Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,588
Tatizo siyo kuwa hatoi. Tatizo ni kuwa anaKWEPA kulipa kwa kusajili baadhi ya mali zake nje ya USA.
Ushahidi uko wapi kuwa anakwepa kulipa? Hivi mami unaijua IRS wewe au unaisikia tu? Yaani ukwepe kulipa kodi na wewe ni mtu prominent hivyo? Hahahaaa huijui IRS wewe.
Hili jambo limelalamikiwa sana kwa sababu ni ukwepaji wa kodi kwa kutumia sheria.
Ushahidi uko wapi? Au maneno ya kibabu Harry Reid wewe unayapokea kama msahafu?
Pamoja na kuwa Sheria unakuwa hujavunja, ila dhamira je?
Kama hujavunja sheria basi ni haujavunja. Hayo mambo ya dhamira ni mambo ya kusadiki tu.
Ni sawa na Baba kuowa Binti yake aliyemaliza miaka 18 nchi ambazo hazikatazi. Sheria itakuwa haijavunjwa ila dhamira!?
Mfano mbovu huo. Utalinganishaje baba kumuoa mwanae wa kumzaa na maneno maneno ya umbea kuwa Romney ana akaunti nchi za nje? Yaani ni mambo mawili tofauti kabisa. Tafuta mfano mwingine.
Utatakaje kuwa Rais wa nchi wakati hata kodi unalipia nchi nyingine?
Uongo huu. Kama kodi halipii Marekani iweje sasa a-file tax returns zake Marekani?