Foreigners Dominate Shipping Industry in Tanzania

kisimani

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
550
154
Salaam wanabodi....

Pitia link hii uone jinsi serikali yetu ilivyolala na huku watanzania wakiendelea kunyanyasika nchini mwao.

http://dailynews.co.tz/index.php/local-news/10751-foreigners-dominate-shipping-industry

Swali langu, hivi ni kweli serikali hawajui hawa foreigners walivyojaa kwenye haya makampuni ya shipping huku wakivunja sheria za nchi??

Hivi serikali haijui rushwa iliyotumika kuanzisha haya makampuni hata kuonekana wazawa wanamiliki 50% wakati ni uwongo?

Watanzania wenzangu, badala ya kujadili mambo kama haya ya msingi yanayofanya vijana wanaomaliza chuo kuwa mtaani huku nchi ikikosa mapato lukuki kutokana na uzembe wa mfumo unaoongoza pamoja na utawala mbovu uliopo sisi tunakaa kujadili the so called mfumo kristu na udini....jamani tubadilike.
 
ujue foreigners wanajua wanachokitaka! rais wenu ni dhaifu, serikali yake ni dhaifu times 2, wananchi ni mabingwa wa porojo! what do u expect?? waacheni foreigners wale, waibe mpaka wachoke!! na nyinyi muwachwe mpumuwe........! badala ya kuandamana kudai mambo ya msingi kama haya, mmekazana kudai vitu ambavyo hata chanzo chake hamkifahamu!
 
Serikali yenyewe ni ya kifisadi. Kila sector inhini ni mbovu kupindukia. Viongozi wa CCM wanachaguliwa kwa rusha lukuki katk ngazi zote. CCM kama itaendelea kushika dola waTZ tusiwe na matumaini yeyote.
 
Kuna mtu hapa alisema jana kuwa tukipata viongozi wazelendo, Tanzania inaweza kuwa kama Marekani au Ulaya. Wengi wetu hawaamini lakini hii ni kweli. Watu hawajuhi jinsi gani serikali inavyopoteza mapato kwa tamaa za wachache. Viongozi wanapewa Tsh 20m wanasign mikataba ya $20b unategemea nini. Kuna viongozi wanapesa nje ambazo hata vitukuu vitaziacha. Tanzania watu wanakufuru.
 
ujue foreigners wanajua wanachokitaka! rais wenu ni dhaifu, serikali yake ni dhaifu times 2, wananchi ni mabingwa wa porojo! what do u expect?? waacheni foreigners wale, waibe mpaka wachoke!! na nyinyi muwachwe mpumuwe........! badala ya kuandamana kudai mambo ya msingi kama haya, mmekazana kudai vitu ambavyo hata chanzo chake hamkifahamu!

Kitu kinachonishangaza ni waziri pamoja na Sumatra kubisha taarifa hizi......hivi lini viongozi wetu watatumia information kama input kwenye utendaji wao???

Sheria zipo wazi lakini zinakiukwa na mamlaka husika wanasema wapo sahihi...Jukumu la kufanya uchunguzi kama wamedanganywa ni la nani???? Au mpaka tuunde tume au kamati jamani???

Inatia uchungu sana sana......watanzania wenzangu tunahusika na kudanganya kwa ajili ya njaa ya siku moja???

Ipo siku tutasema baaaasiiiii....
 
Back
Top Bottom