Fred Saganda - Rafaeli (Lyrics)

Kindoemmanuel

Member
Dec 5, 2021
6
10
Ilikuwa Jumapili nikamwona Rafaeli amekaa juu ya nini?...
Ni juu ya baiskeli
Namuuliza anaenda wapi kanambia anaenda Ferry
Huko Ferry ni kwa nani?
Kwa lile jitu tapeli
Sasa utamwona wapi?
Atakuwa kwenye meli
Kwenye meli ndiyo wapi?
Ndiyo huko huko Ferry
Baadaye namuona huyo huyo Rafaeli anacheza na nani?
Na yule dada Mary
Namuuliza Rafaeli, hapa ndiyo Ferry?
Anasema siyo hivyo,
Unajua mwenzio nimeharibikiwa na ile baiskeli
Nategemea kwenda kule Oysterbay
Nako huko ntamkuta brother Mtei
Yeye ndiye atakaye nipunguzia bei
Ya spea za baiskeli

Chorus:

Ah, ni namna gani, Ah, ni jinsi gani? Tuta win maishani mpaka siku tunasema buriani
Ah, ni namna gani, Ah, ni jinsi gani? Tuta win maishani mpaka siku tunasema buriani
Ah, ni namna gani, Ah, ni jinsi gani? Tuta win maishani mpaka siku tunasema buriani
Ah, ni namna gani?
Ah, ni jinsi gani? (Yesu wangu)

Kesho yake nikatoka moja kwa moja kwa Rafaeli
Nikamkuta nyumbani anasikiliza CD ya R. Kelly
Nakamuuliza Rafaeli unayo CD ya Makaveli?
Akaniambia ana Makaveli, R. Kelly na Mariah Carey
Sisi hatukukaa...
Tukatoka moja kwa moja haoo! Mpaka kwenye baa
Unaambiwa watu walikuwa wamejaa
Kengelenji zimeshangamana baiskeli na motokaa
Basi tukaagiza masanga pale na kitimoto
Tukaanza kupata moja baridi moja moto
Wakati tunaendelea eh...
Kidogo tu huyoo! Akatokea mzee Urassa
Na ile Land Cruiser yake new model ya kisasa
Power Engine 2.4 Pulling System ya kisasa
Unaambiwa ni Automac kuanzia viti hadi vitasa
Basi alikuwa na laki tatu mfukoni
Akajishika kiunoni akatuangalia usoni
Akatudharau akaingiza mkono mfukoni
Akatoa pesa akaweka pale mezani kisha akaenda chooni
Sisi basi tukaanza kulewa...
Tukalewa, tukalewa Yesu wangu!
Tulilewa, tulilewa, tulilewa, tulilewa
Wakaongezeka ndugu zetu kutoka sehemu mbalimbali za KIlimanjaro;
Marangu, Machame, Uru, Kishumundu, Kibosho,
Mwika, Vunjo mpaka Kibororoni
Unaambiwa Tarakea mpaka huku sehemu za Rombo
Wote pale wakawa wamemiminika
Massawe alikuwepo, Mareale alikuwepo
Shirima alikuwepo, Mangi alikuwepo
Mlema alikuwepo, Ndosi alikuwepo
Mlei alikuwepo, Assey alikuwepo
Mama Prisca alikuwepo, Mama Manka alikuwepo
Minja alikuwepo, Kilua alikuwepo
Na huyu mtoto anakaa mtaa wa pili nani huyu?
Chuwa! Hahahaa! Eti Chuwa naye alikuwepo

(Rudia Kiitikio)

Wakati tunaendelea kupata pale masanga na kitimoto
Rafaeli na Massawe haoo! Wakatoka
Sikujua kinachoendelea nikajua wanaenda kuruka majoka
Kwasababu kulikuwa na mziki wa Reggae, Charanga
Na ule mziki wa kufokafoka
Akilini mwangu nilikuwa nafikiri kwamba mambo yataenda yakifanya nini?...
Hahaa! Yakienda yakinyooka
Kumbe huko walikokwenda walienda kuchokoza wake za watu walikuwa wameketi
Wakaanza kuwashikashika mabegani mpaka zile sehemu zao nyeti
Basi wamezao nikaona wamechukia,
Maneno machafu waanza kuwatupia
Kinabo wewe! Mwache mke wangu kima we unamshikia nini huko?!
Mara huyu kamtukana mwenzake sijui kamwambia fala wewe?!
Huyu kamrudishia maneno yaleyale imradi tu ikawa vurugumechi
Basi wale wanaume nikaona wamebeba mawe
Wakataka wamponde nayo Massawe
Basi Rafaeli akamrukia teke mmoja wao akamwangusha palepale! (Mungu wangu!)
Akataka akimbie... hajafika mbali akakamatwa na nani...?
Na yule afande Chale.
Asa mi nikamwambia afande Chale;
Basi naomba umruhusu huyu Rafaeli nyumbani akalale
Akanambia ni lazma kituoni huyu Rafaeli leo akalale
Sasa nikaona sina tena la kuwafanya
Rafaeli ndiyo huyo tena ameshaulowanya
Kwanza mimi kichwani lager zishanchanganya
Ikanibidi ningoje nijue kesho kitu gani nitafanya
Basi, kama Rafaeli ndo kama ameua
Basi pesa zangu zote polisi watakuwa wamechukua
Yesu wangu yelewii!
Pesa ni maua, maana maua hunyauka vilevile huchanua

(Rudia Kiitikio)

Big up kwa wote nigaz from Kibosho
Nigaz from Marangu
Nigaz from Mwika
Nigaz from Rombo, Moshi mjini,
Old Moshi and many many places
Representing the area.
Wachagga tupo. Hatuko nyuma kwa Hip Hop (Yeah)
Big up to Mama Prisca popote ulipo
Big up to Mama Manka popote ulipo
I'm telling you I'm presenting this shit for real
If you dont care' pack up your bags and luggage and go home
This is how we do, mtatutambua Wachagaa mwaka huu.
 
Back
Top Bottom