Katika hali isiyo ya kawaida juzi katika viwanja vya stendi ya zamani mjini bunda,waziri wasira akiambatana na mbunge wa musoma vijijini ndugu Mkono kwa kile ambacho walikiita mkutano wa elimu katika mchakato wa katiba mpya ambapo walikumbana na zomea zomea hasa wananchi walivyoonyesha kukerwa na sheria inayowabana ya kuelimishana kuhusu katiba kwa madai kuwa kazi hiyo lazima ifanywe na tume tu!!!
Bila kutarajia wasira alibanwa ni kwanini anatoa elimu hiyo wakati sheria hiyo iliyosainiwa na bosi wake hairuhusu hivyo naye amevunja sheria na ashitakiwe,kutokana na kubanwa huko wasira alisema wananchi hawakuelewa vizuri sheria hiyo lakini wananchi walionyesha kuchachamaa na ndipo wasira alipovunja mkutano huku zomea zomea ikiendelea.
Swali langu
Je hivi walipokuwa wakitunga sheria hii ya hovyo hawakujua kwamba hata wao inawabana?au nao ni sehemu ya tume?
Je inakuwaje mpokea maoni maoni ndiye awe muelemishaji?
Naomba kuwasilisha wakuu