FT: Marumo Gallants 1 - 2 Young Africans | CAF Confederation Cup 17.05.2023

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,033
Marumo Gallants wapo nyumbani kuwaalika Young Africans katika mchezo wa marudiano ya nusu fainali ya CAF Confederation Cup kwanzia saa 1:00 usiku kwa hapa nyumbani Tanzania.

Mechi ya kwanza iliyopigwa juma moja lililopita Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hivyo matokeo yoyote ya ushindi kwao, au droo yataivusha Yanga na kuipeleka Yanga katika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Kila la heri kwa Yanga, Taifa zima tupo nyuma yenuπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
================================================

Updates:
45' + 1 Mayele anawapa Yanga goli la uongozi

2nd half sasa:
53' Bado Yanga anaongoza na ana miliki mpira kwa utulivu mkubwa

54' Aucho na Katlego wa Marumo wanapata kadi za njano mara baada ya kugombana

56' Musonda akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga goli anajikuta akipaisha mpira juu

57' Marumo wanapata goli lakini linakataliwa baada ya mfungaji kuwa katika eneo la kuotea

60' Katlego anaisumbua sana beki ya Yanga, Marumo wanatawala mechi kwa dakika hizi

61' Goallllllllllllllllllll
Kennedy Musonda anawapa Yanga goli la pili baada ya kazi nzuri ya Mayele

63' Yanga wanafanya sub, wanaingia wachezaji watatu Aziz Ki, Moloko na Mzize huku Bangala, Aucho na Musonda wakienda nje

65' Yanga wamerejesha umiliki wa mpira wao

67' Mpira unachezwa kwa kupokezana na kushambuliana kwa zamu

69' Yanga leo wanazuia vizuri mipira ya kona, Marumo walipata kona mbili lakini zimezuiwa vizuri na mabeki wa Yanga

70' Mashabiki wanaishangilia Yanga ambao wengi wao waliojitokeza hapa uwanjani ni Watanzania waishio Afrika Kusini.

71' Zawadi Mauya anaingia kuimarisha ulinzi. Kocha Nabi anaamua kujilinda zaidi baada ya uongozi wa goli 2

75' Mpira umesimama kupisha Mayele atibiwe

76' Edgar Manaka wa Marumo anapata kadi ya njano baada kumchezea rafu Mzize

78' Mayele anatoka huku akichechemea na Farid Mussa anachukua nafasi yake

79' Mawinga wa Marumo wanaamua kuchezea mpira na kupiga chenga baada ya kuona kimahesabu wana mzigo mzito

82' Yanga wanamiliki mpira lakini wanashindwa kutumia nafasi wanazozitengeneza

83' Yanga wanakosa nafasi ya wazi ya kuandika goli la 3

88' Yanga wanapata faulo mara baada ya Moloko kufanyiwa madhambi

89' Yanga wanalishambulia goli la Marumo kwa kasi

90' Marumo wanapata goli ni 1-2

Dakika 4 zimeongezwa

FT' Marumo 1-2 Yanga
Aggregate: 1-4

Yanga wanaingiiiaaaaaa Fainali kwa mara ya kwanza.
 
Marumo Gallants wapo nyumbani kuwaalika Young Africans katika mchezo wa marudiano ya nusu fainali ya CAF Confederation Cup kwanzia saa 1:00 usiku kwa hapa nyumbani Tanzania.

Mechi ya kwanza iliyopigwa juma moja lililopita Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hivyo matokeo yoyote ya ushindi kwao, au droo yataivusha Yanga na kuipeleka Yanga katika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Kila la heri kwa Yanga, Taifa zima tupo nyuma yenuπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
game saa ngap?
 
Kila ls kheri mabingwa

IMG_20230508_191855.jpg
IMG_20230424_092039.jpg
 
Eenhee! Wanasemaga usiku wa deni haukawii kukucha na kwetu sisi Timu ya Wananchi ndo tulikuwa tunataka ifike tupate kumalizana na hizi dakika 90 zilizosalia.

Kila la kheri Timu ya Wananchi katika kuweka historia ingine.

#DaimaMbeleNyumaMwiko.
 
Back
Top Bottom