SAWEBOY
JF-Expert Member
- Apr 6, 2011
- 241
- 173
Wakuu wana JF,
Kuna tetesi kuwa ukifungua fixed account ya 10Million ktk benk za Exim, CRDB, Posta bank, NBC limited au NMB, kwa kila baada ya miezi mitatu - inazaa faidi kati ya sh. 1.8 mill up to 2.1 mil.
Hii ina maana kuwa kwa muda wa mwaka 1, yaani 12 months unakuwa umepata faida ya sh.7.2 million up to 8.4 milion
Je, hizo habari zina ukweli wowote? Kwa anayefahamu plse naomba tufahamishe na sisi ili tuweze invest soon ktk hiyo fixed account.
NB: Nimeuliza hilo coz nipo mbali kidogo, huku madongo kuinama ningekuwa jirani ningefanya follow up nije na data kamili
Asanteni,
Nawasilisha
=================

Katika benki za biashara kuna aina tatu za akaunti, kwa kiingereza zikifahamika kama ‘Savings account’, ‘Current accounts’ na ‘Fixed accounts’
Ukiachana na majina ambayo benki itaamua kuipa akaunti husika lakini huangukia katika aina hizo za akaunti. Namba moja ni akauti ya kuhifadhi pesa ambayo mara nyingi huwa na gharama za uendeshaji na hela yake hupungua kadiri inavyozidi kukaa benki
‘Current accounts’ hii ina sifa kuu ya mtu kuweza kutoa kiwango zaidi ya alichonacho katika benki husika. Mara nyingi huwa wanaziita akaunti za biashara na mwenye akaunti katika aina hii huwa na kitabu cha hawala/hundi
‘Fixed account’ hii ni aina ya akaunti ambayo inalipa mara baada ya muda wake mliokubaliana kuisha. Hii tu huweka pesa benki kwa muda fulani benki nyingi huanzia miezi mitatu, na mtu hatoruhusiwa kutoa hela kwenye akaunti yake hadi muda waliokubaliana kufika
Aina hii ya akaunti hutoa riba kwa aliyeweka hela na haina nyingi hazina makato ya uendeshaji. Aina hii ya akaunti ni moja kati ya uwekezaji mzuri kwa mtu asiyeweza kashkashi za biasahara au akiwa amepata hela ya ghafla na hajui afanyie nini
Ni sawa kuweka hela benki lakini ukiweka kwa ‘savings account’ ni sawa na kuweka mfukoni na muda wowote unaweza kuitoa, lakini ‘fixed account’ mtu hawezi kutoa hela hadi muda utimie
Ukiachilia mbali kuwa na gawio baada ya muda, akaunti hizi pia hutumika kama dhamana ya mikopo kwa taasisi mbalimbali
Signed
Oedipus
Habari ndugu,
Sasa ni hivi, kila bank inatofautiana kutokana na faidaunazoweza kupata kwa kutumia fixed accounts, pia faida inategemea kiwango chafedha na muda unaoziacha pesa zako.
Zaman niliwah kuziona za Exim Bank ilikuwani asilimia chini kidogo ya kumi. Nimejaribu kutazama kwenye web yao kabla sijakujibu itappears wameiondoa ile table iliyokuwa nayo.
USHAURI WANGU
Jaribu kutembele matawi mbali mbali ya benki, utapata maelezo mazuri na kuchagua mwenyewe. Ila kumbuka kuna kitu kinachoitwa compounding yaan tuchukue mfano Benk X wanatoa 8%per annum, then ukiweka 5mil per annum unatarajia kupata lak 4 kwa mwaka.
Hivyo basi mwaka wa pili haitakuwa 8% ya 5mil ila ni 8% ya 5.4mil ukijulisha na ile faida yako ambapo itakuwa 432,00 kwa hiyo itaendelea hivyo hadi mwaka wako watano.
Good luck with your investment, na hongera kwa kuwaza hivyo maana Fixed Deposit ni confirmed profit