Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,642
109,015
1. Tangaza haraka Kuzuia vile Vijiwe vyote vya Kukodisha Mapira / Matairi ya Kuogelea

2. Kisha amrisha wanaotaka Kufanya hiyo Biashara Kwanza wajisajili Kwenu (Serikalini) na wekeni Ada / Tozo Kubwa ili kama kuna Watakaojitokeza basi wawe ni Watu Serious na siyo hawa Wahuni walioko

3. Kwa kila atakayejitokeza mlazimisheni awape Picha zake na mjua Makazi yake na taratibu zingine za Kiusalama dhidi yao zifanyike kama njia ya Kuwadhibjti.

4. Kuwe na Chama chao Beach Boys ambacho Kitatambulika nanyi Mamlaka na walazimisheni Wanachama wao (nikimaanisha Vijana wao Wanaofundisha Watu Kuogelea Baharini) wawe ni Watu very Professional na Ethical pia

5. Serikali (Mamlaka) iweke Matangazo katika Beach zote (tena yawe Makubwa) kuwa Mabinti / Wanawake ambao watafanyiwa Ukatili huo wapige Simu upesi kwa Mamlaka zenu ili Wahusika wakamatwe.

6. Himizeni kwa Beach Goers Wote hasa Wanawake / Mabinti kuwa kama wanataka Kufundishwa Kuogelea na Beach Boys basi wawachukue wale ambao ni qualified na kutoka sehemu husika.

7. Beach Boys wote watakaowepo iwe ni AMRI lazima wawe na Vitambulisho na Uniform ili irahisishe hata Kujulikana mapema wakifanya huu Uhuni wao.

8. Katika Beach zote wekeni Eneo Maalum (ndani ya Maji) la Watu Kufundishwa Kuogelea kwani moja ya Mbinu Kubwa itumikayo na hawa Wahuni (Beach Boys) ni kwenda na Wahusika katika Directions ambazo hakuna Watu Wengi na kwenye Kina Kirefu kisha wanafanya huo Uhuni wao.

9. Mkazo uwekwe zaidi kwa Watu Kujifunza Kuogelea katka Vituo Maalum au Shule za Uogeleaji (hasa Swimming Pools) ili basi wakiwa wanaenda Baharini wawe ni Wajuzi na siyo Watafuta kujua Kuogelea ambako hukutana na hawa Wahun

10. Tungeni Adhabu Kali na isiyo na Huruma dhidi yao ili Kulimaliza hili tatizo na kuleta Nidhamu katika hayo Maeneo husika (Beaches)

11. Ili Kuwakamata tumieni huu Mtego wa kuwatafuta Mabinti (Wanawake) Watatu tu ambao wanajua kweli Kuogelea au mkiweza Wachukueni wa pale Navy Kigamboni kisha Wapandikizeni katika kila Beach.

Wakiwa huko Wahimizeni wajifanye hawajui kabisa Kuogelea kisha wavalie Nguo za Kutamanisha na wawe Wanajibebjsha kwa hao Beach Boys.

Wakati mnapanga hili pia mnawapanga Watu (huku nchi Kavu) wakiwa na Camera za Ujasusi wanawachukua ili kuwa na Ushahidi very Vivid ambao hawataweza Kuruka.

Pia hakikisheni mnawatafuta Wavivu na Mitumbwi yao ili wakati mnazifanya hizi Oparesheni nao Wawe wanajifanya kama vile wako Baharini wanaendelea na Shughuli zao za Uvuvi.

Kisha hawa Mabinti / Wanawake ambao mtawapanga Wajirahisi kwa Beach Boys (ambao napendekeza lazima Wawe ni Wajuzi wa Kuogelea hasa) mtawaambia wakishaingia tu kwenye Maji na kupelekwa Maji Marefu na kuanza Kuombwa Ngono au kutaka Kubakwa upesi sana watoe Ishara kwa wale Wavivu mtakaowapanga watakaokuwa Eneo Jirani na kwa Askari wengine ambao mtakuwa mmewapanga huku nchi Kavu.

Mkishawakamata hawa Wachache watataja Mtandao wao Wote na Kutajana (huku mkiruhusu na Sisi Raia tuwatje Adabu kidogo kwa Vipigo vya kishalubela) pale pale Baharini ili kutoa Signal kwa Wenzao wengine kuwa sasa Serikali kwa Kushirikiana na Raia Wema (akina GENTAMYCINE) mmeamua / tumeamua Kuwadhibjti.

Na baada ya hapo tu mnaondoka nao kwenda Polisi ili kuanza taratibu zingine za Kisheria ila naomba Adhabu ya Viboko ama 6 au 12 isikosekane na Kifungo kirefu

12. Na katika Vijiwe vyao vyote hao Beach Boys huko Baharini baada ya Kuwasajili Kisheria kama nilivyoshauri hapo mwanzoni pia himizeni / lazimisheni kila Kijiwe kiwe na Utambulisho wa Namba na Jina Kubwa lililoandikwa

13. Ikiwapendeza himizeni / lazimisheni kila Binti / Mwanamke aendae Kuogelea Baharini aende na Pila / Tairi lake kutoka Kwao / Kwake kwani Wengi Wao wakati Mwingine hujikuta wanajngia Majaribuni hadi Kulalwa kwa Kukosa tu Vifaa hivi.

14. Tangazeni kabisa Binti / Mwanamke ambaye kwa Upumbavu na Uwoga wake bila kusahau Tamaa zake za Mwili akikubaliana na huu Uhuni wa hawa Wahuni Beach Boys na likampata la Kumpata asije Kulaumu Mtu au Serikali

15. Mwisho tengezeni Vipindi Maalum katika Redio na Television vya Kutoa Elimu na Kuonya juu ya Ukatii huu mkubwa huku mkihimiza kila Beach Goer (Mpenda kwenda Kutembea Baharini) awe ni Mlinzi wa Mwenzake pasipo kujali ni Ndugu yako au si Ndugu yako

Ni haya tu Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D nakuomba yafanyie Kazi yote na GENTAMYCINE nakuhakikishia hapa hapa JamiiForums kuwa Tatizo hili utalimaliza na Kuokoa wengi.

Nimekuheshimu sana kwakuwa navutiwa na Utendaji wako mzuri wa Ushirikishaji wa Wadau na nakuahidi kukupa Ushirikiano zaidi kwa Mambo / Masuala mengine ya Kijamii ukihitaji kwani 97% ya Maisha yangu ya kila Siku ni kuwa na Jamii na kuwa na Uwezo mkubwa wa Kuchunguza Jambo, Kulifuatilia, Kulijua, Kulirekodi katika Ubongo wangu, Kulikabili Kifikra na Kimatendo na kutoa Suluhisho la Dharula, la Kati na la Kudumu.

Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D tafadhali kama utakuwa na Zawadi yoyote ile Kwangu GENTAMYCINE (itakayokupendeza) kwa hiki nilichokuandikia hapa basi utakitangaza hapa hapa JamiiForums kisha utaipeleka katika Ofisi za JamiiForums Kawe Avocado na utampa JamiiForums Founder Mtani wangu wa Kihaya na Kaka Maxence Melo na yeye atajua wapi atanipata na Kuiwasilisha Kwangu kwa Niaba yako.

Na nikutoe Hofu Dada (Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D) hata kama hutonipa Zawadi yoyote ile bado nakuhakikishia nitaendelea kukupa Ushirikiano wangu mkubwa bila Kinyongo na Usununu.

Kila la Kheri Mheshimiwa

Tupo pamoja.

Akhsante.

Wako GENTAMYCINE Nahodha wa Kudumu wa wana JamiiForums wote duniani.
===
Uamuzi wa Wizara soma Waziri Gwajima: Kuna haja ya kuweka mfumo maalumu wa kuwatambua "Beach Boys" maeneo ya Fukwe
 
Ulisema uko bize sana lakini nashukuru umepata muda wa kurejea na maoni yako. Nimeyapokea, nasoma vizuri nione la kufanya kwa kuwa mambo mengi yanauhusiano wa kitimu, yaani "sectoral". Ngoja niratibu, Ili mradi linaenda kwenye jamii, basi wizara yetu ngoja ione jinsi ya kufanyia kazi na utasikia mrejesho. Ubarikiwe Sana.
 
Ulisema uko bize sana lakini nashukuru umepata muda wa kurejea na maoni yako. Nimeyapokea, nasoma vizuri nione la kufanya kwa kuwa mambo mengi yanauhusiano wa kitimu, yaani "sectoral". Ngoja niratibu, Ili mradi linaenda kwenye jamii, basi wizara yetu ngoja ione jinsi ya kufanyia kazi na utasikia mrejesho. Ubarikiwe Sana.
Tuko pamoja sana Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D nawe pia Ubarikiwe mno tu katika Utendaji wako Wizarani na Maishani mwako pia.
 
ulisema uko bize sana lakini nashukuru umepata muda wa kurejea na maoni yako. Nimeyapokea, nasoma vzr. Nione la kufanya, kwa kuwa mambo mengi yanauhusiano wa kitimu yaani "sectoral". Ngoja niratibu, Ili mradi linaenda kwenye jamii, basi wizara yetu ngoja Ione jinsi ya kufanyia kazi na utasikia mrejesho. Ubarikiwe Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Cc: emrod

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!!
 
Popoma katika ubora wake...ushauri mzuri kwa kweli dada zetu wanaliwa uroda sana na hawa wajinga.

Ushauri mzuri sanaaaa. Tatizo nani wa kutekeleza
Asante. Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D ameahidi Kulifanyia Kazi na Kuchukua haya Mawazo yangu Tukuka 15 ili Walimalize. Tumpe muda na tuwe na Subira pia kwani ni Jambo / Suala Mtambuka na la Kisekta. Kikubwa kapokea Ushauri.
 
ulisema uko bize sana lakini nashukuru umepata muda wa kurejea na maoni yako. Nimeyapokea, nasoma vzr. Nione la kufanya, kwa kuwa mambo mengi yanauhusiano wa kitimu yaani "sectoral". Ngoja niratibu, Ili mradi linaenda kwenye jamii, basi wizara yetu ngoja Ione jinsi ya kufanyia kazi na utasikia mrejesho. Ubarikiwe Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mh kwanza safi kwa kua active lakini kwakweli inakupaswa hili ulichukulie serious, miaka mingi huo mchezo upo na watu wanaambukizwa magonjwa na kuzalilishwa pale coco beach.

Usione huruma katika hili ukipuuza inaweza siku ikatokea hata kwenye ukoo au familia yako.
 
Ushauri mzuri sana.

Ila juu ya swala la kutafuta NAVY kwa ajili ya kufanya operation ya kuwakamata wahuni wepesi kama hao ni kulishushia hadhi jeshi letu tukufu.

Isitoshe, operations za kijeshi zinaenda kwenye mambo mazito haswa. Si kwamba nadharau sana Unyanyasaji wa kijinsia unaotendwa na Beach Boys, ila ni jambo dogo sana likitiliwa maanani na vyombo husika. Polisi waamue tu kulivalia njuga.

Wataalam wa sheria watanisaidia na watanisahihisha. Kumshawishi mtu atende jinai ili uweze kumuwajibisha haitakiwi. Kwenye muktadha wa haki, atakushinda mahakamani. Ninachomaanisha, kuwachukua NAVY na kuigiza huku wakijirahisha sana kwa hao Wahuni kisha baadae wawatie nguvuni, haikubaliki. Ukusanyaji wa ushahidi ni jambo rahisi sana kwa vijana wa hovyo.

Vingine, umesema vema sana.
Mh Dkt. Gwajima D atayazingatia.
 
Back
Top Bottom