Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,765
- 218,382
Mwamba wa Siasa za kisasa kwenye eneo la Maziwa Makuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema ambacho ni Chama kinachoungwa mkono na watu wengi zaidi nchini Tanzania, huku takwimu zikionyesha kwamba kina wanachama hai zaidi ya mil 15, atazungumza na Waandishi wa Habari wa Kimataifa na wa ndani ya Nchi.
Jambo la kufurahisha ni kwamba mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa kisasa kwenye makao makuu mapya na ya kisasa, Mikocheni D'Salaam.
Kaa tayari kwa ajili ya kupata Mwongozo mpya na Dira ya Taifa kwa 2024.