Form 4 2008, form 6 2011. Bado nina sifa ya kusoma chuo??...,

Raelish

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
489
162
Habarin wadau wa elimu hapa., ni kijana wa kiume niliyepitia mitihan kadhaa katika maisha yangu, nimezaliwa kt familia duni sana, ni duni hasa yaani hata kipato cha laki 2 kwa mwaka ni shida(ni historia ndefu acha niishie hapa sitaki nikumbuke zama zile), Nilijitahd 'kiume' kupambana mwaka 2008 nikamaliza pale kibaha boys lakini sikulipa kabisa ada, nikafaulu na nikaendelea na kidato cha 6 huku mkoani kwangu(Ruvuma) nako nikamaliza kwa mchepuo wa sayansi,CBG.. kutokana na sababu za kimaisha nikafanya vibaya,nako pia sikulipa ada kabisa,HIVYO SIKUWA NA VYETI VYOTE KWA SABABU SIKUMALIZA ADA, nimewah kuja hapa na kujarb kuomba msaada nikaonekana kama tapeli, of course sikumlamum yoyt nikafuta chozi nikashukuru.. namshukuru Mungu kuna kibarua nimepata na nahisi mpaka mwezi wa 10 hivi naweza kugomboa vyeti.. je naweza kujiunga na chuo chochote mwakani au muda umeshanipita niache tu., RESULTS. FORM IV; kisw C,civ C,geog D,eng C,math D,bios C,chem C,phys D,b/knw C. FORM VI; chem S,bios S,geog S,g/s S,bam F
 
Unaweza ku soma mkuu ,nashauri utafute vyuo vya serikali ukasome masomo ya utabibu,kilimo au mifugo ndio kuna ajira za kuaminika,tuwasubirie wachangiaji wengine!
 
mwakani mkubwa huwez tabili,sera za nchi yetu zina mwezi mchanga,fanya hima mwaka huu.
 
Back
Top Bottom