheri juu ya mashauri ya kheri katika vipindi vya kuishi kwa wanajamii wenyewe. Hili la pili linaweza kuchukua sura ya kujaribu kutangamanisha maisha duniani yenye kudhahirika kwa ncha mbili—kuzaliwa na kufa ; na upande ‘usionekana’ wa ‘mauti’.

Kwa kuwa masukumo wa mkuu wa maisha yenyewe ni matakwa ya hamu yenye kuhitaji mwili wa kudhahirishia hayo, wakati mwingine ‘ufunuo’ juu ya mambo ya mauti hutumika kama kioo cha matokeo ya utumikishi mbaya wa jinsi hiyo hiyo ya mwili kwa wale waishio. Na wakati mwingine huzungumza ya madaraja bora zaidi ya ‘kuishi’ ambayo mtu aweza kuyaendea. Na ‘ufunuo’ huwa na sura mbili—hai na mfu. Ufunuo mfu ni ule uliokujakuchukua sura ya mashauri ya kifalsafa juu ya safari za maisha ya wanajamii. Ufunuo hai ni ule ambao mtu mwenyewe afunuka kupata kujua hakika ya uzima na kheri ya vyote na nyakati zote. Kwa maana jinsi ile ile ambapo mashauri ya kiuelewa miongoni mwa wanajamii yaweza kutofautiana upana ama vina ; ufunuo nao huwa na vina vyenye upeo tofauti katika kuyatambua mashauri juu ya ngozi za sura mbali mbali za kimadhahirisho.

Basi jamii hufanywa na watu, na mtu ni jinsi ya mbegu... Kwa namna yake mtu katika sura ya mbegu hufanyika na ‘hamu ya chakula’—usemaji wa Plato, pia kusema matakwa ya hamu. Na hivi mbegu hii huhitaji mwili ulio ni ardhi ya nchi ili kuitimiliza ndoto yake ya kukua zaidi na kustawi kwa jinsi yake. Nayo mbegu hiyo angali huanza chini kwenye giza, maji na joto hutafuta kukua juu kufuata mwanga uliojuu ya nchi, ule uletwao na jua na kuja kuwa mti mkubwa. Kwa sehemu ya elementi za mwili wa pale ilipo yaani ardhi inapopandwa, mbegu hii itasanisi hivyo na ‘nishati’ ya mwangaza wa jua kujisuka na kuchuka sura yenye kuongezeka na kukua zaidi ya pale ilikoanzia. Na katika kuelekea ukomavu na mwisho wa pumzi ya ukuaji na ustawi ; mti huu utafanya maua, kisha kuwa matunda yenye mbegu. Nazo mbegu zitapofika ardhini safari ya mti mwingine itaanza kwa jinsi ya ‘neno la mti’ lilivyo. Ikiwa mti na ‘neno la mti’ ndiyo mbegu yenyewe hasa basi kufa kwa mti ni kupotea kwa ‘neno la mti’, ikiwa ‘neno la mti’ huoona tu na jinsi ya kusukika kwa mti kwa kadri ya mbegu yenyewe basi mbegu ni kioo tu cha kuakisi msuko wa mti. Basi kwa jinsi hii palipo na ‘neno la mti’ ndipo mfano wa kusema ni ‘Mbingu’ ya wasikirifu na wenye hekima ; na mbegu ni mfano wa mtiririko wa sura ya masababisho na matokeo yake ya kudhahirika ilivyokatika mwili wa kuakisi nia yaani mwili wenyewe wa madhahirisho.
 
Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi seh. III
5 Septemba 2011 saa 12:23 Asubuhi

Dunia hii ambayo Aristotle alilenga kuichunguza kwa kuitazama kwa macho haiwezekani kamwe kuona ‘siri za mbingu’ kama vile mti wenyewe usivyoweza kuonekana hata katika mbegu yake. Basi Hekima itaelekeza kuelewa utangamano wa dhahiriko na ‘Neno la Uzima’ kwa vitu vyote kwa jinsi ya kwamba, kukua na kuongezeka ndiyo amri ambayo kila chenye ‘chembe-nia’ ya ‘kuwa’ huja kutii ili kuchukua nafasi. Lakini katika sura hasa ya mwili wa kudhahirika hakuwezi kuwa na refu lisilo na ncha... Na hivi hili linaleta utanabaishaji wa namna moja juu ya amri hii na ustahimilishwaji wake. Vitu vyote hujitokeza kwa jinsi ya pumzi ya namna yake ambayo itadhahirisha ukiasi wake katika minajili ya kuchambua ‘ukuaji’ na ‘wakati’. Lakini kikubwa hasa katika kudhahirika si mwili wenyewe wenye kudhahirisha hayo mawili... Mti hukua toka kwenye mbegu hadi kuwa kima chake na si kukua mpaka kulifikia jua lenyewe. Pale kipindi chake cha mwili wa dhahiriko umefika tamati basi tayari kutakuwa na mbegu nyingi zilizotapanywa kungine ; kupitia mbegu hizo hamu yake ile ile inaweza kuhifadhika mwili na kukirimika kukua. Na hivyo hata kama chembe-nia imekuwa ni yenye ‘jinsi ya u-moja’ katika mkondo wa madhahirisho daima katika marefu na mapana yake kutafanyika kitovu cha mwendelezo zaidi wa mchezo ule ule na kutohitaji refu lisilo na mwisho katika mwili ule ule.

Na huo utakuwa ni mzunguko kwa safari iliyo ni ile ile.

Vile vile dalili ya kwamba safari zote ni mizizi iishiayo kwenye shina moja la ‘wakati’ ; zile safari zenye kupandizwa huku na kule katika jamvi la wakati pasipo kumaanisha ‘unyoofu wa wakati’ ila tu mseto wa yote yenye kuweza kuonekana/kudhahirika.

Hapa twastahili kujifunza shauri la kupanda na kushuka ; kwenda mbali na kurudi nyumbani.

Katika visa vitokenavyo na maisha ya Yesu kina kile kinachoongelea ‘siku arobaini’ za mfungo ‘jangwani’ na mashauri ya ndani ya Yesu katika kushukiwa na ‘roho wa ubatizo’ ; na hivi kukaa kwake pembeni ili kuitafari dhamira yake juu ya sura na sifa ya huduma iliyoihisi kuhitaji kuitekeleza ndani ya jamii yake. Kwani na baada ya hapo ndipo inapotajwa kuanza huduma yake ya kutangaza ‘habari njema’ kwa watu wote. Labda ni yeye mwenyewe aliyekujashuhudia hata yale aliyokuwa mioyoni mwake wakati akipitia hayo—kwa watu wengine ; ama ni mtu mwingine aliyekujahifadhi kisa fulani kwa mchanganyiko wa tukio halisi na mashauri yaendenayo na hilo tukio katika simulizi la kufundishia jambo fulani lihitajikalo kupokelewa na wanajamii katika vina mbali mbali. Kwa kuwa tunajua kwa miaka mingi hata baada ya Yesu kupotea katika ardhi ya Palestina, simulizi la visa na mafundisho yake yalikuwa bado kuandikwa rasmi ila tu kuwa ni mtindo wa makusanyiko wa mafundisho madogo madogo ya kurithishwa kwa masimulizi na nyaraka za barua miongoni mwa ule umma uliokuwa ukifuatisha huduma yake kwa mapana ya jamii zingine.

Na hivi hili ni kweli katika kisomo cha historia, watu wa siku za nyuma si walikuwa ni watunza kumbu kumbu la mtiririko sahili kabisa ila tu walikuwa na namna za uandishi ambazo zilikuwa zikichanganya ‘usahihi’ wa tukio na ushairi ; vile vile ushairi wa mafumbo, ishara za kukoreza hisia na mapambio katika simulizi. Hakukuwa na jinsi ya uandishi kama ulivyokatika ulimwengu wa leo wa habari na historia juu ya mtu, jambo ama tukio.

Mtu yeyote kwa mfano, anayedhani kisa cha ‘nyoka’ aliyeongea na mwanadamu ni kweli ya kihistoria huyo atakuwa anajichanganya mwenyewe... Hakuna kitu kama hicho kinachoweza kutokea katika hali ya kawaida ila tu kwa namna ya ishara ya ukweli fulani ifananayo na picha hiyo—inayoweza kuhifadhika katika simulizi la wahusika waliohaishwa na wengine waliobunika sura. Basi ni jinsi hiyo hiyo binadamu anatokea kwenye silika ya kupenda kuchanganya ukweli wa kimatukio na upambo wa kufikirika ili kupeleka mbele na kufikisha ujumbe kwa mwingine.

Siku za nyuma watu hawakuwa na utajiri wa vifaa vya kuandikia na kuhifadhia maandishi ama kufyatua nakala na hivyo uwezo wao ulikuwa na kikomo katika uadilifu wa ‘habari halisi’ juu ya mtu ama jambo. Ndicho hichi kikomo hasa kilichobidisha kutia ‘nakshi’ habari inayopaswa kubaki katika jamii ili kuwa na utamu na urembo vile pia kuvuta masikio na hisia ; na hivyo kufanya watu wepende kuvitunza visa vya kusimulika na kuvirithisha kwa wengine.

Hii pia inahusu visa vya mashujaa na miungu wa makabila.

Haya yalikuwa ni fasihi ya aina yake ni yenye kumulika ukuwakujia wa kiakili, sanaa na mawasiliano ya kijamii katika kuhifadhi ‘vihamba’ vyake vya maadili na busara yenye namna yake kheri katika kudumu kwa utamaduni wao.

Basi lile shauri la Yesu katika kuishi pekee ‘jangwani’ kunaleta simulizi la ‘majaribu matatu’ kwa Yesu toka kwa ‘Ibilisi’. Kukipangilia kisa ili kuleta maana bora ya uwezekano inaweza kusemwa hivi : Baada ya ‘Ubatizo’ wenye kusimulika pale Yordani, Yesu alifunguka fahamu kwa jinsi ya ‘Ufunuo’ wa jinsi ya rohoni na ulimteka sana akili kiasi cha kuhitaji kujitenga na watu na shughuli zao za kila siku ili apate kutafakari uingiliano wa ‘ufunuo’ huo na ‘ustawi’ wa jamii yake ikiwa kuna chochote chenye kuweza kufaa hasa. Jangwa si tu kumaanisha ukavu wa nchi na michanga, lakini ni kujitenga mbali kiakili hadi hali isiyo na msaada wowote kwa wakati na mahala kwa jinsi ya utumikivu wa mwili. Kudumu pale tu ambapo fahamu yatawala na mtu kujimulika yeye mwenyewe na hapo kabisa alipo.

Siku ‘arobaini’ si lazima iwe ni siku arobaini kwa jinsi ya hesabu ya kawaida. Arobaini ni mzingo wa mraba kwa jinsi ya pande za vizio vya kadri ya ukumi-ukumi vya urefu wa mapana yake—kama ilivyohesabu ya vidole vya miguu na mikono na ishara ya ukamilifu wa ncha zote za nia kwa kuuchora wakati kwa namna yake ya ndani ya mwanadamu. Kufunga ni ishara ya kujinyima mahitaji ya kawaida ya mwili na ili labda pia kuzijua siri zake kukutana ‘pumzi ya uzima’ isiyotokana na asili ya mwili wenyewe ila kukutana na mwili katika namna ya utangamano wa aina yake. Haya yote kutokea kwa yule mtu anayekirimika kujua ukweli wa kanuni za ‘kuishi kwa mwili’ na uweza wa nguvu wa pumzi isiyoonekana kwa macho na kuzitambua nguvu zake zenye kuhaisha na kutenda kazi kwa maajabu yake ya utangamanifu na ‘uumushaji’. Kwa mtu asiyekirimika ; hili limeleta utamaduni wa kuiga kufunga kwa minajili ya ‘toba’ ; ukirifu wa dhamira mbaya zitokanazo na tamaa ya mwili, mawazo mabaya na dhamira mbovu juu ya maisha ya mwanadamu mwenyewe kupitia kujitazama. Lakini katika mfano wa Yesu, hakuna ishara hasa ya ‘toba’ bali kuna ‘upimwaji’ wa dhamira yake juu ya mambo fulani na kusudi ‘vimvuli’ vya jinsi ya ‘mashauri ya juu’ ipate kutathminika na kujengewa ‘msimamo wa nia’ ya kuhudumia jamii ikiwa mashauri hayo ni mazito kuliko wastani wa kawaida wa watu kuelewa na kutangamanishia kazi—kama jinsi ilivyo katika hali ya kawaida wanadamu hawatambui hakika ya uwepo wa ‘pumzi ya uzima’ ila tu wakimaizi jinsi yake ya kudhahirika waitwavyo hiyo ni ‘pumzi ya uhai’ kwa mwili.

Basi katika kisa cha Yesu jangwani husemwa alijaribiwa na Ibilisi nayeye akamshinda huyo na hivi kuwa ni ‘mwokozi’ kwa wengine wote waliokatika ‘himaya’ ya Ibilisi kupitia huduma yake ‘kulishuhudia neno’ na habari njema. Na hivi tukague ‘majaribu’ na ‘Ibilisi’ katika muktadha mzima wa mambo na mtu mwenyewe.

Kutokana na kuchukulia masimulizi juu ya ‘mambo ya kiroho’ kwa juu juu ; watu wengi hudhani Ibilisi ama shetani ni nafsi iliyo nje na nia-utu wao. Hiyo si kweli. Ibilisi ni mtu mwenyewe na ‘kisogo’ cha dhamira yake. Wengine huchukulia visa vyote vya namna kama ile ya masimulizi ya vita ‘mbinguni’ vya malaika ‘wema’ na ‘wabaya’—wabaya kushindwa na ‘kutupwa’ duniani ; kuwa ni tukio la ‘kihistoria’. Hiyo si kweli. Haijawahi kutokea hasa kwa mtiririko wa masimulizi. Ukweli ni kwamba vita hivyo haina mahala pa jana, wala kesho kwa kuwa vita hiyo ipo hapa na sasa. Na hili halina budi kudadavuliwa fumbo lake.

Uzima wa milele ni ‘Kweli’ iliyopo na hali isiyoshikwa na ‘wakati’ wowote. Madhahirisho yote yanachukua sura na hivyo ‘muda’ kubidi kutokea kujiazimu mbainisho wa ‘Kweli’ na ‘si Kweli’. Lakini hakuwezi kuwa na ‘si Kweli’ ila tu kwa kuwa inakirimika ‘ndani na nje’ ya ‘Kweli’. Vyote vinavyofanyika katika ‘usikweli’ hata ikitokea kuwa ni vilivyohaishwa vikijitambua kwa jinsi ya ‘wakati’ wake haviwezi kung’amua ‘Kweli’. Itokeapo kile kilichohaishwa katika ‘usikweli’ ‘kikataamulika’ kuwa moja na ‘Kweli’ hicho kinamaizi mara moja wakati wote si tu ni chochote ila ile ‘Kweli’ katika ukamilifu wake usiyogawanyika na wala kupotoka katika jinsi ya maonekano yote kama ‘sura ya wakati’ yaani madhahirisho na matukio. Na hivi jinsi yote ya viumbe vinavyofanyika katika madhahirisho kufungwa na kamba zake zenye kugundisha dhamira na utashi wa hivyo viumbe na ulimwengu wa madhahirisho yake. Bila ya hizo kamba ‘Usikweli’ hauwezi ‘kuishi’ ndani na nje ya ‘Kweli’.

Kisomo cha leo juu ya akili na fahamu ndicho kitasaidia kung’amua lugha za watu wa zamani katika kuzungumzia mashauri mbali mbali yenye kugusa moja kwa moja utabia ya mtu, imani, utambuzi, fahamu mbalali, fahamu jua, utofahamu kumbaizi, na ufahamu-jua kumbaizi. Kwa kuwa haya yote, kwa mtu, yana mapelekeo ya moja kwa moja kwa ishara za nidhamu ama mapepe, kuhangaika ama kutulia , ‘ugonjwa’ ama kuwa ‘sawa’.

Imani inamuunganisha mtu na ‘sura ya kheri’, utambuzi ni kitendo cha akili kwa wakati kumaizi uso wa jambo lilotwalo na fahamu za mwili, ama kumaizi jambo liletwalo na mawazo au fikra. Utambuzi hutokea katikati ya fahamu mbalali na fahamu jua—yaani ziwa la mawazo tuli ilivyomfano wa mbalamwezi iliyodakwa na maji kama ‘fahamu mbalali’ na hivyo fahamu jua kuwa ni mchemko wa mawazo mapya ambapo katika uso wake ndiyo mawazo mapya huzaliwa na kuwa ya moto kwa wakati halafu yakapoa na kwenda chini kwenye baridi.

Jamii inahitaji kisomo endelevu katika muktadha wa kutambua upana na kujifunza ili kutumia maarifa katika minajili ya taaluma za saikolojia ya kawaida na saikolojia ya paranomo. Miongoni mwa wanajamii wenye kuzungumza kiswahili ni hamu yangu maneno mbalimbali ya kiingereza yapate tafsiri ya moja kwa moja kutoka kwenye yale ya kiingereza ; iwe kwa kutohoa, ama labda kuweka tafsiri-mbinu. Hii itarahisisha kupanua haraka uwanja kwa visomo kwa kuwa maarifa katika lugha ya kiingereza yamepanuka sana na yanaendelea kupanuka kila kukicha. Na mimi nimetumia tafsiri-mbinu kama ‘fahamu mbalali’ kuwa sawa na ‘subconscious mind level/domain’, ‘fahamu jua’ kuwa kama ‘conscious mind level/activity’, ‘utambuzi’ kuwa kama ‘Cognition ; ~ Process’, ‘utofahamu kumbaizi’ kuwa kama ‘collective unconsciousness’. ‘Ufahamu jua kumbaizi’ kuwa kama ‘Superconscious/ness State of Mind’. Kuwa maneno haya yatawezesha kudadavua ilivyobora zaidi mashauri juu ya mtu, maumbile ya asili, habari na mawasiliano.

Haya hayakamiliki bila kisomo cha sibatenia ‘Cybernetics’ na saikolojia kwa jinsi uchanganuzi wa vitendo vya kiuchunguzi wakutoka nje. Lakini kwa namna ya uchunguzi kutoka ndani, sayansi haitanabahi hili hasa kwa sasa, lakini ni makusudi yangu umma wa waswahili waanze pia na jinsi hii ya uchunguzi katika mwili wa visomo vyake vyote vipasavyokuwepo na kwa manufaa yake. Kuwepo na uhifadhi wa mashauri na visomo kwa manufaa ya wengi.

Mtu anapochunguza ulimwengu toka ndani yake hujenga uelewa hata wa mambo yasiyothibitishika kwa mwingine ila tu kueleweka haraka au hata maramoja kwa mwingine aliyepita katika njia yenye kufanania ya kiuchunguzi. Ni kisomo hichi chenye kumulika mashauri ya Paranomo ‘Paranormal’ –ugutu wa hisia za fahamu hata nje ya jinsi mwili wa mtu ; na Uwimbiakili ‘Psychic’— kadri ya kuweza kuona mambo nje ya macho ya kawaida ama kushawishi/kushawishika na kupokea ‘picha’, ‘nia’ au ‘neno/fikra’ kwa jinsi ya akili na pasipo sura dhahiri ya kimaada. Kuwepo na uhifadhi wa mashauri na visomo kwa manufaa ya wengine pia wenye nia kupenyeza ndani zao.

Na binadamu anapokuwa na mwongozo bora huitengeneza njia kwa ajili ya ile ‘Hekima’ na kisomo chake toka hapo ni huwa ni chenye manufaa si kwa jinsi ya nje tu ila ya ndani pia. Kisomo cha leo kinamfaa mtu kwa jinsi ya nje lakini kikamwacha yeye maskini katika hazina ya utu wake. Na hivi haijalishi binadamu anakiri ama kutambua ‘udumavu’ wake katika hilo, kuelewa kanuni za mambo ya kiroho si ‘hiyari’ ni lazima kwa mwanadamu yeyote mwenyekutafuta kukirimu mengine na hali yeye ni mwenyewe kukirimiwa. Na kusudi pia ustawi wake upate kuinukia juu kuakisi chanuo kamili la ua katika kukatiza kwa kipindi cha muda uhitajikao.

Na hivi tutazame mtu, mdhahiriko wa nyakati za mtu na nafasi ya huo katika wakati mzima wa madhahirisho yote na hivyo wakati.

Kisa cha Yesu ‘jangwani’ kilikuwa ni mkato wa shauri zima kuhusu uakilifu na ‘mbegu’ zake za msukumo katika mtu ili kuchukua sura katika ustawi wa binadamu.

Jaribu la kwanza husimulika lilitokana na ‘njaa’. Aliposikia njaa Ibilisi akaja akamwambia mbona yeye ni mtu mwenye kufanyika uwezo sasa, maana anaweza kuyaambia mawe yageuke kuwa mkate nayo yakatii ‘neno’ lake, si afanye hivyo tu ? Tofauti na inavyochukulika juu juu, shauri la mkate ni lugha ya ishara kuhusu tabia za ‘utafunaji’ ili kushibisha matumbo kama mwenendo wa tabia moja inayoweza kumgeuza mtu kuwa ni mbinafsi. Yesu alipofunuka katika ufahamu wa kristo, baada ya ubatizo wa mto yordani, alingia katika ufahamu jua kumbaizi ; kwa jinsi hiyo aliweza kuona vitu vyote wa jinsi yake ya kuwa ni namna ya mitetemo katika ‘bahari’ ya madhahirisho yake. Alijua vivyo hivyo kila kadri ya kitetemo hushikilia hadhi ya usifa wa kitu na hivi mtu yeyote kutoka katika kina fulani cha utambuzi ndani ya fahamu kumbaizi akiweka nia ya mitetemo ya kitu chaguo lake katika macho ya kawaida ; kusudio ya hicho kubadilika, haraka madhahirisho ya umbo la kitu hubadilika kuitikia taswira ya akitakacho kwa ‘neno la lake’ ndani ya fahamu jua kumbaizi.

Ilikuwa ni fahamu ya jinsi ya akili ya kawaida na mashauri kutoka katika vina vya fahamu mbalali kuwa kwamba Yesu alipotuama kutoka kwenye vilele vya ufahamu wa juu ; alikumbuka njaa yake na kufikiria kama akili yake ya zamani ‘ilivyozoea’. Kwani ndiyo hiyo ilijifikirisha ikiwa kila kitu kinaweza ‘kujazwa pumzi’ kikabailika mitetemo hadhi na sura si anaweza tu hata kugeuza jiwe la pembeni ili kuwa mkate ili kuondoa njaa ? Lakini hapo hapo dhamira yake ya kheri hata katika fahamu jua yake ndiyo iliyomkumbusha hilo sio sahihi hasa. Kwa kuwa katika mpango mzima, kila dhahirisho lina nafasi yake na hivi si busara kwa kuwa mtu ni aliyetaamulika kujua siri za kubadilisha maumbo basi aende kufanya hivyo ili kujiridhisha hitaji lake kimwili. ‘Hekima’ ikamjia zaidi katika mashauri yake ya kwamba ikiwa kila kitu kinaweza kustahimilishwa na ‘pumzi ya uzima’ si ni hivyo hivyo na yeye aweza kustahilishwa kwa ndani pasipo kuhitaji kubadili jiwe kuwa mkate, kwa kuwa jinsi hiyo ingalikuwa ni tu mzunguko wa ubatili wa vitendo. Basi ndipo busara ilipomkaa Yesu kuzidi mashauri yake yote ya akili ya kawaida katika kuyatambua ‘matatizo’ ya mahitaji ya kimwili ; vile si busara kutosheleza kimoja kwa gharama ya kukibadili umbo kingine bila ridhaa yake. Kwa kuwa vitu vyote vina uhai wa aina yake katika mpango mzima hata kama macho ya kawaida hayang’amui hili. Na ndiyo jicho la staha—mara alipotambua hilo ‘akaomba’ hiyo pumzi kumkirimu, na ikiwa hivyo na njaa yake ikatokewa bila ya kutia chochote mdomoni.

Jaribio la pili husimulika kuchukuliwa kwa Yesu hadi kwenye ‘kinara cha hekalu’ halafu kuambiwa na Ibilisi atijupe chini kuthibitisha ufadhiliko wake kwa Mungu. Kuwa juu katika kinara cha hekalu ni ishara ya mtu kuwa katika mahala pa kutanabahi ukamilifu wa maadili yenye kuendana na kanuni za kiroho katika hali yake ya ‘kuinuliwa’. Katika kueleza mahusiano ya mambo ya ulimwengu wa kawaida na ule uliofichika, mambo ya dunia hutajwa ni ya chini na yale ya kiroho hutajwa ni ya juu. Mtu mwenye kuingia kutahamaki moja kwa moja mambo ya juu hutajwa ni mtu aliyeinuliwa katika ‘utukufu’ wa ile ‘Kweli’ na tena ndiyo fahari ya ‘Mbingu’—kwa kadri ya ukamilifu wake unavyoruhusu kukwea juu sana ilivyosawa na kusema kupenya ndani sana katika siri ya ‘Uzima’. Na hivyo kipande cha simulizi hili ni kielezi cha pale mtu aliyekatika ngazi za juu za utambuzi wa kiroho, dhamira ya utu-nia ya mazoea ya kinadamu hujakumshawishi kujaribu kuchepuka na ukweli wa kanuni anazotahamki dhidi ya zile kawaida ; lakini kwa mujibu wa kisa cha Yesu, alitambua hilo sio lazima kwani ulimwengu wa ‘kuinuliwa’ si wa mashaka na hivyo hakuna la kupimwa hasa kwa kulinganisha sura za mienendo yake ya hali. Na nguvu idhihirishayo kani mtuo kwa dunia, kuvivuta vitu vyote juu sura ya dunia kwenda chini, hainachochote cha ‘kujaribiwa’ kwa kanuni ya ‘kupea juu’ kujako na hali ya kuzama katika ‘hazina isiyokauka’ ya kiroho. Kwa kuwa kani mtuo ni ‘dhahiriko la wakati’ na angali watu si wenye kutambua hilo moja kwa moja ; ili kutunza na kuhifadhi vyote juu ya uso wa dunia kwa sura yake.

Ufunuo wa kiroho, japo humwingia mtu katika ‘vipindi vya muda’ mfupi ama mrefu, hii inaendana na uwezo wa mtu ‘kujikwatua’ toka hali moja ya ufahamu wa kawaida na kuingia katika ufahamu ulioinulika ; tena ndani ya vipindi hivyo dhana ya ‘wakati’ hupwaya kabisa shauri lake. Basi ‘kujitupa’ ili kuanguka chini ni ishara ya mmoja kushawishika kwa jinsi yake kujaribu kulazimishia matarajio kati ya ulimwengu wa wakati na ule usio wakati. Hii hutokeo pale mtu anapokuwa ni ‘mgeni’ wa kutahamaki ulimwengu upitao wakati, na hivi sehemu ya uakili wake yenye bado kujifunga na utu-nia wake kumshawishi kufikiri michakato ya mambo kwa mazoea yake ‘yalioandikwa’. Lakini mtu huyu mgeni yampasa kufanya chaguo kutoka katika ‘uchanga’ na ugeni hadi katika imani ya yote ya jinsi ya chini na ya juu na hivyo ‘Kweli/Mungu’. Kila linalotokea duniani kwa mapana yake yote ni kwa kheri ya vyote vya kwake ; lakini binadamu wenye ushawishi wa dhamira na utashi ndani ya nafsi zao, na katika upofu juu ya kuwepo kwa kanuni za ukamilifu wa juu katika ‘kinara cha hekalu’ ; wao hujikwaa na mambo ya dunia na kujichanganya wenyewe katika tafsiri za matokeo ya matendo yao ; ikiwa watashtukia kukumbuka siri za ‘kukwatuka’, wao watakuwa wana wa ‘Mungu’ wa vyote na hivyo wataweza kuinuliwa toka kwenye uharibifu hadi kwenye kheri halisi na kwa neema zake.

Jaribu la tatu la Ibilisi kwa Yesu husimulika habari ya yeye kupandishwa hadi juu kwenye kilele cha mlima na kuoneshwa miliki yote na fahari ya nchi ; halafu Ibilisi kumtaka Yesu amsujudie ili apate hivyo vyote kuwa mali yake. Katika kielezi hiki, ndiyo sura ya unafsi wa mtu huja ‘kutahinika’ katika kujichukulia kwake dhidi ya kumbukumbu na mapambo yake ndani ya nyakati. Ni jaribio katika uwanda wa uadilifu wa kimawazo, ambapo mtu ‘mgeni’ katika utaamuliko wa kiroho hupimika dhamira katika kile akionacho kustahili heshima ya nidhamu yake kiroho. Ikiwa kwa jinsi yoyote anapenda kujifunga na fahari za nchi na ‘kumbukumbu’ ya jina lake, basi yeye atakuwa amemuangukia Ibilisi ili kumuabudu, na yeye ataishi daima kukirimiwa kwa kiasi cha Ibilisi kuweza kumwongoza.

Katika hali ya kawaida watu huishi wakazaliana na kustawi. Jamii pana katika kilele cha jicho moja, huzaa dhamira ya mtu kuishi kutimiza ‘wajibu’ wake miongoni mwa wanajamii wake. Wanajamii wanajinsi yao ya kutambuana na kuheshimiana miongoni mwao. Kuwa mtu wa kaya, mume ama mke kuna heshima yake, watoto na mali ni ndoto ya uhakika kwa ustawi, miliki na urithi juu ya sura ya nchi. Kaya hukumbukwa kwa majina ya koo zao na heshima walizojijengea katika jamii yao pana. Binadamu huzaliwa na kufa, si chochote kati ya watoto wala nazo mali; ambavyo mtu hupita navyo katika mlango wa mauti. Na hivi ni sehemu tu ya mapenzi mema kwa vizazi, na tena kwa jinsi ya ukaribu wa damu, vizazi hurithishana urithi wao. Binadamu ainuapo macho yake juu humaizi jinsi yeye alivyo ni ‘mweupe’ na mtupu wa hazina ya kweli ; hili hujengea hofu kwake yeye ya utupu wa ubinadamu wake dhidi ya kadhia zake za maisha. Na hivi binadamu wa jinsi ya ndani kabisa ambapo hutafuta kujijengea ‘jina’ ambalo kwa hilo maisha ‘yatawakumbuka’. Jina hilo si chochote ila muakisiko wa fahari zote na maisha kama vile inavyoazimu ‘kujijua’ katika ulimwengu wa madhahirisho na wakati. Lakini ‘jina’ hilo huwa ndio kiegemeo cha jitihada zake zote dhidi ya majaliwa yake. Na vivyo hivyo, mwanadamu katika ‘kuinuliwa’ ndani ya ufahamu wa kristo ; adui wa mwisho kumkatalia mkataba naye ni nafsi yake yeye mwenyewe iendeshwayo na nafsi-roho yake na hali ni muakisiko uliopinduka sura na hadhi toka kwenye mbegu ya kweli yake ya milele. Kwa kuwa sura ile ile ambayo mtu huamini utu wake ulivyo na mipaka, yeye hawezi kumuona ‘mungu’ ila tu kwa jinsi hiyo hiyo na ‘kumuabudu’ kwake ni kutaka upendeleo katika majaliwa yake kwa kadri ya udhanifu wake.

Kwa hivyo kwa sehemu hii katika jaribio la tatu inaweza kufafanuliwa kuwa Yesu alikataa sehemu ya unafsi wake ambao ndiyo huwa ni msingi wa kutafuta jina na umaarufu miongoni mwa watu wa mataifa, na fahari zao zote, kwa jinsi zote ambazo binadamu hufanya kwa kushindana na saa za kusogea kwa mauti zao. Na kuanzia hapo kukiri Nia moja na ‘Kweli’ ambayo ni utumishi pale panapohitajika ; pasipo kuendeleza kulea ubatili na kujilisha upepo. Pia hapa ndipo tunajifunza juu ya nidhamu ya heshima kwa watu na wanajamii—Wake kwa waume na watoto ; pasipo misingi ya kutafuta ‘ukuu’, utawala na sifa za kawaida za watu wasiohisi mambo makuu yenye kuneemesha na kustahimilisha maisha yao.

Na ndiyo jinsi Yesu aliishi ni ‘Mfalme Mfilosofia’ miongoni mwa watu wale ambao hawakumtambua—maana tafsiri za wenyeji wake zilikuwa na mapokeo ya kutarajika kuja kwa ‘nabii kiongozi’ mkombozi na mwenyekuleta ‘mamlaka’ mapya ya wayahudi.

Husemwa baada ya kushinda majaribio hayo matatu Ibilisi alimwacha na halafu ‘malaika’ wakamchukua Yesu na kumhudumia. Na ndipo baada ya hapo alianza huduma yake kwa wanajamii wake akionesha uwezo mkubwa wa kuleta mashauri mapya na kufundisha. Akizungumza jinsi ya ‘kuingia’ katika ‘ufalme’ kwa uhitaji wa kujisafisha kwanza, kubatizwa kama ilivyoishara ya tendo la kuzamishwa kwenye maji na kuibuliwa lililofanywa na binamu yake Yohana ili kupata ‘jina’ jipya... Jina lakuwa ‘mwana wa mungu’ na vile Paulo alizungumza kuwa ni ‘Kiumbe Kipya’ na ‘Mtu Mpya’. Isivyo kama katika utumikivu mwingine wa maisha ya kila siku pamoja na uadilifu wake.

Basi tukague ishara za ‘maji’, ‘Ibilisi’, ‘Malaika’ na kitendo sanaa cha kupata jina jipya la kuingia ‘Ufalme wa Mbingu’.

Mafundisho yenye kuzidia mbali uelewa wa maumbile ya kawaida ya mtu na uzima ; huwa ndani ya kisomo cha kumuelewa mtu na hasa kule ‘alikochipukia’ na hivi ‘kuwepo’—yaani ndivyo tunaita hii leo ni Ontolojia. Mashauri ya ontolojia katika vizazi vya watu mbalimbali duniani, mara nyingi hufutikwa na lugha za ishara kuliko habari kamili. Ulimwengu wa leo ni ulimwengu wa habari na mashauri ya moja kwa moja katika ufundi na utumikishi wa taarifa/maarifa halisi katika wakati.

Ni kutokana na hili la wakati tulipo sasa lipo hitaji la kutafuta lugha mpya ambapo masimulizi yote ya kiontolojia yaliyopata kuwepo miongoni mwa mataifa na makabila ya wanadamu yatapata mahali pake pa kuelezwa na kuweza kufafanulika muktadha wake katika sura kamili ya mambo na mkunjuko wa wakati.

Hili linawezekana kupitia kisomo cha ‘Akitipu’ zenye kuongoza ramani za msukuko wa sura mbali mbali za michakato ya ukuaji na ustawi wa jamii katika kukatiza kwa vipindi maalum vya mng’amuliko fulani wa mzunguko kamili ya kuja na kuondoka kwa vilele vya ustawi wa wanadamu. Ingawa watu hudhani mambo yanayotekea ni mapya, pamoja na upya wake huwa kuna mtindo ambao madhahiriko yote kujifinyanga katika wakati.

Ndani ya madhahiriko yote kuna vichochezi vya sura ambayo hupelekea hata viumbe hai wenye utashi kama mwanadamu pamoja na mambo yao yote kuwa ndani ya vichochezi hivyo. Hivi huweza kuchukua sura ya kama hata dhamira ya mtu na kumbe ni sehemu tu ‘mpango mzima’ wa uzima wote hata kupitiliza ‘wakati’ wenyewe. Navyo ni sehemu ya uzima wote lakini kwa jinsi ya namna yake ya ajabu ; kuwa ni kama ‘mchanganyiko’ wa ukamilifu wa jinsi ya mafikara ya yote yenye kuwezekana(yasiyodhahiri kwa macho), yale yaliyokwisha kudhahirika na yale ambayo bado hayajadhahirika. Binadamu ni sehemu wa haya kwa mujibu na tena kadri ya alivyofanyika ndani yake kwa ‘ngozi za mifanyiko’ mbali mbali na pia ngazi mbali mbali za ufahamu na utambuzi kwa wakati katika kumfungamanishia yeye na hayo yote. Ndiyo haya hasa makutano ndani yake yahusishayoufahamu jua, fahamu mbalali na utofahamu kumbaizi.

Basi katika kisomo cha Akitipu tunajitahidi kutafuta kuujua ule ‘wavu’ uliotanda kote na kukokota misuko ya madhahirisho mbalimbali kutoka katika ‘bahari’ isiyoonekana ‘ya ukamilifu wa jinsi ya mafikara ya yote yenye kuwezekana’. Kwa kutumia akitipu tunatafuta kutambua tabia za watu na dalili za mienendo yao yote, kutokea na kupotea, kufumika ustawi na kutoweka kwake, mtandao wake wa nje na ule wa ndani wa mahusiano ya watu na uzima wao. Vivyo hivyo kwa Dunia, Nyota na vyote vyenye kuonekana katika udhahiri wa macho hata pia katika kaleidoskopi zake zote. Ni kama vile haswa kusemwa ‘jeometria ya wakati’ na uso wa maumbile yake.

Hayo tukijaribu ‘kuyaona’ yakichukua sura katika ‘bahari’ ya ‘uzima wa milele’ ; Nuru iangazayo yote na kufanya yote na hali hayo yote si chochote kubakia tu ile ‘Kweli’.

‘Ibilisi’ na ‘Malaika’ ni Akitipu. Binadamu hawezi kumaizi baadhi ya tabia za kufanyika matokeo ndani ya maisha yake ili kwa lugha ya akitipu zilizohuishwa. Hili linaweza kueleweka vizuri ikiwa mfanyiko wa ubongo wa binadamu unavyoweza kupenyezwa kisomo chake.

Binadamu ana ubongo uligawanyika katika pande mbili—ubongo wa kushoto na ubongo wa kulia. Japo kunamgawanyiko huu, kila pande ni jinsi ya kioo kabisa na mwingine. Jinsi hiyo pia inafanya kama vile isivyowezekana mkono wa kulia ukabadilishwa kuwekwa upande wa kushoto, kama hivyo hivyo kinyume chake.

Ubongo wa upande wa kulia kwa mfano huonekana kuwa ‘hai’ na vitendo vilivyokatika namna ya ‘picha’ na sura zote zenye kufanana na hivyo. Ubongo wa upande wa kushoto huonekana kuwa ‘hai’ na vitendo vya uchanganuzi na vitendo vya kufikiri. Kwa jinsi hiyo mazungumzo na kumbukumbu ni mchakato unaohusisha namna ya utangamano wa pande zote mbili za ubongo. Ukiondoa umahususi wa ubongo kama namna ya misokoto mirefu iliyojikunjamania ndani na hivi ‘kukoleza’ ukali kwa ‘fahamu’ zitokanazo na mikondo yote ya neva za fahamu katika usakiti wake. Kwa kawaida binadamu ana fahamu hai na tuli yaani zile ambazo kwa wakati anazitambua kuendelea katika mwili wake na zile asizozitambua na angali zipo.

Ngozi yote mwanadamu ina vipokezi vya taarifa ambavyo ni muhimu katika ‘kuhuisha’ utabia wa mtu dhidi ya mazingira yake. Vivyo hivyo huwa kwa fahamu zote tano. Kupitia ubongo ulioanzia katika uti wa mgongo fahamu zote za mwili wa mwanadamu huishia kunyongorotea mahala fulani katika ubongo uliokatika fuvu la kichwa. Sayansi hadi hii leo ni yenye kasumba ya kwamba ubongo ndiyo mashine kuu ya mwili yenye kuratibu kila kitu... Hii siyo lazima kuwa kweli ; kwa nje ni rahisi kudhani hivyo ila ikiwa mfanyiko wa mwili kuanzia katika seli moja hadi kuja kuwa muundiko wa mjumuiko wa seli nyingi katika mwili uliokomaa utazamamwa vizuri kunauwezekano wa kung’amua uhusiano wa ‘mishipa-sauti’ ya moyo na ‘kitovu-moto’ cha ubongo—hivi viwili ndivyo hufanya uzima wa mtu na viumbe vingine vyenye jinsi hii ya mfanyiko.

Kutoka kwenye ‘kitovu-moto’ cha ubongo mwanga-habari huwaka na kuangazia mwili wote taarifa za uwezekano wa kujisuka kwake na ubongo ndiyo mtandao wa kwanza kutumia tumia sehemu ya huo mwanga kusuka na kuratibu mienendo yote hata mwa mujibu wa ‘maandishi’ yalitungika na mwili wenyewe na tena yenye kuhama toka mwili mmoja hadi mwingine kwa jinsi ya matendo ya mwili kama kujamiiana. Ni ubongo huo huo pia ambao huweza kubadili taarifa za mwili kuwa mawazo na hisia na hivyo hivyo kubadili fikra kuwa nia kwa kufungua sakiti za kuamsha matendo ya mwili ambavyo mwili hutumika kama chombo cha kudhahiria nia fulani itokanayo na ‘mmiliki’ wa mwili wenyewe. Tofauti na inavyodhanika kwamba kitendo cha kufikiri hutokea kwenye ubongo, hiyo inaweza kuwa siyo kweli yenyewe hasa ; ubongo ni daraja lililo kama transmita na risiva ya mahala penye kuweza kuchakatisha mawazo. Na hapo hapo ubongo unaweza kuwa ni kama ‘lensi’ inayokusanya ukali wa mawimbi ya mawazo ili yang’amulike kwa jinsi ya ‘utambuzi’ wa kimwili—kama vile habari za kimwili kwa jinsi hiyo hiyo zaweza kuchakatuliwishia mawazo.

Ni nia yangu miongoni mwa wanajamii wa kitanzania kuwe na fikra za ziada na pana zaidi katika kuzidi kupanua kisomo kizima cha mwili, fahamu na utambuzi hata kupita yale mashauri ya kisayansi yaliyopokelewa pamoja na utokamilifu wake. Azma yangu ingalikuwa ni kusongesha mbele yale yaliyopokelewa kwa kisomo zaidi pale ambapo nafasi inaruhusu kwa mtu kufanya uchunguzi wa kina—katika mwelekeo wowote ule bila kuhofu mwelekeo usio wa kawaida wa mambo. Siku zote kuna ugumu kuvunjilia mbali mipaka, lakini hili halipaswi kuendekezwa daima. Watu wafanye visomo kwa faida binafsi na kwa faida ya wote. Isiwe tu kwamba mtu apaswa kufanya mambo kwa faida ya wote na hali faida yake ‘binafsi’ haina maana ; ni upuuzi pia mambo kuwa hivi. Na hivi jukumu la wanajamii wote kuhakikisha uchunguzi na utafiti wa jinsi zote mbili unakubalika na kutengenezewa mazingira bora ya kumea kwake.

Chimbuko la ‘moto’ wa kitovu cha ubongo si ubongo, na hivi kinyume na udhanifu wa mtu kuwa ni mwili, mtu si mwili. Mwili hujisuka kwa jinsi ya elementi za mwili wa dunia na hewa. Lakini ‘utu halisi’ wa mtu haufanyiki hasa kwa elementi za dunia na hewa ya kuvutwa puani. Kuna kasumba katika kisomo cha hata sayansi ya leo kusema kwamba kila anachofanyikia mwanadamu kimwili ni kwa nguvu za mienendo ya kubomoka na kujengeka kwa chembe chembe za chakula zake, akistasabahi hayo kwa lugha ya kisomo chake cha baiyolojia, kemia na fizikia. Kusema kuwa misingi ya mabadilishano ya kinishati yaambatanayo na kubomoka na kujengeka, nishati husharabiwa ama kutolewa kutumika katika kitendo cha kazi na ndivyo fizikia hushughulika na haya. Kwamba hadhi ya maumbile chembe huja kubainisha mpangilio wa kuundika kwa vitu vyenye kustahili kuitwa ni 'maada'; na hivi chembe chembe za jinsi mbali mbali zina jinsi mbalimbali za kufungamana ili kuchukua sura mpya ya kuundika sifa na hadhi, ndivyo kemia huambaa na mashauri vya visomo vyake. Pia kuwa chembe chembe za maada huweza kujijenga katika mfumo wenye 'uhai' na kudhihirisha taratibu zenye kukubalika kuwa ni 'hai' kwa kadiri ya visomo vyenye kutajwa chini ya jina la Baiyolojia.

Kisomo cha baiyolojia hudhanifu 'uhai' ni sifakazi itokanayo na tabia za kifizikia na kikemikali tu. Hii ni Si kweli; ndiyo maana kisomo cha baiyolojia si ni 'kikamilifu' hasa. Si yote ni yenye kufahamika vema katika mifumo vya viumbe hai na mienendo yake. Ni mapenzi yangu jamii ya watanzania walitambue hili na kulijengea mkondo kwa mawezekano ya kuchimba na kutanuka zaidi. Kufanya hivi si tu kutaongeza maarifa lakini pia ndiko hasa kutatuletea majibu kwa baaddhi ya matatizo yanayoweza kujitokeza kwa wakati na jamii ikakosa suluhu na ukwamuzi. Maradhi yatokanayo na mambo kama ubovu katika mishipa ya fahamu, mjengeko mbovu wa mwili kwa kuzaliwa na jinsi zote za maradhi yenye kupelekea msuko tenge wa miili ni shughuli inayotaka uwanja wa ujuzi na maarifa kutanuliwa. Kuambaa ambaa na visomo kwa jinsi ya Aristotle hufanya jamii ya wengi ikiwemo hii ya watanzania kudhani kila 'ukweli' lazima ukadirike kwa jinsi yake dhahiri; na kama lipo jambo lisilo ni dhahiri basi hiyo ni 'si sayansi'. Huu ni upumbavu. Azma yangu ni kutaja bayana kuna mambo katika kisomo daima hayatakuwa dhahiri lakini upo ufundi mbadala kwa jinsi ya vile vitendo kiaristotle unaoweza kunatabahi vina vipya vya visomo. Na hii ndiyo lengo mojawapo la Oganam ya karne ya 21 juu ya njia ya tatu.

Upande huu wa kisomo usiohitaji upekee wa mbinu za kiaristotle, umekuwepo hata kabla ya Aristotle na ni mwenye umri mkubwa kama mwanadamu mwenyewe. Baada ya Aristotle kuwepo kiwakati, ni kwamba tu binadamu aliamua kutendea haki fahamu zake za mwili kwa maarifa na visomo vyenye kufaa 'kumbukumbu' lake. Kwa kuwa kisomo hiki pia kina utumikivu wake wenye nguvu katika kuimarisha misingi ya ustawi na maendeleo ya watu yenye 'kupangilika'. Labda kote duniani binadamu wamekuwa na jinsi ya visomo vyao ndani ya jamii lakini kutokulenga kuleta jinsi ya mpangilio kwa ustawi wao kwa jinsi ya moja kwa moja hiyo iliishia kufanya visomo vyao visiwe rasmi katika minajili ya mapana ya jamii. Na hivi mengi yaliishia katika mahusiano ya mtu na mtu na ama ikitokea yakafahamika kwa wengi huwa ni tu habari isiyoweza kukitwishwa chini misingi yake.

Ni jambo sililofahamika kwa watu wengi kuwa hata 'wanasayansi' wa mwanzo katika chimbuko la mapana ya visomo vya leo walikuwa ni watu wenye kujaribu kupatanisha maarifa ya kuonekana na yale yasiyo yakuonekana. Bacon aliyevuvia kizazi cha wanasayansi wa mwamzo mbinu bora za visomo na kutokomeza kasumba katika kuelewa mashauri ya asili; yeye mwenyewe alikuwa ni mtu wa 'utambuzi' wa jinsi ya kiroho. Watu wengi tu kama Robert Boyle(fizikia, --gesi na mtanuko, mgandamizo, joto), Isaac Newton(fikizikia,-- mwanga, mienendo ya miili na nguvu tawalifu), Johanes Kepler(fizikia, -- mienendo ya miili ya mbinguni, mizunguko yake, umbali toka juani na urefu wa vipindi vya mizunguko kamili), Rene Descartes(Hisabati, fizikia--Jeometria bapa, aljebra) Leonardo da Vinci(sanaa na fizikia, --ubunifu, uvumbuzi na udhanifu wa kimstakabhari) Michael Faraday(fizikia na kemia, --umeme na usumaku, mpitisho wa umeme katika vimiminika vya tindikali/chumvi chumvi), Blaise Paschal(Fizikia, Hisabati,--mgandamizo na ombwe katika mtungiko wa gesi katika chombo, jeometria bapa, nadharia yumkinifu, mienendo ya vimiminika, dhahania ya mwendo pepetua), John Locke(Baiyolojia/Tiba,--sayansi za jamii, sheria na haki za raia), Benjamin Franklin (fizikia,--nguvu za umeme radi)Thomas Jefferson(hisabati, historia,--sayansi za jamii, mwandishi la tamko la uhuru la marekani, msanifu wa utenganisho wa tawala ya nchi na dini, utambuzi wa upekee wa kila raia, udhanifu wa sheria 'isiyompa' mtu 'liberiti' ila kutambua hiyo katika mtu, upingaji wa mtaasisisho za mabenki, upingaji wa dhana ya madeni ya kurithi kulingana na amana za kibenki, dhahania ya katiba kutokuwa 'msahafu' katika vizazi vya wanajamii, upingifu wa nguvu za majaji wa mahakama kuu kuwa ni wa 'mwisho') nk walikuwa ni wajumbe wa jumuiya za siri zilizoazimia kuleta mwamko wa 'hekima' ya zamani katika mwili mpya wa mawazo na kisomo cha mwanadamu.

Wengi miongoni mwa hawa wakisambaza machapisho ya mashauri anuai juu 'nguvu' zisukumazo maisha na maajaliwa ya mwanadamu—kufanya hivi kwa wazi wazi na wengine kufanya hivi kwa kuficha utambulisho wao halisi ili kulinda shughuli zao katika ofisi za umma, taasisi za kidini au hata ajira zao katika taasisi za elimu za juu. Wengine wakifanya hayo kwa kuchanganya baadhi ya visa vya mafundisho ya Yesu na wasikirifu wengine waliopata kujitokeza kabla na hata baada yake katika kuchochea udadisi wa mafumbo yenye kuambatana na mapokeo. Wengi miongoni mwa hawa wakianzia kwenye misingi ya mapokeo yenye kuzungumza juu ya mawezekano ya ubadiliko wa maumbo na hadhi kutokana na 'nguvu' za ndani za 'mfilosofia' mwenye busara. Vile visa hasa vya 'ma-alkimiya' wenye kutafuta mbinu za kubadili chuma cha 'daraja la chini' kuwa 'dhahabu safi' kwa kutafuta 'jiwe la mfilosofia' lenye kuleta uwezo. Bacon alikosoa mtindo wa majaribio ya kisayansi yenye kutarajia 'miujiza' labda kwa kuwa alikuwa akijua sehemu nyingi ya visa vya mapokeo ni tu masimulizi ya ishara lakini si lazima iwe kama inavyosemwa kwa juu juu. Wanasayansi wengi wa siku hizo za mwamko ndiyo waliingia hasa kwenye kuvunjika kwa ndoa ya kupendana na mabadiliko ya 'miujiza'; na kujikita kwenye vitendo vyenye kuweza kurudiwa na kutoa matokeo yale yale ikiwa viwango vile vile vya majaribio vikizingatiwa ili kusimamisha 'ukweli' wa jambo.

Hili si kwamba linabatilisha mafumbo yaliyomo katika mapokeo ya alkimiya kwa mfano. Hujulikina hata Yesu alikuwa akifundisha alkimiya ingawaje mapokeo mengi yalivuka vizazi kwa kuvutikia kwao na siri za 'miujiza'. Udadisi ndio daima humuongoza mtu wa kiuchunguzi na huo daima huanza na pale ulimbo wake unapomnasa katika kutahayari fumbo fulani. Wanasayansi wa mwanzo walinata kwenye ulimbo wa 'miujiza kamili'; majaribio yenye kuweza kufanya na kuthibitisha kisomo kilichosimama na si kusifika kwa mazingaombwe. Ingawa wengi walikuja kupendezwa na 'sanaa' hii yenye ushawishi wa maarifa dhahiri; wapo wengine ambao walizidi kuvutika kwenye mengi 'yasiyoarifika'. Hayo ambayo 'hayaarifiki' bado yanafutika mapana yote ya visomo vya mwanadamu ijapokuwa mwanadamu sasa anakuwa 'mjanja' sana kukwepa mashauri yanayoelekea kwenye mafumbo ya maumbile, nishati na uzima. Na kwa kuwa uwingi wa umma hauna namna mahsusi ya uchimbaji wa kisomo, maarifa mengi yana ukomo wa tasnifu zenye 'kusifika' kuwa ni bora—si kwa kuwa zinakidhi 'uhakika' ila tu kwa dhahania zake zilizo na 'mahadhi'; kwa kutambulika hivyo miongoni mwa wanataasisi wengi chini ya mashauri yake.

Basi pamoja na maendeleo yote ya sayansi katika siku hizi; upo upande wake uliona athari kubwa na mbaya zitokazo na wanataaluma kuwa na 'upofu' wa kujitakia juu ya upande mwingine wa kisomo usiohitaji mashauri yatokanayo na 'vipimo' vya utazamaji. Katika shauri hili tunaweza kuingia moja kwa moja katika kutazama kwa juu na 'kuhisi' jambo lililo 'geni' katika kukubalika.

Wanataaluma wa baiyolojia wanaweza kusema kifaranga aliyetokana na yai la kuku amefanyika kutokana na ule ute uliokuwamo kabla ya yeye kutungika na kukamilika kuja kutotolewa. Na siajabu hili limezaa shauri ya yai kuwa mboga yenye 'virutubisho' vyote vya mwili. Hii ni kwa kuwa katika mashauri yajayo na kisomo cha kemia, fizikia na hisabati; nishati yote iliyostahimilisha mabadiliko ya utokeaji na ukuaji wa kifaranga ndani ya yai ni jumla ya nishati iliyohifadhika ndani ya ute na kiini kwa kuhifadhika dhidi ya halijoto izungukayo yai. Ujazo wa yai ndiyo huja kuwa ujazo wa mwili wa kifaranga na pia chembechembe zote alifanyika kifaranga na ndizo zilezile zilizofanya ute mwanzoni. Sasa yai ni kati ya maumbile ya ajabu ya uhai; udhanifu wa kawaida wa kisayansi kulingana na mashauri yaliyotangulia yataleta tasnifu isiyokuwa ya ukweli juu ya yai na hatua za mtokezo wa kifanga. Kwa jinsi hiyo hiyo ya kutazama maumbile kwa nje imepata kuonekana kuwa kuku anaweza asile virutubisho vyenye kubeba madini ya kalsium na badala yake akawa anakula hata chembe za udongo zenye 'mika' ambayo ndiyo huwa na madini ya potasiamu. Uchunguzi unaonesha kadri kuku alapo 'mika' na akakosa kula chakula chenye madini ya kalsium kwa muda mrefu bado anaweza kutaga mayai yenye maganda ya kalsiumu ya kutosha. Lakini kuku anayekosa 'mika' na kalsium huishia kutokutaga mayai imara yenye kalsiumu. Yapo majibu kadhaa yanayoweza kudadavuliwa kutokana na matokeo ya uchunguzi huu lakini nichague moja ambalo hushangaza wachunguzi; inaonekana viumbe katika mchakato wa kuishi si lazima wale 'kiasi' kwa 'kiasi' cha madini na vitamini ili kuwa na 'afya bora' kama visomo vya leo vya sayansi ya virutubisho inavyoshawishi ukubali kwa watu. Na tena uchunguzi unaonesha hata kama kiasi cha kalsiumu kipindi cha ute ikipimwa na kuja kulinganisha na kiasi cha kalsiamu inayouunda mifupa ya kifaranga hivi viwili vipimo havina uadilifu. Mwili wa kifaranga una kalsiumu nyingi kuliko inavyowezekana kabla kutungika kwake toka kwenye ute... Je, mifumo hai inaweza 'kujitengenezea' madini na virutubisho vya jinsi tofauti hadhi na maumbile yake ya msingi? Kulingana na yai jibu la swali hili ni NDIYO.

Sayansi katika shauri hili inajiwekea mikingamo yake yenyewe kwa kung'ang'ania 'vipimo' na 'kiasi' hadi katika mifumo ya viumbe hai na kumbe namna za viumbe hai vinapitiliza kweli ndogo ndogo za kisayansi. Kulingana na hili peke yake kwa mfano, jamii hufundishwa matumizi ya mbolea za 'chumvi chumvi' katika kilimo ili 'kukuzia' mazao vizuri na haraka. Lakini ukweli wa kuchunguza ni kwamba ardhi yenye kutiwa mbolea za chumvi huonesha dalili za kukuza mazao haraka lakini baada ya misimu michache rutuba ya ardhi huathirika vibaya, na ile 'neema na hakika' ya mazao huanza kudorora na kupelekea hali ya mazao na mavuno kuwa mbaya.

Kisomo cha kemia na fizikia kinamapungufu yake makubwa kabisa pale mashauri yake yanapochukuliwa kwa 'ujumla' wake na kubebeka toka kungine. Kwa mfano mwingine, hudhanika kuwa nguvu zinazostawisha mwili wa viumbe wanyama hutokana na chakula pekee... Yapo majaribio yanayoweza hata kubatilisha hili shauri na mojawapo ni kama lile la mafundi wa kufunga wenye kuweza kukaa masiku, majuma na hata miezi pasipo kula. Vimekuwepo visa vya watu wachache wenye kudhihirisha hili miongoni mwa wanajamii lakini ni wanasayansi wachache wamebahatika kuchunguza finomena hii na kushuhudia 'jambo lisilolakawaida' kuendelea katika miili ya watu kama hawa.

Inafahamika kuwa mimea ya nchi kavu huwa na jinsi yake 'kujitengenezea chakula' kwa kitendo kinachotajwa ni 'usanisi na mwanga wa jua'. Aghalabu ni kwenye mimea na katika mwili wa wanadamu hudhahirika uwezekano wa 'kutengeneza chakula' ama 'vitamini' kutokana na mwanga wa jua; lakini si ile sehemu ya ukweli mwingine usiobayanika kwa wachunguzi wa jinsi ya macho na vipimo.

Miongoni mwa watu wa Bara la Uchina kumekuwepo kwa mashauri juu ya 'nguvu' yenye kustahimilisha miili 'kutoka ndani'; yaani kana kwamba chakula, maji na hewa kukidhi mahitaji ya 'nje' ya mwili lakini mienendo ya uhai wa mwili hustahimilishwa hasa na nguvu yenye kutajwa ni 'Chi'. Ni 'Chi' yenye kusharabiwa na viumbe hai vyote na kuhuisha maada zake ili kuchuka sura ya 'uzima' wa kimwili. Uzima huu hutajwa kuwa unajinsia za namna mbili katika moja—Yin na Yang. Kuna msemo katika lugha ya kiswahili usemao Lila na Fila havitangamani; kuna uwezokano usemi huu umetoka na mashauri ya Yin na Yang. Kulingana ya 'hekima' juu ya Yin na Yang katika 'Chi', husemwa uzima wa vitu hutegemea utangamano wa Yin na Yang ili viwe 'bukheri wa afya'. Viwili hivi visipotangamana huwa kuja kuwa ni 'maradhi' na si uzima katika mwili wa kiumbe. 'Chi' ni Pumzi ya uzima isiyodhahirika machoni lakini ikabainishwa kwa ishara za matokeo ya hali na hadhi ya viumbe hai. 'Chi' ipo kote na inapenya kote ingawaje yaweza 'kukadirika kujikusanya' pahala penye 'mgongo' wa umbile kama mlimani... Tokea siku za zamani kilele cha mafunzo ya sanaa za mapigano kilifanyika milimani ambako shauri kuu juu ya kutambua 'Chi' lilichukua mkondo wake.

'Kung Fu' ina tafsiri ya kusema 'muda wa kucheza' na ndivyo hivi katika maisha kila kitu ni mchezo. Sanaa za mapigano hukamilika ndani ya mtu kwa kutambua uwezo wa 'Chi' katika kukamilisha sanaa yake hiyo. Na ndivyo mafunzo kamili ya msanii kukamilika kwa kitendo kinachosemekana ni 'kuutupisha' akili; kwani katika hali hiyo ya utupu akili ya mwanadamu inaweza kuwa 'kioo kamili' cha kuakisi mienendo na nguvu ya 'Chi' katika kuchochea 'michezo' yote. Na hivi mtu yeyote mwenye kufikia daraja la 'usafi wa kiakili' husemwa hawezi kushindwa katika pigano lolote na mchezaji yeyote. Na ndivyo hivi hivi hata miongoni mwa masamurai wa Ujapani, ilijulikana kuwa 'ukamilifu' wa mfundwaji wa sanaa ya mapigano hukamilika kimafunzo yake pale anapofikia kutoka 'sawa' katika mapigano na mtu mwingine aliyemjuzi kwa kutangulia. Kwa kuwa katika hali ambayo mtu huwa ni 'mtupu' katika akili aweza kumaizi mara moja hata nia iliyojificha ya mpiganaji mwenzie na hivi akarudisha majibu ya kipigano kubatilisha athari zake. Hichi ni kitendo cha 'muda mfupi' kufanyika lakini pia hutokea 'pasipo muda'--siri yenyewe hasa ya athari ya 'mruko wa kikwantumu'.

'Chi' ndiyo 'Kani--The Force' ilivyo katika filamu za Vita katika Manyota—Star Wars; katika fasihi picha za sinema kama zilivyobuniwa na George Lucas. Dhana ya Lila na Fila ikiwakilishwa na mchezo wa vita kati ya mrengo wa ma-Jedayi na ma-Sithi. Ma-Jedayi wakifanya bidii sana ili waweze kutumia 'Kani' ili kuzikabili kuzishinda nguvu na fujo za ma-Sithi katika mapambano ya Himaya za madola katika ustawi wa Nyotani.

Shauri la 'Chi' ni sehemu ya utambuzi wa kisayansi usiotaka mtindo wa kiaristotle 'kuthibitisha' ukweli wa jambo. Jamii za mashariki walijua namna ya vitendo vyenye 'kuthibitisha' uwezekano wake wa kuwepo. Ikiwa kisomo cha 'Chi' kitapanuliwa kugusa mashauri mengine mengi katika uwanja, wa fizikia, kemia na baiyolojia, sayansi itakuwa ni 'kamili' na 'upanga' ule hasa wa Jedayi. Oganam ya karne ya 21 juu ya njia ya Tatu inaazimu hili.

Kulikuwepo na shauri la kitu kama 'Chi' katika jamii za wanasayansi wa mwanzoni; wao walisikia hayo kutoka katika mapokeo kutajwa kama 'Etha Iwakayo' . Majaribio ya 'kuthibitisha' uwepo ya etha hayakufaulu kutokana na msingi wenyewe hasa wa udhanifu katika kubuni kitendo cha uchunguzi. Mpaka hivi leo husemwa hakuna etha; lakini huu ni upofu tu... na ni swala la kiufundi. Etha 'HAIPIMIKI' na wala haina 'Ukiasi' wowote. Maumbile ndiyo yenye kuzaa picha kama vile 'Chi' imejikusanya kwa wingi hapa ama pale, lakini katika maumbile 'ukweli' ni msigano. Sayansi kwa jinsi ya vitendo vyake imekosa kufaulu kudadavua shauri la uwepo wa Etha kwa kuwa ndiyo hiyo inayodhahirisha hata 'wakati' wa mwanga 'kusafiri'. Msingi wa kitendo uchunguzi cha Michelson-Morley ulipanga sura la jaribio lao kwa udhanifu wa etha 'iliyosimama'.

Etha na 'Chi' ndivyo viwili hasa vilivyotajwa toka zamani kuufanya ulimwengu wote.

Vitu hivi ni 'Nuru' na 'Pumzi ya Uzima'. Madhahirisho yote ni 'Maumbo/Wakati'. Na hivyo kila chenye kufanyika katika madhahirisho kina 'kadri' ya chembe tatu katika moja. Jinsi moja ya Tatu kama 'Nuru/neno', jinsi moja ya Tatu kama 'Pumzi ya Uzima/kuchukua sura ya Umbo' na jinsi moja ya Tatu kama 'Nia'. Kwa ujumla wake wa moja na moja na moja, ulimwengu wote mzima ni 'Kiumbe Hai' –tofauti na mapungufu ya kimtazamo yaliyomo katika utaasisi wa sayansi ya leo katika kukubalika.

Vyenye kufanyika 'ndani' ya ulimwengu huchukua sura yake kwa daraja la 'Nia' kati ya kile kinachodhahirika na 'Ulimwengu'. Vile vile kinachohuishwa katika ulimwengu huchukua sura yake kwa daraja la 'Nia' na 'Pumzi ya Uzima' kwa jinsi ya 'Ulimwengu Hai'. Ulimwengu wote uliodhahirika ni 'Neno linaloishi'. Binadamu amefanyika kwa mfano wa 'Neno Linaloishi' lakini kwa funguo ya 'Nia' anao utashi wa kuamua kuzitambua siri za 'uzima wa milele' ama kusadiki 'mwili wa mauti' na kughafilika na adha zake zote. Siri ya maumbile na 'uzima' inashikiliwa na 'Utangamano uliofichika' uliyo pia ni muktadha wa 'Nia'.

Nyoka kujiviringishia katika Yai ni ishara ya 'Nia' na 'Uwezo' unaofanyikia ndani ya Yai--haya katika kutoa kielelezo cha 'Uzima wa Ulimwengu'. Kwa kuwa nyoka ni kadri ya unyoofu wa mantiki na utumikivu katika 'visomo' vyenye kutanabahi 'viasi'; na hivi ndivyo imekuwa nyoka ni kielelezo cha werevu. Mviringisho ni sifa ya kike ya uumbaji 'inayosiganisha' unyoofu na hivyo nyoka huwa ni alama kwa vyote viwili—akili yenye kumaizi mwelekeo na ile yenye kumaizi 'hadhi' ya mwelekeo. Ni hivi viwili vinavyozaa utambuzi wa 'wakati' katika mtu. Katika maisha, uwezekano wa wakati kutokea ni kwa sababu tu ya uwepo wa 'jinsi ya kiume' na 'jinsi ya kike'. Viwili hivi vikiwa katika 'Ndoa kamili'; hakuna 'wakati' na ni 'Uzima Kamili'. Lakini katika maumbile yaliyohuishwa 'Ndoa' ya 'jinsi ya Kiume' na 'jinsi ya kike' huja kwa utangamano maalum. Katika kila kile cha kiume kuna sehemu ya ukike na katika kila kile cha kike kuna sehemu ya ukiume... hii huleta 'mvutano' kati ya 'jinsi ya kiume' na ile 'jinsi ya kike'. Yin na Yang ni kielelezo cha 'Jinsi ya Kike' na 'Jinsi ya Kiume'.

Katika jinsi ya mfumo ndani ya mfumo, 'Nia' ndiyo hufanya 'Mwana'--hadhi ya chembe yenye mwelekeo na kutafuta 'kudhahirika'--ilivyo mbegu. Uzima ni 'uambukizaji uhai' na hivyo katika viumbe hai vyote vyenye kufanya jinsi ya 'uzazi' ; mazao yake hustahimilishwa na 'Uzima wa Vyote' na ulioko kote. Katika maungano ya kimaumbile ‘nia ya msingi’ ni habari/neno la jinsi ya chini, lakini 'Nia kuu’ huja kwa nafsi-roho na hasa katika kumzungumzia mwanadamu. Hata hivyo nia zote huneemeshwa na 'Uzima wa Milele' na huku zenyewe zikiakisi 'marefu' ya uhai. Marefu ya uhai ni neno liliandikwa katika jinsi ya msokoto wa chembe za kimwili. Pumzi ijazapo 'nguvu' neno hili, lenyewe huhaisha mienendo ya kimaada kukirimu hadhi ya kuwa ni kiumbe hai mpaka pale mwili huo utavyokosa 'kusharabu' pumzi kwa uadilifu wake.

Yai hujakutotoa vifaranga kwa mchakato unahusisha 'maada za ndani' yake na nguvu zisizotokana na maada yenyewe moja kwa moja. 'Namna' ya nuru na pumzi huhaisha kiumbe kipya katika yai na kusuka mwili wake katika mazingira fulani. Hili haliko katika yai tu, seli zote za uhai zinadumishwa nguvu kwa 'jinsi ya nuru' na 'jinsi ya pumzi' isiyoonekana kwa vipimo. Jinsi hii ya hivi viwili kudakwa na 'pete' ya uhai inayojulikana katika uwanja wa sayansi kama DNA. Umbo la 'pete' ni umbo lenye uwezo usiowakawaida wa 'mpitisho' wa 'wakati' na 'habari/neno' lisilo na umahala.

Inafahamika katika sayansi kuwa katikati ya seli yenye uhai kuna kiini chenye kuongoza mienendo yote ya mabadiliko ya uhai wa seli husika na humo ndani yake hukutwa 'jinsi ya misokoto pacha' inayopachikwa jina la 'utepe wa DNA'. Utepe huu huwa hasa ni 'pete' ya misokoto ya 'nyuzi' mbili ambazo hujizungusha kujisokota kulingana na kiasi cha ukali wa 'tindikali' iliyomo katika mfumo wake na hivi kusema kadri ijisokotavyo ndivyo 'maji maji' husukumwa nje na mnyongoroto kuwa mkali zaidi (B DNA, muundo wa uonekanao katika seli za kawaida za wanyama). Maji ni chombo shikilivu muhimu katika muonekano wa DNA kwa wakati. 'Maneno manne' yanayofanya DNA ni adenaini A—adenine, sitosaini C—cytosine, guanaini G—guanine na Thaimaini T—Thymine. Haya ndiyo hujirudia rudia katika msuko wote wa DNA katika 'kuchora' picha yake ya muundiko. Hizi hufanyika kwa maada zenye mfanyiko wa kuunda mienendo hai ya seli na uwepo wake katika vimimika vya kwenye seli hurahisisha msuko zaidi wa DNA pale seli inapoelekea kugawanyika na hivyo kuhitaji 'DNA pacha' ya kuendeleza 'Habari' za ususi wa seli na shughuli zake nyingine zote.

Uchunguzi wa DNA katika ugani wa fizikia umepata kufunua mawezekano yasiyo ya kawaida yatokanayo na hiyo. Gariaev kutoka Urusi, mwaka 1985 aligundua 'Athari Kizuka'--Fanthom Effect, alipokuwa wakifanyia kazi 'upipichumwa'-upigaji picha za kiuchunguzi mwanga—spectroscopy, kwa 'ribosamu' na 'kolagini'; katika taasisi ya fizikia, Urusi. Matokeo ya utafiti wake kamili alikuja kuchapisha mwaka 1991 na baadaye kutoa kitabu kulingana na kikundi chake cha kisomo maalum kilichopendekeza humo kitabuni shauri la natharia ya 'Jinomi yenye Msingi wa Mawimbi'--Wave Based Genome. 'Athari Kizuka' huonesha wazi machoni jinsi ya ugani mpya yenye kuvutia udadisi katika kuzungumzia vijinafasi vidogo vidogo vya muundiko 'ndani' ya ombwe—vacuum substructure; kwa kumulikia hiyo sehemu yenye 'Athari Kizuka' kwa Biru(jinsi ya mwanga isiyo ni mseto wa mawimbi mbalimbali ila namna ya namna ya mkusanyiko wa mawimbi mengi ya jinsi ya wimbi moja lenye nguvu na mwelekeo bayana, Laser) pamoja na namna ya mwanga wa kawaida. Na kama ilivyo ada, japo itifaki za jaribio ni zenye kubana ugumu, jaribio liliweza kurudiwa Moscow na huko Starnford na hivi ni 'ukweli' wenye kuthibitika.

Mawaidha ndani ya shauri la Jinomi yenye Msingi wa Mawimbi ni yenye kudadavua ukweli wa kwamba palipo na DNA pana sifakazi kama ngamuzi/kompyuta ya uhai ambapo ‘jinsi ya mawimbi’ huchimbuka--yenye sifa kuu tatu za kimsingi (1) kama 'vijineno' vilivyo katika muktadha wa lugha ya mwanadamu (2) Kromosamu, ambamo ndani yake huwepo DNA, ina hadhi ya kuweza kufanikisha sifakazi mbili--kurusha na kupokea mawimbi yachukuayo 'vijineno' na vile vile kung'amua maana wakati wa kupokea; kufungashia maana wakati wa marusho na (3) Kromosamu hufanya kazi kama 'chanja' za utengenezaji hologramu(holografia).

Holografia ni neno lenye kuwakilisha ufundi wa 'kupiga picha' wenye kuleta taswira ya mwonekano wa vina vya pembe zote tatu za uono yaani '3D'. Ufundi huu huja kwa kugonganisha 'miale' miwili toka katika 'chanzo cha mwanga' kulengwa kuishia kwenye uso wa 'kihifadhi picha'. Mmoja kutoka katika chanzo ni wenyekuja kuakisika toka kwenye 'kipigwacho picha' hadi kwenye uso wa 'kihifadhi picha'; na mwingine moja kwa moja toka kwenye chanzo kile kile, na kwa wakati mmoja--kwa jinsi tu iliyogawanyika njia; kwenda hadi kwenye uso wa 'kihifadhi picha'. Miale hiyo ili kufanya hologramu ['holo'-kamili, 'grafe'-andiko/mchoro/picha; kigiriki] yapasakuwa na 'unyoofu' na 'ukali' sawa wa jinsi ya mawimbi yake. Hili hufanikishwa kwa kutumia 'jinsi ya chanja' ya mpenyesho mwanga iliyo na mwachano sawa kwa 'nyufa' zake ndogo ndogo sana kadri ya 'urefu wa wimbi' la kuchujwa kupenyezea mbele. Vile vile hili linawezekana kwa kutumia biru, namna ya nuru yenye 'rangi moja' isiyo na asili ya 'mchangamano' ili kudhahirisha kadiri ya zile rangi za sekondari... Haya yote katika mpangilio maalum huwezesha upigaji picha yenye 'taswira ya ujazo' ilivyokutokea kama kile kitu kilichopigwa kilivyonekana kabla ya kupigwa picha ya holografia. Hii inamaana mara baada ya kupiga picha ya holografia, kile kitu kilichopigwa picha kikiondolewa lakini mwanga wa 'miale rangi moja nyoofu' kumulika pale pale palipopata kuwa na kitu na hapo hapo kumulika 'kihifadhi picha' basi kile kitu 'kitajitokeza' kuonekana kama vile kimewekwa tena mahala pale pale na kwa ujazo wake...

Hivyo ndivyo mfano pia 'Athari Kizuka' inavyokuwevyo kwa 'kuzuka' katika sehemu na hali kilichoasili ya kweli hakipo tena.

Jinsi hii ya shughuli itendekayo ndani ya seli za uhai inafunua ufunguo muhimu sana wa maarifa. Penye DNA pana 'kalamu' za kuandika/kuchora maumbo ya uhai na nyenendo zake za tabia katika miili ya viumbe hai. 'Sura ya umbo' katika fumbo lake, haiko popote pa umahala na ndivyo kuwa sayansi ya baiyolojia inayokubalika katika taasisi nzima; hudhanifu 'habari' yote ya msuko wa mwili huifadhiwa katika DNA. Lakini kumbe DNA hiyo hiyo ikianza kuhusishwa na vitu kama 'Mwanga' ama 'Sauti' huanza kuonesha dalili zisizokuwa za kawaida! Yumkini kusema sura ya viumbe hai ni 'kizuka' kitokanacho picha iliyoko 'mahala' pasikoonekanika. Hili katika kisomo cha uchunguzi ndani ya ugani wa baiyolojia, kimeleta nadharia ya 'Baiyoholografia ya Kikwantumu'--Quantum Bioholography.

Sauti nayo kwa jinsi ile ile ya 'kuchanjisha' mawimbi yaweza kuleta namna ya 'holografia ya kisauti' ambayo nayo hutumika katika kukadirisha chanzo cha sauti inayopimwa kule inakotokea.

'Mawimbi' na mfanyiko wa 'Unyoofu' kurahisisha mdhahiriko wa sura ya jinsi ya 'umbo hai' ndiyo ile alama ya Asclepius; Nyoka anayejivingirishia katika jiti.

Asclepius, mganga na tabibu wa kiyunani anayekuja kuwakilishwa katika ngano za kiyunani kama yule mtu aliyetupwa nyotani na kuwa 'ukanda nyota' wa Ophiuchus—'Mbeba Nyoka'. Huo upo katikati ya sekta ya Nge na Mshale; na hivi baadhi ya wanajimu wasiofuatisha mtindo wa mgawanyo wa nyuzi 30 za Zodiaki, huita Ophiuchus kama alama ya 13. Kusemwa kwamba alama 12 hujumuisha Dunia, Jua, Mwezi na Sayari lakini kuhusisha alama ya 13 ni kupenya zaidi kwenye kutambua mwenendo mzima wa mfumo wa Jua katika mfumo mwingine mpana wa 'mafungu unyota' ambako mfumo wetu wa Jua nao huzingusha dhidi ya ukati wake.

Husemwa Asclepius alijifunza siri za 'kughairisha' mauti baada ya kutia machoni nyoka wawili 'wakipeana' mzizi wa uponyaji, na hivi Ziusi, Mungu mkuu wa wayunani, ili kuepusha binadamu wasiwe 'watokufa' alimuua yeye kwa nguvu za radi na kutupia taswira yake nyotani.

Kisa hiki kizuri ni fumbo tu linalozungumzia 'udadisi' na 'hamasa ya kuingiliana kimwili'; kwa kuwa kupeana mzizi ni mbadala wa tendo la kupandikiza upya 'uhai' ambayo ndiyo hutawala 'sindano' ya Nge—nayo hutawaliwa kwa hayo; na nguvu za radi ni alama ya Mshale—alama ya yule mtu mwenye kasi na kulenga kufika katika mbingu; ambayo ni kama vile Asclesius alisulubiwa kwa kupigwa nao.

Nyoka kupeana mzizi pia huwa na kielelezo mbadala cha Nyoka Ouroboros pale 'wakati' unapogusiwa.

Ouroboros ni ile alama ya nyoka anayefukuzia kuungata mkia wake mwenyewe na hivi kutengeneza mduara kamili wa kujikunja. Ni alama ya fumbo la 'milele' ya wakati. Katika Pentauki, vile vitabu vitano vya Musa kutoka jamii ile ya watu kutoka mashariki ya kati, Israeli, huwa kina kisa cha nyoka 'amgongae' mwanadamu kisigino na mwanadamu yule 'aliyeandikwa shurti' la kumgonga huyo nyoka kichwa popote atakapompata. Lugha hizi za vielelezi ni mafumbo ya mfanyiko wa 'uzima' na madhahirisho yote katika wakati wote. Huitwa ni kama simulizi la 'Mwanzo' lakini hii ni kwa kuwa mwanzo wa vyote ni suala lenye kuvuta udadisi wa wanadamu wote katika kutafuta asili ya mambo yote na wakati wote.

Ukweli wa simulizi lenyewe ni kitendo kisicho cha jana wala kesho ila kutegemea tu na 'busara' ya yule aliyekusudiwa kukirimika kwa 'hekima' ya jinsi ya rohoni. Binadamu anayegongwa na nyoka ni ishara ya mauti isiyoepukwa na tena ijayo kwa mtu kwa kuviziwa—pale mtu alipojisahau kabisa kwa nyuma yaani kisiginoni. Vile pia kufanana na kile kisa cha 'Achelis' wa vita vya Troyi katika uyunani ya kale—aliyekuwa shujaa wa mapigano lakini udhaifu wake ulikuwa kisiginoni na ndivyo alikuja kuuliwa kwa kugongwa mshale katika kisigino na siyo kungineko kote katika mwili wake.

Hatua za mwanadamu ni msongo wa vizazi na mwendo wa safari yake ya ubinadamu. Vizazi vya mwandamu havikamiliki ila kwa kuandamwa na mauti. Na hivi shauri kuu la mwanadamu katika kuishi kwake ni kutafuta ile siri ya 'kutokufa'. Jinsi moja wapo ni kuendeleza hatua za uzazi wake; lakini hiyo siyo suluhu hasa. Yeye inampasa kumtafuta yule 'nyoka' mviziaji na 'kumuua' kabisa kwa kumponda si kwingineko kungine ila kichwani. Uadui wa nyoka na mwanadamu ni fumbo la wakati na kutupia kwake mkono dhamira ya kuishi kwa mwanadamu kusivyo na hakika ya kudumu. Sehemu ya ukweli wa maisha ambao husabisha mtu kufa daima utamchochea mwanadamu kutafuta maarifa na ukweli wa shauri lake la kuwa hai.

Na binadamu hawezi kuwa na amani mpaka afumbue fumbo la 'wakati' na 'uzima'. Uvumbuzi wa tendo la kujamiiana katika mwanadamu unaleta na adha ya 'kutambua' hakika ya mauti. Kwa kuwa uzazi ni ncha moja; na mauti ni ile ingine katika fimbo ya wakati—hakika ya kwamba 'hakuna refu lisilo na ncha'; kila chenye mwanzo hakikosi mwisho. Maisha na vitimbi vyote vya mwandamu kujisokotea katika 'wakati'.
 
Kutoka: Mwongozo hai kuelekea Uhuru Halisi seh. IV
5 Septemba 2011 saa 12:25 Asubuhi

Husimulika kwenye simulizi la 'mwanzo' jinsi mwanamke alivyodanganyika na 'nyoka'... Husemwa katika kisa: nyoka alimfuata mwanamke akamwambia: eti, umeambiwa usile matunda ya 'mti wa katikati'? Naye mwanamke kwa haiba yake yake ya kitoto kuhakiki hivyo na kubayanisha zaidi angalizo la ada ya 'mauti' itakayojiri endapo watakula. Lakini nyoka akamwambia kama vile kusema--kula tunda kutawapa ujuzi wa mema na mabaya na wao watakuwa kama mungu na hilo ndiyo wamezugwa... Naye mwanamke akaja kuyaona matunda ya mti wa katikati ni yenye kufurahisha na kupendeza 'machoni' akayachuma na kuyala na kumpa na mwenzie mwanaume wakala wote... Ndipo ghafla wote wakajishtukia wapo uchi... wakaona aibu.

Kisa cha mwanamke ni kielelezo cha ukweli mmoja kuhusu fahamu za mwanadamu. Wanawake wako karibu sana na maumbile yao kuliko jinsi walivyo wanaume. Na hivi wanawake pia wapo karibu na mazingira na kuvutika kupendezwa na faraja zake. Na ndivyo hivyo hivyo wanawake wamefanyika juu ya miili yao; mwanaume ni mtu ambaye jinsi ya kwanza ya 'kumjua' mwanamke ni kwa misukumo ya udadisi. Mfanyiko wa mwanamke kimaumbile huzidi mashauri yake yote yenye jinsi ya 'unyoofu' ulio ni kawaida ya nidhamu yake kiakili. Mwili wa mwanamke hujibainisha na ule wa kiume kwa maumbo yake yenye mviringo, na hali mwanaume ni mwenye maumbo nyoofu. Amkaribiapo mwanamke, mwaume udadisi wake huweza kuchukua sura ya kugusa na kupapasa kwa kuwa jinsi hivyo hutafuta kuaarifika na 'siri' za umbo la mwanamke... Lakini mwanawake wanajinsi tofauti ya akili ifanyavyokazi inayojitofautisha na jinsi ya kiume. Wanawake ni watu saikolojia ya undani kwa kuanzia; na wanaweza kubakia hivyo maisha yao yote. Mwanamke asiyejua mume toka kuzaliwa kwa mfano, ikiwa hataingiliwa na misukumo ya milazimisho toka nje anaweza kubaki ni bikira maisha yake yote na wale yeye asione ajabu. Kwa kuwa wanawake ni wenye kujifurahisha mawazo na ndoto zao za ndani na hata kuzimwagilia na kustahimilisha ndani ya tumbo hilo hilo la ndoto. Ndoto za mwanamke zisipoingiliwa na kukatishwa zinaweza kubakia ni uwezekano tu. Na ndivyo ndoto za mwanamke 'hukamilishwa' na 'nia' kutoka nje ili zijekuzaa matunda. Ni kama vile katika simulizi ya kisa cha Binti mfalme aliyelala usingizi kusubiri busu la mwanamfalme ili aaamke na kufanya harusi yenye mwanzo wa furaha ya milele kufuatia. Na ndivyo wanaume hufanyika kwa saikolojia ya nje ambayo ndiyo hasa hudhahirisha 'nia';-- ya kupanda vilima na kushuka mabonde, kukata vichaka na kutandua bui bui walioizunguka kasri; kuingia ndani na kumkuta binti mfalme mzuri aliyelala usingizi; kumbusu na nakujikuta ndiyo kamwamsha.

Lakini nia bila mwongozo haiwezi kuzaa matunda. Mwanaume ni mpofu kujua ni wapi pa kulenga katika mwili wa mwanamke ili kukamilisha 'maarifa' yake. Kugusa pekee yake hakutoshi na mwanaume kwa jinsi hii kusemwa, huanza udadisi kwa jinsi ya kuhangaika na kuchezea maumbile tu. Lakini kitendo mbadala hufanyika katika mwanamke. Mwili wa mwanamke ni mwili uliojaa na moto wa msisimuko kote katika mwili wake. Mwanamke anao uwezo wa 'kujisikia' kwa kila kitu juu ya mwili wake, na huo hafundishwi kwa maana 'upo damuni'. Na hivi inaweza hata kusemeka mwanamke ndiye mvumbuzi wa msisimuko wa mwili na hata kutambua kitovu cha hisia zote kuwezekana kusisimuka zipo mahala karibu na uvungu wa kiuno chake. Na hili huwa hata bayana wa watoto wadogo... Watoto wa kike huanza kujua nguvu ya viungo vyao uzazi mapema kabla ya wale wakiume. Jamii hukemea tabia za watoto kujigusa gusa sehemu hizo kitendo ambacho 'hushtuwa' watoto na kuanza kuwajengea dhamira ya hatia na aibu. Hii ni kwa kuwa binadamu mwenyewe hana busara ya kushughulika vema na nguvu za maumbile na hata yale ya uzazi.

Basi hii ndiyo kusema ni mwanamke aliyemuongoza mwaume kulijua tendo la kujamiiana na si vinginevyo katika picha ya mienendo. Wote wawili yumkini hawakutambua wanachofanya lakini pale kitendo hicho kilipokamilika ndipo tahamaki ya aibu ikawaingia kwani 'kujua' vilele vya kutaniko la kimwili daima ni mapinduzi makubwa kimwili, kiakili na kiroho kwa mtu mume na mtu mke. Hupelekea kung'amua 'ubinadamu' wao katika muktadha wa vitu vyote vinavyowazunguka; na ndivyo hufuatia kutambua shauri la uzazi, kuwajibika na ustawi kwa 'nguvu' ya jasho lao.

Kisa cha mwanamke aliyedanganyika bustanini ni kisa cha binadamu wote. Ni jinsi ya kike katika 'utofahamu kumbaizi' wa akili za binadamu wote ambao huchochewa ubinadamu ili avuke daraja lake na nia na utashi. Nyoka ambaye ni ishara ya werevu wa ulimwengu wote mzima wa madhahirisho ambao huchochea binadamu kutahamaki maumbile na ufungamano wa utamu wake ama muonekano wake na jinsi zake. Mtoto awapo mdogo yeye yu hajui kuwa ipo siku moja yeye atakuwa ni 'mtu mzima'. Kwa yeye ataudhania utu uzima kwa jinsi yake ya utoto. Katika uzima wote wa maisha yapo mazingira ambayo husukuma watu kuachana na 'utoto' wao lakini hapo hapo huwatupa katika uwanja wa mapambano na maalimwengu. Mazingira hayo ni sehemu ya msingi wa mpango wote mzima wa 'Uzima' kwani pasipo hayo kungesingekuwa na 'kukomaa'. Pia 'wakati' katika ndoto si sawa na wakati katika 'kukomaa' na ndivyo daima katika maisha kuna nyoka mwenye kushawishi mwanadamu ajaribu kuuingia ulimwengu wa 'nyakati thabiti' na aachane na utete wa mawazo. Naye binadamu huuingia ulimwengu wa 'wakati thabiti' kwa aibu ya yale 'mambo ya utoto' na kuzitenda kazi ili kumfaa 'nia' yake thabiti na si ndoto za alinacha. Utoto ni muhimu kwani kwa huo binadamu huweza hudhanifu hata yale 'makuu' yasiyowekana mara moja; lakini ingelikuweje ikiwa binadamu huanza kwa mawazo ya moja kwa moja ya 'vipimo' na 'kiasi'?

Basi si 'Mwanamke' kama ichukulivyo na kusomwa juu juu katika visa kama hivi ndiye 'aliyekosea'; ubinadamu wote unakosea wakati wote pale unapoanguka katika majaribu kwa visa vyote vyenye vya kufungamana na 'wakati' na hata raha zake kwa minajili ya matamanio; na ndivyo Ouroboros huwa ni nyoka mwenye kufukuzia kuung'ata mkia wake yeye mwenyewe. Na kwa muktadha mwingine ndivyo hukutwa picha ya Ouroboros ikizungushia kati picha nyingine za kitoto kichanga kikichezea fuvu la kichwa cha mwanadamu. Ni kielelezo cha uzazi, uchanga na mauti ndani ya milele yote ya ubinadamu.

Kufa na kuzaliwa tena kwa ubinadamu hushikiliwa na mhimili wa mwanamke ama jinsi ya kutunga na kudhahirisha maumbo yote ndani ya nyakati. Na hapo ndiko twajifunzako mambo mawili yahusuyo uhai—ustahimilishaji na uponyaji katika muktadha wa sifakazi itambulikayo kama UPENDO.

Pale ambapo pana 'muundo wa daraja la nia' pana uwezekano wa mkirimiko wa jinsi ya nishati iwezezayo kukirimisha ustahimilishaji na uponyaji wa mienendo ya kiuhai. Nishati hii ni Upendo; na ni yenye jinsi yake maalum yakuonekana kujifungamanishia ndani yake usifa-akili wa mawezekano yote katika ulimwengu. Huu nguvu zake huhuisha tu vile vyenye mpangalio maalum wa ndani yake ili kuwa 'hai'; vile vile hudhahirisha sura za 'mgando' wa maumbile mengine.

Mpangilio wenye mawezekano ya kushikilia maumbo yote katika sura zake 'hai' na zile za 'mgando' ni Upendo ule wenye kufutika maumbo yote yaliyodhahirika. Palipo na usafi wa kuyabayanisha mawili haya--namna ya Pumzi ya Uzima hudhirisha utukufu wake katika mienendo ulio pia ni utukufu wa usifa-akili uliyofanyikia ulimwengu wote kwa nyakati zote. Ndivyo hiyo pia huitwa ni 'Pumzi Takatifu'. Ipo kote na mote lakini utambuzi wa mwanadamu kwa wakati unaweza kutomaizi ukweli wake dhahiri. Pumzi Takatifu ndiyo huleta utangamano wa vitu vyote vya jinsi ya nchi na mbingu kwa mawimbi yake ya Uzima.

DNA ni 'muundo wa daraja la nia' na hivi ndani yake upo uwezo wa kukirimika na mawimbi ya uzima kama ule unaostahimilisha mienendo yote ya Dunia, Mwezi, Jua, Nyota na Mbingu. Habari zijazo na haya mawimbi ndiyo huongoza mienendo yote ya uhai kwa seli husika na kwa jinsi ya mapana ya sura yake; na vile vile panapo dosari yoyote katika maumbile uhai yanayoathiri msimamo wa mustakhabari wa seli, mawimbi ya uzima ni 'Tiba' ya kurekebisha mpotoko wa mienendo. Mienendo yote ya shughuli katika seli za uhai ni jinsi ya mawimbi na hivi ile dhana ya 'urefu wa wimbi' inaingia pia katika mashauri. Penye 'urefu wa wimbi' na hapo hapo jinsi ya kutaka kutanabahi kasi ya mitetemo, panahitaji la kizio cha 'wakati' ili kukadirisha na kutofautisha jinsi ya mawimbi tofauti ikiwa twataka kufanya kisomo cha kuendana na 'vipimo' na 'viasi'. Lakini kwenye seli na hata mkusanyiko wa seli wenye kuja kuunda kiumbe kizima mienendo yake yenye kutokana na jinsi ya mawimbi mengi yafanyayokazi kwa wakati mmoja; hayo hufanya hivyo kwa jinsi tuiitayo ni utangamano. Ikiwa miendendo ya shughuli mbalimbali katika seli yapaswa kuchangamana na kuchanganyika mwongozo maalum wa 'mizunguko' ya vitendo hukidhi kufanya 'vizio' vya nyakati katika viumbe hai. Na hivi miili ya viumbe hai kama mwanadamu kwa mfano; ni jinsi ya mchangamamo na mchanganyiko wa 'mizunguko' ya namna nyingi ya vitendo, mingine ikiwa midogo midogo na mingine mikubwa mikubwa yote hiyo kutosha kumdhahirisha mwanadamu 'mzima'.

Ipo athari moja katika uono wa macho ambayo hutumika katika ubunifu ufundi wa kihandisi kujenga vyombo vya umeme kama luninga na redio. Vyote hivi viwili ni vyenye kutumia kanuni za mawimbi kutenda 'miujiza kamili' ya utumikivu wa ufundi wa mambo. Mawimbi yenye kusaidia mwanadamu kuchakatisha 'habari' akilini ni yenye jinsi ya 'upana' sana kuliko yale yanayoweza kuchakatishwa na umeme kwa tabia zake. Umeme huishia kuweza kupitishwa katika vitu yabisi ama vimiminika lakini huo huo pia unaweza 'kunyongorotwa' na 'kunyooshwa' katika mzunguko wake wa 'kutiririka' kutoa 'mawimbi'. Mawimbi hayo yanaweza kubayanishwa kama 'kiasi' na 'mwelekeo' katika mzunguko wa mtiririko kwa umeme uitwao ni 'sakiti'. Basi katika sakiti, kidude kinachofahamika kama 'koili' ni jinsi ya mnyongoroto wa kipitisho umeme kama waya; na kile kidude kifahamikacho kama 'kapasita' nacho ndiyo hasa kinachofanyakazi kama 'nguvu za radi' zirushavyo 'cheche za moto' kati ya usawa mmoja hadi mwingine. Na kapasita ndicho ambacho ndani yake kimetengenezwa kama 'nyuso' mbili za vibati vyenye kuweza kupitisha umeme vikiwavimetenganishwa na 'utupu' uliojazwa hewa au kijikaratasi kilichotiwa nta au kimiminika chumvi chumvi nk ili mradi hivyo vyote huwa na jinsi tofauti ya uwezo 'kuhifadhi' zile 'cheche za moto'. Kwa kuwa kapasita hutokana neno la kiingereza lenye maana ya 'chenye unafasi wa kuweza kubeba'--capacitor. 'Koili' hutokana na neno la kiingereza lenye maana ya mnyongoroto—coil.

Umeme ni namna ya 'nishati' yenye jinsi mbili kwa wakati mmoja—'jinsi ya maji' na 'jinsi ya moto'. Vidude vya utundu wa kucheza na umeme ndivyo hutumika kulingana na tabia hizi mbili umeme kwa kadri itakiwavyo. Basi 'jinsi ya maji' ndiyo ina ugani wake wa mashauri ya 'Umeme Mtiririko' na jinsi ya moto ina ugani wake wa 'Umeme Simamivu' . Jinsi ya maji hutaja 'elektroni' katika uwianishi wa vipimo na mashauri; na wakati jinsi ya moto hutaja 'chaji' katika uwianishi wa namna ile ile. Si lazima mashauri ya chaji, elektroni na hata umeme wenyewe kuwa sawa kabisa 'kiudhanifu picha' na vile basi inavyosemekana katika taaluma yenyewe ya umeme; lakini ni bora kuyaelewa na kuyatambua mazingira yake ya mpangilio wa vitendo na matokeo.

Utundu na uchunguzi umeleta ujuzi, na hivi katika sayansi; umeme umeleta mapinduzi ya kutoka ule uwanja wa maarifa peke yake hadi kuja kuwa maarifa na ufundi.

Kutoka jinsi ya kidude kimoja kimoja katika kuunda sakiti za umeme ili kutoa matokeo yaliyosanifiwa; ujuzi na ubunifu umeleta mbele usanifu shindilivu kimuundo kutegemeana na ubora na pia uvumbuzi wa namna mbalimbali za vipitisho vya umeme. Mapinduzi makubwa ya usanifu na ufundi yamekuja na maendeleo ya kuvumbuka na kutumika kwa 'vipitisho nusu' vya umeme katika kubuni vyombo ya utumikivu wa kiumeme. Haya mapinduzi ndiyo yamezaa ulimwengu wa 'uelektronishi' kama sayansi ya udhibiti mwendo wa elektroni kwa kutumia vipitisho nusu vya umeme.

Vipitisho nusu vya umeme ni vile vidude vinavyoweza kutengenezwa jinsi yake hata katika nafasi finyu sana na huku vikileta matokeo yanayokidhi utumikivu wa umeme—katika mashauri ya muktadha wa kiingereza hutajwa ni 'semi-conductor' devices. Hivi ni vile vyenye tabia ya kuweza kupisha umeme katika mazingira fulani na hapo hapo kuwa na uwezo wa kutokupitisha umeme katika mazingira tofauti. Mazingira hayo inaweza kuwa halijoto inayokizunguka kidude hicho ama 'mweleko' wa mkondo wa umeme ikiwa vinatumika njiani katika sakiti ya umeme. Mara nyingine 'namna ya miale ya mwangaza' huathiri hadhi ya tabia zake vile pia mfano wa hata miale isiyoonekana kwa macho lakini ya jinsi wa mwangaza wa kawaida kama vile katika kidhibiti kazi za chombo tokea mbali—remote control. Vidude hivi kwa maumbo yenyewe hasa ni vyenye jinsi isiyo ya chuma ila kuwa kama tu mawe yalivyo. Na ndiyo jinsi ya mawe katika sura ya mchanga huwa kuwa ni malighafi katika kuundia sakiti za elektronia kwa hata sura iliyojifinya sana nafasi. Sura hii yenye kujifinya nafasi ndiyo hufahamika kama 'Sakiti Jumuizi'--integrated circuit, IC ambapo usanifu wa muundiko wake hughairisha ulazima wa kutumika kwa jinsi ya moja moja; kwa vidude vingi vya aina ya 'kikinzaji'--resistor, 'dayodi'--Diode, 'Tranzista'--Transistor na jamii zingine zote za jinsi ya dayodi, tranzista ikiwemo na kapasita katika mazingira yasiyo mapana. Sakati Jumuizi ndiyo ile huonekana kama kashata nyeusi za mstatili ama mraba yenye vijimeno vingi katika pande zake mbili ama zote nne. Vijimeno hivi wakati mwingine hukunjwa kuwa 'miguu' na kushikizwa na chuma laini ya risasi katika vimbao vya kiuelektronishi.

Dayodi ni kidude chenye hadhi ya kuweza kuruhusu mwelekeo mmoja wa mtiririko wa umeme na Tranzista ni kidude chenye hadhi ya kukutanisha sakiti mbili za umeme na kuatharisha mitiririko ya umeme kushahibiana kote kote. Kidude hichi basi ndiyo pekee huwa na miguu mitatu lakini kisicho namna ya sakiti jumuizi. Hivi ndiyo jamii ya vidude katika ulimwengu wa elektronia vinavyofanya kuwepo kwa uwezekano wa 'ukuzaji' wa 'viasi vya mawimbi' ili kuwezesha sifa kama vile kutoka kwa sauti iliyokuzwa kupitia spika toka kwenye kipokelewo cha sauti—maikrofoni na amplifaya na halafu basi vile vile kuweza kurekebisha ukubwa wake kwa ufundi mwingine unaohususha labda kuzungusha 'fungulio' la sauti ama kubonyeza mahala.

Ni muhimu kufahamu mashauri ya uelektronishi ili kuielewa fizikia iliyofanyiwa kazi na vile vile kutangamanisha visomo vya maumbo. Na toka kwenye mashauri haya tunasogea mbele na kumbukumbu la 'uwezekano wa ukuzaji wa mawimbi' kifizikia, lilio ni shauri la msingi wa tranzista; na basi kubakiza 'ufanyaji wa mawimbi' katika sakiti na utumikivu wake.

Sakiti inayofanywa kwa vidude viwili vilivyo ni koili na kapasita ikitiwa moto wa umeme 'hutetemesha' kiasi cha umeme na mkondo ndani yake. Kasi ya mtetemo ni mpishano wa 'kiasi' cha nguvu ya umeme utendekao kati ya koili na kapasita. Kadri nguvu iongozekavyo katika kapasita kwa mfano; itakuwa ni kioo cha mteremko wa nguvu katika koili. Kinyume chake pia ni sawa—kuongezeka kwa nguvu katika koili ni kuteremka kwa nguvu katika kapasita. Basi ndivyo hivi viwili hujifanyia ncha mbili za vilele vya nguvu—kimoja kinapokuwa juu sana ndiyo wakati huo ho kingine huwa chini sana. Kwa jinsi hiyo hii nguvu huwa ni pumzi itayodumisha mapokezano ya kuhamishiana nguvu mpaka pale pumzi 'itakapokauka'. Kwa kawaida pumzi ya umeme hukauka ikiwa sakiti ya koili na kapasita haitastahimilishwa kwa mfululizo wa 'moto'. Na ndiyo maana uelektronishi huhitaji umeme endelevu katika sakiti kwa kuwa vidude vinavyoweza kubaki na moto kwa kitambo fulani ni koili na kapasita tu. Na hivi pia siyo kusema 'vinaweza kutoa nguvu' la hasha. Umeme unaweza kusukuma sakiti ya koili na kapasita na jinsi nyingine ya vitu kama vidude mbalimbali vya kiuelektronishi na sakiti jumuizi ambavyo vyote kwa pamoja vinavyoweza kutumia umeme kudhahirisha kazi.

Kasi ya mitetemo ya nguvu za umeme katika sakiti ya koili na kapasita daima huwa ni ile ile na haijalishi ni kiasi gani cha moto wa umeme kimetumika 'kutekenya' mwenendo wake. Hii ni sifa madhubuti inayoleta uhakika wa mawimbi yanayotarajiwa kufanyiwa kazi ili kufanikisha lengo la hata kusafirishwa mbali. Na sakiti ya koili na kapasita pia huitwa ni 'sakiti ya utetemeazi' kwa kuwa huweza kutekenyana na nyingine iliyo nje yake. Utetemeazi ni tabia ya kimaumbo ambapo kitu kimoja chenye kutetema chaweza kuambikiza kingine kutetema ikiwa kuna mshahibiano wa maumbile na vipimo kwa namna maalum. Ni jinsi ambavyo waya mbili zilizokazwa huweza kuambukizana mitetemo ikiwa mmoja utakung'utwa kupigwa. Maana ile ambayo haikukung'utwa ikisogezwa karibu na ile iliyokung'utwa huanza pia kutetema na kutoa sauti kwa jinsi yake. Basi sakiti ya utetemeazi ndiyo ile katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'resonant circuit'.

Mawasiliano ya kimawimbi husaidiwa uwezekano wake kwa sifakazi ya sakiti ya utetemeazi kwa pande zote mbili; ile yenye kurusha mawimbi na ile yenye kupokea mawimbi. Katika mazingira ya uwezekano, sakiti ya utetemezi itafaa 'kurusha mawimbi' pale kasi ya mitetemo yake itakapofikia kiasi fulani ikadirishayo kwa kutajwa ni frikwensi ya kurushika. Maji, hewa na anga vina mpitisho wake wa mawimbi wenye kuanzia na viasi tofauti vya frikwensi. Frikwensi ya mawimbi inayokidhi masafa ya kurushwa hewani ndiyo kuchanganywa na habari ili hiyo ipokelewe inakotegwa kunaswa. Mawimbi yaliyobebeshewa habari yanaponaswa huchujwa kiuelektronishi ili kuibakiza habari inayotakiwa.

Katika kurusha habari ni frikwensi moja tu inayotumika kwa habari na hivyo sakiti ya utetemeazihutumika kupanga masafa ya marusho pasipo haja ya kurekebisha-rekebisha kiasi cha frikwensi. Katika mapokezi ya mawimbi sakiti ya utetemeazi huwa na namna ya kuweza kurekebishika ili kunasa mawimbi mbalimbali wakati hata wakati. Hili huwezekana kwa kurekebisha upana wa zile 'nyuso' zinazotazamana katika kapasita; kwani kadri nyuso mbili za kapasita zinaposanifiwa kusogea kama vile kisu cha kukunja kinavyoweza kukunjua visu vyake mbali mbali na huku havigusani yenyewe kapasita itapelekea utetemeazi tofauti kwa kadri ya ukubwa wa utazamano wa nyuso. Kusanifu hivyo kapasita ni rahisi kuliko 'kuzidisha' ama 'kupunguza' minyongoroto ya koili ambako pia kunapelekea uwezekano ule ule. Lakini tekinolojia ya kisasa huweza kufanikisha kitendo cha kubadili frikwensi katika sakiti ya utetemeazi kwa kutumia aina ya kapasita iliyo ni jinsi ya dayodi kwa hapo hapo; ambayo kwa kadri ya nguvu ya umeme uliounganishiwa moja kwa moja kwa hiyo--hufanya 'namna ya mwanya/pengo' katikati ya namna mbili za vipitisho nusu vya umeme vinavyoifanya hiyo. Basi badala ya kuzungusha ili kurekebisha frikwensi, jinsi ya umeme unaoongezwa ngazi kwa ngazi unaweza kufanikisha kile kile kwani huo umeme husababisha mgandamizo wenye kudhibiti 'upana' wa pengo na hivyo tena--hatautetemeazi waweza kuhama kutoka uwezekano wa frikwensi moja hadi ingine. Hii ndiyo hutumika katika vyombo vya kiuelektronishi vya leo kama redio za simu za mikononi, ama jinsi zote za udhibiti wa kubonyeza... Jinsi hii ya kurekebisha mdako wa mawimbi ndiyo huenda kwa jina la 'mrekebisho uliosanifika unamba' kwa kuwa ufundi huu umetokana na ufundi wa kudhibiti tabia za sakiti kwa 'Uelektronishi wa Jinsi ya Namba'. Basi mrekebisho ulisanifika unamba ndiyo ule katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'Digitally Synthesised Tuner'. Uelektronishi wa Jinsi ya Namba hutajwa ni 'Digital Electronics'.

Na sasa tuukague ulimwengu wa mawimbi na habari.

Sauti au picha haviwezi kutumwa hewani kitekinolojia pasipo utumikivu wa mawimbi. Kwa bahati nzuri sauti nayo ni mitetemo na hivi yaweza kuchanganya na mitetemo ya kiumeme na kurushwa hewani kama kitu kimoja. Hili linafanikiwa kiurahisi kwa kuwa sauti inaweza kufua umeme wenye jinsi ya mawimbi kwa mitetemo yake juu ya chombo maalum kinachofahamika kama maikrofoni. Pia zipo aina za maikrofoni ambazo zitumikapo kama kidude cha ukinzani katika sakiti ya umeme; basi ukinzani waweza kutetema kadri sawa na sauti inayoangukia juu ya kiwambo chake chenye kutetemeshwa na sauti. Hili linafanya mkondo wa umeme katika sakiti kubadilika kushahibiana na mitetemo ya sauti na basi nguvu za umeme zinaweza kugemwa kama mawimbi ya kiumeme.

Mawimbi ya kiumeme huchanganywa na frikwensi toka katika sakiti ya utetemeazi katika sakiti nyingine maalum ya 'umodutulishi'--mchakato wa kuchanganya habari mawimbi na mawimbi ya kurushia hewani. umodutulishi hutoa zao la mawimbi yaliyo tayari kwa marusho; yenye hadhi ya aidha 'umodutulishi kimo' au 'umodutulishi frikwensi'. Katika umodutulishi kimo ndiyo wimbi la marusho hutetema hewani kote na huku 'ukali' wake ukinepa kwa kadri ya mitetemo wa mawimbi ya ile habari hasa. Pale mawimbi haya yapokelewapo ule mnepo huengulia na kuchakatuliwa ili kubaki mawimbi ya kiumeme yenye kukuzwa na kuendesha vyombo vininge vya kielektronishi ili kugezwa habari kamili nje chombo chenyewe na kwa hadhira kupitia spika.

Jinsi hii ndiyo katika redio hukutwa skeli ya mitabendi ya 'AM'--kwani hili huwakilisha 'Amplitude Modulation'. Kwa upande wa umodutulishi frikwensi mnepo hufanyika katika 'kasi' ya mtetemo wa 'frikwensi ya marusho' ambayo yaweza kunepeshwa kwa kiasi chake na hali mawimbi yakapokeleka nasakiti mtetemezi iliyotegeshwa kufaa katika wigo wa masafa ya 'FM'--kwani hii huwakilisha 'Frequency Modulation'. Basi kwa kawaida wigo wa masafa ya umodutulishi frikwensi hufanyika katika mitetemo ya kasi zaidi kuliko ile inayotumika katika umodutulishi wa kimo. Katika nadharia za mawasiliano, kadri mitetemo ya kasi inavyotumika ndivyo 'habari' inavyoweza kubebwa kwa 'ufanisi' zaidi na pia ubora. Umoditshi wa frikwensi si tu unawezesha marusho wa matangazo bora kwa sauti, iwe muziki ama vinginevyo; lakini pia unatija kwa 'weupe' wa dosari. Hiii ni kwa kuwa katika jinsi hii ya mawasiliano mwingiliano wa 'makelele' yenye kuweza kuchafua habari moja kwa moja hakuna. Kwenye umodutulishi wa kimo habari inaweza 'kuchafuliwa' na kelele zitokanazo milipuko ya cheche ama mashine zenye kutumia umeme zinaweza kuwa karibu na chombo pokelevu cha mawimbi. Basi ndivyo wigo wa masafa wa 'FM' ndiyo hutumika zaidi kwenye matangazo ya idhaa za burudani na taarifa kuliko 'AM'. Vile vile jinsi hiyo hiyo ya umodutulishi wa frikwensi ukifanyika kwa jinsi ya 'uelektronishi wa unamba'; huleta 'Mawasiliano ya unamba' yaliyo ni bora kuwezesha hata mawasiliano ya simu za viganjani na pia mikonga ya simu yenye kuenenda kwa mawasiliano ya angani.

Kuwezesha mawasiliano ya picha na sauti mchanganyiko wa jinsi zote mbili za umodutulishi hutumika kwa wakati lakini katika wigo wa masafa ya juu zaidi ya kimawimbi yenye kuja kurushwa hewani ili kuwezesha namna ya habari nyingi kutumwa kwa mfungasho mmoja. Kila uzi wa habari, tuuite 'sigino' hutiwa kwa nafasi ndani ya mtiririko wa mawimbi wenye jinsi ya kiarifu cha 'ufungu' wa habari. Kiarifu hichi ni alama ambayo katika kupokewa kwa mawimbi ya habari, ule uzi wa habari—sigino utakadirisha mafungu yake yenye kujumishia 'habari' ya picha na pia sauti katika kipindi cha muda mfupi mfupi sana. Basi hiyo alama ndiyo huarifu mwanzo na mwisho wa fungu la taarifa; ambao kwa jinsi yake hushaibiana mfumo wa picha katika luninga. Sigino ya habari hutangamanishwa na sigino ya kutengeneza picha katika kioo cha luninga kwa kiarifu cha umuda. Mchakato huu ndiyo jinsi hufahamika ni usikronizi wa mienendo.

Ni katika hadhi ya usikronizi twatanabahi jinsi ya kisomo muhimu sana katika ushahibishaji wa mienendo. Tekinolojia inafanya 'miujiza kamili' ya ajabu sana kwa ufundi wa usikronizi wa mienendo katika minajili ya wakati. Pasipo huu mawasiliano ni muhari. Si tu katika uelektronishi ndipo tunamaizi uwezekano wa hadhi za usikronizi lakini ni ukweli uliobayana kuwa mienendo hata ya shughuli za seli katika mwili huwezekana kwa jinsi ya usikronizi wa michakato yake. Mpokezano wa majira huitwa nirithimu; na mpangilio jinsi ya shughuli zote za uhai wa seli hufuatisha 'rithimu' ambavyo pia ni kusemakujisikronizia na vipindi vya majira. Ili jinsi ya mawimbi na majira katika mwili ndiyo hufahamika kama 'rithimu ya kidaiyurini'--diurnal rhythms. Panapo mzunguko wa vitendo na majira kama vile usiku na mchana pana rithimu ya kidaiyurini.

Basi ndivyo hata uwezekano wa kusafirisha picha kwa ajili ya luninga katika mawimbi ya kiumeme hewani husanifiwa. Ili picha itengenezwe kuonekana katika kioo cha luninga huwa kunamzunguko wa uchororaji wa picha. Kitendo hichi hufanyika haraka sana kuliko macho yanavyoweza kumaizi uchoraji huo ukitendeka hata atazamapo kioo cha luninga. Na ndipo katika shauri hili tunajifunza finomena ya kipekee sana katika mwili wa mwanadamu. Kinyume na inavyoweza kudhanika katika hali ya kawaida na tena ile ya watu wengi; fahamu za kuona kwa macho za mtu si ni endelevu katika utanabahifu. Fahamu kama 'kugusa' ni ya karibia papo kwa hapo; vivyo hivyo kwa harufu puani, na kuonja ulimini--kwa kuwa hizi zote huendana kwa jinsi ya 'mguso' baina ya vipokezi vya taarifa za kimwili na mazingira chochezi yanayouzunguka mwili. Lakini tujapo kwenye kuona na kusikia; kitu tofauti hutendeka katika muktadha wa kuchakatisha 'habari'. Ni kupitia macho na masikio ndipo mtu hupokea 'uzi wa habari' na hivyo ili kumaizi hiyo mchakato hufanyika katika ubongo wake ili kuengua 'habari' kutoka kwenye mwanga ama sauti wenye kubebea ndani yake habari. Kisomo cha uchakatishi wa taarifa na 'uenguaji' wa habari ndani ya viumbe hai ndiyo hufanyika katika ugani wa kisayansi katika mashauri ya 'sibanetia'.

Vipokeo vyote vya taarifa na habari katika mwili wa viumbe hai kama mwanadamu huratibiwa na ubongo katika uchakatishaji bainifu. Habari haiwi habari mpaka kuwepo na rejea ya kumbukumbu ya mashauri sehemu fulani katika uratibu wa ubongo. Kumbukumbu haiwezekaniki ila tu kwa uwepo na uwezekano wa 'nia' kuchukua mkondo ili kurahisisha finomena ya 'kuandika' kinachopokelewa kama habari ili kuwa kumbukumbu yenye kufaa manufaa ya rejea. Basi ndani ya mwanadamu kwa mfano, ipo nia inayomwezesha yeye kukusudia 'kunakili' habari na pia ipo 'nia' ndani yake inayohifadhi kila kitu kinachoendelea hata kama mtu mwenyewe hakusudii hivyo moja kwa moja. Ufahamu jua nafahamu mbalali ndiyo uwanja wa mchezo wa nia za jinsi zote mbili. Ndivyo hivi ufahamu jua unaweza kufananishwa na sehemu ya bonge la barafu iliyo upande wa juu wa bahari na wakati huo huo fahamu mbalali ndiyo ule upande uliozama ndani ya bahari—bahari ya utofahamu kumbaizi. Juu ya uso bahari ndiyo hufanya ufahamu jua kumbaizi. Barafu ndiyo basi ugani wa upeo maizifu wa mtu kwa wakati katika madhahirisho. Na hapa ndipo pana dalili ya kuwa ipo sehemu katika utambuzi wa binadamu na viumbe vyote ulioungana; huo si mwingine ila muktadha wa utofahamu kumbaizi ndani ya 'wakati' na hapo hapo 'ufahamu jua kumbaizi' nje ya wakati.

Basi na huo ubongo kwa ile jinsi ya upande wa kushoto na na ile ya kulia ndivyo kupitia usikronizi wa 'habari' hutafsiriwa ama kutiwa alama za uhifadhiko wa kimakusudi katika akili ya mtu; kwa jinsi isiyofahamika sana katika mashauri ya saikolojia ya juu juu ya miongoni mwa wanataaluma wa leo, kila kitu katika maisha yote ya mtu hunakilika mahala palipofichika nje na 'nia' yake ya kawaida. Lakini je, taarifa huingiaje katika ubongo wa mwanadamu?

Sauti hushabihishwa na kumbukumbu za sauti ili kumaizi habari na hili huwezekana kwa kusoma 'sahihi' ya mawimbi ya sauti yenye mfananio wa kumbukumbu fulani. Kila kinachosikika nje husikishwa tena kwa jinsi ya ndani ya ubongo ili kuleta 'utambuzi'. Ni kitendo kinachohusisha usikronizi wa habari yenyewe na kwa upande mwingine hapo hapo 'usimyulizi' wa mfananiko wa taswira sauti katika ule mchakato wa 'kuita' kumbukumbu. Usimyulizi ni kuibua taswira ya mfano itakayozimua mwangaza wa kuteka jinsi kama hiyo hiyo ya picha kama ipo katika wigo wa kumbukumbu za fahamu jua ya mtu mwenyewe. Huko ndiko huleta 'kujua' katika akili na utambuzi wa jambo. Basi ndivyo hivyo mtu akumbushwaye kitu kilichosahaulikia mbali hutajiwa visifa-sifa vya jambo ili 'aunde picha' na ikiwa hivyo visifa vinakidhi haja atagutuka na vile kana kusema anhaaa! Kumbe ni ~... Usimyulizi ni kuunda kadiri ya mfananio wowote wa kitendo ama picha kwa makusudio maalum ya kubashiri uwezekano wa uhalisia wa jambo usio wa hapo hapo. Ndiyo katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni muktadha wa 'Simulation'.

Jinsi hiyo hiyo ya uitaji wa kumbukumbu hutendeka ili kutafsiri picha itokanayo na macho ya mtu. Lakini katika macho uono huja kwa kukusanya taarifa za jinsi ya seli moja moja nyingi zipatikanazo ndani ya goroli la jicho, juu ya ngozi ya uso wa ndani kwa kila jicho na tena kutazamana kimwelekeo na mwingio wa nuru machoni—paitwapo retina. Ubongo ndio huunganisha taarifa moja moja ya kila seli ili kudhanisha taswira ya kile kilichoinngia katika uono wa macho. Lakini hapa ndipo hasa pakugusia tena hadhi ya usikronizi. Seli za uono katika macho, huwahazisomomi picha endelevu kama ambavyo ni rahisi kudhania; seli za uono huona picha kwa 'kubakia' na taarifa kwa kitambo fulani. Kitambo hichi ni kifupi mno ijapohali kipo katika uhalisia wa mchakato wa kuona. Macho 'huona upya' kadri ya kila baada ya '1/25 ya sekunde'. Na ukweli huu ndiyo hutumika kuendesha sifakazi ya kuchora picha katika vioo vya luninga ama vile vya kompyuta. Picha katika vioo huchorwa kwa mpangilio wa mafungu yaitwayo fremu na hizo hurushwa kwa kasi ya fremu 25 kwa sekunde ama zaidi kufaa uonaji wa watu. Kwenye vyombo kama kompyuta, kulingana na matumizi ya kinachotazamwa na ubora unaotakiwa; kasi ya kuchora picha inaweza kuongezwa kwa kuchagua frikwensi ya kuanza upya kwa picha ambayo huja na jina la 'Refresh Rate' katika mpangilio wa mchakato wa kuonekanishia picha.

Basi ndiyo mawimbi ya kiumeme hewani hubeba 'uzi wa habari' na kiarifu cha mwanzo wa mafungu ya picha ili kufanikisha usikronizi wa fremu ya kwanza hadi ya mwisho kwa kila sekunde inayokatiza katika kupokea 'taarifa' katika luninga. Katika 'mawasiliano ya unamba' taarifa zaidi zinaweza kufungamanishiwa na mtiririko wa habari juu ya idadi ya fremu kwa sekunde, mwanzo na mwisho wa mafungu yake, sauti na hata zingine zenye kuweza kutafsiriwa katika king'amuzi cha mawimbi na habari kilicho mahususi.

Katika ufundi wa kutetemesha uzi wa mawimbi ya habari kwa matangazo ya kiluninga tunajambo moja muhimu la kufahamu pia. Pamoja na rangi zote zionekazo katika luninga, ukweli ni kwamba ni rangi tatu tu--nyekundu, kijani na bluu; ndizo zenye kuakisika katika sigino--uzi wa mawimbi, na mitetemo yake ya marusho ya mawimbi ya kiumeme. Na halafu 'fremu za picha' ndani ya sigino si chochote ila mzunguko kamili wa mistari inayochorwa kutoka kona moja ya fremu kwa juu kushoto, mwendo wa kutoka kushoto hadi kulia katika ulalo wa mapana ya mstatili; halafu kurukia chini mstari unaofuata kwa jinsi hiyo hiyo na tena na tena hadi mstari wa mwisho wenye kukamilisha fremu moja. Fremu inayofuatia ni mzunguko huo huo wa kuanza juu kabisa kushoto na kuishia chini kabisa kulia. Hii hufanyika hivyo hivyo kwa jinsi ya zile rangi tatu kwa jinsi inayoendana nukta kwa nukta na huku kila ya hiyo moja ina taarifa yake yenyewe. Kwa ajili ya manufaa ya ufundi wa usikronizi, fremu zote zinaviwango sawa vya idadi ya mistari na uwiano wa mapana na marefu ya mstatili yanayotambulika kusanifiwa utendaji wa vyombo vya kiuelektronishi; pia kwa viwango vya taifa moja hadi lingine kwa minajili ya kuchagua. Luninga za kisasa hata hivyo zinauwezo wa kutambua jinsi sigino ilivyo na kujibadilisha ufanyaji kazi wake ili ziweze kuchora picha katika vioo vyake ikiwa uwiano wa mstatili si sawa na uwiano unaokuja na fremu za picha katika sigino. Ndivyo hivyo huweza 'kukata' sehemu ya juu na ya chini ili picha ienee katika mstatili wake mpana; ama kufanya mstatili mdogo ndani ya kioo chake ikiwa uwiano wa fremu toka kwenye sigino ni wa mstatili mpana vile basi kufanya picha iliyoendelea katikati ya utepe mweusi wa juu na chini.

Ni muhimu kujua jambo kuhusu rangi hizi tatu yaani nyekundu, kijani na bluu. Hizi ndizo zile zenyekutajwa ni rangi za msingi. Kutokana na hizi; rangi zote zenye kudhihirika machoni zaweza kufanyika. Hizi ndizo zile rangi tatu ambazo zikiwakilishwa kwa miduara mitatu inayoingiliana utaniko wake basi huleta rangi zile rangi Saba za upinde wa mvua--katika zile sehemu za maingiliano ya nafasi. Picha nzima ya rangi katika kioo cha luninga inaweza kufanyika kutokana na kuchanganya mmuliko wa chembe tatu tatu katika utenganisho wa vijinukta vingi vilivyopangiliwa katika kiwambo cha picha. Kila chembe ikiwakilisha mwanga aidha wa nyekundu, kijani na bluu. Katika luninga za kizamani, zile zenye jinsi ya chogo, uelektronishi wake unategemea ufundi wa kumulika chembe hizo tatu tatu kwa jinsi ya 'bunduki' inayolenga 'risasi' chembe moja kati ya tatu kulingana na nguvu ya habari ijayokudhahirisha sehemu ya picha kamili; jinsi kama ni aidha, nyekundu, kijani ama bluu. Bunduki zote tatu hulenga hizo chenye kwa mwendo uliosikronizishwa na hivyo ndiyo vile kuchora ile mistari ya kutokea upande wa juu kushoto hadi upande wa chini kulia. Bunduki ni jinsi ya kurunzi inayomulika jinsi ya miale nyoofu kuelekea kwenye kila chembe yenye kuwakilisha moja ya rangi tatu. Hizo chembe huwa ni aina ya madini ambayo yakimulikwa na miale ya namna hiyo yenyewe huwaka mwanga aidha wa nyekundu, kijani ama bluu kulingana na yalivyofanyika—madhini ya fosfa nyekundu, fosfa ya kijani na ile ya kibluu. Miale hiyo kuitwa ni miale ya 'elektroni' lakini hivyo ni kwa kuwa ufundi wake wa kuisababisha kutokea huwa unahusu kuunguza waya katika kila bunduki iliyoko nyuma kabisa ya lile chupa kubwa-- ambalo ndiyo hasa limtungi linaloleta chogo la kioo cha luninga; na halafu ikiwa jinsi ya umeme mkali sana unaokuzwa na kidude kiitacho 'busta' utapandikizwa kati ya ncha mbili moja ni yenye kugusana na waya wenyewe unaoungua na ncha nyingine kuwa ni ule uso wote unaoshikilia chembe za rangi, basi ndiyo miale hiyo huonekana kana 'kusafiri' kutoka kwenye bunduki hadi kwenye hizo chembe za rangi. Nazo hizo chembe za rangi zina sifa moja mahsusi, mara tu zilengwapo na miale ya hiyo miale zenyewe huwaka mwanga hapo hapo. Ni ajabu lakini kweli kwamba kuwaka na kuzima huko kuendenako na miale inayolenga na huku ikisogea kutoka upande wa juu kushoto hadi upande wa chini kulia kuikamilisha fremu moja ya picha—katika kiono cha mtu anayetazama luninga hutafsiri kama ni picha halisi na wala si vipande vipande vya 'vimulimuli'. Haya ni matunda ya usikronizi na kasi ya kitendo chenyewe katika mizunguko yake ya vitendo na tena kwa muda mfupi kwa macho kutotambua.

Katika luninga za kisasa—luninga bapa, kiwambo cha mchoreko wa picha kinachofanya kioo cha luninga huwa na jinsi ile ile ya chembe tatu tatu lakini zenyewe si chembe yabisi mfano wa madini ya fosfa katika kupangiliwa kwake ndani ya mistari inayokamilisha mfanyiko wa fremu. Badala yake huwa ni vidimbwi vilivyo katwa vizuri katika miraba miraba halafu ndani yake kukawekwa 'vimiminika kriyisto'—chembe-mawe maji. Kriyisto ni jinsi ya muundiko wa kimaada wenye sura ya mgando kama wa jiwe na tabia zake zote uang'avu na 'ukioo' wa jinsi ya kupitisha mwanga na vile basi uakisivu. Chumvi--dawa ya jiko ni kriyisto; huwa na ung'aavu lakini ukioo wa wake haupitishi mwanga. Chumvi huweza kuyeyuka katika vimiminika kama maji. Vimimibiko tofauti huleta hadhi na kadiri tofauti ya 'uyeyuko' na ndiyo hufanya upana wake mahsusi wa mashauri ya kisomo cha chumvi katika kemia na fizikia. Ni katika utaaluma wa uelektronishi ndimo mashauri ya kifizikia ya chumvi na hasa kuhusishwa na mwanga hutumika kiufundi wa kusanifu matumiko ya kikazi.

Ni tabia ya baadhi ya vimiminika kriyisto kupitisha mwanga ama kutopitisha mwanga pale viunganishwapo kiumeme na umeme katika hali ya mkondo geu wa kasi fulani. Kasi hiyo ya ugeugeu wa mwelekeo wa mkondo wa umeme kati ya ncha mbili; nayo pia huwa na kizio cha ufrikwensi. Hii ni kama ilivyokatika zile saa za mkononi ambazo huchora maandishi ya majira ya wakati kwa 'wino mweusi'. Ule 'wino mweusi' ni kimiminika kriyisto ambacho kikiunganishwa na frikwensi kadhaa ya kiumeme basi hugeuka kukinga mwanga usipite kabisa. Kiwambo chenye kubeba vimifereji vyenye kuunda picha ya maandishi kikiwekwa juu ya uso wa jinsi ya kioo akisivu kufaa, pale vimifereji hivyo vikingapo mwanga kutokufika katika kioo kutafanya mtazamaji aone kama 'wino mweusi' wa maandishi. Basi ndivyo hivyo hivyo katika viwambo vya picha katika luninga bapa huwa na jinsi ya 'chujio' kwa mwanga wenye kutoka ili kuonekana katika kioo cha luninga; kufanywa hivyo kwa matumiko ya vimiminika kriyisto. Chembe zote katika hali ya moja moja, hufanyika kwa chujio yake inayoruhusu mwanga kutoka ama kutokutoka kwa muktadha wa rangi zote tatu katika kila kimraba. Kuwashwa na kuzimwa ni zao la usikronizi unaoendesha mpangilio wa hivyo hivyo kwa kioo chote katika kukamilisha kila fremu ya picha. Mwanga wa vinukta vyekundu, kijani ama bluu waweza kutokea kwa kichujio na kurunzi kwa rangi hizo kutokana na mwanga mweupe uwakao wakati wote nyuma kabisa ya kiwambo cha picha kwa jinsi ya muakisiko wa taa za pembeni kioo chenyewe—isivyodhahiri lakini katika picha ya nje ya kioo cha luninga. Vinukta vinavyofanikisha utokeo wa rangi huboreshwa ufanisi kwa kuwa ni sehemu ya 'Filimu-Tranzista Nyembamba' na pia 'Dayodi Itoayo Mwanga' ambavyo ndiyo hufanikisha kitendo cha kuwasha ama kuzima kwa mwanga na muktadha wote mzima wa usikronizi unaoendana na uelektronishi wa unamba.

Basi ndiyo hivi kwa sanaa na tekinolojia, leo hii kuna hata vyombo vya kiuelektronishi vinavyobebeka na kuhamishika kiurahisi vyenye 'kioo cha picha za rangi' kuanzia simu za viganjani, saa za mkononi, gemu za kiuelektronishi, vidude kama IPOD nk. Hivi yote hufanyika kwa kujumuishia ndani yake tekinolojia za vioo-picha jinsi ya 'vimiminika kriyisto'-- kutajwa kama 'Liquid Crystal Display' kwenye maelezo juu ya makasha, muktadha wa lugha ya kigeni. Katika kiingereza, mashauri ya uelektronishi miongoni mwa wazungumzaji wa lugha hiyo hutaja kwa ufupi 'TFT LCD' kuwakilisha 'Thin Film Transistor Liquid Crystal Display' ilivyo tuseme ni Kioo picha cha vimiminika kriyisto katika muktadha wa 'Filimu-Tranzista Nyembamba'. Pale ufundi unapohusisha Dayodi Itoayo Mwanga ni ndiyo mashauri ya kiingereza hutaja na pia 'LED'--Light Emitting Diode.

Kama ilivyokatika kuonesha picha, mchakato kama huo huo hudhahirika katika 'uchukuaji wa picha' toka kwenye jicho la kamera. Picha inayopita kwenye lensi ili kurekebisha umbali na mapana ya picha kuchujwa mara tatu kwa wakati mmoja ili kupata jinsi tatu za fremu zenye kunakili rangi nyekundu, kijani na kibluu. Fremu hizi hundwa kwa chembe ndogo ndogo ya 'Kidude cha ncha za kuunganishwa kwa chaji' ambavyo hufanywa kwa uelektronishi wenye kuhusisha tabia za kapasita na papo hapo jinsi moja ya rajisi rahisi ya mtungiko wa chaji ndani ya upahala panapoweza 'kusomwa' hivyo kiuelektronishi. Chaji ambayo huweza 'kuyeyuka' pale mahala itungikapo kwa kusababisha mkondo wa umeme ndani ya sakiti; hiyo yafanyika mahala palipo ni kama ule 'uwazi' kati ya nyuso mbili za kapasita ama kiwambo kisichopitisha umeme kati hizo--kisipitisho. Ndivyo hivyo kapasita pia ni kidude kinachoweza 'kuhifadhi' nguvu za umeme; maana ikiwa chaji imejazwa katika hiyo hubaki humo mpaka sakiti iiunduliwe kukamilisha njia ya mzunguko wa umeme, na hapo ndipo umeme utatiririka mpaka chaji iishe. Katika vile kidude cha ncha za kuunganishwa na chaji, namna ya kitako cha madini ya silikoni iliyotoneshewa kidogo elementi za boroni, huwambwa juu yake kwa utando wa kampaundi ya silikoni daioksaidi (SiO2, kimfanyiko wa molekyuli). Juu ya utando huo ndio kushikamanishwa na vipitisho vitatu vya umeme vyenye kutumika na zoezi la kuchakatisha 'uzi wa habari' kwa kadri ya ukali wa umeme unaojitokeza kutokana na chaji zinazojitengeneza katika kitako cha Silikoni iliyotoneshewa boroni kulingana na mwanga unaoangukia kila chembe moja ya kidude cha ncha za kuunganishwa kwa chaji na hasa kitakoni pake. Katika mashauri ya kiingereza kidude cha ncha za kuunganishwa kwa chaji ndicho hutajwa kwa jina la 'Charge-coupled Device'--CCD na kile kiwambo kilicho ni 'kisipitisho' cha kiumeme hutajwa ni 'dielectric'.

Mpangilio wa 'CCD' ndiyo huchakatishwa kwa jinsi ya usikronizi ili kuutengeza 'uzi wa habari' utakaotiririshwa kama mawimbi ya kiumeme hadi kungine mbali ama kuhifadhiwa kiuelektronishi. Kwa kuwa usikronizi kama kitendo cha kujitengemea huendana na uchakatuzi wa muda na vipande vya taarifa, ni muhimu pia kufahamu 'ukamilifu' wa 'mapatio kamili' ya 'kung'amulia' taarifa toka kwenye taarifa inayopokelewa. Kwanza kabisa ni kusema kipo kiwango maalum kwa vizio vya wakati baina ya urushaji na upokeaji. Vizio hivi huandamishwa kwa frikwensi za 'kung'amulia' taarifa ambavyo ndiyo hasa majira ya uwakati; pia huitwa ni kasi ya saa. Ikiwa kwa mfano sampuli ya uzi wa habari imesikronizika kasi ya saa kadri ya 'kilohetzi moja' basi wakati wa kupokea habari itang'amuliwa toka kwenye taarifa ikiwa kasi ya saa kuchakatisha kukomboa habari nayo ni 'kilohetzi moja' kamili. Kinachobakia ni ile tu ishara ya kutambua mwazo na mwisho wa kila sampuli ya uzi wa habari utiririkao. Ndivyo hivi mawasiliano yote huchukua sura yake okiondoa pekee yake matangazo ya radio ambayo huwa si yale yenye jinsi ya usampuli wa uzi wa habari. Matangazo ya redio huwa na usampuli wa uzi wa habari ikiwa mawimbi yake ya kiumeme yameambatanishiwa 'taarifa za ziada' kama ilivyo siku hizi katika matangazo ya wigo wa masafa ya mitabendi za 'FM' huweza kufungamanishiwa na taarifa za jina la kituo na taarifa nyingine fupi fupi kwa wakati. Katika matangazo ya Redio ama Luninga ya jinsi ya mawasiliano ya unamba haya huendana na usampuli wa uzi wa habari wakati wote.

Kiuelektronishi, 'mapatio kamili' ya kasi ya usampuli kwa uzi wa habari hutokana na maboresho yasakiti ya utetemeazi kwa kufungamanishwa na tabia ya mitetemo ya kriyisto yabisi maalum. Madini kama ya 'Kwatzi', ni kriyisto yenye tabia ya 'kutetemesha' mkondo wa umeme(pasipo kujali ukubwa wa mgandamizo wa kiumeme) kwa kasi ya frikwesi iliyo ni moja daima. Sifa hii ndiyo inayofanya madini haya kutumika kote penye umuhimu wa ukadirisho wa kasi ya saa katika kuchakatisha ung'amuzi wa habari. Hivyo daima kriyisto ya kwatzi itakutwa kwenye vyombo vya kurusha, vyombo vya kupokea na vyombo vyote vyenye kuendana na uchakatuzi wa sampuli za uzi wa habari. Pia kwenye vyombo vyote vya kiuelektronishi vinavyohusisha saa na namna ya uratibu kwa rajisi ya wakati. Kriyisto ya Kwatzi hutumika hata kwa ukubwa wa chembe ndogo sana kwa muonekano lakini kukidhi mahitaji. Sakiti ya utetemezi yenye ile kasi yake ya 'mtetemo asilia' iliyo ni sawa na ule mtetemo asilia wa kwatzi kuchakatishwa pamoja kiufundi ili kuhakikisha kugemeka kwa kasi ya mitetemo isiyoyumba kabisa na hivyo kufaa sana kwa shughuli mbalimbali za kiuelektronishi. Mitetemo asilia ya sakiti ya utetemezi haitoshi kukidhi uthabiti wa kasi ya saa ifaayo shughuli mbalimbali.

Mawasiliano angani ni jiwe la msingi katika hatua za ustawi na maendeleo ya mwanadamu. Ni ishara ya mengine mengi yatakayofuatia na hata kubadilisha sura ya jamii yote na mustakhabari wake. Si tu kimawasiliano na uchukuzi peke yake bali pia katika muktadha wa unyambuliko wa kiutu.

Maendeleo makubwa ya ulimwengu wa leo wa habari ni matunda ya 'uelektronishi wa kimawasiliano'; na katika huu tunashuhudia mwanzo wa mwanadamu 'kuvuna' mawezekano yaliyo katika uwazi wa nafasi na mbingu. Kutuma ujumbe/habari hata mahala pa mbali na hivi pia kuletewa 'habari' yoyote yenye mapenzi mema ndiyo mwanadamu--hata kabla ya huu uwezekano alipatwa na njozi na maono ya mfano wa 'malaika'. Yeye aliliona hili kwa jinsi ya mtu mwenye mbawa, arukaye hata mbawa na hivi mwenye kuzidi kadiri za umbali na kasi ilikutokea. Na yeye alilichukulia hili kama mfadhiliko kwa ujumbe kati ya mtu na Mungu na kwa nia njema. Lakini hii pia ni akitipu muhimu kuelewa jinsi ilivyojichimbia ndani sana ya fahamu mbalali iliyozama kwa kiasi chake ndani ya utofahamu kumbaizi. Kutoka katika utofahamu kumbaizi, fahamu mbalali ya mwanadamu ilipitisha 'ujumbe' kwa 'fahamu jua' ya mtu iliyowakilishwa kwa sura ya 'mtokezo wa malaika'. Malaika ni daraja ambalo binadamu vile vile amepata ufunuo wa hata yale yasiyokuwepo katika jamii yake kufahamika.

Binadamu hana uwezo wa kumaizi ukweli ulio ni dhahania mno; na hivi ufunguko wake hufanyika kuja kwa muktadha wa namna ya kipekee. Wakati mwingine huo huhitaji daraja lenye kumaizika sura ya upokezi wa 'taarifa/ujumbe/maaria' kuufaa 'ufahamu jua' wake. Ni kama vile kusema binadamu hawezi kuielewa lugha ngeni mpaka pale yale maneno ya lugha ngeni yamekuwa ndani ya fahamu yake kawaida ambayo ndiyo ufahamu jua. Ili kung'amua habari/ujumbe wowote kwa wakati binadamu hushughulika na upande wake wa ufahamu ulio ni ufahamu jua.

Uwezo wowote ambao unaweza kupitiliza ufahamu jua ili kung'amua habari; huo unaleta mashauri ya 'Paranomo' ya utambuzi kwa mwanadamu; huu pia ni uwezekano lakini usio wa kawaida sana miongoni mwa watu wengi; mara nyingine kujitokeza katika kulingana na mazingira fulani. Paranomo ndiyo yaweza kuhusisha hisia za kiakili zijitokezazo zaidi ya zile za milango ya kawaida ya fahamu kwa mtu na tena zenye kiasi chake cha usahihi kiutambuzi. Ufahamu jua katika hali ya kawaida hukamilisha kitendo cha utambuzi kwa kukutanisha hisia pokezi za kimwili, kumbukumbu na fikra/mashauri ya akilini. Paranomo hutanua hisia pokezi kutoka zile zilizomwilini mwa mtu na hata zaidi ya hizo—hali pia isivyo ni moja kwa moja.

Muktadha mintarafu paranomo unapohusisha ile jinsi ambavyo 'vifungu' ama 'uzi wa habari' ama pia namna ya ushawishi wenye kuweza kutoka kwenye wigo wa akili ya mtu mmoja hadi mazingira yake ya nje na kinyume chake pasipo zile jitihada za kimwili, kama vile kutamka na kutenda, ila tu kwa nguvu ya nia na akili tupu ndiyo ugani hasa wa chenye kuweza kutajwa ni 'Saikia'. Na vile vile yaweza kusemwa mambo ya Paranomo ni vipawa vya Saikia. Mawezekano ndani ya Saikia ya mwanadamu ni pamoja na kitendo chenyewe cha ufikirivu na utambuzi uendenao na kumbukumbu ama kuzidi mipaka ya kawaida na hivi kuhusisha ukionambali, usikiambali, uelewambali na uisharifu. Haya ndiyo katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'clairvoyance', 'clairaudience', 'clairsentience' na 'intuition'. Saikiakwa minajili ya vipawa vya akili ndiyo hutajwa katika mashauri ya kiingereza ni 'Psychic'. Msimamo mzima wa mtu kiakili kwa wakati ni Saikia ya mtu; 'Psyche' katika mashauri ya kiingereza.

Nuru ya Ufahamu, utambuzi na kumbukumbu ndiyo husokota nyuzi zote za msuko wa UTU na 'ujifahamuko'; ndani ya wigo wa Ufahamu Jua wa mtu. Utambuzi ni mfungamano wa Fikra na Hisia kwa kila urajisi wa neno ama tendo ndani ya Saikia ya mtu na kumbukumbu lake lote katika ufahamu jua—kwa nukta ya wakati wowote. Kwa kuwa hisia zote ni jinsi ya kimiminika kama ilivyo kwa 'maji'; fikra ni kama 'barafu' katika bahari ya ufahamu kamili. Kwa jinsi ya mchanganyo wa 'joto' na 'baridi' binadamu anaweza kufanya matone ya 'barafu' za mafikara. Nayo matone ya barafu yaweza kuja kufanya mabonge juu ya uso wa 'ujifahamu' wa mtu na pia chini; katika kuelea kwenye mapana ya bahari inayowezekanisha mabonge yote. Basi kwa mfano huu, ni miale ya Nuru ya Ufahamu yenye kumjalia mwanadamu uwezo wa 'kusababisha' hali ya joto ama baridi ili kurajisi jinsi ya mafikara yote katika madhahirisho katika utumikivu wa kumbukumbu lake na 'kujiona' katika kioo chake cha utu.

Kwa kadri mtu anavyojifahamu na kwa minajili ya kumbukumbu yeye atazidi kujisokotesha nyuzi za maisha yake kwa msingi wa mafikara yake. Maisha kwa jinsi yake; huakisi kile mtu akitendacho kwa matokeo yajayo kwa mujibu wa kanuni za maumbile. Kwa jinsi ya mizunguko na majira kila fikara ama neno ambalo mwanadamu hukirimu haja ili kudhahirika--kwa kukusudia ama kutokukusudia; hilo huja kuchukua sura kwa nguvu za kimaumbile. Kuna vile vitu ambavyo mwanadamu hupanda kwa nje kwenye mazingira yake na basi pale majira sahihi yanapowadia yeye huvuna kutokana na kile alichokipanda. Kuna vile ambavyo hata pasipo kutambua jinsi atendavyo nje ndivyo vile apandapo ndani katika ufahamu mbalali; hivi navyo hubaki kuwa ni ushawishi wa kichinichini utakaokuja kumtia mtu kwenye uwanja wa mavuno ya jinsi yake. Mawazo yote na mafikara ya mtu ni mbegu katika gurudumu la wakati. Majira sahihi yafikapo binadamu huvuna matokeo ya faida ama hasara kwa mawazo yake yote. Kwa kuwa mawazo ni vizio vya nia-utu kulingana na fikra na hisia za mtu mwenyewe; hivi ni kama vipande vya sumaku inayovuta ama kuvutika katika mazingira ya jinsi yake ili kufiti sura na maumbo.

Haba na haba hujaza kibaba ndiyo kanuni inayotawala misukumo ya mikondo midogo midogo kuweza kuunganika na kufanya msuko mmoja mkubwa na wenye nguvu ya jumla ya yote na mwelekeo mmoja uliodhahiri. Kila msukumo wa wazo ndani ya mwanadamu ni wenye kupanda hatia ama uhuru katika muktadha wa haki wa kanuni za maumbile. Wakati ndiyo huhukumu yote kwa nguvu zilizofanyikia katika maumbile yake na madhahirisho. Mkusanyiko wa mawazo ya jinsi ya uharibifu ama uharibiko yatamvuta mtu katika mazingira ya uharibifu na matunda yake. Mkusanyiko wa mawazo yenye ujenzi yatamsukuma mtu katika kiu ya kuunda na kutanua ustawi wake. Panapostahili stahili ujenzi binadamu akiwa na nia-utu iliyo ni mbegu ya mafikara mema atajaliwa kheri na maumbile na azma yake kutimizwa. Kulazimisha kujenga pale ambapo mazingira na wakati si sahihi binadamu atavuna taabu na kujihangaisha. Ujenzi hutaka werevu wa akili na utangamano wa maumbile na nyakati—siri yenyewe hasa majira na mizunguko iletwayo na 'Pumzi ya Uzima'. Binadamu akoseapo kanuni anaweza kusahihisha adha yoyote imsibuyo kwa kuendana na njia ya usikronizi wa mwendo wake na kanuni za kheri ya maumbile yote. Dosari ya makosa ya mwanadamu husahihishwa kwa nia safi na uongofu katika njia ya katikati yenye kheri kwa yote. Mwendo huu ndiyo utangamano wa nia-utu katika mtu na nia-uzima wa vyote. Dosari ya makosa kwa mwanadamu si hesabu kwa matendo yake bali ni upotofu wa nia yake kwa wakati na pia mshahara wa ubovu katika nia-utu wake kwenye mfichamo wa ufahamu mbalali wake.

Maumbile yote yamefanyika kwa hekima ya namna yake ambapo hakuna chochote kinachoweza kukimbia athari za matendo yake. Kadri mtu asababishavyo jitahada zozote matokeo humrudia kwa kadri ya stahiki za nguvu zake katika kitendo cha mgongano wa madhahirisho yote. Kuna yatendayo na matokeo yake huonekana kuja upesi ama kadri ya kusemama hapo hapo; na yale ambayo huleta athari za matokeo katika kusonga kwa vipindi. Hii yote ni kwa kuwa ulimwengu wote tuuona kwa macho ni tumbo la uzazi kwa hata yale yasiyodhahiri kwa ufahamu jua wetu kung'amua mara moja na hali pia tumbo hili hukirimu hata uwezekano wa mdhahiriko wa maumbo kwa mafikara yetu mabovu ndani yaufahamu mbalali. Yapo mambo yatokeayo katika jamii ambayo ni mavuno ya mtu mmoja mmoja na yapo ambayo ni mavuno ya kiukundi—ukijiji, ukimtaa, ukimji, uki-Jiji, utaifa. Pia yapo mambo ambayo ni mavuno kwa uanadamu wote duniani.

Hakuna mwanadamu asiye na kadri ya dosari inayomkutanisha yeye na wengine walioko katika mazingira yake ila ikiwa tu ameyatambua madeni yake katika makundi ya watu na kuweka nia ya kuyalipa na kuacha kulisha ubatili na upotofu wa kanuni zenye kheri ziongozazo madhahirisho yote.

Ndivyo 'Karma' imekuwa ikifundishwa katika mashauri ya dini nyingi kutoka mashariki. Kinachokwenda katika mzunguko hurudi; kinachopandwa huvunwa. Pia kuwa binadamu yuko kokote pale anapojikuta kuwapo kwa kuwa ana karma katika muktadha wa deni na hapo alipo. Na pia mtu huzaliwa pale ambapo msimu ni sahihi ili karma yake kuvunwa na majira na mazingira ya yale anayoyakuta mahali. Mtu huzaliwa mahala kwa kheri ama ubaya kwa kadri ya mbegu yake iliyofichamia katika ufahamu mbalali; ndani ya ufahamu mbalali pia kuna kumbukumbu hata kwa yale asiyomaizi kupata kuyatenda katika muktadha wa ufahamu jua wake. Na hivi kila nukta ya mwanadamu ni hukumu yake ikiwa hamaizi mbegu za nia-utu wake zichipukiazo kutokana na matendo aliyotenda kungine katika muktadha wa ufahamu mbalali. Mengi ya mawazo na fikra na usadikifu wa watu si 'mawazo mapya' kama wanavyoishi kujifahamu; bali ni fikra na mawazo waliyodumisha toka kungine hata nje ya wigo wa maisha yao wanaoujua. Na basi ni mpaka pale mwanadamu anavyokirimika kujua hata yale yaliyofichika ndani ya ufahamu mbalali wake ili aweze kubatilisha ushawishi wa uchafu wa mawazo yake hawezi kumaizi yeye 'Haki' iliyofanyikia ulimwengu wote. Haki hii ni hai na endelevu; si kama vile hasa ilivyopatwa kuzungumzwa kwamba husubiri siku fulani. Kwa kuwa watu wa zamani walifaa kwa mambo ya zamani na mashauri kuwafaa visomo vyao na mapana yao. Leo hii kisomo hiki hiki kinafunua mambo makuu zaidi na binadamu hana budi kutahayari upokeo wake kwa hekima kuu kuliko kumbukumbu lolote la maneno na masimulizi.

UHURU wa mtu ni kujinasua na kamba zote zinazomfunga mtu na mtu, pia mtu na mazingira hata katika muktadha wa ufahamu mbalali na mbegu zake za fikra-hisia kikumbukumbu. Lengo la mirengo ya kiroho kwa imani za kimashariki toka zamani ilikuwa ni kuupata huu Uhuru—Kisaikia, kimwili na kihisia; na ndivyo ilivyo hata kwa siku zote. Daima uhuru kamili huhusisha muktadha wa hata yale yaliyofichika toka kwenye upande wa nje wa ustawi wa wanadamu wote na tena jinsi ya mtu mmoja mmoja.

Ikiwa kwa muktadha wa mawazo na matamanio yake yeye mwenyewe mwanadamu hukirimika kuzaliwa mahala hata pasipo kumaizi kanuni zilizopelekea yeye kuzaliwa hapo; ni ishara ya kwamba yeye mtu si huru. Kila mwanadamu anawajibu wa kutafuta muktadha wa sababu za yeye kuzaliwa mahala; la sivyo yeye si mwenye kuwajibika na kweli ya ukirimiko wa uzima wake na ustawi wake pale alipo. Pia yeye hawezi kuwa huru na yale ambayo hajayashtukia kutawala majaliwa yake na hivi anakuwa 'mteja' wa usadikifu wowote usio ni hekima madhubuti ila mashauri ya mpito na ahueni. Kwa kadri anavyokirimika kutambua toka ndani, muktadha wa majaliwa yake kutokana na matendo yake yeye mwenyewe ndani ya nyakati za ndani na nje; kwa uzuri na pia ubaya yeye anao 'utashi' ambao ndiyo basi ngazi ya msingi kwa ukombozi wa mtu mwenyewe. Kwa kuwa kheri humshika mkono kumwongoza yule aliye na nia thabiti na uwajibikaji kwa jumla yote ya matokeo ya kazi zake. Mwanadamu ana kheri anapokiri makosa yake na kuyakubali kwa moyo wake wote na huku akiomba ndani ya 'roho' mwangaza wa wongofu kwa njia yake. Kwa saburi, maovu yote ya mtu husafishwa kwa moto wake wa nia safi na marekebisho ya dhamira katika mwendo wa safari yake yote mpaka pale atakapotakasika kabisa. Na hata atakasikapo mwanadamu anaweza kwa kupitia 'nia moja na Roho wa Uzima wote' kuchagua majaliwa yake kungine kokote katika msongo wa wakati na mahala—naam, hata kwa maisha mengine mbali na wigo wa maisha yake kipindi cha sasa.

Namna ya kumbukumbu inautumikivu kwa 'ukuwa' wa mtu katika muktadha wa nia na dhamira. Kumbukumbu ni kimvuli cha maarifa ya yote katika wakati wote na mawezekano yote. Ipo namna inayoweza kuleta shauri kuwa kila litendekalo katika majaliwa ya vitu vyote ndani ya nyakati ni sehemu ya uwezekano wenye kutathminika wa madhahirisho na maumbo yote hata kama ndani ya madhahirisho hayo kuna mkondo wa kuweza kuchagua baadhi ya maamuzi ndani ya viumbe vyenyewe. Kuna muktadha wa vitu kuwa kwamba vimepangwa na hali havijapangika kwa wakati huo huo -- kusema basi jumla ya yote huwa na sura dhahiri pale upana wa matukio unapotathminiwa. Hili katika ulimwengu wa fizikia ni huleta mashauri yenye nadharia za dhana ya kwamba 'haiwezekani kukadirisha mwendokasi na unafasi wa chembe zifanyazo tonadari ya maada' na hali tonadari yenyewe yaweza kutathminiwa hayo mawili katika uhalisia wake. Hili ni shauri la mfizikia Heisenberg--kwa mfano; na huitwa 'Kanuni ya Utohakika ya Heisenberg'.

Jinsi ya tabia na hadhi ya tonadari ni yenye kufanana kabisa na chembe msingi kwa utu na roho katika kufanyika kwa mwanadamu. Hivi ni vema kuyapitia mashauri yahusiyo muundiko wa chembe na chembe katika kuyafanya maumbo. Minajili ya utohakika wa kung'amua unafasi na kadiri ya mwendo kwa chembe zidhaniwazo kufanya tonadari ndiyo hiyo hiyo huweka ombwe katika utambuzi wa mwanadamu katika kudadavua 'kiini' cha uzima wake. Kwa mfano mtu aweza kusema kuwa kwake mtu ni 'hakika'; lakini je' iweje kuwa yeye ni mwenye kujimaizi ujitambuko wake na wakati mwingine asiwe hivyo? Nukta moja ya wakati mtu ni mzima na bukheri wa afya, wakati mwingine yeye yu mgonjwa na hajiwezi na tena zaidi wakti mwingine yeye ni mwenye kulala katika mauti na tena asije kumka tena... Kiini cha ujitambuo wa unafsi katika mwanadamu kitovu chake ni wapi hasa? Kwa maana ni hicho tu labda ndiyo 'hakika' yenyewe—hivyo basi mwili wenyewe usiwe ni hivyo. Ikiwa mtu huwa na 'utambuko' kwa kujimaizi nafsi yake ni nini sehemu ya kumbukumbu katika kujibainisha kwake hakika ya kuwa ni nafsi moja?

Kumbukumbu ya mambo na unafsi wake mtu japo yaweza kuwa ni 'kioo cha ujitambuo' yenyewe hiyo yaweza kabisa isiwe 'kweli' na wala 'hakika' yenyewe... Sasa kipi basi ni hakika? NI kawaida ya kuwa binadamu anayosilika ya kujibainisha 'ukuwa' wake kwa kumbukumbu la matendo yake lakini je, hili ni shauri la kweli ya utu wake kabisa kabisa? Yumkini kumbukumbu ina utumikivu wa kadri ya umuhimu kabisa katika ulimwengu wa madhahirisho lakini kumbukumbu yote ni 'usikweli'. Kadri ambavyo kumbukumbu ni usikweli lakini kubidi kukidhi haja ya 'ujitambuo wa mpito' basi hilo litakuwa wazi kuwa ni ile hali yenye kuwezeshwa na akili ya mtu mwenyewe yenye kufikiri na kuendesha mashauri ya wakati hadi wakati-- na pia iko sehemu ya akili ya mtu isiyo na sililka ya namna hiyo. Sehemu ya akili isiyo ni chombo cha mafikara ila tu sitaajabu ya 'mgundisho' wa tafsiri ya uwezekano wa mtu kujitambua; kwa minajili ya kumbukumbu lake na kwa jinsi ya 'kioo cha kujiona' tuuite ni 'akili ya juu' nayo hutenda kazi kwa mtindo tunaoweza kuuita ni 'dhahania'. Wazo tupu lililo ni mfano wa mbegu ni dhahania. Jinsi ya dhahania katika muktadha huu ni ile sura isiyo bayana ya jambo pana na hali yenyewe ni kama ule muhtasari mzima unaohifadhi ukweli wa lenye kujakufahamika vema baada ya vitendo vya kawaida vya matendo ya akili ya chini ya mtu kuchukua mkondo wa mizunguko wake wa mafikara na udadavuaji. Akili ya chini na ya juu ya mtu vyote kwa pamoja hufanya saikia ya mtu; nayo humuandama yeye kwa mapana yote ya kujitambua uzima wake.

Saikia ya mtu yeyote ni siri ya mafumbo kwa uelewa wa mtu nayo mazingira yake na hiyo huja kuzaa tathmini ya nidhamu ya mtu mwenyewe na nia yake. Upo uwezekano wa kutosheleza kusema kwamba-- Saikia ya watu wote, vitu vyote na uzima wote huwa na mahala ambapo hukutana ki 'maana na kheri' ya mienendo yote. Lakini katika muktadha wa dhahania binadamu kwa jinsi ya mtu mmoja mmoja, hukinga 'maji' kwa wakati mawezekano ya kujifafanua yeye wenyewe katika minajili ya majaliwa na mustakabari wake na hivi kuazimia mielekeo ya nia yake tokea kwenye mawezekano mapana zaidi ya dhahania ya utu na uzima wote.

Ili kutia hamasa ya 'ujitambuo' wa mtu, kumbukumbu la mtu humchochea yeye katika kuyabayanisha mapana ya kuchagua na kuamua mashauri ya 'utu' wake kulingana na mfululizo wa matendo yake na uhifadhiko wake katika maisha na mazingira aishiyo na kutokea kule atokeako. Nidhamu ya 'utu' ni kutaniko la mtu, mazingira yake na ung'amuzi wa mema ama mabaya katika kutanabahi ustawi wake yeye mwenyewe. Na hivi katika wanadamu wote kumbukumbu yaweza kuwa ni kimvuli cha kuegama na kinga kwa yale yasiyofahamika. Hapo hapo mwanadamu akusudiapo kutanua zaidi wigo wake ndivyo hata wigo wake wa kimvuli huongezeka. Mwanadamu daima yuko katika mapambano ya mazoea na yale mageni kwake. Mageni huweza kumletea hofu yeye lakini ikiwa mtu ni mwenye kushirikisha akili yake ya juu yeye aweza kushinda adha ya kumbukumbu na mashauri yenye kasumba na hivi huweza kuongozwa na dhahania katika kukabili mawazo mapya na wigo mpana zaidi wa maisha.

Akili ya chini ya mtu ni yenye kusumbuka na kumbukumbu na vina vya tafsiri dhidi ya utu wa mtu mwenyewe. Lipo daraja linalounganisha akili chini na ile ya juu ya mtu mhusika mmoja; wateosofia huita hili 'antakarana'. Uwezo wa mwanadamu kuzidi akili ya kawaida-- iliyo ni ile ya chini ni hafifu; na hivi ni katika mazingira maalum hutokea kwa mwanadamu kutumia mawezekano yaliyo katika akili ya juu. Na hivi wanadamu katika wingi wa idadi na silika ni wenye 'utambuo' mdogo wa yale yanayofanya saikia yao. Basi ndivyo hivi watu waweza kuwa watumwa wa mazoea yao duni na hafifu na hali wao wasione lolote lililopungua katika ustawi wao. Wale wote wanaoanza kuvuka daraja la antakarana daima wataonekana ni watu wa 'mashauri ya ajabu ajabu' na ufikirivu usio wa kawaida. Hawa ndiyo wale watu ambao huleta mabadiliko makubwa katika jamii zao hata kama jamii inayowazunguka haijaweza kwa wakati wake kuwatambua kwa matunda ya michanyato yao.
 
Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi seh. V
5 Septemba 2011 saa 12:26 Asubuhi

Elimu yenye kuegama katika kumbukumbu ndiyo shughuli iliyotapakaa kwa sehemu kubwa ya watu wa mataifa-- ambavyo pia ni kielelezo cha jinsi gani tamaduni zao huhifadhika kwa mashauri yenye kupenyezwa kutoka kwa wakubwa kwenda kwa wadogo. Ule uwezekano mwingine wa kiakili ambao waweza kuleta mashauri mapya huonekana ni 'kipaji' maalum kutokana na mtu mmoja mmoja na kumbe huenda hiyo ni jinsi yenye kuwezekana kwa kila mmoja pia; ijapokuwa tu kule 'kulala usingizi' kumewashika wengi basi na wao wakashindwa kuamka. Wachache walioamka waweza 'kutotambulika' miongoni mwa wale wengi waliousingizini. Huku kutoka usingizini, watu huamka kwa jinsi ya mtu mmoja mmoja; na wao huzindua watu wengine kutoka katika ule 'utabia wa kishirika' ulioni mpofu kwa zile hasa adha halisia za ujinga wa kutokutambua muktadha mzima wa mtu na mazingira yake kwa wakati. Wakati unapotimia wanadamu walioamka watawaamsha wengine wengi wasio zinduka kwa msisito wa muktadha mpya wa elimu usioegemia katika utumikivu wa kumbukumbu pekee ila pia kwa dhanania na uishirafu ujao kwa akili ya juu. Huu ndiyo utakuwa muundo wa elimu katika Zama Mpya ambayo itashughulika na sayansi ya antakarana ili kuleta usanisi wa mashauri ya akili ya kawaida ya mtu na muktadha wa uadilifu wa maumbo na nyenendo zote za maisha na uhai. Kwa kuwa elimu ijayo kwa minajili ya kumbukumbu ni 'mfu'-- ila tu hiyo 'hupata uhai' kwa nidhamu ya kimtazamo inayofanya muktadha wa usikronizi na 'mafikara hai' ya uzima wote.

Muktadha wa elimu wenye kutanabai marefu ya mtu kwa kuzaliwa na kufa kwake katika jamii yoyote duniani yaweza kusemwa kuwa yote si sahihi kwa kadiri ya uhakika wa matukio. Kwa kuwa jinsi zote za kutanabahi marefu na mapana ya madhahirisho ni zao la kumbukumbu na ile fanusi(sifakazi-- mfano wa utambi uwakao kutoa mwanga ndani ya taa ya mafuta || hisabati, mahusiano ya elementi za utathminifu katika muktadha wa mafungu ya kadri ya kusema ni seti) ya Uzima uletayo udhahiri wa 'uhai' wa kitu ama viumbe. Ndivyo hivi Historia na Jiografia vizingumziavyo katika mashauri ya kiuchambuzi wa matukio na tarehe ama tena basi kusema watu na kudumu kwao katika maeneo yenye mipaka juu ya sura ya nchi na zile kazi za wao kujishughulisha katika mazingira yao hayo husika ni ile tu seti ya muktadha wa nje wa mambo; kwani kote katika wakati iko hali kwenye kila nukta yake ambamo hiyari yake yeye mwanadamu yaweza kubadili mwelekeo wa mustakabari wake na hivyo kubadili 'taswira' ya utu wake pia.

Basi elimu bora yenye kumfaa mwanadamu kwa kila nukta yake ya kuishi ni ile yenye kumtia yeye yale mashauri ambayo hayatamfunga yeye na kilichopita bali kumuandaa yeye na hata mielekeo mingine tofauti ndani ya kanuni za mienendo na tabia za mazingira yanayomzunguka. Tathmini dhidi ya madhahirisho na wakati ya mtu, ikiwa yaongozwa na mashauri ya 'kumbukumbu' kuna uwezekano wa udhanifu wa kimawazo usio sahihi japo waweza kufaa katika mazingira haya ama yale. Katika sura pana mno yaweza kutokuwa sahihi, vilevile katika sura ya muktadha mdogo sana wa nafasi yaweza kuwa si sahihi pia.

Na hivi muktadha mzima wa msimamo wa maisha ya mwanadamu duniani ni wenye kuhitaji mashauri ya hekima ili kutangamanisha sehemu ya mienendo ya maisha ya mtu na ile mienendo mipana ya ulimwengu na madhahirisho katika wakati.

Japo mtu hufanyika na kuwa kiumbe, hakika ya 'utu' wake yaweza kuwa ni marefu na mapana sana ya 'wakati'. Vyote vifanyavyo sura yake katika ulimwengu wa maumbo na wakati ni tu mfumiko uliosukwa kwa 'ukweli' ulihifadhika nje ya hata mwili wake mwenyewe. Na hivi maisha yake kuzunguka mhimili usionekana na hali 'ukikatizia' kwenye mwili wake na huku ukihuisha nuru ya ufahamu wake dhidi ya vyote vingine vilivyodhahirika. Hakika ya 'utu' yaweza kuwa ni mapana ya zaidi ya urefu wa safari moja ya mtu kutoka kuzaliwa hadi mauti. Kwa kadiri hii basi, kuzaliwa na kufa si kitu ila tu sehemu ya 'mpango mzima' wenye kutangamanisha utumikivu wa maumbo na sura katika muktadha wa uzima wote. Hata mtu akijitahidi sana kupata kina katika nuru ya ufahamu wake ataanza kuihisi hakika ya 'uto kufa'; lakini kwa mashaka ya akili yake ya chini atabaki ni mtumwa wa mashauri ya 'marefu yenye ncha'. Kadri mtu afanyavyo antakarana ndani ya Saikia yake, yeye huanza kuwa na ujasiri wa kuchunguza mambo yote na basi hufika wakati utangamano kamili wa mashauri na maono kwa jinsi ya ndani humfunilia 'Kweli' ya uzima wote.

Katika muktadha wa Uzima wote hakuna 'ukiasi' na hivi pia hakuna 'upahala'; hili huzungumzika kuwa ni 'Roho' au hasa tuseme 'Roho wa Uzima'. Muktadha wa Utu 'huzunguka' katika 'Roho wa Uzima', japo kusema haya yote ni dhana tu katika urahisishaji wa kudadavua mashauri. Roho ni kitu kisichoweza kuja kuonekana na wala kudhahirika kwa jinsi tufahamuvyo maumbo yote. Na hivi hakuna kitu kama 'roho' mfano wa chembe ndani ya kitu au mwili wa kiumbe. Shani ya sura ya mambo yote katika madhahirisho na wakati ni Roho. Shauri la 'Roho' halina budi kutatiza ung'amuzi wa kawaida kwa akili ya mtu kwa kuwa Roho ndiyo kitu pekee chenye 'Uhai' na 'Uzima'. Na hivi tutajapo 'nafsi-roho' au roho ya kitu fulani ni tu kutanabaisha muktadha wa mbegu ipatikanayo katika mwili wa madhahirisho ama wakati ambamo sura ya 'uhai' na 'uzima' inayaweza 'kuhuishikia' maumbo na kuyapa hayo sura ya mienendo ndani ya mienendo ndani mipaka ya uhifadhiko katika mifumo ndani ya mifumo--yote haya katika sura ya upana usio na mwanzo wala mwisho.

Kutokuwapo kwa 'mwanzo' wala 'mwisho' ndiyo huleta shauri la muktadha wa uzima wote kutokuwa na mwanzo wala mwisho. Na hivi 'Roho ya Uzima' haijapata kuwa na mwanzo na wala haitakuwa na mwisho. Binadamu hujibabaisha yeye mwenyewe juu ya mashauri ya yenye mwanzo na mwisho kwa kuwa 'utambuko' wa unafsi wake ni wenye kukirimika katika ulimwengu wa madhahiriko. Penye madhahiriko pana mienendo, penye mienendo pana wakati; na hivi muktadha wa 'Roho ya Uzima' katika mashauri ya kiuwakati hutajwa ni 'Uzima wa Milele'; na hapa tena akili ya chini ya mwanadamu hujikwaa mwendo kushindwa kuikamilisha safari ya kuimaizi 'Kweli' ya 'Mpango Mzima' ilivyo ni Roho.

Japo maumbo huchukua sura ya mienendo, picha ya maua yake katika uwezekano wa kutathminika kwake kinjia na sura huwa ni 'fikara' katika mbegu ya kiroho. Uhakika wa hiyo mienendo ni hizi basi tuziitazo ni 'Kanuni za Asili' za maumbo kwa hali na tabia zake tuwezazo kuona na kurajisi katika kumbukumbu zetu; nazo zikawa ni sahihi katika kila muktadha wake katika wakati na kwa tena kwa mazingira tunayotanabahi uhalisia wake. Utu nao husukumwa kwa miingiliano ya mienendo ya jinsi nyingi japo vituo vyake katika mapito yake ndiyo huzaa taswira tuitajayo kama 'nafsi' na pia 'kheri' ya kufanyika kwa jinsi ya uanadamu. Tofauti na inavyodhanika kwa wengi ya kuwa utu ni ule ufupisho wa uhai wa mwili, upana wa kuyatazama maisha unaweza kufunua kwa mwanadamu muktadha mungine wa ukweli kuhusu uanadamu. Bila huo mashauri yote ya mwanadamu ni yenye kutambaa chini kama mtoto mchanga na halafu ni dumavu. Ni upeo ujao na kina cha mafikara na ufahamu ndivyo antakarana ya mtu huimalika na hata kumng'amulisha yeye pia yale ambayo watu hufa na kuzaliwa na kufa na kuzaliwa bila kutambua uhakika wake katika vizazi vyote vya wanadamu.

Maumbo yote ni maua ya Roho—Ulimwengu wote umefanyika kwa jinsi ya Ua la Uzima. Uzuri na Urembo unaofanyikia madhahiriko yote na wakati ni kutaniko la mienendo katika mifumo inayoingiliana na hivi kufanya vituo vya sura na ishara ya usifaakili unaofanya vitu vyote. Usifa akili huu ni fanusi ya Uzima—muktadha wa unyoofu na mawimbi yaliyoko kote na mote. Mawimbi haya husukuma 'chembe' za maumbo kutungika katika udhahiri wa sura na migando kwa neema ya nguvu ya 'unyoofu'. Jinsi hii pia ndiyo muktadha wa usumaku na umeme utawalao madhahiriko yote. Usumaku na umeme hufumanishwa na roho; na katika madhahirisho yote ni mbegu ya utatu—jinsi ya miale ya nuru na usumaku na uhifadhiko wa hayo yote mawili katika mapana zaidi. Hivi kuendelea pasiko kikomo. Uvumbuzi uliodhirisha penye usumaku pana umeme ndiyo pia uliodhihirisha penye ugani wa umeme au sumaku katika kupambanishwa kimraba—kadri ya mielekeo ya mitiririko ya nguvu kwa kile chenye jinsi ya umeme na kile chenye jinsi ya usumaku, hivi viwili huzaa msukumo wa mwendo katika mwelekeo wa tatu ulio ni mraba kwa uwanda wa usumaku na umeme wenyewe; kitendo cha kuepana na hivi kusogea mbali. Katika mashauri ya taaluma ya umeme husemwa ni 'sheria ya Lenzi'; ile yenye kufafanua ufuaji umeme au utengenezaji mwendo katika mitambo yenye kuzunguka kiumeme. Hii pia ni siri ya mfumiko wa madhahirisho yote. Mielekeo ya kipande tatu hufanya ule kama ni muktadha wa marefu, mapana na kina kwa tofali la mraba. Na ni jiwe la msingi katika kutathmini hali za maumbo na mienendo yote.

Ijapokuwa maumbo huweza kujipanga na kuitengeneza sura fulani bayana, hili hufanyika kwa muktadha wa maumbo mengine yaliyo madogo zaidi katika muktadha wa madhahirisho yote. Madhahiriko mengine huchukua sura kwa mitiririko ya maumbo yenye kubadilika muktadha wake katika bahari ya mawimbi ya uumbiko wote; hii bahari isiyokuwa na mwanzo wala mwisho wa mapana yake. Madhahiriko yenye sifa hii hayatathminiki kwa bahari yenyewe ama mawimbi ila tu ule uchochezi wa kufikia 'Ua' fulani. Basi ua hili huwa ni mbegu na tena huwa ni 'unyoofu' wenye kuweza kuratibu mpangilio. Hili kuwezekana tu pale ambapo pana kipeo cha tatu cha hadhi ya madhahiriko yote; kile chenye kukirimu mfanyiko wa sura ama umbo—hili hufanya 'kizio' cha umbo ama chembe; namna ya uhifadhiko wa sura ya maumbo toka katika mapana ya kiujazo yasiyo na kikomo. Maumbile yote kwa jinsi ya ukutano wa 'unyoofu' na 'mawimbi' hayana 'hakika ya milele'. Hakika ipo kwenye yote mawili uwepo na utowepo wa vitu vyote. Na hivi yote yaliyodhahirika si 'Kweli' kamili ila tu kujumuisha yale yasiyodhahirika—Roho ni yote mawili kwa 'wakati mmoja'.

Twaweza kutanabahi muktadha huu wa udhahiriko wa maumbo kwa kulifikia lile fumbo la Yai na Kuku. Swali la kipi kilianza kati ya Yai na Kuku; limekuwa ni msingi wa mdahalo wa kifalsafa na sayansi ya maumbo. Pia limekuwa ni fumbo katika kujaribu kusimamisha mashauri yasiyo na mzozo juu ya maumbo na asili; uwepo wa yote na kile kilichoyafanya yote—asilishi ya halisia yote. Ikiwa kifaranga cha kuku hutotolewa kutoka katika yai, sasa je, bila ya yai awezakufanyika huyo kuku? Yai hutagwa na kuku, sasa je, bila ya kuku laweza kufanyika hilo yai? Basi tena, iweje tupate kusema ni kile hasa kilianza kati ya kuku na yai?

Kadri hiyo hiyo huleta utata katika muktadha wa udhanifu kimawazo katika kuzungumzia ulimwengu na mungu. Watu wa makabila mbali mbali wanamashauri yao yenye kumzungumzia 'Mungu'. Wakisema ni Mungu aliyeumba ulimwengu wote; swali linaloweza kukaribishwa kwa kufuatia huwa ni basi kwamba kuuliza na yeye huyo Mungu aliumbwa na nani tena? Kwa kuwa vyovyote vile katika muktadha huu, falsafa zote za wanadamu hupwaya kwa kukosa 'maana' ya dhati. Na ndilo tatizo la msingi katika mashauri yenye kufuatisha dhana na mantiki. Basi ndivyo huja maelezo yenye msigano katika udadavuaji wa muktadha mzima wa wezekano halisi kwa ukweli wa jambo na mambo yote. Wapo wanaodai kusema Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na yeye hakufanywa na yeyote mwingine; makabila mengi duniani aghalabu shauri hili lipo miongoni mwa mashauri ya dini zao za asili. Inasikika kupata kusemwa pia kuwa Mungu 'hakuzaliwa' na wala 'hakuzaa'... Lakini haya yote ni kukadirisha tu ugumu wa kufumbua fumbo lenyewe katika minajili ya dhana na mawazo ya jinsi ya utumikivu wa akili ya kawaida ya watu wenyewe.

Kuku na Yai ni nelibini--'kaleidoskopi' ya uzima kamili wa kadri ya vyote viwili; kumaanisha basi nimang'amung'amu ya madhahirisho—mabadiliko endelevu yenye kubadilishana sura na mwonekano kwa kadri ya haraka na harakati zake na tena ndani ya vituo vya muktadha wa kiumbe; mbele ya macho ya mtazamaji. Kadri iwezavyo kuzungumzwa kusemwa ni kibayolojia, muktadha kamili wa kiumbe chenye kutajwa hai ni jumuiko la chembe ndogo ndogo zenye kuungana pamoja katika kudhahirisha sifakazi maalum; wakati mwingine yaweza kuwa chembe moja pekee ama mkusanyiko chembe kufanya muktadha sifakazi moja kama 'tishu' na tena hata 'tishu' na tishu' kufanya hadhi kazi pana zaidi. Chembe chembe hizo ndiyo 'kizio' cha muktadha wa uhai wenyewe wa kiumbe hai chote kizima. Katika mfanyiko wa viumbe hai ni chembe hai hukomaa na kugawanyika kimaumbo kamili na hivi kuongezeka ukubwa kwa kadri ya jinsi ya kiumbe hai husika. Ifikapo ukamilifu fulani wa kimaumbo kiumbe halisia huchukua sura yake ya uhai na kukidhi ufafanuzi wa hicho 'kuwa hai'. Kisha katika muktadha wa jinsi ya kiumbe kimoja hicho nacho hukunjuka sura ya shani yake na kudhahirisha harakati, mielekeo na mienendo ilivyo hiyo minajili ya nelibini kulingana na kudra zake za kufanyikia.

Yai ni mapana ya kituo kimoja na kuku kuwa ni kituo kingine. Katika kuku twaona 'hiyari' ya wawili ili kutunga yai moja. Huchukua tembe na jogoo kugusana kimwili ili kutunga yai. Basi kumbe huitaji yai na yai ili kufanya kuku na kuku kusudi yai-kuku-yai kudumu mwenendo wake kinelibini. Na hivi katika yai hakuna 'hiyari' ila tu ubidifu wa kuwa aidha jinsi ya kike ama ya kiume. Kati ya yai na kuku kuna mpaka wa muktadha wa kuja kudhahirika 'kuku'. Yai laweza kustahimilisha mawezekano yote iwe ya kike ama kiume lakini kuku hana budi kufanyika kwa jinsia. Akiwa tembe hawezi kuwa jogoo na akiwa jogoo hawezi kuwa tembe; ila kwa namna ya kipekee, yenye kuhusisha 'kutaniko la kimwili' na tena palipo na jinsia mbili ni moja yenye uwezekano wa moja kwa moja kuendeleza madhahirisho. Jinsia hiyo ni ile ya kike. Ni jinsia ya kike yenye uwezo wa kustahimilisha mtungiko wa maumbile yenye kuja kufanya madhahirisho ya kiumbe na jinsia ya kike au kiume; na hivi basi kubakiza kuwa katika jinsi ya kiume ndiko kwenye mbegu ya jinsia moja kwa wakati na halafu kwa kutawaliwa na 'mazingira' fulani yasiyofahamika vema lakini kuhusisha uwiano wa kimazingira yenyewe ya kuwapo kwake viumbe hai na saikia jumuizi--hali ya 'kutotabirika' kwa jinsia itayofuatia baada ya kitendo cha 'kutaniko la kimwili' na mtungiko mpya.

Kufanyika kwa kiumbe hai ni kwenye kubeba sehemu ya utambuko wa kimwili na jinsia. Viumbe hai kama wanyama si vyenye kujitambua kwa kila kitu kinachofanya ama kufanyikia ndani ya miili yao. Utambuzi wa kimiili huwa na kadri ya 'uso' tu wa miili yenyewe na mengine yote ni maendelezo ya utumikivu wa akili za viumbe vyenyewe. Kwa mfano mwanadamu hawezi kwa hakika kushuhudia kuwa ana maini ndani ya mwili wake na hayo yamekaa wapi ndani yake; hawezi kusema maji na chakula katika mwili wake husagwa vipi na kusharabiwa katika mwili wake wote. Pia hawezi kueleza pumzi avutayo ni yenye kustahimilisha vipi viungo vya mwili wake na mapana ya kutumika kwake. Hawezi kuzungumzia haya kwa hakika na angali yote yakiwa ni sehemu ya muktadha 'unaotathmini' uzima wake kwa wakati na msukumo wa pilika zake za kila siku. Viungo vyote vya ndani ya mtu na viumbe pia hufanyika kwa tishu zile zenye kufanywa kwa chembechembe ndogo ndogo na tena zilizo ni 'kizio' cha uhai—seli. Hata viungo vya ndani vya nyama kama moyo na ubongo vyote ni kutaniko la tishu zifanyazwo kwa seli za idadi nyingi sana sifanyazo kazi kwa utangamano unaratibiwa na 'mawimbi ya uzima'. Mawimbi haya ndiyo yale yenye kuja kwa sura ya rithimu. Rithimu hii huratibu tabia na mabadiliko ya seli zote; kuanzia kutungika, kukomaa na kufa. Na hivi japo kiungo chaweza kuonekana kudumu kwa miaka mingi, seli zinazounda viungo hivyo si za muda mrefu kama dhahiriko la kiungo chenyewe. Seli nyingi katika miili ya viumbe hutungika, kukomaa na kufa na hali uzima wa kiumbe kuonekana uko pale pale... Hata mwanadamu afikapo uzeeni, mwili wake wote ushakufa seli nyingi sana na mara kadhaa kulingana na rithimu na majira yaletwayo na mawimbi ya uzima. Kwa kuwa seli hufa kwa kupokezana na nyingine mpya zilizotungika na kuongezeka, mtu kwa kadri ya utumikivu wa akili yake yeye hujionana ni yule yule siku zote za kuishi kwake.

Basi ndivyo tunaweza kusema wazi 'mtu' ama 'kiumbe' si mwili hasa. Kinyume na inavyochukulika na kufikirika hata katika ulimwengu wa sayansi leo ya kwamba mtu hufanyika na 'kutosha' kuwa mtu kwa ile mifumo na mienendo yote ya kimwili; huu si ukweli—ni nusu ukweli ulio ni hatari kuliko uongo kamili. Kwa kuwa ile sehemu yake yenye kuonekana kama ni ukweli kuwa ni hivyo yaweza kumzuzua mwenye kutazama na kumpelekea yeye kwenye hitimisho la mashauri lisilo sahihi. Uongo kamili hukosa shikilizo katika halisia; lakini 'nusu ukweli' inacho kiungo chenye 'kujishikiza' kwenye 'halisia' kamili. Basi mtu ni 'kweli' iliyochanganyikana na 'usikweli' na tena kwa jinsi ya ajabu kujitahidi pamoja katika kudhahirisha sura ya 'utu'. Mwanadamu kiumbe kinachobebwa na viumbe katika michakato ili kukirimika 'sura' yake. Utu ni mbegu ijayo kwa muktadha wa 'Saikia' kamili ambamo ndani yake mna yote 'yanatosha' kukadirisha muktadha wa mtu katika kudhahirika juu ya mwili wa nyama.

Ndani ya Saikia kuna muktadha wa vitu vitatu kuchambulika kipekee--nafsi-roho, akili na nafsi. Nafsi huhusisha muktadha wa akili, kumbukumbu ya mtu kujichukulia katika mazingira yake akitumia mwili kama chombo cha 'uhalisia' wake. Huu ni upande wa chini wa akili ya kawaida; upande wa juu wa akili huwa ni dhahania kwa uadilifu wa kiutu kwa unafsi wa mtu mwenyewe. Haya yote huakisi mawezekano ya Ua la ndani la mtu lililo ni nafsi-roho; sehemu ya sura ya 'mpango mzima' kwa utu ndani ya Roho wa Uzima wote. Nafsi-roho ndiyo hii 'Sonafi' katika mwingiliano wa mwili, akili na uzima—Jua la utu lenye kuungazia uwezekano wa neema zote za mfanyiko na mdhahiriko wa ubinadamu.

Uhalisia wa Saikia ifungamanavyo na mwili ni jinsi ya msalaba; japo mwili hutungika na kufa, saikia ya mtu ya mtu haitungiki na kufa na mwili. Mapana ya kuzaliwa na kufa si mapana na marefu ya Saikia ila tu mkatizio wa Saikia yenyewe katika mfanyiko wa mwili. Saikia ni 'mgeni' katika mwili na tena mpangishaji tu. Saikia huchanua na kukomaa katika mwili na huku ikiendesha mwili kwa sura ya hivyo hivyo na hali mwili ukatapo pumzi Saikia 'hujikunjia ndani' kama mbegu yenye kusubiri na kuhitaji pahala pengine penye kustahili hiyo kumea na kuchipua tena. Mbegu ya 'utu' ina usiku na mchana kama ilivyo katika mizunguko mingine ya kiuhai yenye kuja na misimu na majira—rithimu zifuatishazo namna ya 'mawimbi ya uzima' na 'wavu' wa maumbo-wakati. Iwapo katika giza huwa ni 'chembe ya ndoto' na mang'amu ng'amu yake; japo hayo yote huwa ni ya mpito tu. Yale ambayo watu wa makabila huzungumza kuhusu 'mahala pa wafu' ni sehemu za mpito ambazo 'hazina uhalisia' wa kutosha kuneemesha 'mbegu ya utu'. Ni pahala penye giza tororo ama mbalamwezi kwa Saikia ya mtu japo upo ufundi wa kutumia sehemu hiyo ya mpito katika 'kuhifadhi' kwa kana vile 'kugandisha' kadri mbali mbali ya uwezo na karama mahususi zilizopata kufikiwa na kutambuliwa ndani saikia ya mtu aliyeachia mwili. Na basi Sakia ya mtu huweza kunasa katika wavu wa maumbo-wakati na kudhahirika mtu mwenye kuishi upya.

Saikia ya mtu inasapo katika mtungiko wa mwili mpya hutuama kama ngozi ndani ya ngozi kiutumikivu wa akili—kama vile kitunguu kinachofutikwa na maganda yake ya nje na ndani. 'Sehemu ya nje' hufanya muktadha tuli wa akili katika ufahamu mbalali na ile ya ndani kuwa chipukizi la 'Saikia changa' na hai--kuendana na mwili na mazingira mapya. Ndiyo hivi kuwa kila jambo ambalo mtu hutenda katika ulimwengu wa madhahirisho hubakiza kumbukumbu katika Saikia ya mtu mwenyewe. Katika kiini cha saikia na mwili ndipo sonafi hutawala shani ya yote na kudra za kipekee kwa mtu katika 'mapana' ya wakati na uzima wa mwili. Sonafi ni mhimili wa 'utu' katika mtu. Sakia ni kioo kinachooakisi sehemu ya nuru yake kujijenga rangi na muktadha wa kimadhahiriko. Sonafi imefanyika kwa kweli yenye kupita jinsia ile ya kike ama kiume... Na hivi kudhahirika kwa mtu katika mwili wa kike au kiume ni matokeo tu katika ulimwengu wa madhahiriko. Kadri Saikia nasavyo mwili yaweza kunasuka na tena kunasa tena na tena... Kitendo cha hiki ndivyo kusema utwaaji mwili na marudio yake. Ndivyo hivi mtu aweza kuvuna alichopanda hata maisha mengine nje ya upana wa kipindi cha uhai wake mmoja. Ukoseaji katika njia zenye kheri katika kanuni za 'Roho wa Uzima' hubaki kuwa ni deni katika saikia ya mtu nayo hutawala majaliwa yake katika hata mwili mpya kwa kuwa ni sehemu akili ya mtu huyo huyo kutokana na ushawishi wa fahamu mbalali. Yale yote yenye asili ya ushawishi wa mawazo na hisia kama chuki na hofu hudumisha udhaifu katika saikia ya mtu yenye kuzaa unyonge wa mtu hata maisha mengine. Vile vile misukumo ya vitendo yenye kuambatana na hisia kali hubaki katika saikia ya mtu kumchochea yeye na yale yatakayo mpa yeye sifa ya 'hamasa' ya nguvu hata katika utwaaji mwili mwingine ambao haukusababisha uhalisia huo.

Watu na jinsi mbalimbali za kitabia na kisaikolojia huzaliwa kutokana na matunda mbalimbali ya matendo yao yaliyopita katika muktadha wa utwaaji mwili na Saikia. Saikia hufanya ladha ya mtu mwenyewe kwa kadri anavyohusiana na mazingira—madhahirisho na wakati. Ukali ama upole wa mtu ni mazao ya nuru ya sonafi ilivyochakatishwa katika saikia ya mtu. Yale matendo yenye matendo 'machafu' ya mtu kutinga nuru kupenya na kuakisi hiyo kwa matumizi hasi ambayo yatapelekea marudio ya 'uchafu' na pia mtu kuvutika katika uchafu zaidi. Matendo masafi ni utendaji wowote wenye kheri na tena unaoendana na karama njema za 'roho wa uzima'. Kila mtu afanyavyo yenye kheri yeye hufunguka zaidi kutambua yale ambayo 'Roho wa uzima' wote hukirimu katika ile njia ya mchanuo wa utu. Matendo masafi ni matendo yajayo na 'usafi wa moyo'. Usafi wa moyo hutambulika na kurajisiwa katika Saikia ya mtu pale matendo yake yanapokuwa si yale yenye kuakisika na sura ya uchafu bali ile kheri ya mienendo yenye kudhahirisha mhifadhiko wa viumbe hai na maumbo yote katika mazingira ya utu. Uchafu huja kwa mawazo mabovu, ujinga na kasumba na hivi binadamu kwa asili ni kiumbe aliye katika uwanja wa mapambano. Silaha yake kuu ni nia yake safi na isiyo na mawaaa katika kila analoazimia kutenda—kuwa kwamba basi hilo lipate ile kadri ya kheri na kumuepusha yeye na mikosi. Hili lafanikishwa kwa yale mawazo safi yaliyorajisiwa katika saikia yake kwani hayo hujenga nguzo imara katika kukabili ujinga na mazoea mabovu. Na hivi binadamu daima aweza kusafisha maovu yake kwa kuitafuta ile nia safi yenye kuongoza katika usahihi wa katikati. Kufanya hivi basi, kutaisafisha njia yake na majaliwa yake kwa kadri ya stahiki ya usafi wake, asili ya makosa yake na 'msongo' wa wakati.

Basi viumbe vyote kimefanyikia kwa saikia za namna yake ambayo ndiyo msingi wa 'muumbiko' wake na mustakbhari katika madhahirisho na wakati. Lakini ipo tofauti moja ya muktadha mzima wa kiasili kwa saikia ya viumbe hai vyote. Hiyo hubainisha mfanyiko wa Saikia za vingine vyote kubakiza mwanadamu kwa ardhini na wale Pomboo; pia jamii za Nyangumi katika bahari. Wanyama, miti, mimea, wadudu, vijidudu na samaki huwa na 'Saikia mmeguko' ambayo ni sehemu ya Saikia ya mama Dunia. Naam, Dunia ni kiumbe hai na tena chenye namna ya ufahamu wa namna yake. Mwanadamu ni mwenye sonafi katika Saikia yake inayotawala na kuendesha hadhi ya utu wa jinsi moja moja. Wanyama, miti, mimea, wadudu, vijidudu na samaki huwa na 'saikia ya kimakundi' na tena 'kutawaliwa' na sonafi ya Dunia. Pomboo na jamii za Nyangumi hutawaliwa na saikia kama ilivyo kwa mwanadamu lakini ndani ya muktadha wa saikia pana yenye kutawaliwa na sonafi ya kipekee yenye kudra zenye kulingana na nyota za mbali.

Mhimili wa maumbo yote na mwendelezo wake ni shani ijayo kwa mapaji ya sonafi ambayo ni karama na pia neema ya 'Roho wa Uzima'. Basi ni kwa jinsi hii roho ndiyo yenye kuchakachua mienendo yote na kuipa kadri ya hesabu, mawiano na hadhi pale ambapo 'miale' na 'mawimbi ya uzima' vichakatapo ili kuchukua sura dhahiri. Kama ilivyo karama katika nuru, ndivyo ilivyo kudra katika mbegu za maumbo na muktadha wa madhahiriko katika kote penye mawimbi ya uzima. Miale na Mawimbi ipo pote na kote na hivi 'Roho wa Uzima' ni yote na mote. Na hivi basi si Yai na wala Kuku chenye kumtegemea mwenzake hasa; vyote viwili vinafanyika kwa muktadha wa cha tatu kisichodhahirika katika ulimwengu wa sura. Kunabahi ulimwengu wa maumbo pekee yake ndiyo kwaweza kupotosha ukweli wa jambo na mambo ijapohali ndiyo msingi wa utambuzi wa mwanadamu katika hali ya kawaida. Na pia hata vipimo na tathmini vyaweza kuleta kadiri ya 'mapengo' katika ukadirifu wa mabadiliko kimaumbo kwa kuwa katika mifumo ya viumbe hai kuna fizikia ya kwa nje na nyingine ya kwa ndani. Ni hii ya kwa ndani ambapo kile cha Tatu hufanya mhimili wa kuchakata na fizikia ya nje kwa tabia, hadhi na mabadiliko ya kimaumbo.

Fizikia ya kwa ndani ndiyo hutenda 'miujiza' ya kadri ile ya baiyoholojia ya kikwantumu. 'Tatu' ya Yai ni kadri ya chochote chenye kugawanyika katika mazaliano ama mazidishano ya kiuhai. Kanuni itawalayo uwezekano huu haitegemei hesabu wala kiasi chochote katika muktadha wa madhahiriko ya mapana ya maumbo ya uhai wenyewe ila tu kufanya usikronizi kwa 'uhitaji' na 'uweza' katika nguvu ya kuifanya sura ya kiumbe na hivi pia basi kuistahimilisha mienendo yake ili 'kuhifadhi' sura za madhahiriko na kustawi kwake ndani ya mawimbi ya uzima wote. Mawimbi ya uzima ni bahari isiyokuwa na mwisho na hivi hata tatu ya kiumbe ni 'chembe ya mbegu la fikara' katika mapana ya mabahari isiyokuwa na mwisho kwa jinsi ya kimafikara. 'Roho wa Uzima' ni yote na mote, na hivi maumbo yalidhahirika na yale yasiyodhahirikia hushududia muktadha kwa 'Kweli' yenye kuhusu kinachopata kuwepo. Basi ndiyo kwamba japo kwa jinsi ya majira na 'msongo wa wakati' vitu hubadilika kuwa kimoja hata kingine, kwa ndani kabisa kweli ni ile ile moja katika madhahiriso yote; ni utatu wa 'Mpango Mzima'--Yaliyodhahirika, Yasiyodhahirika yote katika 'Roho wa Uzima'. Ndivyo hivi kuwa 'Roho wa Uzima' ni Mwanzo na Mwisho kwa lolote lenye kutanabahiwa katika utumikivu wa akili ya kawaida ya mwanadamu. Kwani na yeye mwanadamu ni sehemu ya mpango mzima japo ni rahisi pia yeye kudhania vinginevyo. Katikati ya Yai na Kuku ndipo kuna siri isiyo ni kuku wala yai—hapo ndipo 'Kweli' huwa. Palipo Yai, kweli hufutika hilo Yai, na palipo kuku kweli hufutika huyo kuku. Na hivi ni katika ile nukta tu ya katikati ya magawanyo kamili ya kimaumbo na majira yake kamili ndipo siri za 'mawimbi ya uzima' na 'mbegu ya sura' za maumbo yaweza kung'amuliwa--kama vile pia katikati ya kuvuta na kutoa pumzi ama kutoa na kuvuta pumzi. Kadri hii huleta 'usufuri' kwa hatima ya 'vina' vya mienendo yote na maumbo.

Kusingelikuwepo na saikia, huu uhalisia wa maumbo ya kiuhai usingelikuwepo pia. Kwa maana maumbo hayawezi kuwa na ile kadiri ya kudhahirika na kutodhahirika kwa mifanano ila tu kwa muktadha wenye kuhifadhi migando ya sura na mienendo ya kuundika maumbo. Saikia ndiyo yenye kufungamanisha mawezekano ya kimaumbo pamoja na ufahamu wenye nia kwa kiumbe katika muktadha wa misukumo ya kiuhai ya bila ya kufundishwa. Kwa mfano utumbo katika mwili wa mwanadamu, huo haujapata kufundishwa na mtu na wala mazingira yake yenyewe ili kusukuma na kusharabu virutisho vile vitokanavyo na chakula ili viingie katika mikondo vya damu itiririkayo kuzunguka mwili mzima kufaa hitaji la viungo vingine vya mwili—toka siku kwanza seli za mwanzo za utumbo hujua 'wimbo' wa shughuli yake pale wakati uwadiapo. Kila seli ya uhai ina 'ujuzi-mbegu' wa jinsi yake kabisa.

Viumbe vyenye kufanyika kwa jinsi ya mkusanyiko wa seli kama mimea na wanyama pia wadudu huwa ni muktadha wa 'seli moja' isiyodhahiri yenye kustahimilisha sehemu ya muktadha wa zile seli zenye kudhahirika. Huu muktadha hukamilika kwa daraja la Saikia ya kiumbe kwa kuwa hii yaweza kuooana na sehemu ya saikia ya seli na kufanya 'saikia jumuizi' kwa kiumbe kilichovivaa viumbe. Ndivyo hivi basi akili ni chombo chenye utumikivu kwa viumbe hai vyote na kila kiumbe chenye kufanyika kwa mkusanyiko wa seli kina akili--iwe ni mmea, mnyama, mdudu ama samaki... Japo muktadha wa akili yenyewe ni wa kipekee kwa kila kimojawapo. Akili ya viumbe haifanyiki kwa chembe yoyote iliyodhahiri ila tu ule muktadha wa maumbo usiodhahirika moja kwa moja katika ulimwengu dhahiri.

Saikia ya kiumbe ndiyo hufanyika kwa mapana ya 'kukamata' kumbukumbu ili kufaa utumikivu wa 'ujitambuo'. Katika wanyama, mimea na wadudu kuna jinsi zake tofauti za kumbukumbu na hiyari kwa yale yaliyoingia katika kumbukumbu iliyo ni sehemu ya akili--iliyo ni sehemu ya Saikia. Sehemu ya tabia za mimea kama vile kufikia kile kituo cha ukuwakujia wa kuwa na miba ili kujilinda kutafunwa na wanyama ni mazao ya saikia jumuizi ya aina ya mimea yenyewe. Mimea kuwasiliana kwa kutoa gesi na kuchochea mabadiliko kwa ladha ya majani yake ili kuzua twiga asitafune majani yake machanga ni sehemu ya maendeleo ya saikia ya namna hiyo ya mimea ya miti. Vivyo hivyo huwa kwa yale majani ya maua yenye kula wadudu ama yale yenye kunywea yaguswapo. Pia ndiyo basi kusema ni mchanganyiko wa kudra na ukuwakujia kwa mimea yenyewe kama vile miwaridi ipatayo kuota katika tabia nchi ya ukavu na kufanya miba karibu na vikonyo vyake katika kulinda maua yake yenye harufu nzuri na fahari ya kipekee.

Kumbukumbu hufaa kusindikiza mabadiliko ya kisura ; hali kile chenye kutumia hiyo hubaki na kule kujiona kikiendelea kudumu kama kiumbe hai kimoja kisichofanyika kwa jinsi ile ya seli ndogo ndogo zenye kutokea na kufa katika majira mapana ya kipindi cha uhai wake. Saikia ya mwanadamu ina akili yenye kuzaa tafsiri ya kujitambua kama ni kuwa mtu na hali kumbe 'utu' ni muakisiko wa mapana ya minyororo ya madhahirisho ya hata chembe ndogo ndogo sana za kimaumbo katika tu hii kumbukumbu; na huku pia hayo yote kukirimika kwa neema ya ile nuru ya ufahamu na muktadha wa ufananio kwa lile 'Ua la utu' lisilodhahirika ila tu kwa 'mafikara-mbegu' katika 'Roho wa Uzima' na kuchakata kwa 'Wakati'.

Pasipo utumikivu wa kumbukumbu kila tukio daima lingalikuwa ni jipya pasipo 'ushawishi' kwa lile lililolitangulia. Nia isingalikuwepo-- na hivi hata 'maana iliyofichika' isingalikuwepo pia kwa yote. Wakati pia usingalikuwa, maana yoyote na wala shauri la 'Roho wa Uzima'.

Kutambua uthabiti wa maumbo ni shauri lililoandama daima wafikirifu katika vizazi vya wanadamu. Hata kwa wale Wayunani kabla ya zile siku za Socrates kulikuwepo na mashauri mbalimbali kuhusu kufanyika kwa uumbaji wote.

Ndipo tunamtazama mtu aliyefahamika kwa jina la Anaximander; aliyepata kuwepo takribani kati ya mwaka 619 mpaka 540 KK—Aliyepitia shule ya mwalimu na Mkuu aliyemtangulia aitwaye Thales; na yeye Anaximander katika siku zake kuwahesabu Anaximenes na Pythagoras miongoni mwa wanafunzi wake. Huyu huchukulika ni mtu wa kwanza kutoka kwa jamii ya wayunani kupata kuandika mashauri mbalimbali kwa muktadha wa kisomo chake kuwa risala kwa kuielezea asili-- kwa watu wengine kunakili na kusambaza ifaavyo. Kipindi alichoishi kilikuwa ni kati ya kile kipindi cha mapinduzi makubwa ya kiakili na kiufahamu na hivi kuakisika katika minajlili ya tawala na ustawi wa watu kote duniani. Hii basi ni kadri ya kipindi cha miaka 2500 nyuma; na sifa za makundi ya watu, makabila na mataifa yalipitia minyambuliko ya sura kama vile ilivyokuwa bayana huko katika bara la Asia katika nchi za Bara la Uchina, Bara Hindi, Irani, Mashariki ya Karibu na Uyunani ya Kale.

Anaximander alikuwa ni mpendekezaji wa Sayansi—mtu mwenye kutafuta msingi kwa mashauri yenye kudadavua mienendo ya asili. Na hivi yeye alikuwa ni mtu mwenye kutizama na kujaribu kulielezea jambo ama mambo; na hasa nyanja mbali mbali za ulimwengu dhahiri. Kutaka kwake kujua asili ya ulimwengu kulisukumwa na udhanifu kwa imani yake ya kuwa kila kitu katika ulimwengu dhahiri husukumwa na sheria kwa utaratibu fulani—kama ilivyo katika nazo jamii, chochote chenye kwenda kinyume kwa kutibua mizania ipasayo uhalisia wake hicho hakitadumu. Na kama ilivyo kwa wafikirifu wengine wa siku zake, kiu yao katika kupata kuyajua mambo iliwasukuma katika nidhamu ya visomo vya aina mbalimbali—mambo kama yale ya elimu ya Anga na Nyota ilivyo ndiyo kusema ni Unajimu; pia juu ya maumbo. Ndipo hapa pia neno 'fizikia' pia limetokana na lugha yenyewe ya kiyunani kumaanisha 'ma/umbo' ya asili--physis.

Kutokea kwenye Ngano za visa vya Miungu kama vile simulizi la tawala za mpangilio wa manyota na asili yake—kusema ni kosmogoni; kama ilivyokuwa ikichukulika katika Hesiod na Pherecydes; Zeusialikuja kukita mpangilio wake kwa kuwasambaritishia mbali wale ma-Titani waliokuwa wakitishia hali ya utulivu na uenda sambamba wa maumbo na mienendo yake katika Mbingu--yaani utangamano wake. Anaximander alikuwa ni mwenye kusisitiza ya kuwa mipangilio na mienendo ya maumbo si yenye kutawaliwa na nguvu ya jinsi ya mamlaka moja yenye kuamua kila kitu; bali maumbo yote hasa yana muktadha wa kijeometria na hivi basi kuwa na vitovu na njia zake mbalimbali katika kuchukua kwake sura na kudhahirika. Basi ndiyo kuwa akapata kutia msisitizo matukio yote ya nguvu za asili kama vile radi, pepo na mvua--vyaweza kuelezwa ama kutathminiwa kwa muktadha wa nguvu za asili iliyofanyika katika ulimwengu wa mazingira yake yenyewe pasipo na kutaliwa na 'miungu' kama ngano za zamani za wayunani zilivyoshuhudia picha ya maumbo, ulimwengu, mienendo na asili.

Vitovu na njia vinaweza kusakwa ili kudadavuliwa kimashauri kwa kile kitendo cha kujaribu kuitathmini mienendo na kanuni zake. Ndiyo basi husemwa pia Anaximander ni kati ya wanasayansi wa mwanzo kabisa walioamini muktadha wa vitendo ili kukamilisha uchunguzi na tena ndiyo kufanya kisomo juu ya jambo. Na yeye kupata kufanya hivyo na kuandika kumbukumbu la majaribio yake ambayo mengi hata hivyo yalipotea-- na hata katika zile siku za Plato na Aristotle karibia mashauri yake mengi yalikuwa yamekwisha sahaulika.

Ni katika muktadha wa jeometria ndipo basi Anaximander alidhanifu dunia kuwa ni kitovu kwa maumbo yote ya mbinguni na hivyo miili yote yenye kuonekana juu huzunguka dunia. Picha kamili kwa 'ukweli' ilikuwa ngumu kwake na hivi yeye aliishia katika kudhani dunia ni kama kopo la mviringo lenye uso wa juu wenye kufanywa na bahari na mabara ya watu halafu kimo chake ni theluthi ya kipenyo chake; miili yote huzunguka kwa chini ya kopo hili. Makadirio haya yalifanyika kukidhi kudadavua asili ya misimu na maonekano ya miili kama vile jua na mwezi. Basi muundo huu kuogelea katika mapana yasiyokuwa na kikomo na halafu ndiyo basi kutojishikiza kokote.

Katika kulitilia mkazo uhai wa mienendo ndivyo hivi Anaximander alijaribu kueleza asili na mwanzo wa yote kama mwenzake aliyemtangulia huku wote wakijitahidi kujinasua na mapokeo ya kingano. Hata hivyo yeye akijaribu kufuatisha maadhi ya viini vya mashauri yaliyotangulia. Ndimo hapa basi ile dhahania kwa dhana ya 'Aperioni' na Arkh ilivyokuja na kusababisha muktadha wa mashauri ya Anaximander.

Kwa kuwa mwalimu aliyekuwa akimtangulia, Thales, alikuwa ni mwenye kusema ulimwengu unaelea katika bahari ya maji isiyokuwa na kikomo basi yeye Anaximander akadhanifu ile dhana ya 'Apeironi' isiyokuwa na kikomo--akijibandua kutoka katika udhanifu wa maji kuwa ni asili ya kila kitu kilichokuja kuumbika na pia kuongeza dhahania ya 'Arkh' ili kuja kufafanua asili ya maumbo yote.

Ilikuwa ni nia yake kufungamanisha Aperioni na 'Arkh' ili kusudi Aperioni ionekane ni kama kitu-tobo kilicho ni kitovu kisicho tathminika ukatikati pake, basi hivyo kufananishwa na kina; na hali pia Aperioni yenyewe ni kubwa pasipo kikomo—kitu kama 'mwayo' wa uumbaji wote. Kuwa kwake Aperioni katika Arkh basi ni kufanya yote mawili kuwa ni moja la umilele na kadri isiyo na umri. Kusema hivi ndiyo kule kwenye kwenda sanjari na mashauri ya 'usivyokufa' na 'umuda' wa kile kisicho na kikomo.

Aperioni ni mhimili ambao arkh hutiririka kukirimu sura za maumbo na mienendo na hali ikikamilisha ile dhana ya kila kitu kilichofanyika hurudi katika jinsi yake ya kabla. Kilichofanyika kwa jinsi ya Udongo kurudi kuwa ni udongo tena. Basi kama vile waliomtanguliwa walivyopata kuzungumza maumbo kufanyika kwa 'elementi' nne za msingi zilizo na ardhi, maji, hewa na moto-- kosmogoni zote zilianza na kule kujaribu kutambua ni elementi ipi hasa ndiyo ilikuwa ya mwanzo. Thales alikuwa ni mwenye kusema maji; na Anaximander alikuwa ni mwenye kuzungumzia Arkh na Aperioni.

Mwanafunzi wa Anaximander aliyeitwa Anaximenes alikuja kuondoa 'ufumbo' wa Arkh kwa kusisitiza tabia tupu za zile elementi nne kwa kupita kwa wakati, hutosha kueleza mabadiliko ya sura na maumbo ya vitu vyote.

Ili kufanya sifa za kosmogni kuendana na maumbo yalivyofanyika na tena kutokana na zile asili za elementi; mashauri yaliyofuatia yaliegama katika tabia za elementi zenyewe kama kusema tabia zile za ubichi, ukavu, wepesi wa kushika moto na kupoa. Ndiyo hivi Anaximenes alikuja kupinga dhana ya huo mwanzo wenye kuanzia na maji na yeye kudai ni Hewa ndiyo iliyoanza... Kwa kuwa kutoka katika maji huwezi kupata moto kama lifanyikavyo jua; basi hewa yaweza kukidhi kueleza moto na vinginevyo katika huo mwanzo. Na yeye Anaximenes basi kuwa ni mtu wa awali aliyetumia ukaguzi wa mabadiliko ya hali na maumbo kama msingi wa kufafanua kweli za kimaumbo yenyewe katika kupita kwa muda—kama vile kuzungumza, mfano, maji kuwa kana kwamba ni matokeo ya mvuke--kusema ni hewa; uliokuja kupoa kutoka kwenye ile 'hali ya joto' kuja kwenye 'hali ya ubaridi'.

Ni Aristotle aliyekuja kufufua sehemu ya muktadha wa jitahada za Anaximander kwa kujitahadi kukadirisha picha za kimashauri yake na ule mwongozo kwa kukifanya kisomo chenye kuchambua maumbo na tabia za asili kwa msingi wa mtazamo wa kiuchunguzi-- kwa yale madogo madogo yenye kuja kuzaa mapana ya kisomo cha jinsi yake. Ili kukidhi haja yake ndiyo yeye akaleta shauri la 'sabustratamu' yaani 'maada ya msingi' kupunguza 'ufumbo' wa kile cha awali kilichopata kuitwa ni Arkh.

Aristotle alikuja kurasimisha neno 'Arche' kutoka katika neno 'Arkh' lenye kumaanisha mwanzo wa kitu—kule kitokako hicho kwa asili yake. Kulingana na kosmogoni ya kiyunani iliyotajwa kuja na simulizi laHesiod kutoka siku za kale za wayunani, na ndiyo ilifahamika kwa Anaximander na yeye Aristotle;arche ya yote ni 'mvurugiko'--'usosura' usio na kikomo. Ulitajwa huo na Hesiod kama 'mvurugiko manani' wa kimsingi kabisa ambao kutokana nao kila kitu kilikuja kutokeza kuwa na 'usura'. Hii ilielezwa kama tundu kubwa lisilo na mwisho—'mwayo shimo' ambako ni kwenye mizizi ya Dunia, Anga, Bahari na 'Tartarusi'. Katika kosmogoni ya ki-'Orfeusi' husimulika juu ya yule Kronosi asiyezeeka—kuwa alifanyiza 'Aither'--Aitha pamoja na 'Mvurugiko' na basi kulifanya Yai la rangi ya fedha kwa Aitha manani—ambalo kutokana nalo kila kitu kilikuja kutokea.

Na Aristotle ndiye alikuja kupendekeza vitu vyote ni jinsi moja ya kimaada ambayo katika mchanganyiko wake na 'hali' tofauti tofauti ndiyo huja kuzaa kadiri ya Ardhi, Maji, Hewa na Moto. Kama vile kusema: 'maada msingi' + joto joto + ukavu = moto, 'maada msingi' + 'joto joto' + ubichi ubichi = Hewa, 'maada msingi' + baridi + ubichi ubichi = Maji, 'maada msingi' + baridi + ukavu = Ardhi.

Japo Aristotle alikuwa ni mwenye kuvutia sana kwa ufundi wake wa kisomo chenye mantiki na kujaribu 'kuyalaza' mashauri yote katika mizania za kimantiki, yeye alikuwa akigusia tu mashauri yale juu ya mambo yasiyo dhahiri--'kutojisumbua' kudadavua mashauri ya hayo kwa mapana ama kina ; vile basi kama alivyopata kugusia udhanifu wake wa kuwa mbingu imepata kufanywa kwa 'elementi ya Tano'. Ile elementi ambayo Plato alipata kufundisha uwepo wake na yeye Aristotle kudokeza hivyo katika kazi yake ya 'Juu ya Mbingu'--Kuhusu kuumbika kwa Mbingu.

Katika siku za akina Aristotle na Plato kuna uwezekano wa mashauri yao mengi kuwa ni yenye kufanyika kutokana na ushawishi wa chini chini toka kwa majirani zao wa Kihindi na Waajemi; kulingana na yale yaliyokuwa yakizungumzwa na kuaminika na mapokeo ya hao.

Kutoka Bara Hindi kulipata kuwepo mapokeo ya kiveda. Kumbukumbu na rejea za kileo zinakadirisha Veda, kama makusanyiko ya tungo za maelezo kwa mambo ya kiroho, ilichipuka kati ya miaka 1500 hadi 500 KK; japo asili ya veda kiukweli yaweza kuwa zamani sana hata kupita hapo. 'Veda' inatafsiri ya 'Maarifa' na hasa yaliyotokana na ma-Rishi wa zamani katika Bara Hindi. Katika nyakati za zamani palipata kutokea wimbi la watu 'waliochanua' kiroho kama mchipuo wa uyoga mwingi juu ya ardhi katika Bara Hindi; mchanuo huu ulio ni epifani ama pia kusema ufunuo mananifu--ni kitendo cha mtu kufunguka kiroho na kuzama katika raha ya kuogelea katika 'mwili' mkuu wa uzima wa maumbo na nyenendo zote. Nyakati fulani zinazoshuhudiwa kupata kuwepo, wapo watu waliopata kuwa na epifanina kutokana yale yaliyowatokea na kufanyika bayana katika akili zao walijaribu kuwasilisha picha na maelezo ya yale yaliyowezekana--kuwasilisha mfananio wake kusudi wale ambao hawajapata ule ufunuo wapate kubaki na masimulizi ya kimwongozo. Wao waliongea katika lugha fulani yenye kushahibiana maneno fulani kama vile ule msisitizo wenye kujirudia sana juu ya 'Hiki' na 'Kile' katika kueleza uhusiano wa maumbo dhahiri machoni na ile 'Kweli' ya Uzima wake isiyoonekana kwa macho wala kusikika kwa masikio; vile vile hata mioyo ya watu haijapata 'kuonja' ladha ya utamu wa hisia zake juu ya yote. Lugha yao pia ilikuwa ni mchanyiko wa utenzi na ushairi kwa kuwa wao walikuwa ni watu wenye ufunuo wenye raha sana katika kuzama ndani ya 'kweli'.

Watu hao, ndiyo kusema marishi; japo walikuwa ni mtu mmoja mmoja na tena kila mtu kivyake vyake, baadhi ya yale waliyoyashuhudia kwa kuyaeleza kuhusu ulimwengu wa kiroho ilidhahirika kwa watu wa kipindi kile kushahibiana na kuonekana kama ni wenye kuzungumza lugha moja yenye uashirifu wa jambo kuu. Basi sehemu ya yale waliyokuwa wakiyatamka ama kuwakilisha kwa watu yalikuja kutunga mwili wa veda; mapokeo yalianza kwa mdomo na mbinu za kiuhifadhi ulio ni ukaririfu kiakili; na halafu kadri yalivyokutana na mwanzo wa kisomo cha maandishi, yakaja kunakiliwa na kutajwa miongoni mwa waandishi na wanakisomo kama 'samhita'--makusanyo ya tungo na semi kutoka kwa wale waliopata kujua na kuishuhudia 'Kweli'. Pia mwongozo kwa wasiofahamu ili wapate kufahamu mambo makuu kuhusu ulimwengu na neema istawishayo watu na kuleta taratibu za kiutamaduni na zaidi ili kuwa hao wenye kupokea hayo waweze kufuatisha maarifa yenye kupelekea jamii kwenye mwangaza na kheri.

Lugha iliyotawala katika siku za Marishi ni lugha ya kisanskriti; na ndiyo lugha ambayo kisomo cha siku zile kilijisheheneza umashuhuri wake kimatumizi. Na pia ndiyo lugha iliyopata kuwa na ushawishi na tena mama hata kwa lugha nyingi za leo za Ulaya na Asia—kama ilivyo leo kwa lugha ya kiingereza kutawala visomo na matanuko yake kwa nguvu ya ushawishi; kilatini pia kimewahi pia kuwa ni lugha ya visomo miongoni mwa wanavisomo... Lakini kisanskriti kilipata kuwa na mfano kama huu hapo siku za zamani sana. Na ndiyo hivi hata kuna maneno mengi ya kiingereza, yananyoosha mkondo wake hado kwenye asili ya maneno ya kisanskriti. Vivyo hivyo kwa lugha nyingi za ulaya kiasi kwamba inaleta udhanio wa kuwa sehemu kubwa ya watu wa makabila ya ulaya huwenda wamewahi kupata kuwa sehemu ya Bara Hindi au ndiyo kusema wana asili ya kupata kuchangamana wa watu kutoka huko ama hata kutokea huko.

Kwa asili mapokeo ya kiveda yanaangukia katika namna ya makundi manne makubwa yaliyo ni mikusanyo ya 1. Rigveda, 2. Yarjuveda, 3. Samaveda na 4. Atharvaveda. Haya yote hufanya sehemu muhimu wa ustawi na ustaarabu wa Kihindu. Yalijitokesha na kushamiri tangu miaka maelfu kabla ya kuzaliwa kwa Yesu aiitwaye pia kristu kule mashariki ya kati. Hapo awali kabisa mwili wa mapokeo ya kiveda ulihifadhika kwa mafunzo ya kukariri na kughani katika mitindo maalum yenye kuweza kuhakiki uhifadhiko wa tenzi na habari zibebazwo. Na hayo makundi manne tofauti yalikuwa yakiendana na taratibu maalum za kuhusisha utumiko wa utenzi wa kiveda. Toka siku za zamani, Veda husemwa ni zao lililotokana na kazi isiyo ya mwanadamu peke yake yaani apauruseya; miongoni mwa Wahindu. Husemwa ya kuwa Veda ilikuja kwa 'kusikika' ndani ya watu walioipokea na kutamka kwa maneno kusudi na wengine wapate kufaidika; hili hutajwa kama ni sruti(kisanskriti, pia 'shruti')—'kilichosikika' miongoni mwa Wahindu. Kipindi cha baadaye kazi hizo za mapokeo zilipoanza kunakiliwa katika mtindo wa maandishi ndipo hizo kazi zikaitwa smriti--'Kilichokumbukwa'. Na hivyo jamii ya Wahindu walihusisha Veda na matendo yao makuu ya kiimani, ustawi na ustaarabu.

Rigveda, inayokubalika kutangulia makundi mengine yote ya makusanyo ya kiveda; hukadiriwa kuchipua miaka ya takribani 1500 KK. Hii ni ya kwanza kwa msingi wa 'utatu wa sayansi' iliyofanyika takatifu kwa Wahindu—trayi vidya; na hivi Rigveda ilikuwa ni mapokeo kwa makuhani wa juu wa Kihindu kwa ajili ya mwongozo wa utaratibu mzima wa ibada za Kihindu. Ndani ya tenzi zake kulikuwa na mantra zenye vina maalum vya kitenzi kwa ajili ay kughaniwa kwa sauti katika kusifu 'Brahma'--roho kuu ya uumbaji wote katika sura ya unafsi. Yarjuveda ni mkusanyiko wa tenzi zilizo/zinazoghaniwa kwa sauti ya chini chini katika shughuli za kufanya sadaka za matoleo kwa Brahma. Samaveda hubeba ndani yake tenzi zilizo ni mapambio yenye kuimbwa katika sherehe za ibada kwa Brahma.

Atharvaveda ilikuwa ni mkusanyiko wa mawaidha yenye sura ya tenzi zenye vina na mizani ama vinginevyo kawaida yenye kukazia maana kwa namna za makundi mengine ya Kiveda. Pia ndani yake kulikuwa kunamafunzo ya siri yenye kuweza kuleta uwezo wa kiganga, uwezo wa kuponya maradhi na hata kudhuru wengine walio ni maadui kiakili ama hata kusababisha madhara katika mazingira yenye kuweza kukusudiwa. Na hivi Atharvaveda hubakia ni mapokeo yenye kukanganya maana yake hasa kwa kuwa umuhimu wake kuchukua sura tofauti kwa watu tofauti. Mengine yapatikanayo katika Atharvaveda kuchukuliwa kuwa ni ya zamani labda hata kutangulia Rigveda ama tuseme yalianza sambamba na kujitokeza kwa Rigveda. Na kwa sehemu kubwa ni ujuzi wa kunuia mambo, kughani maneno yenye nguvu za kimazingara, kukinga mtu dhidi ya mapepo, kufukuza maradhi, kuapiza madhara, kufanikishia matakwa ya kimatamanio, kujitakia maisha marefu n.k.

Upande wa kiufundi wa maarifa ya kiveda, ufahamikayo kama Upaveda, ndiyo umeleta ufundi na ujuzi kwa mambo kama vile sayansi ya utabibu ifahamikayo kama Ayurveda. Hii imetokana na Rigveda japo imetanabahika kuingilia na Atharvaveda nyakati zingine. Kutokana na Yarjuveda kulikuja kuwa naDhanurveda—sanaa ya kutumia silaha za Upinde wa mshale. Kutokana na Samaveda kulikuja kuwa na uchezaji muziki uliotambulika ni mtakatifu—Gandharvaveda. Kutokana na Atharvaveda kulikuja kuwa na Shastrashastra.

Ni muhimu kutazama kisomo cha Veda ili kuelewa chimbuko la mambo kama Sthapatyaveda—ubunifu wa sura za majengo, kama ilivyotumika kwa mahekalu na nyumba za kuishi kwa wale waliomudu kuunda; Shilpa—sanaa za mikono ambavyo huwekwa katika Upaveda kwa Atharvaveda. Hayo yote hufanya Veda nne mashuhuri tokea siku za zamani na mapokeo mengine kama Mahabarata,Natyasastra na Puruna kadhaa kupewa jina la pamoja kama Veda za Tano. Na hapo hapo mapokeo kama Bhagavad Gita – 'Wimbo wa aliyebarikika' (Mkasa wa shujaa wa mapambano Arjuna na Krishna Mkuu katika kuiyaingia mapambano ya kivita ya mahala palipoitwa Kuruksetra; palipokuwa ni mahala pa kuhiji pia—Dhamaksetrah) na Vedanta—ukomofu wa veda kwa utimilifu wa kupokea mashauri kutoka kwa wale wenye kuhuisha maana yake kutokana na kutaamulika kwao--Kwa wengine miongoni mwa waumini wa Kihindu pia huchukulika ni sehemu ya Veda kwa nyakati zote.

Lakini kubwa katika kudadavua mapokeo ya veda ni kutambua umashauri wake ambao hapana shaka ulikuja kuathiri hadhi ya sifa na tabia kwa uwezekano wa mapokeo mengine yenye kuja kutokea na kuweza kuunda hata hadhi ya 'dini' ndani na nje ya mipaka ya India. Jinsi yake ya uandishi na ushairi, uhifadhi wake, maudhui na visa vyake vimedondolewa ama kujitokeza tena katika mapokeo na muundo wa dini zingine hata magharibi ya India, naam, Arabuni na mashariki ya kati. Kuna wakati veda ilikuwa ndiyo kisomo chenye umashuhuri mkuu katika nyanja za usomi na uanazuoni ambapo wale wenye kujihusisha na visomo vyake walionekana ni mastadi na watu wa upeo—watu wa vitabu. Kulikuwa na watu wengi tu waliopata kujitokeza kaandika mawaidha ya kina juu ya veda katika kudhihirisha umahiri ama upeo katika kutambua mashauri yajayo na mapokeo ya veda.

Labda ni India tu ambapo utamaduni wa mapokeo ya 'kinadharia' daima yamechuana sambamba na mapokeo ya moja kwa moja ya kutoka kwa wale walioitambua na kuiishi kweli wakati hata wakati. Ni katika hili ndio Vedanta ilikuja kujitokeza kama ukamilisho wa veda kulingana na jitihada za wale waliobaini kweli fulani na toka kwenye ile kweli kujaribu kuzungumzia veda kwa sura bora na yenye msingi imara siyo mapokeo tu ya mdomo ama maandishi. Pia ndiyo kuendeleza utamaduni waUpanishad... Yale ambayo watu walijifunza miguuni pa waliotaamulika ama kufunguka kiakili. Ndiyo hivi waliopata kutokea kwenye hata jamii za Kihindu kama Gautama Buddha aliyefahamika awali kama Siddhartha Mshakya; waliweza kufundisha mafundisho mapya yaliyotegemeana na kufunguka kwa fahamu zao na ufahamu wa yote. Tokea kwake yalikuja mapokeo ya U-Buddha yaliyojikita katika mtindo wenye kufahamika toka siku zake kama njia ya Buddha—dhammapada. Hii ni kuweka alama juu ya tofauti ya mapokeo ya kifikra yanayoridhiwa kama habari tupu; kuyatofautisha na yale mapokeo yanayolenga kumletea mtu mwongozo katika njia ya mabadiliko halisi ili kweli aishuhudiayo mtu kuwa ni moja na kweli aliyofanyikia upya mtu mwenyewe. Si Buddha pekee yake aliyefundisha mafunzo ya mabadiliko ya moja kwa moja ya kiutu; wapo wengine wengi walifanya hivyo hivyo kwa namna zao za kipekee na huku wengine wakikumbukwa na wengine kuwa kana wameshahaulika. Wapo walimu na wanasayansi wa zamani kama yule mwalimu mkuu wa Yoga Hatha, Patanjali, aliyefundisha mbinu za mikao, utulivu na ukimya wa kiakili na kimwili vinavyoweza kuleta utangamano wenye kutaamulisha akili ya mtu hata kuinukia na kufika katika ufahamu wa 'Kweli' na 'Nguvu' iliyofanyikia ulimwengu wote... Yupo Krishna aliyefundisha Yoga Bhakti—Yoga ya wanaojitoa moyo wote kwa Kweli ya Krishna iliyo ni Kweli ya ulimwengu wote mzima katika fahari yake iliyofichika mbele za macho ya watu waliokosa mwongozo ili kuona; na hivi kupitia Yoga Bhakti wanaweza kufunguka na kuwa moja na hiyo... Japo mafundisho ya Buddha ndiyo yamekuja kutawala sehemu mbali mbali za India na nje ya mipaka yake na huku yakionekana kuchepuka kutoka kwenye mapokeo ya awali ya kihindu na utamaduni mzima wa kiveda. Na haya pia kuwa mahususi kwa wale wenye kupenda na kutaka kuongoka hadi katika 'Kweli' iliyo ni muktadha wa Ufahamu mkuu wa Hekima na Huruma juu ya masumbuko ya mwanadamu katika zama zote anazoishi na ujinga wa kutotambua asili ya 'Buddha' ndani yao wenyewe...

Haya yote ni mwaliko wa kuingia katika kutambua kuwa daima kumekuwa na misimamo ya aina mbili katika kushika nia juu ya mtu kufuata mkondo wa 'mafundisho' matupu ama mafundisho yaliyo ni taa yenye kumuongoza mtu katika hata ile kweli itakayommeza yeye mzima mzima na kumwezesha yeye kuzaliwa mara ya pili katika 'Kweli'. Ni sehemu ya hili la pili ambapo Plato na baadhi ya wanafilosofia wakiyunani walikuwa wakilitambua lakini walijua hakuna 'lugha' hasa ya kueleza ufasaha wa yote yanayodhahirika. Ilikuwa ni jitihada yao kujaribu kudadavua mashauri ya watu na ustaarabu wao katika kuingiliana na lile 'lisiloelezeka'. Kwa hilo ambalo halielezeki wao walijaribu kutambua kanuni na taratibu zinazoongoza yote yafanyikayo; japo wapo ambao walianza kutotea kwa ujumla katika mashauri ya kueleza 'siri' za ulimwengu wa maumbo na 'asili' yake. Ndivyo falsafa ilivyozaliwa japo hata kwa wayunani si kuwa ndiko pekee jitihada kama hizo zimepata kufanyika... Kutoka Bara Hindi kumepata kuwa na jitihada kama za wayunani hata kipindi kirefu kabla ya siku za akina Plato na Aristotle.

Tutaendelea kuchambua mengine katika kisomo rasmi cha utatu na wawezekano ya kuupangilia upya ustawi na tamaduni za watu ili kuendana na visomo vya leo na mawezekano ya neema zaidi.
 
nimesoma mada hii kwa 20% tuu! bahati mbaya zaidi hata sijaelewa ulikua ukimaanisha nini,labda kwakua siku soma yote. lakini niulize tuu hizo nukuu umezitoka katika kitabu gani? ingawa maana hazipo mbali na biblia lakini nitofauti mno na tulio izoea
 
nimesoma mada hii kwa 20% tuu! bahati mbaya zaidi hata sijaelewa ulikua ukimaanisha nini,labda kwakua siku soma yote. lakini niulize tuu hizo nukuu umezitoka katika kitabu gani? ingawa maana hazipo mbali na biblia lakini nitofauti mno na tulio izoea
 
nimesoma mada hii kwa 20% tuu! bahati mbaya zaidi hata sijaelewa ulikua ukimaanisha nini,labda kwakua siku soma yote. lakini niulize tuu hizo nukuu umezitoka katika kitabu gani? ingawa maana hazipo mbali na biblia lakini nitofauti mno na tulio izoea
 
Yaani mkuu mose sijui niseme nini!? Hahaaa!!
Au kama unaweza kuwa una summarize basi tungeshukuru zaidi!!

Na mimi naomba kuuliza, unaishi hapa hapa Tanzania mkuu!?
 
Always mimi ni mwanafunzi wako mtiifu kwa hizi mada ngumu na fikirishi..kila kipengele ni madini tupu
 
Ah tushukuru; naona kumbe utangulizi uliopo kwenye tundiko la kwanza unahusika...

mpatto, haya yawakiwakilishwayo humo si 'tasnifu' kusema labda 'dhahania' ama 'habari kwa ufupi -- muhtasari' kuhusika; bali ni mitazamo juu ya picha na mapana ya tafsiri ya mambo. Shughuli ya namna hii huwa haina mwanzo wala mwisho.... Ni kuchagua neno na kumulika neno, hivyo wewe ndiyo unakupasa uchague lipi la kuangalia, lipi la kuacha, lipi la kuja kurejea n.k.

Maarifa na hekima ni mambo ya stahere... Wenye kuyafaidi haya walau ni wenye silika ya kutulia, kusikilizia, kuwa wazi kupokea, kutoona wamebanwa na tena wenye kujiachia mazima panapo fursa na mbaraka.

Wakati si chochote katika kuitafuta kweli, roho ya utambuzi daima itakuhakikishia kila jambo na wakati wake na tena ukistahili kujua neno basi utaongozwa kulijua -- wakati sahihi kulijua; si kwa kulazimika kujipangia. JIweke tayari wakati wote, mengine yatakaa sawa.

Hmmm

 
Ah tushukuru; naona kumbe utangulizi uliopo kwenye tundiko la kwanza unahusika...

mpatto, haya yawakiwakilishwayo humo si 'tasnifu' kusema labda 'dhahania' ama 'habari kwa ufupi -- muhtasari' kuhusika; bali ni mitazamo juu ya picha na mapana ya tafsiri ya mambo. Shughuli ya namna hii huwa haina mwanzo wala mwisho.... Ni kuchagua neno na kumulika neno, hivyo wewe ndiyo unakupasa uchague lipi la kuangalia, lipi la kuacha, lipi la kuja kurejea n.k.

Maarifa na hekima ni mambo ya stahere... Wenye kuyafaidi haya walau ni wenye silika ya kutulia, kusikilizia, kuwa wazi kupokea, kutoona wamebanwa na tena wenye kujiachia mazima panapo fursa na mbaraka.

Wakati si chochote katika kuitafuta kweli, roho ya utambuzi daima itakuhakikishia kila jambo na wakati wake na tena ukistahili kujua neno basi utaongozwa kulijua -- wakati sahihi kulijua; si kwa kulazimika kujipangia. JIweke tayari wakati wote, mengine yatakaa sawa.

Hmmm

Sawasawa kiongozi, nakuaminia mno!! Pamoja sana!!
 
Back
Top Bottom