Fizikia ya ajali (The Physics of Accidents): Mabasi yetu yanaundwa au kuunganishwa wapi?

Mkuu umesema mambo ya msingi sana. Kufikiria nje ya boksi badala ya kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu kama vile kuimarisha hospitali ya Tumbi ili iweze kuhudumia majeruhi wengi wanaopata ajali karibu na meneo ya hapo.
Halafu kuna hivi vibajaji na pikipiki kuruhusiwa kubeba abiria kwa maana ya biashara. Kuna mpk wodi pale muhimbili imepewa jina la pikipiki kwasababu ina majeruhi wengi wanaopata ajali ya vyombo hivyo. Solution? again jibu jepesi, vibajaji viwe na miknda (safety belts). Aisee
Labda niongeze swali,tuna think tank nchi hii?
 
Body nyingi zinaundwa mtaani tu, ukienda kuomba TLA mamlaka husika inatakiwa kukagua gari husika lkn hiyo haifanyiki. Angalia ile Grazia iliyoanguka na kuua watu juzi kati pale Mwidu, jamaa anaunda mabody yake Buguruni pale akitumia Chassis za lori tena na vjana wa mtaani. Sasa gari hiyo ikianguka uwezo wa kuhimili unakuwa mdogo hata jinsi ilivochakaa bada ya ajali inathibitisha hilo.
 
Wakuu,mimi ni mdau wa barabara hasa kwa safari za mikoani. Utafiti wangu umegundua haya; ajali nyingi za mabasi zinasababishwa na uzembe wa madereva(80%),ubovu au ubaya wa barabara(15%) na mechanical factor(5%) hapo utaona ni bora kudeal na percentage kubwa rather than dealing with mechanical error! Nitaelezea zote kwa ufupi; madereva wengi wanaoendesha mabasi hawana elimu ya kutosha juu ya usalama barabarani,hawani uhakika wa kipato cha kutosha na pia kutojali aina ya chombo anachoendesha(basi la abiria) na sheria hazina adhabu kali kwa makosa ya ajali barabarani. Speed ya basi njiani wakuu mtashangaa several time nime-overtake basi nikiwa na gari ndogo speed 150, it means bus lilikuwa almost 140 hii ni speed kubwa sana kwa bus la abiria. Naomba nigusie na ubovu wa barabara ambao unachangia ajali kwa asilimia 15, eneo la kibaha hadi dar huwa kuna msongamano sana wa malori,mabus na gari ndogo inapotokea gari zinaovertake ni vigumu kurudi upande wake kutokana na ufinyu wa barabara,pia sehemu zenye kona kali pamoja na miteremko kama mto wami njia ya tanga/arusha n.k. Hii ya mabodi ya mabasi au chasis inachukua asilimia ndogo kwa mfano mabasi mengi ya mohamed ni aina ya marcopolo toka nje(brazil) lakini yanapata ajali,same to scandinavia those days,japokuwa wengi husema tatizo ni matairi labda tujadili hilo!!!kama tairi ni mbovu kwa nini tusijikite hapo? Siamini kama bodi au chasis ndio chanzo cha ajali, HAPANA. Naamini uzembe wa madereva plus speed kubwa na bad timing ya ku-overtake. Nawasilisha
 
Kuna basi la Moro Best lilifungiwa lakini baada ya siku mbili likaripotiwa kwamba limepata ajali na limeua. RPC wa Morogoro, Mama Chialo alipoulizwa akasema taarifa ya kufungiwa kwa basi hilo ndio amezipata kwenye eneo la ajali siku hiyo.

Kwa mwendo huu tunakwenda kweli!
 
Majoja asante sana kwa kutupa mwanga kidogo. Mimi ninaamini kuwa mojawapo ya mabadiliko makubwa ambayo tunaweza kuyaleta nchini na kuanza kuleta maendeleo ya kweli ni kuanza kukataa maelezo ya kishirikina ya mambo yanayotokea. Ni lazima tuanze kuhoji sababu za kisayansi za kwanini vitu fulani vinatokea ni pale tu ambapo labda sayansi haiwezi kutueleza ndipo tunafungua macho yetu na kujiachilia kwa Providence. Ajali ya meli ya Bukoba na hata hii ya juzi ya ZAnzibar ni ajali ambazo zinaweza kuelekezeka kisayansi.

Naamini ajali za barabarani hata kama zinasababishwa na makosa ya watu lakini pia kuna sababu za kisayansi. Kwa mfano, mtu anapokuwa kwenye basi ambalo limeundwa pasipo kufuata kanuni za fizikia za mwendo, au maumbo anaweza kwenda mwendo japo mdogo (80km/h ni mdogo kulinganisha na sisi tu tunaoenda 65-80 M/h (sawa na 104km/hr - 128 km/h) tunaenda mwendo mkubwa sana lakini husikikii mlolongo wa ajali za namna hii hasa zinazotokana na mwendo kasi.

Sasa ni kwamba hatuna vyuo vikuu vyenye uwezo wa kufanya utafiti wa kisayansi kufuatilia tabia za uendeshaji zikoje (driving habit), au kuangalia barabara zetu zimejengwaje au vitu kama hivyo.
 
Wakuu,mimi ni mdau wa barabara hasa kwa safari za mikoani. Utafiti wangu umegundua haya; ajali nyingi za mabasi zinasababishwa na uzembe wa madereva(80%),ubovu au ubaya wa barabara(15%) na mechanical factor(5%) hapo utaona ni bora kudeal na percentage kubwa rather than dealing with mechanical error!

Umefanya utafitihuu kuhusisha mabasi mangapi yaliyopata ajali, madereva wangapi na ulilinganisha na nini? tupe taarifa kidogo ya huu utafiti wako.
 
hongera sana kwa uzi mzuri MM Mwanakijiji karibuni kwa maoni hii ni siku ya usalama barabarani jamiiforums.com
 
Umefanya utafitihuu kuhusisha mabasi mangapi yaliyopata ajali, madereva wangapi na ulilinganisha na nini? tupe taarifa kidogo ya huu utafiti wako.

Kipindi nipo NIT chuo cha usafirishaji tulifanya research nyingi sana, kwa hii ya ajali za mabasi takribani mabasi 76 kati ya mwaka 2000 hadi 2007 na madereva 309 walijadili katika training ya ajali barabarani, hebu jiulize mbona mabasi ya jeshi au polisi huwa hayapati ajali kama ya abiria??? Na yanatengenezwa nyumbu pale kibaha.
 
Tatitizo lingine hakuna mamlaka inayodhibiti uingizaji wa vipuri visivyokidhi viwango vya watengenezaji, leo unakwenda kununua spare unaulizwa ya kawaida, ya china, ya India au Genuine? so unabaki unashangaa maana they all look the same! Ingawa tofauti ni kwenye packing na bei hili ni tatizo kubwa sana, Kuhusu mwendo kasi 80kph ni ndogo sana kama tunataka kujenga hii nchi tuongeze hadi 100-120kph
 
Ajali kadhaa ambazo zimetokea zimetokana na tairi kupasuka hasa tairi za mbele. Kupasuka kwa tairi kunaweza kuwa ni kwa sababu zifuatazo:

1: Tairi ni substandard na haiwezi kuhimili mwendokasi na hali ya barabara
2: Tairi kipara (imekwisha na kuchaa), hivyo kutostahili kutumika
3: Tairi imekwishapitiliza muda wake wa matumizi (Expiry)

Nikizungumzia sababu ya 3. Plastic, mipira pamoja na tairi za magari zina muda wa "exipiry date" tangu ilipotengenezwa kiwandani, mara nyingi ni miaka mitatu from the date of its manufacture. Haijalishi kama ni michellin au nani, tairi kama imekwisha expire, hata kama umeinunua dukani bado mpya haijatumika, lakini kama ime-expire kwa kukaa store muda mrefu, then tairi hiyo itapasuka wakati wowote ikipata joto. Hii ni hakika hasa kwa magari yanayofanya safari ndefu kwenye njia ya lami. Ni watu wachache au wamiliki wachache wa vyombo vya usafiri hata wanaomiliki magari binafsi akienda kununua tairi haangalii "expiry date" ya tairi husika.

Nadhani kuna haja ya kuwa na chombo maalumu cha serikali kufanya uchunguzi wa ajali hasa kwa kujikita katika masuala ya kifundi kama haya. Kwa mfano kama gari imepata ajali na chanzo kikawa ni kupasuka kwa tairi, ninategemea wahusika wachukue tairi waifanyie uchunguzi kuangalia mambo hayo matatu niliyoyaeleza, na kukagua tairi zote zilozokuwa kwenye gari husika wakati ajali inatokea.
 
Au tuombe wazungu waje kutufikiria?

Mzee Mwanakijiji, kwa kumbukumbu zangu yapata miaka kama 3-4 sasa tangu serikali itamke kuwa wenye mabasi hawataruhusiwa kuendelea na mkorogo wa engine za fusso na home-made bodi hasa kwa mabasi yanayoenda mikoani. Lakini cha ajabu waliingilia kati watu wakubwa na zoezi zima limekufa kifo cha mende. Ukiangalia mabasi yanayoongoza kwa ajali -Sumry, abood, hood yote haya yanafanyiwa 'uumbaji' hapa hapa.

Miezi kama miwili hivi nilingia mtaani kuongea na baadhi ya madereva wa mabasi kuhusu hizi ajali na kwa asilimia kuwa walisema mabasi mengi haya ubora kwa sababu engine na bodi haviko sahihi. Na kwa maoni yao kama serikali itaendelea kukaa kimya kuhusu 'hizi major alterations' zinafanywa kwanye mabasi ajali zitaendelea kuongezeka.

Wanasheria wangetusaidia hapa kama inawezekana kumshitaki mkuu wa Sumatra kwa kutoa vibali kwa wamiliki wa mabasi yanayohatarisha usalama wa abiria.
 
Kwa upande wangu mimi nnaona hakuna uwajibikaji kwa kila sehemu husika.Ajali za barabarani husababishwa na vitu vikuu vitatu.
•Sababu zitokanazo na Chombo(Gari)
•Sababu zitokanzo na mazingira(Miundombinu)
•Sababu zitokanzo na binaadamu(Dereva)
Tukianza na Chombo(Gari)mengi ya magari yanayoingizwa kwa kusajiliwa kwa kubeba abiria hayana viwango vinavyotakiwa,hayakaguliwi kabla ya kuanza safari au baada ya kumaliza safari.
Sababu ya pili-Sababu zitokanazo na mazingira,je barabara zetu zinakidhi viwango!?je vibao elekezi vya barabarani vipo na vinaonekana kwa uwazi zaidi!?
Sababu ya tatu ni binaadamu(Dereva/police usalama barabarani/maafisa Wa ukaguzi-Sumatra.Hawa wote nao hawatekelezi kazi zao kwa usahihi.mfano je madereva wanazijua sheria za usalama barabarani na kuziheshimu kwa kuzitii!!?Je madereva wanavijua vibao elekezi barabarani na wanaweza kuvitafsiri na kutekeleza maagizo yake kwa usahihi!!?.Polisi rushwa imewazidi na imefunika makosa yote ya dereva.Sumatra kazi Yao ni kukaa ofisini utafikiri barabara za magari zinakatiza ktk maifisi yao.Kazi ya Sumatra na viongozi waliopo serikalini kwetu ni kutoa matamko kila siku-ukija ktk utekelezaji Wa maagizo yao ni ziro.
Ushauri wangu:
Viongozi wote ktk sekta zote Serikalini,hamkuchaguliwa kwenda kukaa ofisini na kupulizwa na viyoyozi mlichaguliwa ama kuteuliwa na Watanzania muwatumikie Watanzania ambao maisha yao ya kila siku hayapo ktk ofisi zenu bali wapo mtaani so njooni mtaani huku mjoonee.
 
Kumekuwa na hoja za kutupia lawama chassis za malori katika uundaji wa mabasi. Naomba nieleweshwe tofauti hasa ni ipi baina ya chassis ya lori na ya basi, katika suala la ubora? (Suala la urefu wa chassis likiwekwa kando).

Mabasi mengi ya siku za nyuma (kabla ya enzi za Marcopolo) karibia yote yaliundwa kutokana na chassis hizi za malori, leo ni kitu gani kimebadilika? Tafadhali naomba wataalam waje hapa watupe darasa.
 
Au Tanzania ina matatizo ya mainjia kama ilivyo kwa wanasheria?

Kwani Wanasheria wana matatizo gani ? Mi nadhani ukitaka kuchambua fani zote, kwa hapa kwetu, hakuna isiyokuwa na matatizo......
1. wahasibu....hao ndio wameikausha nchi kwa wizi...... ndio wanaiba fedha za miradi na kurekebisha balansi sheets za Halmashauri zetu...maendeleo hakuna;

2. Madaktari....ndio wanatumalizza mahospitalini na kila kukicha unaona watu wanapelekwa India kutibiwa.......

3. Wafamasia....wanatupa dawa za kichina, na wengi wanajidai madaktari kuwapa dawa watu kwenye viduka vyao...na kuwaua kwa wrong diagnosis kwa kuwa wao si madaktari;

4. Waandishi.....wengi ndio wanahatarisha amani ya nchi hii kwa uandishi wao wa kiushabiki...mfano tu magazeti ya leo ukisoma habari za Igunga utastaajabu ya Musa;

List inaendelea.....hakuna fani isiyo na matitizo....matatizo si ya fani bali ya watu.....na kwa taarifa tu.....naamini kabisa wanapotengeneza bodi za magari.....watengenezaji si Mainjinia.....ni hawa mafundi wetu makanjanja wanaolipwa ujira wa siku.....

Yule Mchaga....Sawaya/Kilimanjaro Trans anaweza kuajiri Injinia kweli ? sidhani !
 
siku hizi hayo mabasi wanayaunda kenya ama arusha, lakini kwa mtindo hule hule wa kupeleka chassis za malori, ama wengine wananunua mabody ya mabasi aina ya macropolo kutoka afrika brazil na afrika kusini na kuja kuyapachika kwenye chassis za malori, ni sawa na kuchukua paa la nyumba ya mwingine kuja kuliweka kwenye nyumba yangu, mabasi yanayoingia nchini kama mabasi ni yutong sijui yanatengenezwaje huko china na kwa ubora gani. mamlaka zinazohusika nazo ndiyo hivyo, inakuwaje mara ya kwanza kuingiza chombo nchini lazima uonyeshe kwamba hicho chombo kinakotoka kimekaguliwa na ni ruksa kuwa barabarani wanakupa road licence, lakini inapoisha na unataka kurenew hao hawakagui, yani unalipia tu na unapewa , kama break zinafail ama matairi profile zinaruhusu ama nihaje hakuna anayejali, si mwenye chombo wala mamlaka husika, na hii yote inasababishwa na sisi kila kitu kumsingizia mungu, hivi kama unauthamini kweli huai wako utandesha gari ambalo halina break ama matairi yake kipara kwa kwenda. watu hawathamini huai wao, so ni kazi sana kuthamini wa wenzao. sisi tubadilike, tukibadilika serikali nayo itabadilika
 
bado sijasikia ni wapi mabasi haya yanaunganishwa na ni chombo gani kinasimamia? tuachane na ya Katiba mpya kwanza tuzungumzie right now tusije kudhania katiba mpya itatatua matatizo ya ajali au matatizo mengine yoyote yale. Kuna vitu tunaweza kuvifanya sasa hivi
...Mkuu kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa mabasi mengi ukiacha ya kampuni chache kama Dar Express, Abood huwa yanajengewa mabody Kenya. Miaka ya nyuma Tanzania kuliwa na kampuni moja ya kujenga body za mabasi nadhani ilikuwa ikiitwa Hari Sigh body builders Coy ambayo sidhani kama bado ipo. Nina rafiki yangu mmoja ni dereva wa haya mabasi ya kwenda mikoani alinidokeza kuwa ukiondoa tatizo la matajiri kupenda kununua tairi za low quality ambazo nyingi ni cheap, pia body zinazojengwa Kenyaa haziko well balanced kiasi kwamba basi linapokuwa katika mwendo kazi basi hapo kinachohitajika na uzoefu wa dereva wa basi husika kucheza na kitu wao wanaita " pley ya steering" (sina uhakika na spelling za hilo neno la kwanza ) ili kulituliza basi bara barani sasa kama dererva atakuwa sio mzuri wengi huishia kuyapiga chini kwani hata inapofika muda wa kupishana na magari mengine na hasa malori makubwa inakuwa tatizo mwishowe ni ajali....Suala la quality control ni muhimu hata kama jirani zetu ndio wanachakachua hizo body.
 
Mi nasema tatizo la nchi hii ni ufatiliaji na uwajibikaji na usimamizi tu ndoa hatuna na ndo mana kika kitu kimekaa shakala bagala....vitu vyote mlivyotaja hapo juu ni tatizo na ili vikae sawa ni lazima hayo mambo matatu niliyosema yafuatwe kikamilifu
 
Majoja asante sana kwa kutupa mwanga kidogo. Mimi ninaamini kuwa mojawapo ya mabadiliko makubwa ambayo tunaweza kuyaleta nchini na kuanza kuleta maendeleo ya kweli ni kuanza kukataa maelezo ya kishirikina ya mambo yanayotokea. Ni lazima tuanze kuhoji sababu za kisayansi za kwanini vitu fulani vinatokea ni pale tu ambapo labda sayansi haiwezi kutueleza ndipo tunafungua macho yetu na kujiachilia kwa Providence. Ajali ya meli ya Bukoba na hata hii ya juzi ya ZAnzibar ni ajali ambazo zinaweza kuelekezeka kisayansi.

Naamini ajali za barabarani hata kama zinasababishwa na makosa ya watu lakini pia kuna sababu za kisayansi. Kwa mfano, mtu anapokuwa kwenye basi ambalo limeundwa pasipo kufuata kanuni za fizikia za mwendo, au maumbo anaweza kwenda mwendo japo mdogo (80km/h ni mdogo kulinganisha na sisi tu tunaoenda 65-80 M/h (sawa na 104km/hr - 128 km/h) tunaenda mwendo mkubwa sana lakini husikikii mlolongo wa ajali za namna hii hasa zinazotokana na mwendo kasi.

Sasa ni kwamba hatuna vyuo vikuu vyenye uwezo wa kufanya utafiti wa kisayansi kufuatilia tabia za uendeshaji zikoje (driving habit), au kuangalia barabara zetu zimejengwaje au vitu kama hivyo.

MKJJ thanks kwa comments zako kwa somo hili ambalo ni tete sana kwa wakati huu.
Nafikiri kuna haja kubwa ya kupanua mawazo katika fani ya usafirishaji ili kuwa na wigo mpana zaidi wa kulifikiria suala lenyewe.
"Players" katika fani hii ya usafiri na usafirishaji wamekuwa wengi sana na wote wana act in an uncoordinated manner.
Pamoja na juhudi kubwa za kujenga mabarabara, kununua mabasi na magari,kununua matreni,kununua meli, kununua ndege , usafiri na usafirshaji is a process that has got to be coordinated in a clock work manner.
Na hii ni fani ya usafiri na usafirishaji ni industry in itself-haiwezi kufikiriwa at individual level.
Ajali tunazoziona leo ni matokeo ya fikra finyu zinazo inandama fani hii ya usafiri na usafirishaji.
Tusisahau kuwa katika fani hii every thing is in motion na sio static-motion inamaana an ever changing scenario inayomhusu binadamu at the centre.
Hivyo basi leo nchini Tanzania barabara za speed limit 80km/hr , kuna mabasi yanayokwenda hadi 120-140km/hr.
Miundo mbinu hii haisupport uzito huo na spidi hiyo.Katika barabara kuna kona(curves) ambazo zina mwinuko upande mmoja( super elevation) ili kubebe uzito wa spidi ya gari(centrifugal force).
Barabara zetu nyingi sana za zamani hazina miinuko hiyo, kwa hiyo basi likipita hapo kwa mwendo wa kuruka na likakutana na hatari yoyote mbele wigo wa kujiepusha unakuwa mfinyu kutokaa na basi kubebwa na hizo forces za kuivuta nje ya barabara.
Katika design za barabara optimum speed na uzito wa motokari ni muhimu kufikiriwa kabla ya ujenzi.
Hivyo basi dereva akikuta traffic signs za kuonyesha speed limit hizo si kwa ajili ya mapolisi bali kwa ajili ya usalama wake mwenyewe.

Halikadhalika usafiri wa treni, anga, meli vyote hivi lazima viwe na miundo mbinu pamoja na wafanyakazi wa kutosha kuhakikisha movement zote za vifaa vya abiria na mizigo viko controlled.
Kama nilivyo sema hili somo no kubwa na pana
Lakini bado liko katika uwezo wa waTanzania ku simamia.
Ajali tunazoziona zinatokana na kukosa weledi katika kusimamia , jambo ambalo linasikitisha sana
 
Back
Top Bottom