Lah! Hallaullah!
JamiiForums-503580379.jpg
 
Money Got the power to drive poor people. kuwa maskini sio kuvaa misepwetuko... ila kufanya la kila namna ili kupata HELA.
 
Non sense!
Kosa la JPM ni kuwekeza nchini kwake? Kwahiyo na yeye angeenda kujenga makasri huko ulaya?

Na kwa ujinga wa watanzania watazidi kumchukia ilihali wapo waliowekeza nje. Ni vile tubwao hatuwezi kuwa na ushahidi wa wazi kama ilivyo kwa hayati.


Kwa mfano mwizi anayeiba anajenga shule, anasaidia jamii hawzi kuwa sawa na mwizi anayeend akuhonga bar. ( Imenikumba korean movie-iljimae)😀👍

..waandishi wanasema wamefanya mlinganisho ufuatao na kuona Magufuli amechomoza kuliko wenzake.

1. Chato vs Butiama.

2. Chato vs Mkuranga.

3. Chato vs Lupaso.

4. Chato vs Msoga.

NB:

..uwanja umefunguliwa kuandika vitabu kuhusu Magufuli.
 
Kiukweli nilitokea kumchukia sana hayati Magufuli hasa kwa mambo 'binafsi' hata kabla hajawa rais!

Ila pamoja na yote Magufuli alikua ana afadhali ukimlinganisha na Kikwete au Samia tuongee tu kwa kumtendea haki.

Ni nani hakupapendelea kwao nchi hii?

Nyerere na Mara? Nyerere na akina Butiku?

Mwinyi na Zanzibar/Mkuranga?

Mkapa na kusini?

JK?

Pili kuna haja gani ya kutumia rasilimali kubwa hivyo kuchapisha kitabu chenye maudhui yasiyo na msaada? Lengo ni kujifunza? Kama ni kujifunza si tunayo historia ya Gbadolite huko Zaire sasa DRC? Nani ana fadhili hayo na kwa maslahi gani?

Magufuli ni lost case kwa sasa haya hayatusaidii.

Mwisho tuwe makini sana na waandishi uchwara maana huu ni ulaji unatafutwa kwa mtu na ni njia ya kututoa kwenye reli.
kwa ufupi meko anapaswa afukuliwe hapo walipomzika ajarazwe viboko 12, alafu hiyo mifupa yake tuitupeee huko barabarani mbwa wale. useless

Sent from my M2103K19G using JamiiForums mobile app
 

Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg


Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
 
Huu uharo watanunua hao wapumbavu waliokiandika na mabwana zao waliowapa pesa wajidhalilishe mbele ya uma wa wazalendo.
Hata sisi tulio dhulumiwa korosho tuna uhitaji wa eapot ya kimataifa ! Tena sisi huku tulikuwa na vitu vya maana kuliko bugiti sijui burigi! Huku kuna gesi , wanyama hapo seluo kwa hyo atleast wawekezaji na watalii watakuja na mwewe huku wakitokea direct kwao!
 
Huo ni upambavu wa kiwango cha SGR na kuna mtu kawalipa.Waongee lingine, kwenye suala la miradi hapo wamechemka!
Reli ya SGR inaenda Chato?Mradi wa Umeme Rufiji upo Chato?Bandari kavu ya Kwala ipo Chato?Mradi Ujenzi wa mji Mkuu wa serikali upo Chato?Ujenzi wa vituo vya Afya zaidi ya 300 vipo Chato?Kijazi Flyover ipo Chato?Mfugale Flyover ipo Chato?Barabara ya njia nne Kimara mpaka Kibaha ipo Chato?
Kwa uchache,Waandishi wameongozwa na chuki zaidi ya uhalisia.
JK mwenyewe alipeleka umeme Kijiji cha Hoyoyo, Mkuranga ambapo hakuna mradi wowote bali Umeme alipata Mkwewe Baba yake na Salma na shambani kwa mkewe!
Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambao alizindua mwaka 2014!
Inshort Kibanda na Ngurumo kama wamo humu jukwaani wajue wamejidharirisha akiwemo na Baba Askofu!.Ila Ngurumo nadhani stress za kukimbia nchi zinamsumbua!
"I am the State" bonge la Tittle
 
Back
Top Bottom