Freeman Mbowe atoa shukrani za dhati kwa Wananchi wote wanaoendelea kuchangia Oparesheni 255, aahidi Ukombozi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,732
218,315
Screenshot_2023-09-06-14-02-00-1.png

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akitoa tathmini kutokana na Oparesheni Kabambe ya 255 KATIBA MPYA, iliyotiwa kachumbari ya OKOA BANDARI ZETU, ametumia wasaa huo pia kuwashukuru Wananchi wote waliochangia michango yao ya hali na mali ili kuwezesha Oparesheni hiyo.

Ujumbe wake huu hapa:

Leo, natoa shukrani zangu za dhati kwa watu wote waliowezesha mikutano yetu ya Chadema katika Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, na Mara kuwa mafanikio makubwa. Msaada wenu usio na kifani na uaminifu wenu umetuhamasisha sana.

Nguvu na hamasa iliyodhihirishwa na wafuasi wetu katika maeneo haya ilikuwa ya kuvutia, na inathibitisha azma yetu kwa tunu na maono yetu. Pamoja, tunajitahidi kuleta mabadiliko chanya na mustakabali bora kwa taifa letu.

Napenda kutoa shukrani za dhati kwa waandaji, wajitoleaji, wale waliotoa michango, wale waliotukirimu kwa chakula na malazi, wale waliotutia moyo, wale waliotuombea, wale waliosambaza ujumbe wetu kuwafikia watu wengi, na wote waliofanya kazi kwa bidii nyuma ya pazia kuhakikisha mikutano hii inafanikiwa kwa kishindo. Michango yenu kwa mafanikio yetu ni yakutukuka.

Tuendelee katika safari hii pamoja, tukiungana kwa malengo yetu ya pamoja. Safari inayofuata inaweza kuwa ngumu, lakini kwa msaada wenu, naamini tunaweza kushinda vikwazo vyovyote vinavyojitokeza.

Asanteni sana kutoka moyoni mwangu. Msaada wenu usio na kifani unachochea azma yetu ya kuleta mabadiliko chanya ambayo taifa letu linastahili.

Hatua inayofuata, Nyasa Zone. Tutaonana kazini.
 
Kama chadema wanaweza kuchangiwa wakafanikiwa kufanya mikutano mikubwa namna hii, huu ni hatua kubwa. Awamu hii tunaweza ona mabadiliko makubwa zaidi kisiasa. Mungu ibariki nchi yangu Tanzania
Amen
 
Ukitaka uamini binadamu hatufanani ni haya mambo ya kuchangia michango kitaifa... Yaani kabisa kuna wanaochangia eti. Binafsi vyovyote mtakavyonichukulia sawa tu lakini siwezi kuchangia kitaifa chochote katika mfano wa haya

1.Kuchangia kilabu cha mpira mfano simba na yanga (rejea bakuli la wananchi)
2.Kuchangia chama cha siasa mfano ccm au chadema (rejea join the chain)
3.Kuchangia mtu fulani maarufu mfano wasanii, wanasiasa, waigizaji, mabondia, wanamitindo na kadhalika (rejea fei toto, sajuki, kanumba nk)
4.Kuchangia majanga mfano mafuriko, tetemeko nk (rejea mafuriko ya Kagera)
 
Kama kutoa ni moyo basi wewe huna huo moyo wenyewe
 
Back
Top Bottom