Fukwe (Beach) za Tanzania na hatma yake

Big up Mr Prime minister!sioni haja kubinafisisha Coco Beach!du sasa tutakosa hata sehemu ya kwenda "kujirecreanisha"
 
Pinda Safi sanaaaa kwa uamuzi wako huu!, haya ndo mambo tunayoyataka, ninaunga mkono hatua yako ya kuzuia uuzwaji wa Coco Beach. kwa kweli lile eneo ni eneo ambalo wananchi wanalitumia kwa ajili ya kujiburudisha kwa upepo mwanana, na kufurahia mandhari nzuri ya bahari Tuliyojaaliwa na mwenyezi Mungu, kumuuzia mtu eneo lile kisha awatoze wananchi kiingilio kwa kweli ilikuwa ni dhulma.
 
Hii hatua nzuri lakini mimi nina wasi wasiwasi na wanasiasa kuingilia maamuzi ya manispaa au wilaya kufanya maamuzi yao

Surely wilaya ya Kinondoni wanao jopo la wanamazingira, jamaa wa planning permission,jamaa wa mipango miji na bila kusahau watu wa city council..pamoja na raia wa kawaida ambao wanaweza hujadili mambo haya kabla ya kufanyika maamuzi

sasa naona hapa Pinda anapata credit za bure wakati hii ilikuwa ni straight forward case...

kinachonitisha kama kesho kutakuwa na jambo la muhimu zaidi wanasiasa wakaingilia tutasemaje?
 

“Eti wanasema wanaipendezesha. Nauliza wanaipendezesha kwa ajili ya nani? Mnataka kupambana na jamii… kwa kuwa imeamka na haiko tayari kukubali hilo, nyie watu wa Kinondoni hamna la kufanya?” ...

“Hiyo ni Beach, iacheni hivyo hivyo, tafuteni ‘mabeach’ mengine kama vile Rufiji mkajenge.”
Mtoto wa Mkulima ame come through. LOL!

Mpaka Pinda anamu upstage Kikwete! Ataanza kum-maindi. Watch it!
 


“Kila mwaka zitolewe sh bilioni 10 kwa ajili ya mkoa huu, sh bilioni tatu kwa ajili ya kukarabati mifereji na sh bilioni sita kwa ajili ya kufungua barabara kama ile ya Mabibo, Mburahati hadi Kigogo, ili kupunguza msongamano,” alisema Pinda.

[

3 + 6 = 10 !

Pinda shukran kwa kutetea wananchi, na shukran zaidi kwa kuwapa wawekezaji alternative ya kwenda Rufiji. Wasirukie tu vinavyoelea,wajue vimeundwa.
 
Hii hatua nzuri lakini mimi nina wasi wasiwasi na wanasiasa kuingilia maamuzi ya manispaa au wilaya kufanya maamuzi yao

Surely wilaya ya Kinondoni wanao jopo la wanamazingira, jamaa wa planning permission,jamaa wa mipango miji na bila kusahau watu wa city council..pamoja na raia wa kawaida ambao wanaweza hujadili mambo haya kabla ya kufanyika maamuzi

sasa naona hapa Pinda anapata credit za bure wakati hii ilikuwa ni straight forward case...

kinachonitisha kama kesho kutakuwa na jambo la muhimu zaidi wanasiasa wakaingilia tutasemaje?

Ungewangojea hao wa manispaa mpaka 'hell freezes over' na wasingefanya kitu. Madiwani nao ni wanasiasa na watendaji wa huko wamekubuhu kwa kupindisha sheria! Huu mpira wa coco beach ulianza kuchezwa tangu wakati Kitwana Kondo akiwa meya na bado hawajakata tamaa! Kwa mawazo yangu, kama kuingilia kwenyewe ndiyo huku, mwache aingilie!

Amandla!
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amepiga marufuku uamuzi wa Manispaa ya Kinondoni kuuza kwa mfanyabiashara mmoja maarufu eneo la ufukwe la Coco Beach.

Pinda alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na madiwani wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Karimjee, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya habari kuhusu uamuzi huo unaoonekana kupigwa danadana na kufanywa kwa siri kuvuja na kuandikwa katika vyombo vya habari.

Alisema Jiji la Dar es Salaam limekumbwa na tatizo la migogoro ya viwanja ambalo kimsingi limesababisha kuibuka kwa manung’uniko ya watu kila mara.

“Tatizo la migogoro ya viwanja Dar es Salaam ni kubwa, siku za karibuni tumesikia uuzwaji wa Coco Beach uliofanywa na Manispaa ya Kinondoni. Tumeanza kusikia minong’ono katika hiyo beach. Huyo anayejenga mwambieni ajenge, kwa kuwa kila atakapojenga watu watabomoa.

“Eti wanasema wanaipendezesha. Nauliza wanaipendezesha kwa ajili ya nani? Mnataka kupambana na jamii… kwa kuwa imeamka na haiko tayari kukubali hilo, nyie watu wa Kinondoni hamna la kufanya?” alihoji Waziri Pinda na kuongeza: “Hiyo ni Beach, iacheni hivyo hivyo, tafuteni ‘mabeach’ mengine kama vile Rufiji mkajenge.” Alisema kutokana na umuhimu wa Dar es Salaam na dhamira ya serikali ya kutaka ionekane kuwa ni kioo cha nchi, katika mwaka ujao wa fedha serikali imetenga sh bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha miundombinu.

“Kwa nafasi ya Jiji la Dar es Salaam, lazima tufike mahali tuishawishi serikali, ili kuwekwe mfumo wa kuiangalia kwa jicho la tofauti na miaka mingine.

“Kila mwaka zitolewe sh bilioni 10 kwa ajili ya mkoa huu, sh bilioni tatu kwa ajili ya kukarabati mifereji na sh bilioni sita kwa ajili ya kufungua barabara kama ile ya Mabibo, Mburahati hadi Kigogo, ili kupunguza msongamano,” alisema Pinda.

Aliongeza kuwa, Dar es Salaam ndiyo kioo cha taifa, kwa kuwa ndiyo makao makuu ambapo kuna bandari, uwanja wa ndege wa kimataifa na pia ndiyo chanzo cha treni ya kwenda maeneo mbalimbali nchini.

Katika maelezo yake, Waziri Mkuu alitoa agizo la kuhakikisha wamachinga wote waliopo katika maeneo yasiyoruhusiwa wanaondolewa na kuwekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa kazi hiyo.

“Chonde chonde Mkuu wa Mkoa, lazima tujitahidi tuwe na nidhamu. Hawa wamachinga wanatakiwa wawe katika maeneo waliyotengewa, kwani nimeona hali ya wamachinga imeaanza kurudi. Tusiwaruhusu wakarudi barabarani,” alisema Pinda.

Pia alisisitiza suala la usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam, na kumtaka kila mwananchi katika mtaa wake kujitahidi kuboresha usafi, kwani uchafu unachangia kuzorotesha manispaa kuweza kutoa huduma bora.

Alizitaka manispaa kuvuta kamba ili kuhakikisha suala la kukusanya uchafu linafanywa kwa umakini.

Pia aliagiza manispaa kuzingatia utoaji wa leseni za muziki na vileo kwa watu ambao hawajapewa, na kuwaonya wenye leseni wazingatie taratibu na sheria za leseni walizopatiwa.




juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 10 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hapo Pindisha kula tano, ila tu isiwe ni mbio za sakafuni na jeuri/nguvu ya soda. Maana hamkawii kupindisha

na kukuz , singapore, - 29.05.08 @ 10:01 | #13918

Kwanza kabisa nakupa pongezi Mh. Pinda kwa kuzuia uuzwaji wa Coco Beach. jambo lingine ni kuhusu Jiji la DSM, tatizo kubwa Viongozi wenye dhamana ya kusimamia Jiji hili ni kutokuwa na Vision ya namna gani Jiji hili linapaswa kuwa, na ndio utaona wakati zinafanyika jitihada za kuliboresha bado kuna mambo ya hovyo yanazuka siku hata siku kwa mfano bado ujenzi holela unaendelea kufanyika sio tu pembezoni mwa Jiji hata katikati ya jiji pia.Na huku uswahilini Sheria hazizingatiwi kabisa kwa mfano wenye hizo zinazoitwa Bar (kwa hakika ni Groceries) wanapiga muziki kwa sauti kubwa kabisa kiasi kwamba kunakuwa hakuna kabisa utulivu na wenye dhamana hawachukui hatua yoyote.

na A.S. Mbweni, DSM, - 29.05.08 @ 10:27 | #14021

Hapo Mh.Pinda afadhali umesema ukweli hakuna kuuza na tena akijenga bomoa kama masaki na hakuna fidia. Ili waelewe serikali ina mkono mrefu.

Hapa naendelea kuunga mkono kauli ya Mh. Mkono kwamba haya mambo ya kuuza viwanja mara mbili au maeneo ya wazi wanasambabishwa na elimu mbovu inayoeleta mtazamo finyu juu ya mipango miji. Wataalum wetu je huo sio wakati wakupanua Bunju ,Boko, Mbagala na kigamboni hapo city pabaki hivyo ukiweka usafiri mzuri tena wa usalama wa kufika Bunju na Boko kupitia kwenye bahari na huku kigamboni ukaweka Daraja unafikiri kuna mtu ataagalia hako kacity kwa mtazamo finyu. Hebu tafuteni miradi mkubwa ya kupanua jiji tuacha kuinga wote mjini kwa wakati mmoja na kutoka kwa wakati moja. Kazi kwenu watu wa mipango miji kama kweli mlisoma au kuchugulia mithani pale Ardhi Institute.

na linambasha, Hongkong, - 29.05.08 @ 10:38 | #14026

HIVI NA SWALA LA ROSE GARDEN LIMEISHIA WAPI WAKATI ILE BAR INAJULIKANA KABISA HATA NA MTOTO MDOGO KABISA IKO KATIKA ENEO LA BARABARA????MADIWANI MANFANYA NINI NA MKUU WA MKOA MPO AU MLEWESHWA NA BIA ZA ROSE GARDEN MNASHINDWA KUFATA SHERIA YA MIPANGO MJI??????????????****** ZENU

na munir, dar, - 29.05.08 @ 08:07 | #14036

Nimeshaona kuwa waziri mkuu,amewaona hawa watu wa halmashauri ,niwahuni na ma fi sa di wa haliya juu.Ameamua kiukwe.Na asikomee hapo awafuatilie kuona undai, nilazima watu wa halmashauri wamepewa hongo.Tumechoshwa kusoma taaria za mambo ya halmashauri ,mara kubomoa mara hamishahamisha.Watu wanaishi kama wako kwa makaburu.Maana hujui halmashauri kesho itaropoka nini.Heko Mh WAZIRI MKUU KWA KUWASAIDIA WNYONGE.

na mtzmwenyeuchungu, tz, - 29.05.08 @ 08:27 | #14044

Andikeni majina yenu halisi ili hoja zenu zifanyiwe kazi! tumielewana akina mtzmwenyeuchungu na wenzako!

na mhariri, tanzania, - 29.05.08 @ 09:08 | #14058

kinachotakiwa humu ni hoja na siyo kujua ni nani kaandika, utawajua watu wote wewe? au unataka kuwafanya nini?


na mwenzake na mtzmwenye uchungu, dar, - 29.05.08 @ 09:34 | #14065

Mhe MIZENGO KAYANZA PINDA kama nilivyosema ni chaguo letu wote mungu
amlinde na na mafisadi na atashinda tu
na mimi nipo nyuma yake

na Daniel mugassa, DAR/Tanzania, - 29.05.08 @ 09:42 | #14069

oooh sawa waandishi wa habari muwe wabunifu katika kutatua matatizo ya miji yetu. asilmia kubwa ya matatizo ya Dar es salaam yanatokana na mfumo mbovu wa utwala wa ardhi.

kinondoni wanaongoza kwa rushwa hasa kitengo cha ardhi. kwa nini waandishi hamjafanya uchambuzi wa haya na kuyaweka bayana. Hebu sasa mufanye hivyo na hapo mtakuwa mmesaidia maeneleo ya jiji
letu.

na emanan, germany, - 29.05.08 @ 09:47 | #14071

Dar es Salaam ni Tanzania hii hii. Maamuzi mazuri na ya haraka kama haya yafanyike sehemu zote kuliko na migogoro kama huu wa Dar.

Tunategemea leo au kesho waziri wetu utatoa tena maamuzi kama haya kuhusiana na uwanja wa Nyamagana kule Mwanza. Wananchi hawataki uuzwe na wana sababu nzuri tu wameshazisema,viongozi hawataki kusikia. Wanasubiri mpaka damu imwagike ndiyo waje kukubaliana nao!

Viongozi wanawajibika kwa wananchi. Hivi hawa viongozi wa Mwanza wanawajibika kwa nani? Wakome kutuburuza wananchi maana sie ndiyo tumewafikisha hapo walipo.Watusikilize basi na watambue nasi tuna uelewa wa kutosha pengine hata kuwazidi wao.

Viongozi tujifunze kuwasikiliza wananchi hata walio chini!

na Pius - 29.05.08 @ 10:18 | #14080
[

FONT YAKO DUH!!! inakatisha tamaaa....
 
Worry not, tutaonana nao time ikifika.

Mwanahalisi Tafadhali, kichwa chako cha habari kinatisha.
kusema kuwa ni "Laana kwa watanzania". duh ni maneno makali mno na yanatisha ndugu yangu, kwani laana si kitu cha mchezo.

nikirudi katika mada:
nikikumbuka jinsi nilivyokuwa nikiburudika katika ufukwe wa coco beach hususan kila weekend, roho inaniuma iwapo zitachukuliwa hatua zozote za kuwafanya wananchi wasiendelee kuburudika bure katika ufukwe ule. kipindi cha sikukuu kama eid na christmass coco beach ni kimbilio la wananchi kupata burudani ya upepo mwanana na pia kuogelea.
kumkodisha mtu ufukwe wa Coco beach ni dhahiri kumpa mtu tiketi ya kujichukulia pesa za bure kwa wale watakao taka kwenda pale kuburudika. kama ni maji ya bahari ni maji ya asili, upepo ni upepo wa asili, mchanga ni mchanga wa asili, sasa iweje mtu apewe haki ya kuvuna pesa za bure kwa kutumia vitu vya asili?. kama ni kujenga mahoteli au huduma yeyote atakayoingiza juhudi na maarifa basi hivyo ndo vinatakiwa kutozwa pesa lakini si ufukwe na maji yake.

mimi ninasema hivi !.iwapo ukodishwaji wa huo ufukwe utasababisha wananchi wasiutumie ufukwe free of charge, basi huyo aliyekodisha ufukwe na mamlaka iliyoukodisha huo ufukwe wakae sawa muda muafaka ukifika tutakwenda mahakamani kudai ufukwe wetu. haiwezekani kupelekwa pelekwa namna hii, hapa niko niko serious!.
Time will tell
 
Mie nilisema, watauza kila kitu... hata Ikulu....

Iko siku tutajikuta hata nchi imeuzwa, bila ya sisi wenye nchi kujua. Tutakuwa manamba na watumwa, upyaaaaaaaaaaa!

Ufisadi huu utatumaliza! Haiwezekani jamani! Watoto wetu wataenda wapi kucheza? Tuanzishe private beach ili iweje? Kwa nini tusiandamane kupinga jambo hili? Kwa nini Watanzania tunawaogopa wafisadi namna hii? Mie nikisema tuandamane wengine wataniona hamnazo! Kha!

This is too much! Watoto wetu watarithi nini? Au ndio watakuwa wafagizi na counter clerks kwenye ma-shoprite? Kazi zote za ofisini, kuanzia Serikali hadi Parastatals, Benki, nk, zichukuliwe na wageni? Kwani hata hizo "academic" si ni za watoto wa matajiri tu?

Tunajenga nchi yenye matabaka ya aina gani?

./Mwana wa Haki
 
3 + 6 = 10 !

Pinda shukran kwa kutetea wananchi, na shukran zaidi kwa kuwapa wawekezaji alternative ya kwenda Rufiji. Wasirukie tu vinavyoelea,wajue vimeundwa.

Kwa Bongo nadhani hiyo hesabu ya bilioni 3+6=bilioni 10 ipo na inakubalika kabisa bila tatizo..Hako kabilioni kamoja kameachwa kanaelea-elea tu..Nyani Ngabu anasema ndivyo tulivyo!
 
Waziri mkuu kanifurahisha na sana na hili la kuzuia kwa uuzwaji wa eneo la ufukwe pale coco beach, sasa cha msingi wale wauzaji kutoka manispaa ya k'ndoni lazima takukuru iwachunguze ni kivipi wakubali tu kuuza eneo kama lile? mana pale navojua siku sa sikukuu huwa kunafurika sana sasa wakisha uza pale watu sijui wataenda wapi mana lazima kuwe na vingilio na kama navojua bongo lazima kuwe na vingilia vya kutoana roho...

wadau mnasemaje hapo mi naona ni hatua nzuri sana kwa PM.
 
EYESPY: Not enough done on Coco Beach !

Adam Lusekelo
THIS DAY
Dar es Salaam

I HEAR that Premier Mizengo 'Pete' Pinda this week ordered an immediate halt on the 'development' of Coco Beach. Strange! Doesn't Braza Pinda want a bribe?

Because I know some guys who would gladly take a bribe and gladly sell not only Coco Beach, but the whole country for 30 pieces of silver.

When most of us having almost given up all hope and confidence on many deeds by the government, we get Braza Pinda's move. Well, a big hand should go to him.

But that isn't enough. We demand those Kinondoni Municipal guys to be sacked and taken to court to face charges of corruption. These are the psychological types who will gladly sell their own mothers to get filthy lucre.

We also want to know who are those clowns called Q-Consult Limited. Who told those selfish and greedy guys that Coco Beach needs restaurants, bars and sports facilities?

The clowns don't know that sometimes nature is at its best when left alone. It is there to be enjoyed by all. Not to be owned by 'businessmen' eager to grab filthy lucre at all cost.

I really am worried by those Kinondoni guys who signed the deal. At this rate those guys must be planning to sell the Karimjee Hall or even the State House for investment � bars, restaurants and amusement parks and private toilets.

At this rate we could get Karimjee Tandoori Restaurant. Or Ikulu fish and chips take away! All to be served by trained Field Force waiters. Some people see anything in terms of money. No consideration for others, as long they can make money!

It's sheer madness of course. But our country has been turned into a land of impunity. You, like Kinondoni Municipal crooks, can do anything you want and steal, provided you have the gall to do so. No punishment! That is the unwritten law of the land.

I mean Tanzania has an 800-mile coastline, most of it breathtakingly beautiful. But still those selfish guys have plotted to grab Coco Beach. Why not Bweni Beach? It's more pristine than Coco Beach and quieter!

One wonders what else is being sold under our noses by our increasingly numerous unarmed robbers. Is the great Serengeti National Park still the property of Tanzania or has it been sold to a 'nefarious developer'? Are the elephants in the park ours or they have been bought by some khafiya-wearing Arab 'developer'.

Praise to Braza Pinda for stopping the crime. But still there must be the culture of punishment. Or else the crooks at Kinondoni Municipality, and all other municipalities in the country will simply repeat their evil deeds. And next time they might not be discovered and caught!

Mbwene2@yahoo.com
 
EYESPY: Not enough done on Coco Beach !

Adam Lusekelo
THIS DAY
Dar es Salaam

...Premier Mizengo ’Pete’ Pinda this week ordered an immediate halt on the ’development’ of Coco Beach.

...I really am worried by those Kinondoni guys who signed the deal.

...Praise to Braza Pinda for stopping the crime.

Nina swali moja.

Yaonekana kumbe mkataba ulikuwa umesha sainiwa. Sasa Pinda huwa anapenda kusema mikataba mibovu hatuwezi kuifuta kwa sababu ya wazi kwamba mkataba unakubana kisheria.

Sasa huu mbona ameweza kuufuta kwa tamko hadharani tu?
 
I like Adam Lusekelo, he nailed them down. It's time to take action from bottom to up.
 
Wakulu;

Katika mapumziko ya Mwishoni mwa Mwaka 2008 nilipata wasaa wa kutembelea Beach Zetu maeneo ya Kisiju. Lakini pia huko nyuma niliwahi kutembelea Beach za Kigamboni na Bagamoyo na zote kwa urefu wa kilometa za kutosha. Pia niliwahi kutembelea beach za Mtwara.

Findings:

Kwa shuhuda za wenyeji wa maeneo hayo ni kuwa sehemu kubwa sana ya beach hizi imeuzwa kwa Wageni toka nje ya nchi ingawa uendelezaji bado haujaanza.

- Sitaki kuamini kama hizi habari ni za kweli . . .

- Sitaki kuamini kuwa Serikali haijui lolote na wala haina mipango makini ya kuendeleza beach zetu wala uhifadhi . . .

- Sitaki Kuamini kuwa Watanzania ni mbumbumbu kiasi hiki na tumelala usingizi wa Pono wakati chetu kinachukuliwa maana hata bei wanazouziwa ni za kutupa . . .

- Sitaki Kuamini . . . Sitaki kuamini . . . Sitaki kuamnini . . . . Hakuna watu wa kulipigia kelele hili wala wa kutuokoa . . .

Somebody tell me kama naota tu ama nini? Tusemezane!
 
haya, juzi wakati wa sherehe za uapndaji miti (sic) Kikwete anazilaumu tena manispaa kwa kushindwa kuendeleza beaches. Kinondoni walipojaribu kufanya hivyo kupitia kwa mwekezaji, Pinda aliwakataza. sasa wafanye nini?
 
haya, juzi wakati wa sherehe za uapndaji miti (sic) Kikwete anazilaumu tena manispaa kwa kushindwa kuendeleza beaches. Kinondoni walipojaribu kufanya hivyo kupitia kwa mwekezaji, Pinda aliwakataza. sasa wafanye nini?

hizo manispa husika haziwezi kufanya hivyo katika mpango wa kuhifadhi mazingira , maana ni jukumu lao, wakitaka private contribution kuna njia zifaazo kama kuweka matangazo ya biashra, na pia biashara zingine ambazo zitalipa kodi, kama Speed Boats, surfing, Piers na vitu kama hivyo., kwani wenzetu wana ziendeleza namna gani beaches zao, kwa kuziuza au kuwa na miradi endelevu.
 
Back
Top Bottom