Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 123,081
- 232,782
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akitoa tathmini kutokana na Oparesheni Kabambe ya 255 KATIBA MPYA, iliyotiwa kachumbari ya OKOA BANDARI ZETU, ametumia wasaa huo pia kuwashukuru Wananchi wote waliochangia michango yao ya hali na mali ili kuwezesha Oparesheni hiyo.
Ujumbe wake huu hapa:
Leo, natoa shukrani zangu za dhati kwa watu wote waliowezesha mikutano yetu ya Chadema katika Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, na Mara kuwa mafanikio makubwa. Msaada wenu usio na kifani na uaminifu wenu umetuhamasisha sana.
Nguvu na hamasa iliyodhihirishwa na wafuasi wetu katika maeneo haya ilikuwa ya kuvutia, na inathibitisha azma yetu kwa tunu na maono yetu. Pamoja, tunajitahidi kuleta mabadiliko chanya na mustakabali bora kwa taifa letu.
Napenda kutoa shukrani za dhati kwa waandaji, wajitoleaji, wale waliotoa michango, wale waliotukirimu kwa chakula na malazi, wale waliotutia moyo, wale waliotuombea, wale waliosambaza ujumbe wetu kuwafikia watu wengi, na wote waliofanya kazi kwa bidii nyuma ya pazia kuhakikisha mikutano hii inafanikiwa kwa kishindo. Michango yenu kwa mafanikio yetu ni yakutukuka.
Tuendelee katika safari hii pamoja, tukiungana kwa malengo yetu ya pamoja. Safari inayofuata inaweza kuwa ngumu, lakini kwa msaada wenu, naamini tunaweza kushinda vikwazo vyovyote vinavyojitokeza.
Asanteni sana kutoka moyoni mwangu. Msaada wenu usio na kifani unachochea azma yetu ya kuleta mabadiliko chanya ambayo taifa letu linastahili.
Hatua inayofuata, Nyasa Zone. Tutaonana kazini.